Nenda kwa yaliyomo

Nadharia ya mwanadamu wa miaka 250

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na nadharia ya mwanadamu wa miaka 250. Ili kufahamu kuhusaiana na kitabu chenye maudhui hii, angalia makala ya Mwanadamu wa miaka 250 (kitabu).

Nadharia ya mwanadamu wa miaka 250 ni nadharia ambayo ikitegemea umoja wa mbinu na sira ya kisiasa na mapambano ya Maimamu wa Waislamu wa madhehebu ya Kishia katika zama za utawala wa Bani Umayya na Bani Abbas inawataja Maimamu hao kuwa ni mwanadamu mmoja mwenye umri wa miaka 250. Nadharia hii ilitolewa na kuzungumziwa na Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kabla ya Mpainduzi ya Kiislamu. Ayatullah Khamenei anaamini kwamba, maisha ya kisiasa ya Maimamu wa Waislamu wa Kishia licha ya kuweko tofauti za kidhahiri, lakini kiujumla ni harakati moja endelevu na ya muda mrefu ambayo ilidumu kwa muda wa miaka 250 na Maimamu wote hao walikuwa katika njia ya kufuatilia na kufanikisha lengo moja, nalo ni kuufanya ubinadamu ustawi na kukwea kidaraja na wakati huo huo kuanzisha jamii ya Kiislamu. Hata hivyo Maimamu hao walitumia mbinu mbali mbali katika kupambana na maadui zao, kila mmoja kulingana na mazingira ya zama zake alizoishi.

Kwa mujibu wa nadharia hii, kipindi cha miaka 250 cha maisha ya Maasumina kinagawanywa katika vipindi vinne:

  1. Kipindi cha subira na kunyamaza kimya.
  2. Kipindi kifupi cha utawala wa Maimamu.
  3. Kipindi cha miaka 20 cha harakati za siri na za kivikundi.
  4. Kipindi cha kuhuisha misingi ya kifikra ya Uislamu kuanzia Uimamu wa Imamu Sajjad (a.s).

Kubainisha nadharia

Kwa mujibu wa nadharia ya mwanadamu mwenye umri wa miaka 250, baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad (s.a.w.w), Maimamu Maasumina (a.s) wanahesabiwa kuwa ni mwanadamu mmoja ambaye, kuanzia mwaka 11 hadi 260 Hijiria daima alikuwa katika hali ya jihadi na mapambano ya kisiasa dhidi ya dhulma na upotofu wa madhalimu na mataghuti wa wakati huo. [1] Kwa mujibu wa nadharia hii, Ahlul-Bayt (a.s) wote walikuwa kama mwanadamu mmoja, ambaye amekuwa akijishughulisha na kupigania kutimia kwa lengo hilo kwa muda wa miaka 250 kimawazo, fikra na lengo maalumu na linaloeleweka. Mwanadamu huyu ametumia viini mbalimbali kwa ajili ya kuwaleta watu wote wa jamii kwenye shule ya kweli ya Uislamu; sifa na viini kama vile Umaasumu (kutotenda dhambi), msukumo (ilhamu) kutoka kwa Qur'an Tukufu na maneno ya Mtume (saww) na ujuzi wa kina wa hali ya kijamii na shule ya Uislamu. Kwa msingi huo, hawajakengeuka kutoka kwa lengo hilo; kimsingi, haiwezekani wao kukengeuka katika mwelekeo wa kuifikisha jamii kwenye Uislamu wa kweli. [2]

Mapambano makali na shadidi ya kisiasa ikiwa kama anuani muhimu zaidi ya maisha ya Maimamu wa Kishia katika miaka hii 250 [3] inaelezea na kubainisha umoja wa shakhsia na haiba ya Maasumina (as) katika suala la jihadi. [4] Kwa mujibu wa nadharia hii, Maimamu wote baada ya Imam Hussein (a.s), kwa hakika walikuwa pamoja naye katika mapambano kwa maana kwamba, walikuwa pamoja katika medani ya Hussein na kupigana bega kwa bega pamoja naye na walipigana dhidi ya adui yule yule ambaye Imam Hussein (a.s) alipigana naye na akauawa kishahidi, lakini sura ya jihadi yao ilibadilika kulingana na mazingira. [5]

Hoja

Kwa mujibu wa Alireza A’rafi ni kwamba, msingi wa nadharia hii unaweza kuonekana katika nukta hii kwamba kwa mtazamo wa Shia, Maimamu wote wa Shia ni nuru moja na hivyo wao ni wamoja katika suala muhimu la jihadi na mapambano dhidi ya adui. Kwa maana kwamba, mtazamo wao katika hilo ni mmoja. Hivyo basi, kila mlengwa anapata maana ya jihadi ya kweli kutoka kwa kila Imamu miongoni mwa Maimamu waongofu. Nukta hii imebainishwa wazi katika al-Ziyart al-Jami’a al-Kabira kwamba asili yao ni moja. Aidha ananukuu hadithi kwa Imamu Ja’afar Sadiq (a.s) ambayo inaeleza kuwa, elimu na fadhila za Maimamu kitu kimoja na anawatambulisha wote kwamba, ni ukweli na uhakika mmoja. [6]

