Nenda kwa yaliyomo

Uadifu wa Masahaba

Kutoka wikishia

Uadilifu wa Masahaba (Kiarabu: عدالة الصحابة) ni nadharia na itikadi ya aghalabu ya Waislamu wa Kisuni ambao wanaamini kwamba, masahaba wa Mtume (s.a.w.w) wote ni waadilifu na ni watu wa peponi. Kwa mujibu wa imani na nadharia hii, haijuzu kuwakosoa masahaba na kueleza mabaya waliyoyafanya na Hadithi za masahaba hao zinapaswa kuchukuliwa pasina ya kujadili na kuchunguza wasifu wa mpokeaji juu ya uadilifu na kuaminika kwake (jarh wa taadil). Wanazuoni na wasomi wa Shia Imamiyyah na kundi fulani miongoni mwa wanazuoni wa Ahlu-Sunna wanaamini kwamba, masahaba wa Mtume (s.a.w.w) ni kama Waislamu wengine na wanapinga nadharia na itikadi ya kwamba, masahaba wote ni waadilifu.

Wanaounga mkono nadharia ya uadilifu wa masahaban wanatumia baadhi ya Aya katika Qur'ani na Hadithi kuthibitisha madai yao. Miongoni mwa Aya wanazutumia kama hoja yao ni Ayat Ridhwan ambayo inaeleza juu ya Mwenyezi Mungu kuwaridhia masahaba. Hata hivyo wapinzani wa nadharia hii wao wanasema, Aya hii inawahusu wale masahaba tu ambao walikuweko katika baia ya Ridhwan (Baiat Ridhwan) na baada ya hapo wakabakia na kutokiuka ahadi na kiapo chao cha utii. Kadhalika kwa mujibu wa wapinzani ni kwamba, nadharia ya kwamba, masahaba wote ni waadilifu inakinzana na baadhi ya Aya katika Qur’an ambazo zinatoa habari ya kuweko kwa wanafiki miongoni mwa masahaba wa Mtume. Katika kukosoa nadharia ya uadilifu wa masahaba kunatumiwa kama hoja utendaji na matendo waliyofanya baadhi ya masahaba ambayo yanapingana na suala la uadilifu wa masahaba kama kuritadi, kunywa pombe, kumtukana Ali, kuwaua Waislamu na kupigana vita wao kwa wao.

Baadhi ya wahakiki wa Kishia wanaamini kwamba, kusisitiza juu ya itikadi kwamba, masahaba wote ni waadilifu ni hatua ambayo ina malengo kama kuhalalisha Ukhalifa wa Makhalifa watatu na kuhahalilisha pia utawala wa Muawiya ibn Abi Sufyan. Kuasisi nadharia ya ijtihadi ya masahaba, hitilafu baina ya Waislamu, kurejelea ufahamu wa masahaba kuhusu Qur’an na sunna, kuifanya hoja kauli na sira ya masahaba na kukubali hadithi zilizonukuliwa pasi na ya kufuata kanuni ya kujadili na kuchunguza wasifu wa mpokeaji juu ya uadilifu na kuaminika kwake (jarh wa taadil) yametambuliwa kuwa matokeo ya nadharia hii.

Sahaba ni Nani?

Makala Kuu: Sahaba

Sahaba ni mtu ambaye alikutana na kumdiriki Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) na alipofariki, bado alimuamini na alikuwa Mwislamu hakutoka katika Uislamu.[1] Makusudio ya kudiriki na kukutana hapa ni kuonana, kukaaa pamoja, kufuatana naye na kukutana hata kama hayakupita mazungumzo baina yao.[2]Hata hivyo, wengine wameongeza masharti na kuweka mpaka kwa ufafanuzi uliotajwa; miongoni mwao, kusuhubiana kwa muda mrefu na Mtume (s.a.w.w), kuhifadhi riwaya na hadithi kutoka kwake, kupigana na kuuawa shahidi kando ya Mtume,[3] na baadhi ya wengine wametosheka kwa kukutana tu au kumuona Mtume kwa ajili ya kupatiwa anuani ya sahaba.[4] Hata hivyo, kwa mujibu wa Ibn Hajar al-Asqalani, mmoja wa wanazuoni mahiri na mtajika wa Kisuni katika karne ya 7 na 8 Hijiria ni kwamba, kile kinachokubaliwa na wanachuoni ni ufafanuzi wa kwanza.[5]

Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, alipofariki Mtume (s.a.w.w) idadi ya maswahaba zake ilikuwa watu 114,000.[6] Wale waliomdiriki Mtume katika utoto wao wanaitwa al-Shabah al-Sighar (masahaba wadogo) na maswahaba wanawake wanaitwa al-Sahabiyyat[7]

Kubainisha Nadharia ya Uadilifu wa Masahaba

Kwa mujibu wa rai ya wanazuoni mashuhuri wa Kisuni, masahaba wote ni waadilifu.[8] Ibn Hajar al-Asqalani anadai kwamba, Masuni wote walikubaliana juu ya uadilifu wa masahaba wote, na akawaita wale waliopinga nadharia hiyo kuwa ni idadi ndogo ya wazushi na watu bidaa.[9] Vile vile amenukuu kutoka kwa Ibn Hazm (aliyefariki 456 Hijiria) kwamba, masahaba wote wataingia peponi na hakuna hata mmoja wao atakayeingia motoni.[10]

Pamoja na hayo, al-Maziri (Muhammad Ali bin Omar al-Maziri mwenye kuniya ya Abu Abdallah aliaga dunia 530 au 536 Hijiria), mmoja wa Maulamaa wa Kisuni yeye anaamini nadharia ya uaduilifu wa masahaba kwa kundi tu miongoni mwa masahaba ambao walikuwa pamoja na Mtume (s.a.w.w) wakamfuata, wakamtukuza na kumsaidia na wakafuata “nuru iliyoteremshwa pamoja naye”[11]. Baadhi ya Masuni wengine wamewatambua masahaba kuwa ni mithili ya Waislamu wengine na wanaamini kwamba, kuwa pamoja tu na Mtume hakumfanyi mtu ahesabiwe kuwa ni muadilifu.[12]

Kwa mujibu wa Ahmad Hussein Yaqub, ni kwamba, makusudio ya uadilifu wa maswahaba ni kuwa, hairuhusiwi kuwazushia uongo masahabah na kuwakosoa, hata kama wamekosea.[13] Ibn Athir ameandika katika utangulizi wa Usad al-Ghabah: “Masahaba wote ni waadilifu na hakuna ukosoaji unaopaswa kuelekezwa kwa yeyote miongoni mwao.”[14] Kwa muktadha huo, baadhi ya wanachuoni wa Kisuni wamesema kwamba yeyote anayemkosoa mmoja wa masahaba wa Mtume ni kafiri.[15]

Kadhalika makusudio ya uadilifu wa masahaba inazingatiwa kuwa ni sifa maalumu ambayo kwayo riwaya na hadithi za masahaba zinakubaliwa. Khatib al-Baghdadi ameandika: Hadithi yoyote inayoishia kwa Mtume, ni lazima kuifanyia kazi pale uadilifu wa wapokezi wake unapothibitika, isipokuwa kwa masahaba; kwa sababu uadilifu wa masahaba umethibiti; hiii ni kutokana na kuwa Mwenyezi Mungu amewahesabu kuwa ni waadilifu na ametoa habari juu ya utakasifu wao.[16]

Hoja za Wanaokubali Nadharia ya Uadilifu wa Masahaba

Ahlu-sunna wakiwa na lengo la kuthibitisha nadharia yao ya uadilifu wa masahaba wametumia baadhi ya Aya na hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kama hoja ya madai yao.[17] Miongoni mwazo ni:

