Mukhayriq
Mukhayriq (Kiarabu: مُخَیْریق) alikuwa ni msomi mashuhuri wa Kiyahudi aliyeishi wakati wa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) na aliyejulikana kwa ujasiri wake usio wa kawaida katika Vita vya Uhud. Katika vita hivi, Mukhayriq, baada ya kukataliwa na jamii yake juu ya ombi lake liliwataka kumsaidia Mtume Muhammad (s.a.w.w), aliamua kwa yeye peke yake kujitolea na kusaidia upande wa Waislamu. Imani yake thabiti katika ushirikianao wake wa kumsaidia Mtume Muhammad (s.a.w.w) ilimchochea kwenda vitani ambapo alifariki akiwa shahidi vitani humo.
Kabla ya kufariki, Mukhayriq alikabidhi mali zake zote kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), zikiwemo bustani saba maarufu kwa jina la Hiitanu Al-Sab'a. Mtume Muhammad (s.a.w.w) alizipokea mali hizo, na ima aliziweka Waqfu kwa ajili ya matumizi ya hisani au alizitoa sadaka. Hata hivyo, baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), binti yake Fatima (a.s) alimwomba Khalifa wa kwanza Abu Bakar, kumkabidhi mali hizo zilizobaki mikononi mwake, zikiwemo bustani hizo na ardhi ya Fadak. Ombi hili lilipingwa na Abu Bakar, lakini baadae, kwa maombi ya Imamu Ali (a.s) na Abbas bin Abdul-Muttalib, uongozi wa bustani hizo ulihamishiwa kwa Imamu Ali (a.s) kupitia Omar bin Khattab.
Kuna maoni tofauti kuhusu dini ya Mukhayriq wakati wa kifo chake. Wakati baadhi ya vyanzo vya kihistoria vikidai kwamba Mukhayriq alifariki akiwa Mwislamu, vyanzo vingine vinadai kuwa alifariki bila kusilimu. Hata hivyo, sifa alizopewa na Mtume Muhammad (s.a.w.w), akimtambua kani "kiongozi na Myahudi bora zaidi", zinachukuliwa kama ni ishara ya kuwa Mukhayriq alifariki hali akiwa ni Muislamu. Mukhayriq anaheshimiwa kwa ujasiri wake na msaada wake kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), na urithi wake wa mali unaendelea kuwa sehemu ya historia muhimu ya Uislamu. Matendo yake ya kujitolea yanaonyesha dhamira thabiti ya katika kuthamini na kuunga mkono haki, hata kwa gharama ya maisha yake mwenyewe. Urithi wake unaendelea kuwa ni kielelezo cha ujasiri na imani isiyo na kikomo kwa watu wote wanaopigania haki na ukweli.
Asili na Hadhi ya Mukhayriq
Mukhayriq alijulikana kama mmoja wa wakuu wa jamii ya Wayahudi [1] aliye kuwa akiheshimiwa kwa elimu yake ya kidini. [2] Yeye alikuwa miongoni mwa wahakiki na wasomi maarufu wa upande wa Ahlul-Kitabu (Wayahudi), akihesabiwa kama mmoja wa Ahbar, [3] yaani, wanazuoni wa dini miongoni mwa watu wa Kitabu. [4] Kwa umuhimu wake katika jamii, Mukhayriq alikuwa na nafasi ya juu miongoni mwa Wayahudi wa wakati wake. Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimtambua Mukhayriq kama ni mmoja wa Wayahudi bora zaidi, [5] jambo ambalo liliimarisha hadhi yake katika historia ya Uislamu. Katika maandiko ya kihistoria, kama vile yaliyotungwa na Zirikli, mtafiti maarufu wa karne ya kumi na nne Hijria, Mukhayriq ametajwa kuwa ni mmoja wa Masahaba wa Mtume (s.a.w.w), hali inayo dhihirisha nafasi na muhimu wake katika Uislamu. [6] Katika kitabu cha "Al-Isaba fi Tamyizi al-Sahaba", ambacho ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya wasifu wa masahaba, maisha na hadhi ya Mukhayriq imeelezwa na kutafitiwa kwa kina. [7] Kitabu hiki kinaweka wazi nafasi maalum ya Mukhayriq katika historia ya Uislamu, ikisisitiza umuhimu wake katika jamii na jinsi alivyo heshimiwa kwa mchango wake, hata baada ya kifo chake.
