Nenda kwa yaliyomo

Kumtukana Ali (as)

Kutoka wikishia

Kumtukana Ali (Kiarabu: سب علي) ni kumsema kwa ubaya na kumlaani. Kitendo hiki kilianzishwa na Muawiya bin Abi Sufiyan. Watawala na wafuasi wa Bani Umayyah walikuwa wakimtusi na kumlaani waziwazi Imam Ali (a.s) katika mimbari rasmi. Kitendo hiki kilidumu kwa takriban miaka 60 na hatimaye Omar bin Abdul Aziz akaja kukipiga marufuku. Pamoja na hayo, Imam Ali alikuwa akiwazuia wafuasi wake kumsema vibaya na kumtusi Muawiya.

Muawiya, Marwan bin al-Hakam, Mughira bin Shu’ba na Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi ni miongoni mwa watawala wa zama za Bani Umayyah ambao walikuwa wakimlaani Imam Ali katika mimbari. Kadhalika Atiyah bin Saad kutokana na kukataa kwake kumtusi Imam Ali aliadhibiwa kwa amri ya Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi.

Baadhi ya Maulamaa wa Kishia wanalitambua suala la kumtusi na kumlaani Imam Ali (a.s) kuwa ni katika vielelezo vya unasibi (chuki dhidi ya Imam Ali na Ahlul-Bayt).

Utambuzi wa Maana

Kadhalika Angalia: Laana

Sabb/kutusi maana yake ni kutoa maneno machafu na mabaya. [1] Ibn Athir ameliweka katika daraja la matusi suala la kulaaniwa na watu. [2] Baadhi wanasema kuwa, kulaani maana yake ni kutusi na kutoa maneno machafu au kumfukuza na kumtoa mtu ndani. [3] Baadhi pia wamesema kuna tofauti baina ya sabb (kutusi) na kulaani na wamebainisha kwamba, sabb ina maana ya kutoa maneno machafu na kulaani ni kumuweka mbali mtu na rehma za Mwenyezi Mungu. [4]

Imam Muhammad Baqir (a.s) amenukuu kutoka kwa Imam Sajjad (a.s) kwamba, alimuacha na kumpa talaka mmoja wa wake zake kutokana na kumtusi Imam Ali (a.s) [5]. Baadhi wanaitumia riwaya na hadithi hii kama hoja ya kuwa, kutoa maneno machafu dhidi ya Ali bin Abi Talib (a.s) ni katika vielelezo vya wazi vya mtu kuwa nasibi. [6] Sheikh Ja’afar Sobhani anaamini kuwa, aliyeweka jiwe la msingi na mwanzilishi wa kusemwa vibaya na kutusiwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni Muawiyah na huo ndio uliokuwa mwanzo wa kuenea unasibi na chuki dhidi ya Imam Ali (a.s) na Ahlu-Bayt (a.s) baina ya Waislamu. [7]

Msimamo wa mafakihi wa Kishia ni kwamba, mtu anayemtusi na kumlaani Imam Ali (a.s) damu yake ni halali kumwagwa. [8]

Historia Yake

Inaripotiwa kuwa, kutukanwa na kulaaniwa Imam Ali (a.s) na Bani Umayyah kulianza katika kipindi cha uhai wake; kiasi kwamba, moja ya yaliyokuwa masharti ya Imamu Hassan Mujtaba (a.s) katika sulhu na Muawiyah ni kuacha kulaaniwa Imam Ali (a.s) katika mimbari. [9] Agizo kwa umma la marufuku ya kunukuu sifa na fadhila za Imam Ali (a.s), marukufu ya kunukuu hadithi kutoka kwake, kuzuia kutajwa kwa wema Ali na marufuku ya kuitwa watoto kwa jina la Ali ni miongoni mwa hatua nyingine zilizochukuliwa na maadui wa Ali (a.s). [10]