  1. Aya zinazobainisha kwamba, Mwenyezi Mungu amewaridhia masahaba kama: (وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِ‌ینَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِینَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّ‌ضِی اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَ‌ضُوا عَنْهُ ; Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa).[18] Kadhalika Aya: (قَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ)[19] ; Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipokubai chini ya mti.[20] Wanazuoni wa Ahlu-Sunna wanaamini kwamba, kuwa radhi Mwenyezi Mungu na masahaba ni hoja ya kuwa kwao wote ni waadilifu na wamesema kuwa, mtu ambaye Mwenyezi Mungu amemridhia na yuko radhi naye, katu hawezi kumkasirikia.[21] Kwa mujibu wa wanazuoni wa Kishia Aya hizi aya hizi hazionyeshi uadilifu wa masahaba wote; kwa sababu kutokana na dhahiri ya Aya ya kwanza, inaweza kufahamika kwamba makusudio ya Mwenyezi Mungu ni baadhi ya wahajiri na Ansari, sio wote.”[22] Katika Aya ya pili, makusudio ni wale maswahaba tu ambao walikuwepo kwenye baia na kiapo cha utii cha Ridhwan na kubakia imara katika ahadi yao. Hao ndio waliokusudiwa na sio masahaba wote.[23] Kadhalika kuamini juu ya uadilifu wa masahaba wote ni jambo ambalo linakinzana na kugongana na Aya ifuatayo ambayo inabainisha kwambva, baadhi ya masahaba walikuwa ni wanafiki: (وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ الأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ ممَرَدُواْ عَلَى النِّفَاقِ)[24] ; Na katika mabedui walio jirani zenu wamo wanafiki.[25]
  2. Aya ambazo zinawatambulisha Waislamu kwamba, ndio umma bora na ni umma wa kati na kati (wastani): (كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ)[26] ; Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu. Na Aya ya: (وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا)[27] ; Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wastani. Baadhi ya wafasiriwa Ahlu-Sunna wamefasiri umma wa wastani kwa maana ya umma wenye uadilifu[28] na wakasema kwamba, licha ya kuwa lafudhi ya umma ni “aam” (inazungumzia kwa ujumal) lakini imeshuka mahususi na makusudio ni masahaba.[29] Hii ni katika hali ambayo, kwa mujibu wa wasomi na wanazuoni wa Kishia, Aya hii inaashiria utendaji na matendo ya baadhi ya masahaba na kwamba, uwepo wao umeufanya umma wa Mtume (s.a.w.w) kuitwa na Mwenyezi Mungu kwa jina la umma bora kabisa, na sio masahaba wote.[30]
  3. Hadithi ya Maswahaba ni kama nyota; katika hadithi hii masahaba wa Mtume wamefananishwa na nyota ambapo yeyote atakeyefuata mmoja kati yao basi ni sababu ya kupata uongofu. Kwa mujibu wa wanazuoni na Maulamaa wa Kishia na baadhi ya wanazuoni wa Kisuni ni kwamba, hadithi hii ni bandia na ya kutunga na inakinzana kikamilifu na Aya za Qur’an na hadithi zingine za Bwana Mtume (s.a.w.w).[31]

Kadhalika kwa ajili ya kuthibitisha uadilifu wa masahaba kumetumiwa Aya zingine za Qur’an[32] na hadithi zingine kama vile: “hadithi ya Karne bora kabisa ni karne yangu” na “msitukane masahaba zangu.”[33] Hii ni katika hali ambayo, miongoni mwa masahaba kulikuweko wanafiki kama ambavyo kuna wengine waliritadi na kutoka katika Uislamu mambo ambayo kwa hakika ni kizingiti ambacho hakiwezi kuzifanya Aya na hadithi tajwa zieleze na kubainisha kwamba, masahaba wote ni waadilifu.[34] Kwa mfano, kwa mujibu wa wafasiri Aya ya Naba’ ambayo inasema: “Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni”'[35] ilishuka wa Walid bin Uqbah ambaye alikuwa sahaba.[36]

Utendaji wa Masahaba

Maulamaa wa Kishia na baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wanaamini kwamba matendo ya baadhi ya masahaba yanakiuka nadharia yao ya uadilifu. Kwa mujibu wa Sayyid Muhsen Amin, watu kama Ubaydullah bin Jahsh, Ubaydullah bin Khatal, Rabi'ah bin Umayyah na Ash'ath bin Qays ni miongoni mwa masahaba ambao waliritadi.[37] Pia, kwa kuzingatia riwaya katika Sahih Bukhari, Mtume alitoa habari ya kuritadi baadhi ya maswahaba zake[38]

Kadhalika katika vitabu vya historia, kuna ushahidi wa tabia na matendo ya baadhi ya masahaba ambayo yanapingana na suala la uadilifu, kama vile kunywa pombe, kumtukana na kumsema vibaya Ali, kwenda kinyume na Imamu muadilifu, na kuwaua Waislamu. Miongoni mwao, Busr bin Artat aliwaua Mashia wapatao 30,000 wa Imam Ali,[39] Mughirah bin Shu'ba alikuwa akimkashifu Imam Ali kwenye mimbari kwa takriban miaka tisa,[40] Khalid bin Walid alimuua shahidi Malik bin Nuwayra na usiku huo huo akazini na mkewe[41] na Walid bin Uqbah alikuwa akinywa pombe.[42] Vile vile imepokewa kutoka kwa Shafii kwamba, miongoni mwa masahaba wa Mtume, yaani Muawiya bin Abi Sufyan, Amr bin A's, Mughirah bin Shu'ba na Ziyad bin Abih ushahidi wao haukubaliwili.[43]

