Nenda kwa yaliyomo

Uzawa wa halali Katika Fiq’hi ya Kiislamu

Kutoka wikishia


Uzawa wa halali (Kiarabu: طهارة المولد), Uzawa wa halali Katika Fiq’hi ya Kiislamu, unahusiana na kule mtu kuzaliwa kupitia njia zinazokubalika kisheria, ambapo mtoto huzaliwa kupitia ndoa iliyofungwa kihalali, yaani kupitia makubaliano ya sharia za Kiislamu. Uzawa wa halali ni dhana muhimu inayotambuliwa kama ni sharti katika mambo fulani ya kidini. Kwa mfano, katika baadhi ya masuala ya kidini, kama vile kushika nafasi ya ijitihadi, mwanazinaa hawezi kukubalika katika nafasi hii, na uzawa wa halali ni miongoni mwa sharti muhimu za ijitihadi. Jambo jengine lanalohitaji sharti hii, ni nafasi ya uimamu wa Sala ya Jamaa au ya Ijumaa, ni lazima awe ni mzawa wa halali, kwani uzawa wa halali unahusiana na hadhi ya imamu huyo. Jengine ni ukadhi (jaji katika mahakama za Kiislamu), ni lazima kadhi awe na sifa ya uzawa wa halali ili awe na uhalali wa kutoa hukumu katika mahakama za Kiislamu. Katika Uislamu, mwana haramu hawezi kukubalika kama ni shahidi, kwa sababu sheria za fiq’hi ya Kishia, shahidi anatakiwa kuwa na uzawa wa halali ili ushahidi wake uchukuliwe kuwa wa kuaminika na halali kisheria.

Katika Riwaya zilizopatikana kutoka katika vyanzo vya Kishia na Ahlu-Sunna, imeelezwa kwamba; kuwapenda Ahlul-Bait (a.s) na Imamu Ali (a.s) ni alama ya uzawa wa halali, huku chuki na uadui kwao vikionekana kuwa ni dalili ya uzawa wa haramu.

Utambulisho wa Uzawa Halali na Umuhimu Wake katika Fiq’hi

Katika Fiq’hi ya Kiislamu, neno halali linamrejelea mtu aliyezaliwa kupitia ndoa sahihi ya kisheria, inayokubalika kwa mujibu wa sharia za Kiislamu, na sio kupitia uzinzi au njia zisizo halali. [1] Uzawa wa halali, unaojulikana pia kama usafi wa asili (طهارت مولد), unashikilia nafasi muhimu mno katika sheria za Kiislamu, kiasi ya kwamba hata haki ya unaathiri pamoja na haki ya kushikilia nafasi mbalimbali zimesimaa juu ya msingi huu. [2] Kuna haki kadhaa ambazo mwanaharamu hawezi kuzipata, miongoni mwa haki zilizoegemea kwenye msingi wa uzawa wa halali ni pamoja na; ukadhi [3] na uimamu wa Sala ya Jamaa. [4] [5]

Miongoni mwa milango ya fiq’hi iliyojadili suala la uzawa wa halali  -unaojulikana kama «usafi wa asili» [6] pamoja na haki mbali mbali za mwana wa zinaa, ni pamoja na; mlango wa ijitihadi ufuasi wa kuwafwata wanazuoni (Ijitihad wa Al-Taqlid), mlango wa Sala za Jamaa, mlango wa ndoa, mlango wa ukadhi na mlango wa masuala ya ushahidi na mashahidi. [7]

Mifano ya Wazawa Halali katika Fiq’hi ya Kishia

Kulingana na fiq’hi ya Kishia, dhana ya halali ni pana zaidi kupindukia fikra ya kuzaliwa kupitia ndoa ya kisheria ya Kiislamu. Kulingana na Kishia dhana hii inajumuisha ndoa nyengine mbalimbali zinazotambuliwa uhalali chini ya mazingira fulani. Hapa kuna mifano ya watu wanaohesabiwa kuwa ni wazawa halali kwa mujibu wa fiq’hi ya Kishia:

  • Mtu aliyezaliwa kutokana na Wat-u bi al-shubha (jimaa ya kimakosa): Hii inarejelea kitendo cha maingiliano ya kijinsia kilichofanyika kimakosa, ambapo baba na mama wote wawili walianguka kimakosa katika tendo la ndoa (kijinsia), kinnyume na kisheria, huku wakiamini kwamba kitendo chao ni halali. [8] Ikiwa wazazi wawili (baba na mama) walikuwa na dhana isiyo sahihi katika uhalali wa kitendo chake (yaani walidhani kuwa wapo katika misingi halali), mtoto wao atahesabiwa kuwa ni halali. Hata hivyo, kama mmoja wao alijua kuwa kitendo hicho ni haramu, mtoto huyo atahesabiwa kuwa mtoto zinaa kwa upande wa aliyefahamu makosa hayo. [9]
  • Mtu aliyezaliwa katika kipindi cha mahusiano haramu ya ndoa: Hali hii inahusisha matukio kadhaa ikiwa ni pamoja na; tendo la ndoa lililofanyika wakati mwanamke yuko kwenye hedhi, ndani ya mchana huku mtu akiwa katika funga ya wajibu, au wakati wa Ihram (hali ya mtu kuvaa nguo maalumu kwa ajili ya ibada ya Hija). [10] Ingawa kitendo chenyewe ni haramu, ila mtoto aliyezaliwa kutokana na hali hizi bado anahesabiwa kuwa ni mwana halali katika sheria za Kishia. [11]
  • Mtu aliyezaliwa kupitia ndoa halali kwa mujibu wa dini nyingine, hata ikiwa ni ya kishirikina: Katika fiq’hi ya Kishia, mtoto aliyezaliwa kutokana na ndoa inayotambulika kisheria katika dini nyingine, iwe ni ya kishirikina au wafwasi wa dini nyinginezo, bado hupata heshima ya kuhesabiwa kuwa ni mwana halali. [12] Wanazuoni wengi wanakubaliana kuwa ndoa katika dini nyingine zinaweza kutambuliwa kama ni ndoa halali, mradi tu zinafuata mila zinazokubalika ndani ya sheria zao. Mafaqihi wa madhehebu ya Kishia wanamheshimu kila mwana aliyezaliwa kulingana na misingi ya sheria za mila nyengine, hata mwana aliyezaliwa kupitia ndoa za maharimu wenyewe kwa wenyewe pia naye hupewa heshima ya uwana halali mbele ya wanazuoni wa madhehebu ya Kishia. [13] Sababu ya wanazuoni wa fiqhi katika suala hili inatokana na Riwaya zinazotambua mila za ndoa za dini na madhehebu mengine, hata ikiwa ni za washirikina. Riwaya hizi zinaheshimu ndoa zinazofanyika katika tamaduni na dini hizo, ingawa hazikubaliki katika sheria za Kiislamu. [14] Baadhi ya wanazuoni pia hutumia kanuni ya Jab (kufumbia macho mambo yaliyotendwa kambla ya kusilimu), ambayo inahusisha msamaha kwa vitendo vya kabla ya kusilimu. Kwa mfano, ingawa ndoa ya asiyekuwa Mwislamu aliyefunga ndoa na mama yake, inahisabiwa kuwa ni ndoa haramu katika Uislamu, ila baada ya kusilimu kwake, vitendo vyake vyote vya nyuma vinafumbiwa macho na havizingatiwi kamwe, na hivyo mtoto aliyezaliwa kupitia ndoa hiyo kabla ya kusilimu kwa mtu huyo, anakubalika kama ni mwana halali. Kanuni hii inatilia mkazo msamaha wa Uislamu kwa wale wanaobadili dini zao na kusikamana na mafundisho ya Kiislamu. [15]
  • Mtu mwenye kutiliwa shaka juu ya uzawa wake, ila wazazi wake wanajulikana: Katika hali ambapo mtoto atakuwa hana uhakika juu ya uzawa wake, au kuna wasiwasi juu ya uhalali wa wazawa wake, mtoto huyo bado huhisabiwa kuwa ni mwana wa halali. Pia Wanazuoni wengi wa Kishia wanakubaliana kuwa, ikiwa wazazi wa mtoto hawajulikani, bado mtoto huyo yabidi kutambuliwa kama ni mwana wa halali. Hii ni kwa msingi unaowataka Wailamu kudhaniana dhana njema, hasa ikiwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kinyume chake. [16]

Fikra hizi zinaonesha kwamba katika fiq’hi ya Kishia, suala la uzawa wa halali si suala finyu linalotanda kivuli chake kwenye mipaka ya ndoa za Kiislamu pekee, bali linahusisha hali na ndoa mbalimbali zinazofanyika chini ya kivuli cha mila na tamaduni mbali mbali.