Mwanzilishi na historia

Nadharia ya “mwanadamu wa miaka 250” ilizungumziwa na Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu. Alizungumzia nadharia hii mwaka 1971. [7] Kulingana naye, kuna mstari wa kisiasa unaoendelea, wenye mbinu mbalimbali, katika fikra na matendo ya Ahlul-Bayt (as) ambao unaonekana katika kipindi hiki chote cha miaka 250, [8] na mwendo wake na maisha yake yamekuwa na mwelekeo mmoja katika kipindi chote hiki na amepewa wahyi na ilhamu (muongozo) kutoka sehemu moja – Qur’an na Sunna - [9]. Pamoja na hayo baadhi wanaamini kwamba kabla yake (kabla ya Ayatullah Khamenei), Sayyid Muhammad Baqir Sadr, mwanafikra wa Kishia kutoka Iraq (1935-1980), naye alikuwa na mtazamo huo huo kuhusu maisha ya Maimamu wa Shia (as). Lakini kwa mujibu wa mtazamo huu, nadharia iliyotolewa na Seyyid Ali Khamenei ni ya "kisiasa zaidi" na yenye "ubunifu" kwa upande wa kimuhtawa. [10]

Alireza A’rafi pia amezungumzia nadharia hii hii kwa anuani ya na umoja wa shakhsia ya Maimamu na anaamini kwamba, imani hii ni mojawapo ya mambo ya wajibu ya ijtihadi ya Kishia na ni moja ya misingi ya fiqhi ya Shia. [11]

Sifa maalumu za duru ya miaka 250

Mchoro jumla wa harakati ya Maimamu wa Kishia

Kwa mujibu wa nadharia ya umoja wa shakhsia ya Maimamu na kwa mujibu wa Shekhe Ali Reza A’rafi mistari na medani mbalimbali za uwepo wa Maimamu inawezekana kuchora taswira ya pande na mielekeo minne:

  • Makabiliano ya kifikra, kielimu na kiutamaduni dhidi ya ulahidi (kumkana Mungu). [12]
  • Kupambana na fikra za kiteolojia na kifikra za madhehebu mengine ya Kiislamu [13] kwa kuzingatia nukta mmbili za kulinda umoja wa Kiislamu mkabala wa maajinabi na kuiwekea kinga miaka ya kiitikadi ya Kishia kwa anuani ya Uislamu asili. [14]
  • Kupambana na ukengeukaji na upotokaji ndani ya Uishia. [15]
  • Mapambano ya kisiasa na kijamii na makhalifa wa Bani Umayya na Bani Abbas. [16]

Mgawanyo wa hatua nne

Nadharia ya mwanadamu wa miaka 250 ni kipindi cha maisha ya kisiasa ya Maimamu (as) ambapo kutokana na tofauti za kidhahiri za vipindi hivi, zimegawanywa katika sehemu au duru nne. [17]

  1. Duru ya Kwanza: Kipindi cha miaka 25 cha kuanza zama za Ukhalifa (kipindi cha Imamu Ali a.s katika zama za makhalifa wa kwanza) ambapo kipindi hiki kinatajwa kama duru ya subra na kunyamaza kimya. [18]
  2. Duru ya Pili: Kipindi cha kuanza utawala wa Maimamu (a.s) ambacho ni kipindi cha Ukhalifa wa Ali (a.s) (35-40 Hijiria) na kipindi kifupi cha Ukhalifa wa Imamu Hassan (a.s). Sifa muhimu kabisa ya kipindi na duru hii ni kupata haki mwenye haki na ustahiki na kuanzisha utawala wa Kimapinduzi kama utawala wa Mtume (s.a.w.w). [19]
  3. Duru ya Tatu: Kipindi cha harakati za siri na kivikundi za Maimamu (as) kuanzia mwaka 41 Hijiria hadi 61 Hijiria. Sifa muhimu kabisa ya kipindi hiki ni kuandaa uwanja na mazingira ya kifikra baina ya wana jamii lililofanywa na askari mujahidina na kuandaa watu ambao wataweza kumsaidia Imamu Hussein (a.s) na kusaidia harakati yake kwa ajili ya kufikia lengo. [20]
  4. Duru ya Nne: Kipindi hiki kilianza sambamba na kuanza zama za Uimamu wa Imamu Sajjad (a.s) na kuendelea hadi mwaka 250 Hijiria. Katika kipindi hiki kulifanyika mambo mawili muhimu: [21]
  • Kuhuisha Uislamu: Jamii ya Kiislamu katika kipindi cha muda mrefu wa utawala wa Bani Umayya na kabla ya hapo, ilikuwa imebadika muundo na misingi ya Uislamu asili ulioletwa na Mtume (saww) ilikuwa imesahaulika. Ni kutokana na sababu hii ndio maana Maimamu walijihusisha na kuhuisha misingi ya kifikra ya Uislamu na walikuwa wakifanya hima na idili ili kusambaratisha fikra zisizo za Kiislamu ambazo zilikuwa zimetiwa katika jamii katika miaka yote hii. [22]
  • Kuundwa chama cha kisiasa cha kimadhehebu na cha siri lengo likiwa ni “kuhifadhi harakati ya fikra asilia ya Uislamu halisi”, “kuanzisha harakati za kisiasa zenye uratibu” na “kuleta mawasiliano baina ya wategemezi wa fikra ya Kiislamu na harakati ile yenye uratibu na mpangilio” ni miongoni mwa kazi na mambo muhimu yanayotajwa kuwa yalifanyika katika kipindi hiki; kwani ikilazimu na katika wakati ambao Imamu ilikuwa afanye harakati ya kupambana na vyombo vya utawala alikuwa akihitajia watu ambao ni askari ambao walikuwa wameandaliwa kwa ajili ya kusudio hili. [23]