Kadhalika, mauaji ya masahaba baina yao ambapo katika vita vya Jamal, makundi mawili ya maswahaba yalikabiliana, ni jambo ambalo halioani na nadharia ya uadilifu kwa masahaba wote; Ibn Abi al-Hadid, mmoja wa Masunni wa Kimuutazila, aliwachukulia Maswahaba walioanzisha vita vya Jamal kuwa ni watu wa motoni, isipokuwa baadhi miongoni mwao kama Aisha, Talha na Zubair kutokana na kutubia kwao. Pia, ana maoni sawa kuhusu jeshi la Sham katika vita vya Siffin kwa sababu ya msisitizo wao wa kuasi. Kulingana na wanafikira wenzake wa Mu'tazili, aliwachukulia Khawarij kuwa watu wa motoni.[44]

Malengo na Matokeo

Waislamu wa madhehebu ya Shia hawajaikubali nadharia ya uadilifu wa maswahaba na wanaamini kwamba maswahaba wa Mtume (s.a.w.w) walikuwa kama Waislamu wengine na hakuna uadilifu wa mtu yeyote unaoweza kuthibitika kwa kusuhubiana tu Mtume.[45] Kwa mtazanmo wao ni kwamba, haiwezekani masahaba wote wa Mtume wakawa wamefikia daraja miongoni mwa madaraja ya taqwa na uchaji Mungu hata iwezekane wote kuwapa sifa ya uadilifu (kuacha madhambi makubwa na kutong’ang’ania kufanya madhambi madogo). Hii ni katika hali ambayo, kwa mujibu wa vyanzo vya historia ya Kiislamu, baadhi ya Maswahaba walidhihirisha imani yao kwa Mtume kwa hofu, kutokuwa na budi na kutokana na kutiwa nguvu nyoyo zao.[46] Kwa mujibu wao ni kwamba, kuzungumzia mjadala wa uadilifu wa Maswahaba kulifanyika kwa malengo yafuatayo, baadhi yake ni:

Kadhalika kuasisi nadharia ya ijtihadi ya masahaba ili kuhalalisha baadhi ya tabia na matendo yaliyofanywa na Maswahaba, kurejelea ufahamu wa masahaba kuhusu Qur’an na hadithi, kuifanya hoja kauli na sira ya masahaba na kukubali hadithi zilizonukuliwa kutoka kwao pasi na ya kufuata kanuni ya kujadili na kuchunguza wasifu wa mpokeaji juu ya uadilifu na kuaminika kwake (jarh wa taadil) na hitilafu baina ya Waislamu ni miongoni mwa mambo ambayo yametambuliwa kuwa matokeo ya nadharia ya uadilifu wa masahaba.[48]

Bibliografia

Suala la uadilifu wa masahaba ni miongoni mwa mambo ambayo Waislamu wa madhehebu ya Suni na Shia wanahitalifiana ambalo hilo limezingatiwa katika athari zilizoandikwa kuhusiana na masahaba,[49] vitabu vya tafsiri,[50] na vya kiteolojia.[51] Kadhalika Waislamu wa madhehebu ya Shia wameandika vitabu vya kujitegemea kuhusiana na hilo ambapo baadhi yavyo ni:

  • Adalat Sahaba; (uadilifu wa masahaba) mwandishi Sayyid Ali Milani mmoja wa Maulamaa wa Kishia katika katika karne ya 14 Hijiria. Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya Kifarsi. Ndani ya kitabu hiki kunakosolewa nadharia ya uadilifu wa masahaba. Mwandishi ameorodhesha baadhi ya Aya za Qur’an Tukufu na mifano ya madhambi makubwa ya baadhi ya masahaba pamoja na kunukuu kauli za baadhi ya shakhsia wakubwa wa Kisuni zinazoelezea kutokuwa waadilifu baadhi ya masahaba.
  • Adalat-i Sahaba dar partuw-i Qur'an, sunnat, wa tarikh; mwandishi wa kitabu hiki ni Muhammad Asif Muhsini mmoja wa Marajii wa Kishia. Katika kitabu hiki uadilifu wa masahaba umetathminiwa kwa mtazamo wa kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu. Mwandishi pia amepinga suala la Mashia kunasibishwa na kauli ya kuwakufurisha masahaba wote.[52]
  • Nadhariyya 'adalat al-Sahaba wa l-marja'iyya al-siyasiyya fi l-Islam; kitabu hiki kimeandikwa na Ahmad Hussein Ya’qubi.[53]
  • Adalat Sahabah, mwandishi Seyyid Muhammad Yathribi.[54]
  • Barresi nazariyeh Adalat Sahaba, mwandishi Gholamhussein Zainali.[55]
  • Nazariyye Adalat sahaba, mwandishi jopo la wahakiki wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s).[56]