Mukhayriq alikuwa ni mtu maarufu na tajiri sana katika jamii yake ya Kiyahudi, [8] akimiliki mali nyingi [9] pamoja na bustani kadhaa ambazo zilikuwa sehemu kubwa ya utajiri wake. [10] Utajiri wake ulimuweka katika nafasi ya pekee ndani ya jamii yake, akijulikana si tu kwa mali zake, bali pia kwa mchango wake katika masuala ya kijamii na kidini. Kuhusiana na asili ya kabila lake, Mukhayriq anatajwa kuwa ni mtu wa kabila la Bani Nadhir [11] au Bani Fityun, [12] na kwa undani zaidi akihusishwa na ukoo wa Bani Tha'alaba bin Fityun. [13] Hata hivyo, kuna vyanzo vingine vinavyodai kuwa alikuwa ni mtu wa kabila la Bani Qainuqa’a, [14] ambapo baadhi ya vyanzo vilimtambua kama kiongozi wa kabila hilo. [15] Lakabu na majina yake mengine yaliyo husishwa naye ni; Nadhriyyu, [16] Israeli, na Israailiyyu [17] (Myahudi). [18]
Kushiriki Kwake Katika Vita vya Uhud na Kifo Chake
Mukhayriq, msomi na kiongozi wa jamii ya Kiyahudi aliye ishi mjini Madina, alionyesha ujasiri wake wa kujitolea kwa dhati katika vita vya Uhud. [19] Kwa mujibu wa ripoti za kihistoria, alijitolea katika vita hivyo licha ya kukataliwa ombi lake la kuwataka watu wa kabila lake kushirikiana naye katika vita hivyo. Mwanahistoria Ibn Hisham anasimulia akisema kwamba; kabla ya vita hivyo, Mukhayriq aliwaomba Wayahudi wenzake kushirikiana naye katika kumsaidia Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika vita dhidi ya maadui wa Uislamu. Hata hivyo, walikataa ombi hilo kwa sababu siku hiyo ilikuwa ni sawa na siku ya Jumamosi, ambayo ilikuwa ni siku takatifu kwa Wayahudi, siku ambayo kwa mila zao huwa hawashiriki katika shughuli zozote zile ndani yake. Kwa ujasiri na imani yake, Mukhayriq aliwajibu kwamba hali ya dharura inayowakabili ilikuwa na umuhimu zaidi kuliko kuzingatia siku ya Jumamosi. alifanya hivyo akijua ukweli wa unabii wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na akahiari kuitanguliza imani ya Uislamu juu ya kanuni za kidini na mila za jamii yake za wakati huo. [20] [Maelezo 1] Wanahistoria kama Waqidi na Baladhuri wanasema kuwa; Mukhayriq aliwaapia Wayahudi wenzake akiwambia ya kwamba; wao wanatambua fika kwamba Muhammad (s.a.w.w) ni Mtume wa Mungu, na kwa hiyo walipaswa kuwajibika katika kumsaidia mtume huyo. [21]
Mukhayriq alikufa shahidi katika Vita vya Uhud,[22] akionyesha uaminifu wake kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kujitolea kwake katika kuitetea haki. Hata hivyo, katika Kitabu cha Al-Taraif fi Ma'rifat Madhahib al-Tawa'if kilichoandikwa na Sayyid Ibn Tawus, kuna simulizi zinazoeleza kwamba; Mukhayriq alikufa kifo cha kawaida na wala hakufa kishahidi vitani humo. [23] Madai haya yanaonekana kuwa ni tofauti na simulizi nyingine za kihistoria na hayapatikani katika maandiko asili ya awali ya Kiarabu. Mukhayriq, iwe kaf kishahidi vitani au kwa kifo cha kawaida, bila shaka yeye atabaki kuwa ni nembo ya ujasiri wa kipekee na ni nembo ya imani isiyoyumba katika kumsaidia Mtume Muhammad (s.a.w.w), licha ya changamoto na upinzani wote aliyopata kutoka katika jamii yake. Mukhayriq ameacha urithi wa heshima katika historia ya Uislamu, akionyesha jinsi kujitolea binafsi kunavyo weza kuwa na athari kubwa katika nyakati za mitihani.