Baada ya kuuawa Othman, wafuasi wake walikataa kumpa baia na kiapo cha utii Imam Ali na walikuwa wakimuonyeshea kidole cha lawama kwamba, yeye ndiye aliyesababisha kuuawa Othman. Muawiya naye akiwa na lengo la kubakisha makabiliano haya alitoa amri ya kutukanwa na kulaaniwa Ali. [11] Marwan alimhutubu Imam Sajjad kwa kumwambia: Wakati Othman alipozingirwa, hakuna mtu aliyemtetea kama Ali. Imam akasema, basi kwa nini mnamtukana namna hii katika mimbari? Marwan akajibu kwa kusema, misingi ya utawala wetu isingesimama isipokuwa kwa matusi na maneno haya machafu. [12] Zamakhshari anasema, katika zama za Bani Umayyah Imam Ali alikuwa akilaaniwa katika mimbari 70,000 kwa ajili ya kuafuata sunna iliyokuwa imeanzishwa na Muawiyah. [13]

Mwenendo wa kutukanwa Imam Ali ulidumu kwa takribani miaka 60 mpaka katika zama za ukhalifa wa Omar bin Abdul Aziz (99-101 Hijria) ambapo alipoingia madarakani aliwapa amri magavana na wafanyakazi wake kuacha kitendo hicho. Ibn Khaldun, mwanahistoria wa karne ya 8 Hijria amenukuu: Bani Umayyah walikuwa wakimlaani mtawalia Imam Ali (a.s), mpaka alipoingia madarakani Omar bin Abdul-Aziz ambapo alituma barua katika maeneo yote ya Kiislamu na kutoa amri ya kukomeshwa kitendo hicho. [14]

Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Umm Salama, Mtume (s.a.w.w) amenukuliwa akisema, kumtusi na kumsema kwa manaeno mabaya Imam Ali ni kama kumtusi yeye (Mtume) na katika nakala nyingine imeelezwa kuwa ni mithili ya kumtusi Mwenyezi Mungu. [15] Allama Majlisi mbali na kunukuu hadithi hiyo inayonasibishwa na Umm Salama amenukuu katika kitabu chake cha Bihar al-Anwar hadithi zingine katika mlango huu. [16]

Muawiya

Kumenukuliwa matukio ya Muawiya kumtukana na kumlaani Imam Ali (a.s); miongoni mwayo ni tukio lililonukuliwa na Tabari, mwanahistoria wa karne ya 4 Hijiria ambapo anasema, wakati Muawiyah alipomteua Mughira bin Shu’ba kuwa kiongoizi wa Kufa alimpa amri ya kumtukana na kumsema vibaya Ali bin Abi Talib na kutilia mkatazo suala la kumtukuza Othman. [17] Kadhalika alimtaka Mughira kuwapeleka uhamishoni wafuasi wa Imam Ali (a.s). [18]

Vilevile baada ya sulhu na Imam Hassan (a.s), Muawiya alichukua baia kwa watu huko Nukhailah na katika hotuba yake, alimsema vibaya Imam Ali (a.s) na Imamu Hassan Mujtaba (a.s) na kutoa maneno machafu dhidi ya [19]

Marwan bin al-Hakam

Kwa mujibu wa kile ambacho Dhahabi, mwanahistoria wa Kisunni, amekitaja katika kitabu chake cha historia, Marwan bin al-Hakam alikuwa mtawala wa Madina mwaka wa 41 Hijiria, na katika kipindi cha miaka sita ya utawala wake, alikuwa akimtusi na kumsema kwa ubaya Ali (a.s) kila Ijumaa kwenye mimbari yake. Baada yake, Saeed bin Aas akawa gavana kwa muda wa miaka miwili na hakuwa akimtukana Ali bin Abi Talib (as). Baada ya Saeed bin Aas, Marwan akawa mtawala tena na akaanza tena kumtukana Ali. [20]