Rejea

  1. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 1, uk. 158.
  2. Shahīd al-Thānī, al-Riʿāya, uk. 339.
  3. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 1, uk. 159.
  4. Yaʿqūb, Nazariya-yi ʿadālat-i ṣaḥāba, uk. 15.
  5. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 1, uk. 159.
  6. Shahīd al-Thānī, al-Riʿāya, uk. 345.
  7. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 7, uk. 679; juz. 8, uk. 113.
  8. Ibn al-Athīr, Usd al-ghāba, juz. 1, uk. 10; Ibn ʿAbd al-Barr, al-Istīʿāb, juz. 1, uk. 2.
  9. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 1, uk. 162.
  10. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 1, uk. 163.
  11. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 1, uk. 163.
  12. Ibn Abī l-Ḥadīd, Sharḥ Nahj al-balagha, juz. 1, uk. 9.
  13. Yaʿqūb, Nazariya-yi ʿadālat-i ṣaḥāba, uk. 15.
  14. Ibn al-Athīr, Usd al-ghāba, juz. 1, uk. 10.
  15. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 1, uk. 162.
  16. Khaṭīb Baghdādī, al-Kifāya fī ʿilm al-riwāya, juz. 1, uk. 64.
  17. Khaṭīb Baghdādī, al-Kifāya fī ʿilm al-riwāya, juz. 1, uk. 64; Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 1, uk. 162.
  18. Qurʾān 9:100
  19. Qurʾān 48:18
  20. Khaṭīb Baghdādī, al-Kifāya fī ʿilm al-riwāya, vol. 1, p. 64; Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba, juz. 1, uk. 162-163.
  21. Ibn ʿAbd al-Barr, al-Istīʿāb, juz. 1, uk. 4.
  22. Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 9, uk. 274; Subḥānī, al-Ilāhīyāt, juz. 4, uk. 445.
  23. Ṭūsī, al-Tibyān, juz. 9, uk. 329.
  24. Qurʾān 9:101
  25. Qurʾān 9:101
  26. Qurʾān 3:110
  27. Qurʾān 2:143
  28. Suyūṭī, al-Durr al-manthūr, juz. 1, uk. 144; Fakhr al-Rāzī, Mafātīḥ al-ghayb, juz. 4, uk. 84.
  29. Khaṭīb Baghdādī, al-Kifāya, juz. 1, uk. 64.
  30. Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 1, uk. 123.
  31. Subḥānī, al-Ilāhīyāt, juz. 4, uk. 443.
  32. Qurʾān 48:29; Qurʾān 57:11; Qurʾān 59:8-10; Qurʾān 9:117; Dūkhī, ʿAdālat-i ṣaḥāba bayn al-qadāsat wa al-wāqiʿ, uk. 42-87.
  33. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba, juz. 1, uk. 165.
  34. Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 9, uk. 374.
  35. Qurʾān 49:6.
  36. Ṭabrasī, Majmaʿ al-bayān, juz. 9, uk. 198.
  37. Amīn, Aʿyān al-Shīʿa, juz. 1, uk. 163.
  38. Bukhārī, Ṣaḥīḥ al-Bukhārī, juz. 8, uk. 121, hadith 6585.
  39. Ibn Aʿtham al-Kūfī, Kitāb al-Futūḥ, juz. 4, uk. 238.
  40. Balādhurī, Ansāb al-ashrāf, juz. 5, uk. 243.
  41. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba, juz. 5, uk. 561.
  42. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba, juz. 6, uk. 482.
  43. Abūriyā, Shaykh al-muḍīra Abū Harīra, uk. 219.
  44. Ibn Abī l-Ḥadīd, Sharḥ Nahj al-balagha, juz. 1, uk. 9.
  45. Shahīd al-Thānī, al-Riʿāya fī ʿilm al-dirāya, uk. 343; Amīn, Aʿyān al-Shīʿa, juz. 1, uk. 161.
  46. Amīn, Aʿyān al-Shīʿa, juz. 1, uk. 162.
  47. Yaʿqūb, Nazariya-yi ʿadālat-i ṣaḥāba, uk. 105-108.
  48. Fakh ʿAlī, Majmuʿa guftmānha-yi madhāhib-i Islāmī.The Discourse on Righteousness of Companions (Persian)
  49. Ibn ʿAbd al-Barr, al-Istīʿāb, juz. 1, uk. 4; Ibn al-Athīr, Usd al-ghāba, juz. 1, uk. 10; Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, al-Iṣāba, juz. 1, uk. 161-165.
  50. Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 9, uk. 374-375.
  51. Subḥānī, al-Ilāhīyāt, juz. 4, uk. 445.
  52. "Righteousness of the Companions in the light of Qur'an, Sunna and History", Hadith.net (Persian)
  53. The theory of "Righteousness of the Companions" and political authority in Islam, Fiqahat Library. (Persian)
  54. "Righteousness of the Companions", Collection of criticism and study. Bookroom.ir (Persian)
  55. A Study on "Righteousness of the Companions". Gisoom Book Network. (Persian)
  56. The Theory of "Righteousness of the Companions". Ahl al-Bayt World Assembly (Persian)

