Misingi ya Madhehebu ya Shia

Kutoka wikishia
Makala hii inahusu Misingi ya madhehebu ya shia. Kwa Misingi ya dini ya uislamu, tazama Misingi ya dini dini.

Misingi ya Madhehebu ya Shia (Kiarabu: أصول المذهب الشيعي), ni itikadi za kimsingi za Madhehebu ya Kshia itikadi ambazo zinajumuisha Tawhiid, Utume, Ufufuo, Uadilifu, na Uimamu. Kwa mujibu wa itikadi na imani ya Waislamu wa Kishia ni kwamba, kupinga na kukanusha msingi wowote kati ya misingi hii ya mwanzo ya lazima (Tawhiid, Utume na Ufufuo, vitu ambavyo ni misingi ya dini humfanya mtu kuwa kafiri, ama kutoamini msingi wowote kati ya misingi miwili hii (Uadilifu na Uimamu) humfanya mtu kutoka kwenye madhehebu ya Kishia na sio kutoka kwenye dini ya Uislamu.

Kuwepo kwa Uimamu chini ya misingi ya dini humpambanua Mshia na watu wa madhehebu zingine za Kiislamu na Mashia kutokana na sababu hii na uthibitisho huu ndio maana huitwa kwa jina la Imamiyah. Vivyo hivyo kuitakidi na kuamini msingi wa Uadilifu, pia huwapambanua watu wa madhehebu ya Muutazilah na Asha'irah na ndio sababu ya Mashia na Mu'utazilah kujulikana kwa jina la Al-adliyah.

Nafasi ya misingi hii

Misingi ya madhehebu ya shia , ni zile asili tano au misingi mitano ambayo ni (Tawhiid, Utume, Ufufuo, na Uadilifu) na hii ndio misingi ijulikanayo na kuitwa kwa jina la misingi ya madhehebu ya shia,[1] vitua ambayvyo ndio misingi na mihimili ya madhehebu ya kishia na ndio vitu vinavyo unda misingi ya itikadi ya madhehebu ya kishia.[2] Kuamini na kuitakidi misingi yote hii, humfanya na kumpelekea mtu kuhesabiwa kuwa ni mshia, na kutoitakidi msingi wowote kwa sababu yoyote ile humtoa mtu kwenye madhehebu ya Kishia au humfanya mtu kutoka kwenye madhehebu ya kishia. Lakini ni vyema ikafahamika kwamba misingi mitatu ambayo ni Tawhiid, Utume na Ufufuo ni miongoni mwa misingi ya dini, misingi ambayo kutoamini msingi wowote kati ya misingi hiyo mitatu pia huwa ni sababu ya mtu kuwa kafiri na kutoka kwenye dini ya kiislamu.[3]

Misingi maalumu

Uimamu[4] na Uadilifu[5] ni misingi miwili maalum ya madhehebu ya kishia:

Uimamu

Makala asili: Uimamu

Imani na itikadi ya kwamba Uimamu (Uongozi wa jamii ya kiislamu na ukhalifa baada ya Mtukufu Mtume Muhammad(s.a.w.w) ni cheo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu (cheo cha kiungu)[6] na hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuna maimamu kumi na mbili watokanao na kizazi cha Mtume(s.a.w.w) wamesimikwa na kuwekwa kwenye cheo hiki.[7] Na majina ya maimamu hao kiutaratibu ni kama yafuatayo:

Kwanini uimamu ukafanywa kuwa ni msingi wa madhehebu?

Kutokana na maneno ya Muhammad Hussein Kaashiful-ghitwaa katika kitabu chake Asili ya Ushia na misingi yake, Uimamu ni msingi ambao huwapambanua mashia na madhehebu zingine za kiislaam.[9] Kwa sababu hii wanao itakidi na kuamini maimamu kumi na mbili huitwa na kutambulika kwa jina la Imamiyah.[10] Na Uimamu umekuwa na kuhesabiwa kuwa ni miogoni mwa misingi ya madhehebu ya shia.[11] Na mtu ambae hatokubali na kuamini misingi hiyo basi hutoka kwenye wigo wa madhehebu ya shia.[12]