Uhamishaji wa Mali Yake kwa Bwana Mtume (s.a.w.w)
Mukhayriq alifacha wasia muhimu wa kutaka mali zake zipelekwe kwa bwana Mtume (s.a.w.w). [24] Kulingana na vyanzo vya kihistoria, yeye walitoa wasia akisema kwamb; iwapo atafariki vitani humo, basi mali zake zipelekwe kwa bwana Mtume (s.a.w.w). [25] Alikuwa na imani kwamba mali zake zitakuwa na umuhimu na manufaa mkubwa mbele ya bwana Mtume (s.a.w.w). Baadhi ya vyanzo vinadai kwamba wasia huu ulitekelezwa baada ya kifo cha Mukhayriq. [26] Katika kitabu cha Ansab al-Ashraf, Baladhuri anasema kwamba; Mukhayriq alikabidhi mali zake kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) wakati akiwa yuhai. [27] Taarifa hii inathibitishwa pia na Muhammad Taqi Shushtari katika kitabu chake kiitwacho Qamus al-Rijal. [28] Wengine wanafikiria kwamba Mukhayriq alikabidhi mali zake mara tu baada ya kubadili dini na kukuubali Uislamu. [29]
Mtume Muhammad (s.a.w.w) alitumia mali za Mukhayriq katika njia za hisani na sadaka. [30] Inaaminika kwamba sehemu kubwa ya mali zilizotolewa kama sadaka na bwana Mtume (s.a.w.w), zilikuwa ni sehemu za mali za Mukhayriq. [31] Wengine pia wamesema kwamba sadaka zote [32] za bwana Mtume (s.a.w.w) zilikuwa sehemu ya mali zilizotangulia kumilikiwa na Mukhayriq. [33] Aidha, kuna maelezo yanayosema kwamba Mtume alizifanya waqfu mali za Mukhayriq, [34] na hivyo mali hizi zinaonekana kuwa ndiyo wakfu wa kwanza ulioanzishwa na bwana Mtume (s.a.w.w), [35] ama kwa mikono ya Mukhayriq mwenyewe au kupitia utaratibu wa bwana Mtume (s.a.w.w). [36] Kwa hivyo, mali za Mukhayriq zilikuwa na umuhimu mkubwa katika historia ya Uislamu. Uhamishaji wa mali hizi kwa Mtume (s.a.w.w) umechangia kuimarisha maadili ya sadaka na wakfu katika jamii ya Waislamu.
Bustani Saba Maarufu kwa Jila la Hiitanu Al-Sab’a
- Makala Asili: Hiitanu Al-Sab’a
Imeelezwa kwamba; mali za Mukhayriq zilikuwa bustani saba maarufu kwa jina la “Hiitanu al-Sab’a”, ambazo zilizo tambulika kwa majina haya: Meythab, Safiyah, al-Dallal, Husni, Burqah, A'awaf, na Mashrabah Umm Ibrahim. [37] [Maelezo 2] Bustani hizi, zilizojulikana kama Hawa-it Rasuli (s.a.w.w), [38] ambazo zilikuwa na mitende bora na yenye matunda mengi zaidi katika eneo la mji wa Madina. [39] Kulingana na vyanzo mbali mbali, baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), Bibi Fatima (a.s) alimuomba Khalifa Abu Bakar kumkabidhi mali zilizobaki kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w), ikiwa ni pamoja na bustani hizi saba na ardhi ya Fadak, ambalo alizitaka zirejeshwe mikononi mwake. Hata hivyo, Abu Bakar alikataa ombi hili, [40] hali iliyosababisha kukasirika kwa Bibi Fatima, ambaye aliona kuwa ombi lake lilikataliwa kinyuma na misingi ya haki. [41] Katika kipindi cha utawala wa Khalifa wa Omar bin al-Khattab, Imamu Ali (a.s) akishirikiana na Abbas bin Abdul-Muttalib walimwomba Khalifa Omar kulisikiliza ombi hilo la bibi Fatima kuhusiana na mali hizo. Khalifa Omar alikubali kutoa baadhi ya mali hizo, ila bado aliendelea kushikilia mashamba ya Fadak na Khaybar. [42] Bustani hizi saba zilipokewa na Imamu Ali (a.s), na baadaye zilikakabidhiwa kwa watoto wa Bibi Fatima (a.s), ikiwemo Imamu Hassan na Imamu Hussein (a.s). [43]
Abu Basir amenukuu Hadithi kutoka kwa Imam Baqir (a.s), isemayo kwamba; Bibi Fatima (a.s) aliusia bustani hizi saba kuendeshwa na Imamu Ali (a.s), na baadae ziendelee kuendeshwa na watoto wake, ambao ni Imamu Hassan na Imamu Hussein (a.s), na baadaye ziwafikie wajukuu wao, ili kuhakikisha kwamba mali hizi zinabaki katika familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Pia mfano wa Hadithi kama hizi zimekuliwa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s), ikionyesha jinsi familia ya bwana Mtume (s.a.w.w) ilivyothamini mali hizi kama ni sehemu muhimu ya urithi na uhifadhi zao za kidini. [44]