Mughira bin Shu’ba

Al-Baladhuri, mwanahistoria wa karne ya tatu Hijiria anasema kuwa, tatizo la Mughira ambaye alikuwa gavana wa Kufa kwa miaka tisa katika zama za utawala wa Muawiya ni kwamba, daima na kwa sura mtawalia alikuwa akimtusi na kumsema vibaya Ali bin Abi Talib. [21]

Hajjaj bin Yusuf

Kwa mujibu wa kile kilichoandikwa na Ibn Abil-Hadid katika sherh na ufafanuzi wa Nahaj al-Balagha ni kwamba, Hajjaj bin Yusuf mbali na kumlaani Imam Ali (a.s) alikuwa akiwaamrisha watu wengine wafanye hivyo pia na alikuwa akifurahia hilo; [22] kiasi kwamba, bwana mmoja alimwambia, familia yangu imenidhulumu kwa kunipa jina la Ali, basi nibadilishe jina langu na unipe cha kuishi, kwa sababu mimi ni masikini. Hajjaj akambadilisha jina na akampatia kazi." [23]

Katika riwaya nyingine, Hajjaj bin Yusuf alilichukulia suala la kumtukana Ali kuwa ni fadhila na jambo la kusifiwa [24] na katika kubainishwa wasifu wa Atiya bin Saad bin Junada Kufi, imeelezwa kwamba, Hajjaj alimtaka amlaani Ali bin Abi Talib, vinginevyo angechapwa viboko 400, lakini Atiya alikataa na alichapwa mijeledi 400 na nywele na ndevu zake pia zilinyolewa.[25]

Kukataza Imam Ali Kutukunwa Muawiya

Katika hali ambayo Muawiya alikuwa ametoa amri ya kutukanwa Imam Ali (a.s) katika mimbari, lakini kabla ya hapo na katika vita vya Siffin Ali alikuwa amepinga na kukataza kutukanwa na kusemwa vibaya Muawiya. [26] Wakati Hujr bin Adi na Amr bin Hamiq al-Khuzai waliokuwa katika jeshi la Ali (a.s) walipomlaani Muawiya na watu wa Sham, Imam Ali aliwakataza kufanya hivyo na katika kujibu swali kwamba, kwani sisi hatupo katika haki? Alisema, sisi tupo katika haki, lakini nachukia muwe ni katika wanaolaani na wanaotoa maneno machafu. Kadhalika katika muendelezo wa maneno yake Imam Ali (a.s) aliwaambia wamuombe Mwenyezi Mungu ahifadhi damu zetu na damu zao, alete sulhu baina yetu na baina yao, na awaokoe kunako upotevu ili kila mtu ambaye hajaitambua haki aitambue na kila ambaye anang’ang’ania batili aache kufanya hivyo. [27]