Uadilifu

Makala asili ya Uadilifu

Ni imani na itikadi ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu sio katika nidhamu ya ulimwengu wala kwenye nidhamu ya kisheria (na uwekaji wa sheria) hutenda na kufanya lililo la haki na wala hadhulumu.[13] Adliyah ambao ni Shia na Muutazilah, wanaamini na kuitaki kwamba uzuri na ubaya wa vitu ni jambo linalo dirikiwa na kubalika na akili, na wanaitakidi kwamba Mwenyezi Mungu ni muadilifu kwa maana kwamba yeye hufanya mambo kwa msingi wa uzuri wa mambo hayo, na hafanyi dhulmah kutokana na ukweli kwamba dhulma ni jambo baya hivyo hafanyi dhulmah kutokana na ubaya wake.[14]

Mkabala wa itikadi hii wafuasi wa Asha'irah wanaitakidi kwamba kigezo cha uadilifu wa jambo na kwamba jambo au tendo fulani ni la uadilifu, kigezi chake ni tendo la Mwenyezi Mungu na kwamba kila jambo ambalo Mwenyezi Mungu atalitenda basi jambo hilo ni jema na ni la uadilifu hata kama kwa mtazamo wa wanadamu litakuwa ni dhulama na udhalimu.[15]

Sababu za uadilifu kuwa miongoni mwa misingi ya madhehebu

Kwa mujibu wa maneno ya Ayatullahi Misbah Yazdiy mwana falsafa wa kishia (1313-1399 S), ni kwamba uadilifu kutokana na umuhimu wake katika elimu ya theologia na kutokana na umuhimu wake katika elimu ya akiida kwa sababu hii huzingatiwa kuwa ni miongoni mwa misingi ya madhehebu ya shia na Muutazilah.[16]Vile vile mwanafikra wa kishia Murtadha Mutwahari (1298-1358 sh) akitambua na kuamini kuwa sababu ya uadilifu kuwa na kuwekwa kwenye orodha ya misingi ya madhehebu ya kishia ni uwepo wa itikadi kama vile kupinga uhuru na ikhtiyari ya mwanadamu miongoni mwa waislamu kiasi kwamba kwa msingi wa watu hao ni kwamba kumuadhibu au kuadhibu na kumpa malipo mabaya mtu alie tenzwa nguvu au alie lazimishwa kufanya jambo kwa nguvu na bila hiyari yake jambo hilo halina uwiano na uadilifu wa Mwenyezi Mungu.[17]

Mashia na Muutazilah , wanaitakidi na kuamini kwamba kutenzwa nguvu na kulazimishwa kwa mwanadamu ni jambo linalo kinzana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu na kwa sababu hii ndio maana wamekuwa mashuhuri na kufahamika kwa jina la Al-adliyah.[18]

Misingi wanayo shirikiana

Mkala asili: misingi ya dini

Tawhiid: (Upweke wa Mwenyezi Mungu:Ni Imani ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, wa pekee asie na mshirika.[19]

Utume:Ni kuamini ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliwatuma watu fulani kwa ajili ya kuwaongoa wanadamu watu ambao ni mitume, hivyo basi aliwatuma mitume kwa ajili ya kuwaongoza na kuwaongoa watu.[20] Na mtume wa kwanza alietumwa na Mwenyezi Mungu ni Hadhtrat Adam(a.s)[21] na mtume wa mwisho ni Hadhrat Muhammad(s.a.w.w).[22]

Ufufuo: ni kuamini kwamba mwanadamu baada ya kifo atafufuka na kuwa hai na pia kulipwa kutokana na matendo yake mema au mabaya.[23]