Mgawanyo wa hatua nane

  1. Zama za Imamu Ali bin Abi Talib (a.s). [24]
  2. Zama za Uimamu wa Imam Hassan (a.s). [25]
  3. Kipindi cha harakati ya Ashura. [26]
  4. Kipindi cha Uimamu wa Imamu Ali bin Hussein Sajjad (a.s). [27]
  5. Zama za Uimamu wa Maimamu Muhammad Baqir na Ja’afar Swadiq (a.s). [28]
  6. Zama za Imamu Mussa bin Ja’afar (a.s). [29]
  7. Kipindi cha Imamu Ali bin Mussa al-Ridha (a.s). [30]
  8. Zama za ukandamizaji na kukata tamaa ya kupata ushindi kambi ya haki, kipindi ambacho kinaanzia katika zama za Uimamu wa Imamu wa tisa Imamu Jawad (a.s) na kuishia katika zama za ghaiba. [31]

Kitabu cha “Mwanadamu wa miaka 250

Makala asili: Mwanadamu wa miaka 250 (kitabu)'

Kitabu cha “Mwanadamu wa miaka 250” ni mkusanyiko wa hotuba za Ayatullah Ali Khamenei kuhusiana na nadharia ya “Mwanadamu wa miaka 250”. Kitabu hiki kilichapishwa mwaka 2011 na taasisi ya uchapishaji ya Sahba kikiwa na kurasa 375. [32] Hadi kufikia mwaka 220 kitabu hiki kilikuwa kimechapishwa mara 85 na kimesharatjumiwa kwa lugha kama Kiarabu, Kiingereza, Kiurdu, Kituruki, Kikurdi, Kiazeri, Sindhi, Kihindi, Kijerumani na Kithailand. [33]

Vyanzo

  • Aʿrāfī, ʿAlī Riḍā. Khurshīd-i ʿashūrā. Edited by Muḥammad Āzādī. Qom: Muʾssisa Ishrāq wa ʿIrfān, 1396 SH.
  • Ghaffārī, Muṣtafā. Az nīma-yi khurdād. [n.p], Muʾassisa-yi Pazhūhishī Farhangī Inqilāb-i Islāmi, 1398 SH.
  • Jabraʾīlī, Yāsir. Riwāyat-i rahbarī. Muʾassisa-yi Pazhūhishī Farhangī Inqilāb-i Islāmi, 1398 SH.
  • Khāmeneʾi, Sayyid ʿAlī. Hamrazmān-i Hūsayn. Muʾassisa-yi Pazhūhishī Farhangī Inqilāb-i Islāmi, 1397 SH.
  • Khamenei, Sayyid ʿAlī. Insān-i 250 sāla. [n.p], Markaz-i Ṣahbā, 1391 SH.
  • Khamenei, Sayyid ʿAlī. Du imām-i mūjāhid. [n.p], Muʾassisa-yi Pazhūhishī Farhangī Inqilāb-i Islāmi, 1396 SH.
  • Najafī, Mūsā. Muʿllifahā-yi tamaddunsāz dar maktab-i sīyāsī-yi Imām Riḍā. [n.p], Ārmā, 1396 SH.
  • Sīyāhpūsh, Amīr. Sīyāsat. [n.p], Muʾassisa-yi Pazhūhishī Farhangī Inqilāb-i Islāmi, 1398 SH.
  • A 250-year-old man, explaining the strategy of Imams during the political struggle (Persian)