Malezi ya mtoto

Kutoka wikishia

Malezi ya mtoto (Kiarabu: تربية الأبناء) au kulea kunamaanisha kuandaa na kujenga misingi ya ukuaji wa mtoto, ili awe na maadili mema ya kidini na kidunia. Kulea mtoto ni jambo ambalo limezingatiwa sana katika riwaya na hadithi za Kiislamu. Katika hadithi za Ahlul-Bayt (a.s), vipindi vitatu vya miaka saba vinazingatiwa kwa ajili ya kulea mtoto, kutoka wakati wa kuzaliwa hadi umri wa miaka 21, na kila kipindi kina masharti na maagizo maalumu.

Kujiepusha na adhabu na matusi, kuheshimu utukufu wa nafsi, kuchunga hali ya kati na kati (kutochupa mipaka) na uadilifu ni baadhi ya kanuni na misingi ya kulea watoto ambayo imetajwa na kuashiriwa katika hadithi. Pia, mambo kama vile kuzingatia hatua mbalimbali za ukuaji, kusomesha watoto, hali ya kunyonyesha, kuwapenda watoto na kuwa makini katika kuchagua mchumba ni miongoni mwa mada zinazojitokeza sana na kukaririwa mno katika hadithi zinazohusiana na malezi ya mtoto. Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu pamoja na tabia ya wazazi.

Sifa maalumu za kurithi nazo zina nafasi katika kulea mtoto. Suala la malezi ya watoto limezingatiwa pia na wanafikra wa Kiislamu. Kuhusiana na malezi ya mtoto, Khaaje Nasiru al-Din al-Tusi, mwanafalsafa na mwanateolojia wa Kishia anaashiria mbinu kama vile kugundua hali ya kimaumbile (dhati) na kipaji cha mtoto, kufanya elimu kuwa ujuzi kwa kurudiarudia na kukumbusha, kukemea, kulaumu na kuadabisha katika wakati wa kukataa majukumu ya kidini na kufanya mambo mabaya na kuwadhuru wengine na kumfanya azoee shida. Ibn Sina pia anasisitiza kwamba, kila mmoja wa watoto anapaswa kulelewa kulingana na hali yake ya kinafsi na kipaji chake maalumu na haipaswi kutwisha kitu na kukilazimisha kwa namna yoyote ile; kwani kufanya hivyo kutakuwa na maana ya kupuuza tofauti katika asili, ambayo hatimaye itasababisha uharibifu.

Umuhimu na Nafasi

Kulea mtoto kunachukuliwa kuwa mojawapo ya haki za msingi za mtoto. [1] Kwa mtazamo wa wasomi na wanafikra, hii ina maana ya kujenga msingi wa ukuaji na kuibuka kwa vipaji vya mtoto. [2] Kulingana nao, madhumuni ya kulea mtoto ni kuboresha engo na pande za kiroho na kimwili za mtoto katika maslahi yake ya kidini na kidunia. [3]

Malezi ya mtoto ni jambo ambalo limezingatiwa sana katika riwaya na hadithi za Kiislamu. [4] Kwa mujibu wa riwaya za Kiislamu, wazazi yaani baba na mama wana jukumu la kulea watoto. [5] Imamu Ali bn Abi Twalib (a.s) anasema akitoa ufafanuz wa Aya ya 6 katika Surat Tahrim kwamba: Suala la malezi ya watoto ni moja ya majukumuu ya Waumini kwa ajili ya kuokoka na moto wa Jahanamu. [6] Katika vyanzo vya Kishia kama ambavyo baba na mama ni sababu ya kupatikana kwa mwili wa mtoto wao, wazazi hao wametambuliwa kwamba, kitovu na asili ya tabia za mtoto. [7]

Katika risala yake ya haki, Imam Sajjad (a.s) pia ameweka sehemu maalumu inayohusiana na haki za mtoto, ambamo ameashira wajibu wa wazazi katika malezi ya kiungu ya mtoto kwa vitendo na elimu, na kuzingatia hatima ya mtoto kwamba, inategemea aina ya malezi ya wazazi [8].

Sehemu ya Risala ya Haki ya Imamu Sajjad (a.s) Kuhusiana na Haki ya Mtoto:

Na haki ya mtoto wako ni: Tambua kuwa yeye anatokana na wewe, baya na zuri lake hapa duniani litanasibishwa kwako. Na hapana shaka kuwa, wewe una jukumu la kumlea vizuri na kumuongoza kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na kumsaidia katika kutii amri za Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo katika kazi na mambo yake, fanya kama mtu anayejua kwamba atalipwa kwa kumtendea mema na kuadhibiwa kwa kumfanyia ubaya. Sheikh Saduq, Man Laa Yahdhuruh al-Faqih, 413 Hijria, Jz 2, uk 622.

