Ruh al-Qudus

Kutoka wikishia

Ruh al-Qudus (Kiarabu: رُوح‌ُ القُدُس)ina maana ya Roho Mtakatifu na ni kiumbe aliyeepushwa na nakisi na mapungufu. Viumbe kama Malaika Jibril ni kiumbe wa Alam al-Amr (ulimwengu ambao vitu haviwezi kudirikiwa kwa kutumia hisi tano), nguvu ya ghaibu, akili amilifu, roho katika roho na mkubwa wa malaika ni mifano na vielelezo vya wazi vilivyotambulishwa kuwa ni Ruh al-Qudus (roho mtakatifu). Katika vyanzo vya Kiislamu, majukumu kama kufikisha Wahyi kwa Mitume, kuwasaidia waumini, mwanzo wa elimu ya Mitume, kuwasilisha hukumu ya Mwenyezi kwa Ahlul-Bayt (a.s) na shufaa Siku ya Kiyama yamenasibishwa na Ruh al-Qudus.

Ruh al-Qudus katika fasihi ya Kikristo ni roho ya tatu katika roho tatu (baba, mwana na roho mtakatifu); hata hivyo baadhi ya wanateolojia ya Kikristo hawajakubaliana na uungu wake. Neno Ruh al-Qudus limetumika katika Qur’ani, vitabu vingine na katika fasihi za Kifarsi na Kiarabu. Kitabu cha “ Tahlil Falsafi va erfan Ruh al-Qudus dar mutun dini (Uchambuzi wa Kifalsafa na Kiirifani Kuhusu Ruh al-Qudus katika Maandiko ya Kidini”. Kilichoandikwa na Fateme Alipoor kinajihusisha kubainisha nafasi na daraja ya Ruh al-Qudus katika imani na mafundushio ya Uzartoshti, Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Utambuzi wa maana na nafasi yake

Ruh al-Qudus ina maana ya Roho mtakatifu na ni kiumbe aliyeepushwa na nakisi na mapungufu. [1] Imekuja katika kamusi ya biblia kwamba, Ruh al-Qudus anaitwa kuwa ni mtakatifu kwa sababu moja ya kazi zake ni kutakasa mioyo ya waumini, na kwa kupitia huba yake kwa Mwenyezi Mungu na Kristo, anaitwa pia Roho wa Mwenyezi Mungu na Roho wa Kristo.[2]

Neno hili limetumika katika Quran na Biblia; Qur’ani imezungumzia kuhusu kuteremshwa kwa Qur’ani na Roho Mtakatifu [3] na kuthibitishwa kwa Yesu naye [4].

Roho mtakatifu ni nani

Kuhusiana na uhakika wa roho mtakatifu kuna mitazamo kadhaa imetajwa:

 • Jibril: Idadi kadhaa ya wafasiri wamemtambua Roho Mtakatifu kuwa ni Jibril. [6]. Kumuita Jibril kwa jina la Ruh al-Qudus kunaashiria utakasifu wake na nafasi na mchango wake katika kuifanya dini kubakia kuwa hai. [7]
 • Kiumbe kutoka Alam al-Amr (ulimwengu ambao vitu haviwezi kudirikiwa kwa kutumia hisi tano): Allama Tabatabai anasema kuwa, Ruh al-Qudus ni kiumbe kutoka katika ulimwengu ambao vitu haviwezi kudirikiwa kwa kutumia hisi tano na sio Malaika ambao kimsingi wao walikuwa na jukumu la kufikisha Wahyi kwa Manabii. [8]
 • Mkubwa wa Malaika: Katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s), Ruh al-Qudus anayelezwa kuwa ni Malaika ambaye ni mkubwa kuliko Jibril na Mikail ambaye alikuwa pamoja na Mtume wa uislamu na baada ya Mtume yupo pamoja na Maimamu wa Kishia. [9] Katika baaddhi ya hadithi, Ruh al-Qudus anaelezwa kuwa ni yule yule malaika ambaye kushuka kwa kumetajwa katika Qur’ani [10] kwamba, yuko pamoja na Malaika katika Laylat al-Qadr. [11]
 • Nguvu ya ghaibu: Ruh al-Quds ni jina tukufu zaidi (A’dham) [12] au nguvu ya ghaibu [13] ambayo kupitia kwayo Issa Masih alikuwa akihuisha wafu. Nguvu hii ipo kwa waumini wote lakini kwa sura dhaifu zaidi na inawasaidia waumini na kuwazuia kufanya madhambi. [14]
 • Kitu cha kwanza kuwepo: Sayyid Haidar Amoli anasema, wanafalsafa wameafikiana kwamba, kitu cha kwanza kuumbwa na kuwepo ni akili; ingawa inatajwa kwa majina tofauti tofauti kama Ruh al-Qudus na akili amilifu. [15]

Majukumu

Katika Qur’ani na hadithi kuna mambo na majukumu yamenasibishwa na Ruh al-Qudus:

 • Kufikisha Wahyi kwa Mitume: Hii kwamba, Roho mtakatifu ni Malika Jibril, basi jukumu lake ni kufikisha ujumbe na Wahyi wa Mwenyezi Mungu kwa Mitume.
 • Mthibitishaji na msaidiaji Mitume na Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Katika Aya za Qur’ani kumezungumziwa kuthibitishwa Issa Masihi na Ruh al-Qudus. Kwa mujibu wa raia ya wafasiri kuthibitisha ni kwa maana ya kuimarisha na kusaidia. [17] Baadhi ya wengine pia wameitambua Injili kuwa misdaq na kielelewzo cha Ruh al-Qudus. [18]
 • Mwanzo wa elimu ya Manabii: Katika baadhi ya hadithi kumetajwa uwepo wa roho tano katika uwepo wa Manabii na Mawasii ambapo Roho Mtakatifu ni miongoni mwao na kupitia kwayo Mitume wanajua vitu. [19]
 • Kuwasilisha hukumu ya Mwenyezi kwa Ahlul-Bayt (a.s): Kwa mujibu wa hadithi, Ahlul-Bayt wanatoa hukumu na maamuzi kwa mujibu wa hukumu ya Mwenyezi Mungu, Nabii Daud na kitu ambacho Ruh al-Qudus anakiweka katika nyoyo zao.
 • Shufaa siku ya Kiyama: Kwa mujibu wa hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), mtu wa kwanza atayetoa shufaa siku ya Kiyama ni Roho mtakatifu. [21]
 • Kuwasaidia waumini: Kwa mujibu wa hadithi mbali mbali madhali waumini wangali wanamuunga mkono Mtume na Ahlul-Bayt, basi Roho mtakatifu atawasaidia. [22]

Uungu

Katika fasihi ya Kikristo ni roho ya tatu katika roho tatu (baba, mwana na roho mtakatifu). [24] Katika biblia uhai umenasibishwa kwake. [25] Kwa mujibu kitabu hiki, wakati waumini wanapotubu humpata roho mtakatifu na yeye huwasafisha kutokana machafu ya dhambi; [26] hata hivyo baadhi ya wanateolojia ya Kikristo hawajakubaliana na uungu wake. Baadhi wamekana shakhsia ya uungu na roho mtakatifu na wanamtambua kuwa ni malaika. [27] Baadhi ya wengine wanaamini kwamba, roho mtakatifu sio kiumbe mwenye kujitegemea; bali ni dhihirisho la Mwenyezi Mungu na wanaamini uungu wake. [28]

Monografia

Kitabu cha “Tahlil Falsafi va erfan Ruh al-Qudus dar mutun dini (Uchambuzi wa Kifalsafa na Kiirifani Kuhusu Ruh al-Qudus katika Maandiko ya Kidini”. Kilichoandikwa na Fateme Alipoor kinajihusisha kubainisha nafasi na daraja ya Ruh al-Qudus katika imani na mafundushio ya Uzartoshti, Uyahudi, Ukristo na Uislamu. Kadhalika katika kitabu hiki nadharia za kifalsafa na kiirifani za wanafikra wa Kiislamu zimetathminiwa. [29]

Masuala yanayofungamana

Vyanzo

 • Āmulī, Sayyid Ḥaydar. Jāmiʿ al-asrar wa manbaʿ al-nūr. Edited by Henry Corbin and ʿUthmān Ismāʿīl Yaḥyā. Tehran: 1347 Sh.
 • Abū Ḥayyān Andulusī, Muḥammad b. Yusuf. Al-Baḥr al-muḥīṭ fī al-tafsīr. Edited by Ṣidqī Muḥammad Jamīl. Beirut: Dār al-Fikr, 1420 AH.
 • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
 • Ḥākim al-Nayshābūrī. Muḥammad b. ʿAbd Allāh al-. Al-Mustadrak ʿala l-ṣaḥīḥayn. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
 • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Muḥammad. Usd al-ghāba fī maʿrifat al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
 • Jīlī, ʿAbd al-Karīm b. Ibrāhīm. Al-Insān al-kāmil fī maʿrifat al-awākhir wa l-awāʾil. Edited by Ṣalāḥ Muḥammad ʿUwayḍa. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya; Manshūrāt-i Muḥammad ʿAlī Bayḍūn, 1418 AH.
 • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
 • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
 • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
 • Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Edited by Ṭayyib Mūsawī Jazāʾrī. Qom: Dār al-Kitāb, 1404 AH.
 • Sulaymānī Ardistānī, ʿAbd al-Raḥīm. Darāmadī bar ilāhiyyāt-i ṭaṭbīqī-yi Islam wa masiḥiyyat. Qom: Kitāb-i Ṭāhā, 1382 Sh.
 • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Tibyān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
 • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusraw, 1372 Sh.
 • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1390 AH.
 • Zamakhsharī, Maḥmūd b. ʿUmar al-. Al-Kashshāf ʿan ḥaqāʾiq ghawāmiḍ al-tanzīl. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1407 AH.
 • Alister McGrath. Darāmadī bar ilāhīyyāt-i masīḥī. Translated to Farsi by Īsā Dibāj. Tehran: Kitāb Rawshan, 1385 Sh.
 • James Hawkes. Qāmūs-i kitāb-i muqaddas. Tehran: Intishārāt-i Asāṭīr, 1394 Sh.