Dini ya Mukhayriq
Ripoti za kihistoria zinaonyesha kuwa Mukhayriq alikuwa akimwelewa vyema bwana Mtume (s.a.w.w), hii ni kutoka na elimu yake ya vitabu vya mbinguni. Hata hivyo, upendo wake wa kuipenda dini ya Uyahudi ulimzuia kufunguka na kusema haki juu ya ukweli na uhakika wa Uislamu. [45] Baadhi ya vyanzo vinaamini kwamba; Mukhayriq alikubali unabii wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na alitamani kuwa miongoni mwa Waisilamu wa kwanza kabisa, ila alijizuia kutokana na hofu ya kuingia kwenye migogoro na viongozi wa Kiyahudi. [46] Kwa mujibu wa vyanzo hizyo, yeye aliendelea na hali hiyo zama za vita vya Uhud, ambapo aliingia rasmi katika dini ya Kiislamu. [47] Vyanzo vingi vinathibitisha kwamba Mukhayriq alisilimu na kutangaza Uislamu wake rasmi. [48] Kuna ripoti zinazodai kwamba; baada ya Mukhayriq kumwamini bwana Mtume (s.a.w.w), [49] alijaribu kuwashawishi watu wa kabila lake, Banu Qaynuqa, kuwamini na kukubaliana na bwana Mtume (s.a.w.w), ila wa walikataa. [50]
Kwa upande mwingine, Ibn Saad (aliyefariki mnamo mwaka 230 Hijria) katika kitabu chake cha Tabaqat aliripoti akisema kwamba; Mukhayriq hakuwa Muislamu kamili, ila alikwenda kumsaidia bwana Mtume (s.a.w.w) katika vita vya Uhud na aliuawa katika vita hivyo. [51] Ndiyo maana maiti yake ilizikwa bila ya kusaliwa sala ya maiti, na mwishowe alizikwa katika pembeni mwa makaburi ya Waislamu. [52] Ripoti hii pia imehusishwa na Waqidi. [53] Ingawa Ibn Hajar, mtafiti wa karne ya tisa, pia aliihusisha ripoti ya Uislamu wa Mukhayriq kwa Waqidi, ambayo ni kunyume na ripoti iliopita inayo jaribu kuukataa Uislamu wa Mukhayri. [54] Kwa upande mwengine kuna taarifa isemayo kwamba; Mtume Muhammad (s.a.w.w) hakumsema chochote kuhusiana na Mukhayriq zaidi ya kumsifu kwa kuseima ni Myahudi baro, si kabla ya vita wala si baada ya vita vya Uhud. Na hata baada ya kifo chake bwana Mtume (s.a.w.w) hakuonekana kumwombea maghufira bwana Mukhayriq. [55] Wengine wanadhani kwamba; Kule bwana Mtume Kumsifu Mukhayriq sifa za kumkweza, na kusuma kuwa yeye ni "Myahudi Bora" miongoni mwa Wayahudi, kuwekwa samamba na Salman al-Farisi akiwa ni "mbora wa Wafursi" na Bilal kama ni "mbora wa watu wa Habasha, [56] ni dalili ya Uislamu wa Mukhayriq. [57]
Maelezo
- ↑ Kuna khitilafu katika vyanzo mbali mbali juu ya habari za Mukhayriq na hali yake ya kimasihi. Khitilafu hizi unaweza kuzipata katika vyanzo vifuatavo kwa mitindo tofauti: Katika kitabu cha Tariikh al-Tabari kilichochapishwa mwaka 1967, Juzuu ya 2, ukurasa wa 531, habari za Mukhayriq zinatangazwa kwa mtindo tofauti. Pia, Ibn Kathir katika Al-Bidaya wa al-Nihaya (Juzuu ya 4, ukurasa wa 36) naye anatoa maelezo tofauti kuhusiana na hali ya Mukhayriq na msaada wake kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Mqriżi katika Imtāʿ al-Asām (Juzuu ya 1, kurasa 160-161 na Juzuu ya 3, ukurasa wa 353) pia, naye anatoa taarifa tofauti zinazohusiana na Uislamu wa Mukhayriq pamoja na maelezo mengine yanayo husiana na maisha yake.
- ↑ Majina ya mabustani haya yamewasilishwa yakiwa na tofauti kidogo katika vyanzo mbalimbali. Tofauti hizo unaweza kuzipata katika vyanzo vifuatavo: Ansab al-Ashraf ya Bladhari (1996, Juzuu ya 1, ukurasa wa 518). Tariikh al-Madina al-Munawwara cha Ibn Shabah (1410 H., Juzuu ya 1, ukurasa wa 173). Uyoun al-Athar cha Ibn Sayyid al-Nas (1993, Juzuu ya 1, ukurasa wa 240). Pia, kuna tafiti za kina kuhusiana na maeneo pamoja na majina hasa ya mabustani zimewasilishwa na watafiti mbali mbali, ambazo utazipata katika vitabu vifuatavyo: Mawsuat Mir'at al-Haramayn al-Sharifayn cha Sabri Pasha (1424 H., Juzuu ya 4, kurasa 806-807). Wafa' al-Wafa cha Samhudi (2006, Juzuu ya 3, kurasa 151-155).