Rejea

  1. Tazama: kitabu: Muhammad Rei shahri, Danesh naameh Aqaaid islaami, 1385 S, juz. 8, uk. 99.
  2. Tazama: kitabu cha Reishahri, Danesh naameh Aqaaid islaami, 1385 S, j8, uk. 97.
  3. Kaashiful-ghitwaa, Aslus-shia ,wa Usoulihaa, Muassasatu Imamu Ali (a.s) uk. 210, Tazama: kitabu cha Imamu Khomeini, kitabut-twaharah, 1427 H, juz. 3, uk. 437-438.
  4. Laahiji, Gohar Muraad, 1383 S, uk. 467, Tazama: kitabu cha Subhani, Al-ilahiyaat, 1417 H, juz. 4, uk. 10.
  5. Misbahu Yazdiy, Aamuzesh Aqaaid, 1384 S, uk. 161.
  6. Kashful-ghtwaa, Aslus-shiah wa Usouliha, Muassasatul-imami Ali (a.s), uk. 211.
  7. Tazama: kitabu cha Laahiiji, Gohar Murad, 1383 S, uk. 585.
  8. Khazzaaz Razi, Kifayatul-athar, 1401 H, uk. 53-55, Swadouq, Kamaalud-din, 1395 H, juz. 1, uk. 253-254.
  9. Kaashiful-ghtwaa, Aslus-shia wa Usouliha, Muassatul-imami Ali (a.s) uk. 221.
  10. Kaashiful-ghtwaa, Aslus-shia wa Usouliha, Muassatul-imami Ali (a.s) uk. 212.
  11. (Adlu) wa (Imamat) az Usoul madhaheb shie wacharaaiye on? (Aaine rahmat).
  12. Kaashiful-ghitwa, Aslus-shia wa Usouliha, Muassasatul-imami Ali (a.s), uk. 212.
  13. Mutwahari, Majmue Athaar, Swadraa, juz. 2, uk. 149.
  14. Subhaani, Rasaailu wa maqaalaat, 1425 H, juz. 3, uk. 32.
  15. Subhaani, Rasaail wa maqaalaat, 1425 H, juz. 5, uk. 127.
  16. Misbah Yazdiy, Aamuzesh Aqaaid, 1384 S, uk. 161.
  17. Mutwahariy, Majmue aathar. Swadraa, juz. 2, uk. 149.
  18. Mutwahariy, Majmue aathar. Swadraa, juz. 2, uk. 149.
  19. Kaashiful-ghitwaa, Aslus-shia wa Usouliha, Muassasatul-imam Ali (a.s), uk. 219.
  20. Kaashiful-ghitwaa, Aslus-shia wa Usouliha, Muassasatul-imam Ali (a.s), uk. 220.
  21. Majlisiy, Buharul-an'waar, cha mwaka 1403 H, juz. 11, uk. 32.
  22. Surat al-Ahzaab, aya ya 40.
  23. Laahijiy, Gohar Muraad, cha mwaka 1383sh, uk. 595, Kaashiful-ghitwaa, Aslus-shia wa Usouliha, Muassasatul-imam Ali (a.s), uk.222.

Vyanzo

  • Imamu Khomeini, Sayyied Rouhullah, Kitabut-twaharah, Tehran, Muassaseye tandhiim wa nashri Aathar Imamu Khomeini (qs), cha mwaka 1427 H/ 1358 S.
  • Khazzaz Raaziy, Ali bin Muhammd, Kifaayatul-athar fin-nassi alal-aimmatil-ithnay ashar, kilicho sahihishwa na Abdullatif Husein kuuh kamari, Qom, Biidaar, mwaka 1401 H.
  • Subhaani, Jaafar, Rasaailu wa maqalaat, Qom, Muassasatul-imamis-swaadiq (a.s), cha mwaka 1425 H.
  • Subhaani, Jaafar, Ilahiyaat ala hudal-kitabi was-sunnah wal-aqli, kwa uandishi na (kwa kalamu) ya Shekhe Hasan Aamuli, Qom, Muassasatul-imamis-swaadiq, chapa ya nne, mwaka 1417 H.
  • Shekhe Swadouq, Muhammd bin Aliy, Kamaalud-din watamaamun-niimah, kilicho sahihishwa na: Ali Akbar Ghaffariy, Tehran, Islamiyeh. Cha mwaka 1395 H.
  • (Adlu) wa (Imamat) az Usoul madh'hab Shiieh wa charaaiye oon?, (Ooiin rahmat, Mushaahadey 9 khordaad mwaka 1401 S.
  • Kaashiful-ghitwaa, Muhammd Husein, Aslus-shia wa Usouliha, kilicho hakikiwa na Alaa Aali Jaafar, muassasatul-imam Ali (a.s) biita.
  • Laahiijiy. Abdur-razzaq, Ghoohar Muraad. Utangulizi wa Zainul-aabidiin Qurbaany, Tehran, nashri Saaye. Chapa ya kwanza, mwaka 1383 S.
  • Majlisiy, Muhammad Baaqir, Buharul-an'waar, Bairut. Daru ihyaait-turaathil-arabiy mwaka 1403 H.
  • Muhammad Rei Shahri, Muhammad. Daanesh naameh Aqaaid islaamiy, Qom, Darul-hadiith, mwaka 1385 S.
  • Misbaahu Yazdi, Muhammd Taqiiy, Aamuzesh Aqaaid, Tehraan Nashri saazmaan tablighaat islaami, chapa ya kumi na saba. Mwaka 1384 S.
  • Mutwahariy, Murtadhaa, Majmuueye Aathar, Tehraan, Nashri Swadraa.