Vyanzo

  • Amīn, al-Sayyid Muḥsin al-. Aʿyān al-Shīʿa. Edited by Ḥasan Amīn. Beirut: Dār al-Taʿāruf, 1419 AH-1989.
  • Abūriyā, Maḥmūd. Shaykh al-muḍīra Abū Harīra. Egypt: Dār al-Maʿārif, [n.d].
  • Bukhārī, Muḥammad b. Ismāʿīl al-. Ṣaḥīḥ al-Bukhārī. Edited by Dār Ṭawq al-Najāt. [n.p]. 1422 AH.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Iḥsān ʿAbbās. Beirut: Jamʿiyat al-Mustashriqīn al-Ālmāniya, 1400 AH-1979.
  • Dūkhī, Yaḥyā b. ʿAbd al-Ḥusayn. ʿAdālat-i ṣaḥāba bayn al-qadāsat wa al-wāqiʿ. [n.p]. Al-Majmaʿ al-ʿĀlamī li Ahl al-Bayt, 1430 AH.
  • Fakh ʿAlī, Muḥammad Taqī. Majmuʿa guftmānha-yi madhāhib-i Islāmī. Tehran: Mashʿar, [n.d].
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb (al-Tafsīr al-Kabīr). [n.p]. [n.d].
  • Ḥamīdī, Muḥammad b. Futūḥ. Al-Jamʿ bayn al-ṣaḥīḥayn al-Bukhārī wa Muslim. Edited by ʿAlī Ḥusayn al-Bawāb. Beirut: Dār Ibn Ḥazm, 1423 AH-2002.
  • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Muḥammad. Usd al-ghāba fī maʿrifat al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
  • Ibn Abī l-Ḥadīd, ʿAbd al-Ḥamīd b. Hibat Allāh. Sharḥ Nahj al-balagha. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Cairo: 1378-1384 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Jīl, 1412 AH.
  • Ibn Aʿtham al-Kūfī, Aḥmad b. Aʿtham. Kitāb al-Futūḥ. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Aḍwaʾ, 1411AH-1991.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba. Edited by ʿĀdil Aḥmad ʿAbd al-Mawjūd and ʿAlī Muḥammad Muʿawwaḍ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Khaṭīb Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Kifāya fī ʿilm al-riwāya. Edited by Abū ʿAbd Allāh al-Suraqī and Ibrāhīm Ḥamdī al-Madanī. Medina: al-Maktabat al-ʿIlmīyya, [n.d].
  • Suyūṭī, ʿAbd al-Raḥmān b. Abī Bakr al-. Al-Durr al-manthūr fī tafsīr al-maʾthūr. [n.p]. [n.d].
  • Subḥānī, Jaʿfar. Al-Ilāhīyāt ʿalā hudā al-kitāb wa al-sunnat wa al-ʿaql. 3rd ed. Qom: Markaz al-Alāmī li-Dirāsāt al-Islāmiyya, 1412 AH.
  • Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. ʿAlī. Al-Riʿāya fī ʿilm al-dirāya. Edited by ʿAbd al-Ḥusayn Muḥammad ʿAlī Baqqāl. Qom: Maktabat Ayatullāh al-Marʿashī al-Najafī, 1408 AH.
  • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islami affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1417 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Edited by Muḥammad Jawād Balāghī. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusraw, 1372 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Tibyān fī tafsīr al-Qurʾān. Edited by Aḥmad Qaṣīr al-ʿĀmilī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Yaʿqūb, Aḥmad Ḥusayn. Nazariya-yi ʿadālat-i ṣaḥāba. Rājiʿa ʿAlī al-Kurānī al-ʿĀmilī. 1429 AH.