Malezi ya mtoto; maudhuri iliyojadiliwa zaidi katika hadithi

Baadhi ya watafiti, kwa kuchunguza idadi ya mada zinazohusiana na kulea watoto katika kitabu cha Usul al-Kafi, wamevihesabu vitu hivi kama mada kumi zinazotumika zaidi:

Kuzingatia hatua mbali mbali za ukuaji, malezi ya watoto, masharti ya kunyonyesha, upendo kwa watoto, umakini katika kuchagua mwenza (mke au mume), kuwa na baraka mtoto mwema, malezi sahihi kwa watoto, mila nzuri, athari ya nidhamu, kuadabisha na adhabu katika malezi na kuwapa majina mazuri mazuri watoto. [9]

Pia, wamegawanya hatua za kulea mtoto, kulingana na riwaya katika sehemu tatu: Kabla ya kuzaliwa, baada ya kuzaliwa, na baada ya utoto na wanaamini kuwa mada ya mara kwa mara kati ya riwaya na hadithi ni hatua za kulea mtoto ambazo ni kama ifuatavyo:

  • Hatua ya kabla ya kuzaliwa: Kuwa makini katika kuchagua mwenza.
  • Hatua ya baada ya kuzaliwa: Kuzingatia yaya (mlezi) au mnyonyeshaji na vilevile kumpa jina linalofaa.
  • Hatua ya baada ya utoto: Kuchunga misingi na kanuni za malezi ya mtoto kama vile kumuadabishha na kumuadhibu mtoto, kumlea kijinsia (kulingana na jinsia yake) na kutekeleza ahadi kwa watoto. [10]

Baadhi ya Nukta za Malezi ya Mtoto katika Hadithi

Katika hadithi zilizopokewa kutoka kwa Maimamu wa Shia, tunaweza kupata nukta na vidokezo vinavyofaa na athirifu katika kulea watoto; kama vile kutokuadhibu (kutotia adabu), [11] kutotukana, [12] kujiheshimu, [13] uwiano katika malezi, [14] kuchunga uadilifu [15] kutimiza ahadi, [16] malezi katika umri mdogo, [17] na kufundisha mambo ya dini na ya kijamii [18]

Mbinu za Malezi za Ahlul-Bayt (a.s)

Baadhi ya wahakiki wamegawanya mbizu za malezi za Ahlul-Bayt (a.s) katika mafungu matatu:

  • Mbinu za uhakika: Mambo kama kuonyesha huba na upendo, ushauri, kukirimu shakhsia na kutobagua;
  • Mbinu za urekebishaji: Mambo kama msamaha, kufumbia macho, kutia moyo, adhabu ifaayo, kucheza, kushirikisha katika sherehe za kidini;
  • Mbinu za kinaya: (kwa njia isiyo ya moja kwa moja): Mambo kama vile ushauri wa siri, kufanya mashindano na kuwaachia watoto baadhi ya majukumu. [19]

Vipindi Vitatu katika Malezi ya Mtoto

Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa Madhehebu ya Shia, kulea mtoto kunagawanywa katika vipindi vitatu vya miaka saba: Katika miaka saba ya kwanza inajuulikana kwa jina la «sharifu na bwana», kipindi cha miaka saba ya pili kinajulikana kwa jina la «mtiifu na kutekeleza amri» na kipindi cha miaka ya tatu kinafahamika kwa jina la «waziri na kiongozi». [20]

Wengine wamezingatia vipindi hivi vitatu kuwa vinalingana na utoto, ubarobaro na ujana [21] na wengine wanaamini kuw, mbinu hii husababisha kuibuka kwa tabia nzuri kwa mtoto na kumpa sifa za kisaikolojia, kihemko na kitabia kulingana na maumbile yake. [22]

Nafsi Safi ya Mama na Utendaji wa Baba katika Kulea Mtoto

Kwa mujibu wa utafiti, katika Uislamu, nafasi ya kurithi ya mama katika kulea mtoto ni zaidi ya ile ya baba. Wakati huo huo, baadhi ya hadithi na Aya ya 28 ya Surat Maryam zimeashiria nukta hii. [23] Kwa sababu katika Aya hii athari ya uchafu wa kimaadili wa mama wa Maryam (a.s) imetajwa katika dhimi za watu wake; ingawa kila mtu alikuwa akijua kwamba mama yake alikufa katika utoto wake. [24] Kwa maana kwamba, Aya hiyo inapinga na kukana madai ya watu hao.

