Kumuandaa maiti

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Maandalizi ya maiti)

Kumuandaa maiti (Kiarabu: تجهيز الميت) kunaashiria hatua na mambo anayofanyiwa maiti kabla ya kuzikwa. Kumuandaa maiti ni wajibu kifai na huwa wajibu baada ya kupatikana uhakika wa kifo cha mtu. Hatua za kumuaandaa maiti ni ghusl, hunuti (kumpaka kafuri maiti katika maeneo saba yanayogusa chini wakati wa kusujudu), kumkafini (kumvisha sanda), kumsalia Sala ya maiti na kumzika. Anayepaswa kutangulizwa kwa ajili ya kumfanyia haya maiti ni walii wa maiti na gharama za haya zinapaswa kutolewa kutoka katika asili ya mali ya maiti. Katika utangulizi wa kumuandaaa maiti, mafakihi wamezungumzia adabu na hukumu za Muhtadhar (mtuu anayekata roho) kama vile kumuelekeza kibla na kumtamkisha shahada mbili.

Hatua za kumuandaa maiti

Makala kuu: Kuosha maiti, hunut, sanda, Sala ya maiti na kuzika

Kumuandaa maiti ni kumtayarisha kwa ajili ya kumzika. [1] Katika vitabu vya fikihi kumebainisha hatua za kufuata kwa ajili ya kumuandaa maiti baada ya kuaga dunia: [2]

  • Ghusl: Katika josho hili, maiti anapaswa kuoshwa mara tatu kwa maji yaliyochanganywa na sidri yaani majani ya mkunazi (cedar), maji yaliyochanganywa na kafuri (karafuu maiti) na kwa maji safi. [3] Ikiwa majani ya mkunazi na kafuri haikupatikani, maiti huoshwa kwa maji safi tu, [4] na ikiwa haiwezekani kumuosha kwa maji, hufanyiwa tayammam (hutayamamishwa). [5]
  • Hunuti (hunuti (kumpaka kafuri maiti katika maeneo saba yanayogusa chini wakati wa kusujudu): Ni wajibu [6] kumpaka kafuri maiti katika maeneo saba yanayogusa chini wakati wa kusujudu yaani paji la uso, viganja vya mikono, magoti na vidole gumba vya miguu, na kwa mujibuu wa kauli ya baadhi ncha ya pua. [7]
  • Kuvisha sanda: Ni wajibu kumvisha sanda au kumkafini maiti ni kumfunika kwa kitambaa. [8] Sanda inaundwa na sehemu tatu ambazo ni:
  1. Mosi: Kitambaa cha chini: Ni kitambaa ambacho kinapaswa kufunika mwili kutoka kwenye kitovu hadi magoti
  2. Pili: Shati (qamis): Ni vazi ambalo linapaswa kufunika mwili wa maiti kutoka mabegani mwake hadi kwenye nusu ya miundi.
  3. Tatu: Kitambaa kirefu: ni vazi ambalo linapaswa kufunika mwili mzima wa maiti, kutoka kichwani hadi miguuni. [9]
  • Sala ya Maiti: Ni wajibu kwa kumsalia Muislamu Sala ya maiti na hilo hufanyika baada ya kuumuosha na kuumkfini na kabla ya kuumzika hata kama atakuuwa nim toto. [10]
  • Kuzika: Ni wajibu kumtia kaburi maiti na kumfukia. [11]

Kwa mujibu wa wanazuoni wa fikihi ni kuwa, miongoni mwa mambo ya kuandaa maiti ni kumuelekeza kibla mtu anayetaka roho (muhtadhar). [12] Kwa uoni wao ni wajibu kumuelekeza kibla muhtadhar (anayekata roho) [13] na ni mustahabu kumtamkisha shahada mbili. [14]

Hukumu za kumuandaa maiti

Katika vitabu vya fikihi kumetajwa hukuumu zinazohusana na kuandaa maiti katika mlango wa tohara. [15] Baadhi ya hukumu hizi ni:

  • Kumuandaa maiti ni Wajib Kifai (wajibu ambao ukifanywa na baadhi unaowaondokea wengine). [16] Hata hivyo Muhaqqiq Bahrani amelitambua hilo kuwa ni Wajib Aini (wajibu kwa kila mtu). [17]
  • Kutekelezwa hukumu za kumuandaa maiti hususan kuzika, kunapaswa kufanyika baada ya kukosekana alama na ishara zote za uhai na kuthibitika kikamilifu kufa kwake.
  • Anayepaswa kutangulizwa akwa ajili ya kumuandaa maiti ni Walii wa Maiti [19] Walii wa maiti ni mtu ambaye kwa muujibu wa matabaka ya urithi, anatangulizwa katika kuchukua urithi ulioachwa na maiti. [20]
  • Ni wajibu kuchukua idhini kutoka kwa walii wa maiti kwa ajili ya kumuandaa maiti. [21] Kwa uoni na mtazamo wa mafakihi ni kwamba, sharti hili halikinzani na kuwa Wajib Kifai (wajibu ambaoe ukifanywa na baadhi unaowaondokea wengine) suala laa kumuandaa maiti. [22]
  • Kama watoto wote wa maiti watakuwa ni makafiri suala la Uwalii wao kuhusiana na kuombwa idhini ya kumuandaa maiti hautakuweko (utaondoka) na ni wajibu kwa Waislamu kutekeleza jukumu hilo. [23]
  • Kwa mujibu wa Sahib Riyadh (aliaga dunia: 1231 Hijria), kama maiti atakuwa ameusia na kumtaja mtu wa kushughuulikia maandalizi yake asiyekuwa walii, kwa mujibu wa mtazamo ambao ni mashuhuri baina ya mafakihi ni kwamba, walii anaweza kumzuia wasii asiteketeze wasia. [24] Hata hivyo kwa mujibu wa fat'wa ya Sistani, [25] Makarim Shirazi [26] na Khamenei, [27] ni vyema kuchukua idhini kutoka kwa walii; na walii ampatie idhini mhusika.
  • Gharama za kumuandaa maiti zinapaswa kutolewa kutoka katika mali ya asili ya maiati na hilo lifanyike kabla ya urithi kugawanywa. [28] Gharama za kumuandaa maiti zinapaswa kutangulizwa mbele ya madeni na kufanyia kazi wasia wa maiti. [29]
  • Kauli mashuhuri baina ya mafakihi ni kuwa, ni haramu kuchukua ujira mkabala wa kazi ya kumuandaa maiti kama kumuosha, kumkafini na kadhalika. [30] Hata hivyo Shahid al-Awwal katika kitabu chake cha al-Durus al-Shar'iyah amenukuu kutoka kwa Sayyid Murtadha kwamba, asiyekuwa walii anaweza kuchukua ujira wa kumuandaa maiti. [31]

Rejea

Vyanzo