Sharti ya Uzawa wa Halali Katika Baadhi ya Nyadhifa na Amali

Kulingana na fatwa za wanazuoni wa fiqhi, uzawa wa halali (yaani, kuzaliwa kupitia njia halali kisheria) ni sharti muhimu kwa baadhi ya majukumu ya kidini na kijamii. Miongoni mwa majukumu yanayo shurutishwa uzawa halali, ni kama ifuatavyo:

  • Uongozi wa Kidini (Marja’iyya): Uzawa wa halali ni moja ya masharti yanayotakiwa kuwa nayo mujtahid, ambapo bila ya kuwepo sharti hiyo, mujtahid huyo hatokuwa na idhini ya kufuatwa kama ni mtoaji fat'wa za kidini (marjaa-taklidi). [17] Wanazuoni kama Shahidi Thani wanasema kuwa masharti ya uzawa wa halali ni jambo lililokubalika na wanazuoni wote wa Kishia, yaani ni lenye mawafikiano baina na wanazuoni (ijmaa). [18]
  • Imamu wa Swala za Jamaa na Ijumaa: Kulingana na makubaliano ya wanazuoni wa madhehebu ya Shia Imamiyya, uzawa wa halali ni sharti la lazima kwa mtu kuwa imamu wa Sala ya Jamaa. [19] Kwa hivyo, haifai mtu aliyezaliwa kutokana na uzinzi kuwa imamu wa sala hiyo. [20] Hata hivyo, ikiwa kuna shaka juu ya uhalali wa uzawa wa mtu huyo, lakini kukawa hakuna ithibati kwamba amezaliwa kupitia tendo la uzinzi, mtu huyo ataruhusiwa kushika nafasi ya uimamu wa sala, hii ni kwa mujibu wa makubaliano ya wanazuoni (ijmaa). [21] Masharti haya pia yanatumika kwa imamu wa Sala ya Ijumaa. [22]
  • Kadhi (Jaji): Uzawa wa halali ni moja ya masharti muhimu kwa kadhi katika kufanya kazi ya kutoa kuhukumu. [23] Kwa hivyo, mtu aliyezaliwa kwa njia ya haramu (zinaa) hawezi kuwa jaji. [24]
  • Shahidi: Kulingana na fatwa za wanazuoni wa fiqhi, mashahidi wanaotoa ushahidi mahakamani ni lazima wawe wana wa halali. Hii ina maana kwamba ushahidi wa mtu aliyezaliwa kutokana na uzinzi (waladul zinaa) hauwezi kukubalika mahakamani. [25]

Sababu za Kumnyima Mzaliwa wa Zinaa Kazi ya Uhakimu na Ushahidi wa Kimahakama

Baadhi ya wanazuoni wa Kishia na watafiti wameeleza sababu mbalimbali juu ya kumnyima mzaliwa wa zinaa nafasi ya kushika nyadhifa za ukadhi na shahidi. Kwa mfano, Sayyid al-Murtadha (Aliyeishi kati ya mwaka 355 na 436 Hijria) mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kishia, anasema kuwa; sababu kuu ya suala hili ni kwamba; Mwenye Ezi Mungu anajua kuwa mtu aliyezaliwa kwa njia ya zinaa hawezi kuchagua na kufadhilisha mema na yale yenye kujenga amani. Hiyo ndiyo sababu ya yeye kunyimwa haki ya kushikilia baadhiya majukumu likiwemo jukumu la kutoa ushahidi mahakamani. [26] Watafiti wengine wakitoa mtazamo wao, wamebainisha wakisema kuwa; "kuto kukubalika kwake kijamii" ni moja ya sababu zinazomzuia mzaliwa wa zinaa kushika majukumu hayo. [27] Aidha, baadhi ya watafiti wanaamini kuwa; kama vile sifa za kimaumbile za mtu zinavyorithiwa kupitia vinasaba (genes), vivyo hivyo sifa za kiroho pia zinaweza kurithiwa. Wao wanaamini kwamba; watoto wanaozaliwa nje ya ndoa halali mara nyingi huwa na mwelekeo mkubwa zaidi wa kufanya makosa ya jinai. [28]

Je, Mapenzi kwa Imamu Ali (a.s) ni Alama ya Uzawa Halali?