Kuhusu athari ya utendaji wa baba katika malezi ya mtoto mwema, baadhi wametaja Aya ya 49 ya Surat Maryam, ambamo imetajwa kuwa Ibrahim alipewa watoto wawili safi (yaani Is’haq na Yaqub (a.s)) ambapo zawadi hii ni matokeo ya Yeye kujitenga na kujiweka mbali na asiyekuwa Mwenyezi Mungu. [25]

Mtazamo wa Wanafikra wa Kiislamu Kuhusu Malezi ya Mtoto

Katika baadhi ya maandiko ya kimaadili, mapendekezo yafuatayo yametolewa kwa wazazi: Kuimarisha staha kwa mtoto, kumfundisha adabu za kula, kuvaa, kupata marafiki, kusoma na kuandika, na kufundisha Qur'ani na hadithi na mashairi mazuri na tabia njema, kuzungumza na kucheza, na hatimaye maagizo yanayohusiana na kipindi cha baada ya balehe, kama vile kusali na kufunga na baadhi ya kazi kanuni na sheria zingine anazozihitajia. [26]

Khaaje Nasiru al-Din al-Tusi, mwanafalsafa na mwanateolojia wa Shia, anapendekeza njia zifuatazo za kulea mtoto:

  • Kugundua asili na kipaji cha mtoto.
  • Kufanya elimu kuwa ujuzi kwa kurudiarudia na kukumbusha mara kwa mara.
  • Kumuadabisha endapo atakataa majukumu ya kidini na kufanya vitendo viovu na kuwadhuru wengine.
  • Kumzoesha shida. [27]

Kwa mujibu wa Ibn Sina, malezi ya mtoto yana hatua sita:

  • Hatua ya kwanza (mwanzo wa kuzaliwa): Kumpa jina zuri na kumnyonyesha maziwa salama.
  • Hatua ya pili (baada ya kumwachisha ziwa): Mchezo na malezi ya kimaadili ya mtoto.
  • Hatua ya tatu (takriban umri wa miaka sita): Kumfundisha mtoto kusoma taratibu Qur'an na elimu.
  • Hatua ya nne: Kumfamisha tasnia na taaluma.
  • Hatua ya tano: Kushughulika na kazi na ajira.
  • Hatua ya sita: Kutengeneza maisha ya kujitegemea. [28]
Kitabu Cha Tarbiyat Dini Kudak (Malezi ya Kidini kwa Watoto), Kilichoandikwa na Muhyi Dini Hairi Shirazi

Ibn Sina vile vile anasisitiza kwamba, kila mmoja wa watoto anapaswa kulelewa kulingana na kipaji chake maalumu na kwa vyovyote vile kitu chochote kisilazimishwe kwa kila mtu kwa njia ile ile; kwa sababu hii ina maana ya kupuuza tofauti za asili, maumbile na dhati ya mtu, kwani kufanya hivyo hatimaye kutasababisha uharibifu. [29] Katika kitabu chake cha Qanun, anataja mpangilio wa mlo kutoka utoto hadi ubarobaro, ambapo katika hilo mbali na malengo ya kitiba anazingatia pia madhumuni ya mafunzo ya kimalezi. [30]

Bibliografia

Kulingana na baadhi ya ripoti, vitabu vya malezi ya mtoto vina anuwai ya juu sana na vimeandikwa kwa mtindo na njia mbili jumla: Baadhi ya vitabu hivyo ni kama vile:

  • Ba kodak Zendegi Kon (Ishi na mtoto), mwandishi: Azar Dostmuhammadi.
  • Usul Taalim va tarbiyat farzand az manzar eslam va elm ravanshenasi (Misingi ya mafunzo na malezi ya mtoto kwa mtazamo wa Uislamu na elimu ya saikolojia), mwandishi Fateteme Baidi ma Akbar Ranjbarzadeh. [31]

Baadhi ya vitabu vingine katika uwanja huu ni:

  • Tarbiyat din kodak (malezi ya kidini ya mtoto); maandiko ya hotuba za Ayatullah Hairi Shirazi. [32]
  • Kitab Tarbiyat Farzand ba ruykard fiqh (kitabu cha malezi ya mtoto kwa utendaji wa kifikihi), mwandishi: Ali Ridha A’rafi na Sayyid Naqi Musavi. [33]

Rejea

Vyanzo