Nenda kwa yaliyomo

Mufsid fil-Ardh

Kutoka wikishia
Makala hii ni kuhusiana na Mufsid fil-Ardh. Ili kujua kuhusiana na Muharib angalia makala ya Muharaba.

Mufsid fil-Ardh (Kiarabu: مُفسِد فِی الاَرض) ni mtu ambaye kwa kufanya baadhi ya madhambi na kuchukua hatua zisizo za mahali pake huharibu uhuru, usalama, uadilifu na utulivu wa umma na kuindoa jamii katika hali ya mlingano na ya kati na kati. Istilahi hii imechukuliwa kutoka katika Qur’an. Kundi la mafakihi likitumia Aya ya Muharaba limekuja na anuani ya kujitegemea ya Mufsid fil-Ardh na kuamini kwamba, maudhui hii iko kando kabisa na Muharaba na kwamba, adhabu yake ni kifo. Kundi jingine limetambua anuani mbili hizi (Muharaba na mufsid fil ardh) kwamba, ni moja na adhabu za anayefanya uharibifu na uchafuzi katika ardhi ni zile zile zilizoainishwa kwa ajili ya Muharaba.

Mafakihi wa Kishia wanaamini kwamba, mambo kama utekaji nyara, kuwa na ada ya kuwaua Ahlu-Dhimmi, kuzoea kuiba sanda, uchawi na kukariri kufanya mambo yaliyoharamishwa ni miongoni mwa vielelezo na mifano ya kufanya ufisadi katika ardhi. Kwa mujibu wa kipengee cha 286 cha sheria ya adhabu katika katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyopasishwa mwaka 1392 Hijria Shamsia, uhalifu dhidi ya usalama wa ndani na wa nje wa nchi, kueneza uongo, kuvuruga mfumo wa kiuchumi wa nchi na kuanzisha vituo vya ufisadi na ufuska ni katika vielelezo na mifano ya kufanya ufisadi katika ardhi na adhabu yake ni kunyongwa.

Umuhimu na nafasi

Ufisadi katika ardhi ni anuani iliyochukuliwa kutoka ndani ya Qur’an Tukufu ambayo kutokana na adhabu yake kuwa kubwa na kali ni jambo ambalo limejadiliwa na kuzungumzwa sana. Anuani ya Mufsid fil-ardh [1] na ibara ya fisad fil-ardh [2] zimetumika katika Aya mbalimbali za Qur’an.

Katika vyanzo vya hadithi na fikihi vya Kishia, hakuna mlango maalumu unaojitegemnea wenye anuani ya “Mufsid fil-ardh” au “Fisad fil-ardh”; hadithi zinazohusiana na maudhui zimezungumziwa na kuletwa katika milango mbalimbali kama mlango wa kisasi, [3] mlango wa adhabu ya Muharib, [4] na mlango wa dia. [5] Kadhalika hukumu zake zimezungumziwa katika mijadala mbalimbali ya kifikihi kama ghasb (upokonyaji), dhima, Taazirat (makosa ambayo katika Uislamu adhabu zake hazijaanishwa, na jukumu hilo lipo mikononi mwa mtawala wa kisheria), kisasi, Muharaba, adhabu (kama kuchapwa mijeledi n.k) na dia. [6]


Tofauti yake na Muharib

Makala kuu: Muharaba

Kundi la mafakihi likitumia Aya ya Muharaba limekuja na anuani ya kujitegemea ya Mufsid fil-ardh na kuamini kwamba, Mufsid fil-ardh ni tofauti na Muharib. Kundi jingine limetambua anuani mbili hizi (Muharib na mufsid fil ardh) kwamba, ni moja. Baadhi ya mitazamo ya mafakihi ni kama ifuatavyo:

  • Imam Khomeini (1902-1989), fakihi wa Kishia na muasisi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran, yeye ametambua kuwa, mufsid fil ardh na Muharib ni kitu kimoja. Kwa mtazamo wake ni kuwa, Muharib ni mtu ambaye anatoa na kujiandalia silaha kwa ajili ya yake ili kutisha watu na kusababisha ufisadi katika ardhi. [7]
  • Muhammad Mu’min Qomi (1938-2019), mmoja wa mafakihi wa Kishia anaamini kuwa, Mufsid fil ardh katika Aya ina maudhui, na kwamba, Muharaba inahesabiwa kuwa moja ya vielelezo na mifano ya kufanya ufisadi katika ardhi. Kwa msingi huo, kila mara anauani ya “Mufsid fil-ardh” inapopatikana, hata kama itakuwa haina anuani ya Muharaba, lakini adhabu nne zilizotajwa katika Aya (kuuawa, kunyongwa, kukata mikono na miguu kwa kubadilisha au kupelekwa uhamishoni) zinahusika katika hili. [8]
  • Muhammad Fadhil Lankarani (1931-2007), Marjaa Taqlidi anasema kuwa, kuhusiana na Mufsid fil ardh na Muharib kuna suala la umuum (hali jumla) na khusus mutlaq (maalumu mutlaki); kwa maana kwamba, kila Muharib ni Mufsid fil al-rdh (mwenye kufanya ufisadi katika ardhi), lakini lakini si kila mfanya ufisadi katika ardhi ni Muharib na si kila mfanya ufisadi katika ardhi anaadhibiwa adhabu za Muharib. [9]
  • Nassir Makarem Shirazi (aliyezaliwa 1927), mmoja wa Marajii Taqlid anaamini kwamba, Mufsid fil-ardh na Muharib ni maneno na mafuhumu mbili tofauti; kwa mfano mtu ambaye anaeneza na kusambaza madawa ya kulevya kwa kiwango kikubwa, ni mufsid fil-ardh, lakini sio Muharib; kwani hajatoa silaha. Lakini mtu ambaye atawatisha watu kwa silaha hata mara moja tu, anahesabiwa kuwa ni Muharib, lakini sio mufsid fil ardh, isipokuwa kama hilo litajikariri. [10]

Hitilafu za kimitazamo za mafakihi kuhusiana na anuani hizi mbili zimekuwa na taathira pia katika sheria ya adhabu za Kiislamu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; [11] kiasi kwamba, katika sheria za adhabu za Kiislamu iliyopasishwa mwaka 1392 Hijria Shamsia, anuani ya ufisadi katika ardhi imetambulishwa kando na Muharaba. [12]

Mifano hai

Mafakihi wametaja baadhi ya mambo kama mifano ya kufanya ufisadi katika ardhi. Baadhi ya hayo ni:

  • Baadhi ya mafakihi kwa kuzingatia baadhi ya adhabu zilizotajwa katika hadithi mbalimbali, wanataja mambo kama kuchoma moto nyumba na mali za wengine, [13] kuteka nyara, [14] na ada ya kuua Ahlu-Dhimma, [15] kwamba, ni katika mifano ya ufisadi katika ardhi.
  • Kwa mujibu wa Muhammad Fadhil Lankarani ni kwamba, uhalifu wote ambao unapelekea kuuawa kama kuzini mwanaume mwenye mke au mwanamke mwenye mume, kuzini na maharimu, kufanya liwati n.k, ni mambo yanayohesabiwa kuwa ni mifano ya kufanya ufisadi katika ardhi. [16]
  • Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kifungo cha 286 cha adhabu za Kiislamu kilichopasishwa 1392 Hijria, masuala kama jinai dhidi ya usalama wa ndani au wa nje wa nchi, kueneza uongo, ukwamishaji katika mfumo wa kiuchumi, uharibifu, kuanzisha vituo vya ufisadi na ufuska au kushiriki katika hayo kwa namna ambayo kutapelekea kukwamisha pakubwa mfumo wa umma nchini, kuzusha machafuko au kusababisha hasara ya mwili na ya mali ya umma au ya mtu binafsi na kueneza ufisadi na ufuska ni miongoni mwa mambo ambayo yametambuliwa kuwa ni katika mifano ya kufanya ufisadi katika ardhi. [17]
  • Baadhi pia wamesema kuwa, mambo kama kuanzisha magenge ya ufuska, uovu na uuzaji wa madawa ya kulevya na mfano wa hayo kuwa ni katika mambo ambayo ni mifano ya kufanya ufisadi katika ardhi. [18]
  • Katika sheria ya adhabu za Kiislamu nchini Iran iliyopasishwa 1392 Hijria Shamsia, uhalifu wa kiuchumi umetambuliwa rasmi kuwa ni kufanya ufisadi katika ardhi [19] na kwa ajili ya kupambana na ufisadi wa kiuchumi kumeainisha adhabu kama kunyongwa. [20] Baadhi ya wahakiki wanasema kuwa, kuainishwa adhabu ya kunyonga kwa wanaofanya ufisadi wa kiuchumi, ni hatua ambayo haina mashiko ya kifikihi. [21]