Kuna Riwaya kadhaa zinazo patikana katika baadhi ya baadhi ya vyanzo vya Kishia [29] na vya Ahlus-Sunna, [30] zinazosema kwamba; mapenzi kwa Ahlul-Bait, hususan kwa Imamu Ali (a.s), ni miongoni mwa ishara za uzawa wa halali, huku chuki dhidi yao ikichukuliwa kuwa ni alama ya uzawa kupitia njia ya zinaa. Kwa mfano, katika vyanzo vya Ahlu-Sunna, kuna ripoti kama hizo zimesimuliwa kutoka kwa Abadat ibn Samit na Abu Sa'id al-Khudri, (ambo wote ni Masahaba wa Mtume (s.a.w.w)), wao wamenukuu wakisema kwamba; ili kuwatambua watoto wa halali, Masaha wa Mtume (s.a.w.w) walikuwa wakiwapima watoto wao kwa kipimo cha mapenzi kwa Ali ibn Abi Talib. Hivyo pale walipokuwa wakigundua kuwa hawana mapenzi naye, walijua kuwa watoto hao hawakutokana nao, na kwamba wao walikuwa ni wazawa wa njia za haramu. [31] Ibn Jazari (aliyeishi kati ya mwaka 751 na 833 Hijria), mtafiti na faq’hi wa madhehebu ya Shafi’i, amesema kuwa tangu zama za kale hadi wakati wake yeye, ilikuwa maarufu kuwa hakuna aliyekuwa na chuki dhidi ya Imam Ali isipokuwa wale waliozaliwa nje ya ndoa halali. [32] Haya yameandikwa pia na Allama Majlisi katika kitabu chake Bihar al-Anwar, ambapo amekusanya hadithi 31 kuhusiana na jambo hili, [33] na katika Mir’at al-Uqul Allama Majlisi amezipasisha Hadithi hizo kusema kuwa ni Hadithi ziliznukuliwa na watu wengi kupitia njia tofauti (mutawatir). [34]

Hata hivyo, kinyume na mtazamo wa Allama Majlisi kuhusu kuenea kwa Hadithi hizi zinazo onyesha mapenzi kwa Ahlul-Bait kama ni alama ya uzawa halali, na chuki kama alama ya uzawa wa zinaa, ila kuna baadhi ya watafiti wa kidini waliopinga usahihi wa baadhi ya Riwaya hizi. Watafiti hawa wanaamini kuwa; wasimuliaji wa Riwaya hizo ima ni wasimulizi wasiojulikani au wanahesabiwa kuwa ni miongoni mwa Maghulati (watu waliopitiliza mpaka katika kuwapnda Ahlul-Bait). [25]

Aidha, imeelezwa kuwa uzawa wa haramu hauondoi uwezo wa mtu kufanya maamuzi sahihi. Kwa hivyo, uzawa huo sio sababu kamili ya kufanya dhambi au kujiepusha na mapenzi ya kuwapenda Ahlul-Bait. Bali inawezekana mzaliwa wa zinaa, kwa hiari yake, akawa na mpenzi na Ahlul-Bait, kama ilivyo kwa watu wengine. Vilevile, pia hakuna ushahidi kwamba kila aliyezaliwa kwa njia halali atakuwa na mapenzi kwa Ahlul-Bait. Hivyo, Hadithi zinazozungumzia uadui wa wazaliwa wa zinaa kwa Ahlul-Bait, haziashirii hukumu ya jumla na ya kudumu; bali zinaonesha kuwa, kwa kawaida, wazaliwa wa zinaa wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kuwa na chuki na Ahlul-Bait kuliko wale waliokuwa na uzawa wa halali, ingawa hili sio jambo la lazima kwa kila mtu. [36]

Rejea

Vyanzo