Nenda kwa yaliyomo

Alam al-Amr

Kutoka wikishia

Alam al-Amr / Alam al-Mujarradat (Kiarabu: عالم الأمر) (Ulimwengu wa Amri) ni ulimwengu ambao hauwezi kudirikiwa kwa kutumia hisi tano na mkabala wake ni Alam Khalq ambao yawezekana kuudiriki kwa hisi tano. Chimbuko la itikadi juu ya Alam al-Amr limetambuliwa kuwa ni sehemu ya Aya ya 54 ya Surat al-A’raf:((أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ; Fahamuni! Kuumba na amri ni zake))

Kupatikana viumbe katika ulimwengu wa amri ni jambo la papo kwa hapo na bila ya kuhitajia kupatikana mazingira ya wakati na sehemu; kinyume na ulimwengu wa kuumba (Alam al-Khalq) ambapo upatikanaji wa viumbe ni kwa sura ya hatua kwa hatua na hilo linategemea mazingira maalumu ya kimaada.

Licha ya kuweko kwa itikadi ya baadhi ya wanafalsafa juu ya kuweko kwa Alam al-Amr, baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba, katika Aya miongoni mwa Aya za Qur’ani neno “amr” limetumika kwa ajili ya kuashiria ulimwengu wa kimaada; kama ambavyo Allama Tabatabai amelitambua hilo chini ya Aya ya 54 ya Surat al-A’raf ya kwamba, Khalq na Amr katika Aya hiyo haina maana ya ulimwengu mbili tofauti na zenye kujitegemea, bali maana yake ni nguvu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu na amri yake.

Utambuzi wa maana

Alam al-Amr ni ulimwengu ambao kinyume na Alam al-Khalq, hauna vitu vya kuhisika na haiwezekani kuudiriki kupitia hisi tano. [1] Kwa mujibu wa nadharia ya Mulla Sadra mwanafalsafa wa Kishia wa karne ya 11 Hijiria ni kwamba; Mwenyezi Mungu ameumba ulimwengu tofauti tofauti ambapo ulimwengu zote hizo zipo katika ulimwengu mbili: Alam al-Khalq na Alam al-Amr. Anasema, Alam Khalq ndio dunia na Alam Amr ni ulimwengu wa mujarradat na kueleza kwamba, ulimwengu huu unaweza kudirikiwa tu kwa hisi za batini. [2]

Mulla Hadi Sabzawari anaamini kuwa, wataalamu wa elimu ya irfan, wamechukua istilahi ya Alam Amr kutoka katika Aya ya 54 ya Surat al-A’raf [3] [4]. Katika kitabu cha Hujjat al-Rafasir, chini ya Aya ya 85 ya Surat al-Israa kumezungumziwa ulimwengu mbili za Khalq na Amr ambapo kwa mujibu wake, mwili wa mwanadamu ni mfano wa Alam Khalq na roho ni mfano wa Alam Amr. [5]

Sifa maalumu

Kwa mujibu wa Nassir Makarim Shirazi tofauti na Alam Khalq ni kuwa, kupatikana viumbe katika ulimwengu wa amri ni jambo la papo kwa hapo. [6] Nadharia na mtazamo wa Makarim Shirazi umetegemea Aya ya 82 ya Surat Yasin ambayo kwa mujibu wake, kila Mwenyezi Mungu atakapo kitu basi hukiamrisha kiwe na kitu hicho huwa. [7] Aya hiyo inasema: Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa

Katika ulimwengu wa amr, viumbe hujitokeza pasina ya irada na amri ya Mwenyezi Mungu na bila ya kuandaliwa mazingira ya kimaada kama wakati na mahali; kinyume na ulimwengu wa Khalq ambapo ili kupatikana hilo, kuna haja ya kuandaliwa mazingira maalumu ya kimaada. [8]

Mitazamo

Baadhi ya wanafalsafa wa Kiislamu wamezungumzia suala la kuweko Alam Amr mkabala wa alam Khalq. [9] Feidh Kashani amebainisha tofauti baina ya Alam Khalq na Alam amr katika kitabu chake cha al-Safi katika tafsiri ya ibara ya: ((لَهُ الْخَلْقُ وَ الْأَمْرُ ; Fahamuni! Kuumba na amri ni zake)). [10] [11]Katika kufasiri Surat al-Falaq, Feidh Kashani ametumia Aya iliyoko katika sura hiyo inayosema: Na shari ya alivyo viumba na kusema kuwa, shari zipo katika ulimwengu wa khalq na katika ulimwengu wa Amr kuna kheri tupu tu. [12]

Pamoja na haya, imekuja katika tafsir Nemooneh kwamba: Qur’ani tukufu imetumia neno amr kwa ajili ya ulimwengu wa kimaada pia; kwa mfano katika Aya ya 54 ya Surat al’A’raf ambayo ni hoja kuu ya ulimwenghu wa Khalq, jua, mwezi na nyota vimetambuliwa kuwa viko chini ya amri ya Mwenyezi Mungu. [13] Allama Tabatabai pia katika kitabu chake cha Tafsir al-Mizan katika kufasiri Aya hiyo, hajazungumzia kuhusiana na kuweko ulimwengu kama huu bali amebainisha tu tofauti zilizopo baina ya ulimwenghu wa Khalq yaani wa Mwenyezi Mungu kuumba na ulimwengu wa amr yaani wa Allah kutoa amri. [14]

Masuala yanayofungamana


Rejea

Vyanzo