Adhabu

Kuna mitazamo tofauti kuhusiana na adhabu dhidi ya kufanya ufisadi katika rdhi. Hitilafu hizi chimbuko lake ni katika kutoa fasili na maana pamoja na uhusiano baina ya anuani mbili hizi yaani “Mufsid fil-ardhi” na “Muharib”. [22] Wanaoamiani kwamba, anuani mbili hizi ni kitu kimoja wametosheka na adhabu zilizoanishwa kwa ajili ya Muharib. [23] mafakihi wakitegenmea Aya ya Muharaba wamefikia ijma'a (kauli moja) kwamba, adhabu ya Muharib ni vitu vinne: kuuawa, kusulubiwa (kufungwa mikono na miguu ya mhalifu katika kitu kinachofanana na msalaba), [24], kukatwa mikono na miguu kwa kubadilisha (kwa mfano kukatwa mkono wa kulia na mguu wa kushoto) na kubaidishwa (kupelekwa uhamishoni). [25] Hekima na falsafa ya kumuadhibu Muharib ni kuhifadhi na kulinda damu za watu wasio na hatia na kuzuia watu wanaotumia mabavu kufanya hujuma dhidi ya uhai na roho za watu, mali na Namus (mke, mama, binti n.k). [26]

Kwa mujibu wa nadharia na mtazamo wa baadhi ya mafakihi, adhabu ya mufsid fil-ardh (ikiwa na anuani ya kujitegemnea) ni kuuawa. [27 Kadhalika kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kifungo namba 286 cha sheria ya adhabu za Kiislamu, adhabu ya mfanya uharibu katika ardhi ni kunyongwa. [28]


Hitilafu kuhusu adhabu ya kunyonga

Sayyied Muhammad Musawi Bujounourd, mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la Mahakama la Iran wakati huo, anasema, kwa mtazamo wa Imam Khomeini mfanya ufisadi katika ardhi hana anuani yake yeye kama yeye ya uhalifu ambayo inastahiki kunyongwa; isipokuwa kama hilo litaambatana na kubeba silaha; [29]. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana katika jibu la barua yake kwa Abdul-Karim Musawi Ardabili, mkuu wa wakati huo wa mahakama ya juu kuhusu kuianisha adhabu ya kunyonga kwa ajili ya wafanya ufisadi katika ardhi alivirusu vyombo vya mahakama kutoa hukumu kwa mujibu wa mtazamo wa Hussein Ali Muntazeri. [30] Muntazeri alikuwa akiamini kuwa, inajuzu kumnyonga mufsid fil ardh.

Vyanzo

  • Fāḍil Lankarāni, Muḥammad. Tafṣīl al-sharīʿa fī sharḥ Taḥrīr al-waṣīla. Qom: Markaz-i Fiqh-i al-aʾimma al-Aṭhār, 1422 AH.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Mukhtalif al-shīʿa fī aḥkām al-sharīʿa. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1419 AH.
  • Ḥillī, Jaʿfar b. al-Ḥasan al-. Sharāʾiʿ al-Islām fī masāʾil al-ḥalāl wa l-ḥarām. Tehran: Istiqlāl, 1409 AH.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Wasāʾil al-Shīʿa. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1416 AH.
  • Ibn Manẓūr, Muḥammad b. Mukarram. Lisān al-ʿArab. Beirut: Dār al-Fikr, 1414 AH.
  • Imām Khomeinī, Sayyid Rūḥ Allāh. Ṣaḥīfa-yi Imām. Tehran: Markaz-i Nashr-i Āthār-i Imām, 1389 Sh.
  • Khomeini, Sayyid Rūḥ Allāh. Taḥrīr al-wasīla. Najaf al-Ashraf: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1390 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1387 Sh.
  • Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh-i al-Islāmī. Musūʿa al-fiqh al-islāmī ṭibqan li madhhab Ahl al-Bayt (a). 1st edition. Qom: Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh-i al-Islāmī, 1423 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
  • Shāhrūdī, Sayyid Maḥmūd. Muḥāraba chīst wa muḥārib kīst?. Fiqh-i Ahl Bayt magazine. No 11 and 12, 1376 Sh.
  • «وجه تفاوت «افساد فی الارض» و «محاربه (The difference between corruption on earth and warfare (persian)). Accessed: 2022/12/31