Rejea

Vyanzo

  • Abu al-Faraj Isfahani, Ali bin Hassan, Maqatil al-Thalibin, Beirut, Yayasan al-A’lami li al-Mathbu’at. 1998/1419 H.
  • Al-Husseini al-Musawi al-ahairi al-Karaki, Muhammad bin Abi Thalib, Tasliyah al-Majalis wa Zinah al-Majalis. Al-Mausum bi Maqtal al-Hussein alaihi salam, Riset: Faris Hasun Karim, Qom, Pasdare Islam, 1418 H.
  • Allamah Majlisi, Muhammad Baqir, Bihar al-Anwar, Beirut, Yayasan al-Wafa’, 1983/1430 H.
  • Askari, Murtadha, Tarjumeh Ma'alim al-Madrasatain, Penerjemah: Muhammad Jawad Karami, Qom, Danishkadeh Ushuluddin. 1386 HS.
  • Baladzuri, Ahmad bin Yahya, Ansab al-Ashraf, Riset: Ihsan Abbas, Beirut, Jam’iyah al-Mustasyriqin al-Almaniyah, 1979/1400 H.
  • Balkhi, Muqatil bin Sulaiman. Tafsir Muqatil bin Sulaiman. Riset: Syahatih, Abdullah Mahmud. Beirut, Dar Ihya al-Turath, Cet. Pertama. 1423 H.
  • Balqanabadi, Hassan, Shawahid Nashb dar Athare Bukhari, Muqaddimah: Najmuddin Thabasi, Tanpa tahun, Tanpa tempat.
  • Dinawari, Abu Hanifah Ahmad bin Daud, Al-Akhbar al-Thiwal, Qom, Mansyurat al-Radhi, 1368 HS.
  • Dzahabi, Muhammd bin Ahmad, Tarikh al-Islam, Riset: Tadmiri, Umar Abdul Salam, Beirut, Dar al-Kitab al-Arabi, Cet: Kedua. 1409 H.
  • Ibnu Asakir, Ali bin Hassan, Tarikh Madinah Dimashq, Riset: Ali Shiri. Beirut, Dar al-Fikr, 1996/1417 H.
  • Ibnu Atsir Jazri, Mubarak bin Muhammad, Al-Nihayah fi Gharib al-Hadits wa al-Atsar, Riset, Editor: Thanahi, Mahmud Muhammad. Qom, Yayasan percetakan Ismailiyan. 1367 HS.
  • Ibnu Khaldun, Abdurrahman bin Muhammad, Diwan al-Mubtada’ wa al-Khabar fi Tarikh al-Arab wa al-Barbar wa Man ‘Asharahum min Dzawi al-Sya’n al-Akbar (Tarikh Ibnu Khaldun). Riset: Khalil Syahadah. Beirut, Dar al-Fikr. Cet. Kedua. 1408 H.
  • Jamshidiha Ghulamreza, Ruhani Muhammad Reza, Alamul Huda, Sayyied Abdul Rasul, Propagandae Bani Umayyeh alaihi Khandane Payombar saw. Majalah Shiah Shenasi, Tahun ketujuh, no. 35, Musim gugur, 1390 HS.
  • Kausari, Ahmad. Barresi Risyehaye Tarikhi Nashibigari. Pajoheshname Naqde Wahabiyat. Siraj Munir. Tahun keempat. No. 16. Musim dingin. 1393 HS.
  • Mughniyah, Muhammad Jawad, Fiqh al-Imam al-Shadiq as, Qom, Yayasan Ansariyan, 1421 H.
  • Sayyied Ibnu Thawus, Ahmad bin Mussa, Bana' al-Maqalah al-Fathimiyah fi Naqdhi al-Risalah al-Usmaniyah, Riset: Sayyid Ali al-Adnani al-Gharifi. Qom, Yayasan Alu al-Bait li Ihya al-Turats. 1411 H.
  • Subhani, Ja’far. Darsname Guzideh Simaye Aqaid Shieh, Penerjemah: Jawad Muhadditsi, Teheran, Mash’ar, 1389 HS.
  • Sheikh Thusi, Tahdzib al-Ahkam, Riset: Musawi Khurasan, Hassan, Dar al-kutub al-Islamiyah, Cet: Keempat, 1407 H.
  • Tabari, Abu Ja’far Muhammad bin Jarir, Tarikh al-Umam wa al-Muluk (Tarikh Tabari), Riset: Ibrahim, Muhammad Abulfadhl, Beirut, Dar al-Turats. Cet. Kedua. 1387 H.
  • Tabrasi, Fadhl bin Hassan, I'lam' al-Wara bi A’lami al-Huda, Dar al-Kutub al-Islamiyah, Cetekan ketiga. 1390 H.
  • Thuraihi, Fakhruddin, Majma' al-Bahrain, Riset: Husaini, Sayyied Ahmad, Teheran, Kitab Furushi Murtadhavi, Cet. Ketiga. 1375 HS.
  • Zamakhshari, Mahmud bin Amr, Rabi al-Abrar wa Nushush al-Akhbar, Beirut, Yayasan A’lami, 1412 H.