Viungo vya sijda

Kutoka wikishia

Viungo vya Sijdah (Kiarabu: أعضاء السجدة أو المساجد السبعة) ni viungo au sehemu saba za mwili ambazo huwekwa chini au hukusa ardhi wakati wa kusujudu. Kwa mujibu wa mafaqihi wa Kishia, wakati wa kusujudu ni wajibu kuweka paji la uso, viganja vya mikono miwili, ncha za magoti na ncha za vidole vikubwa vya miguu viwe juu ya ardhi. Kuweka pua kwenye ardhi pia ni jambo linalopendekezwa.

Mafaqihi wengi wanaona kuwa katika kusujudu si wajibu kuweka viungo vyote ardhini; Bali yatosha viungo hivyo kugusana na ardhi japo kidogo tu. Bila shaka paji la uso limetengwa na kuvuliwa kutokana na hukumu hii. Baadhi ya mafaqihi wametoa fatwa za wajibu katika kuweka paji la uso chini kwa kiwango cha dirham moja ya uso wa mwenye kusujudu.

Pahala anapoweka paji lake la uso mwenye kusujudu wa kusali, ni lazima iwe ni ardhi yenyewe, au chenye kutokana na ardhi, kama vile kipande cha dongo au jiwe. Pia hairuhusiwi mtu kuweka paji lake la uso anaposujudu katika sala juu ya kitu chenye asli ya kuliwa au kuvaliwa.

Dhana juu ya viungo vya sijda

Viungo au washiriki saba wanaoshoriki katika kukamilisha sijda ni viungo saba vya mwili ambavyo ni wajibu viwekwe chini wakati wa kusujudu[1] navyo ni: Paji la uso, viganja vya mikono miwili, ncha au vichwa vya magoti na ncha za vidole gumba.[2] Mada hii inayohusiana na viungo vya sijdah hujadiliwa na kuchambuliwa katika vitabu maalumu vya fiqhi katika mlango wa swala[3]

Hukumu za viungo vya kusujudia

Baadhi ya hukumu za viuongo vya sijdah ni kama ifuatavyo:

  • Kwa mujibu wa mtazamo wa kielimu wa mwanasheria maarufu wa elemu ya fiqhi wa Kishia (aliyefariki mwaka 1186 Hijiria), ajulikanaye kwa jina la Yusuf Bahrani, ni kwamba; Kuweka viungo saba vya sijda chini wakati wa kusujudu ni suala la wajibu.[4]
  • Pia kwa mtazamo wake; Inatosha baina ya ardhi na viungo saba vya kusujudia kupatikana mguso mdogo tu - isipokuwa paji la uso -, yaani paji la uso yabidi kugusa ardhi kisawasawa.[5] Maoni ya baadhi ya baadhi ya mafakihi wengine ni kwamba; Mguso mdogo wa paji la uso na ardhi pia unatosha.[6] Kwa upande mwengine, kuna wanazuoni wasemao kuwa; Ni wajibu kugusisha paji la uso ardhini kwa kiwango cha dirhamu moja (yaani kiwango cha gwaru la dirhamu).[7]
  • Wakati wa kusoma dhikri za sijda, kukiondoa kwa makusudi kiungo kimoja kati ya hivyo saba kutabatilisha swala.[8] Kwa mujibu wa fatwa ya Ayatullah Sistani, mtu anayeswali hata akiwa hasomi dhikri za sijda, ikiwa ataondoa viungo vyake vya sijda kutoka ardhini kwa kwa hiari yake, basi swala yake itabatilika.[9]

Rejea

  1. Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh-i al-Islāmī, Musūʿa al-fiqh al-islāmī, juz. 15, uk. 108.
  2. Baḥrānī, al-Ḥadāʾiq al-nāḍira, juz. 8, uk. 276.
  3. Ṭabāṭabāʾī Yazdī, al-ʿUrwat al-wuthqā, juz. 1, uk. 176.
  4. Baḥrānī, al-Ḥadāʾiq al-nāḍira, juz. 8, uk. 276.
  5. Baḥrānī, al-Ḥadāʾiq al-nāḍira, juz. 8, uk. 277.
  6. Shahīd al-Thānī, Masālik al-ifhām, juz. 1, uk. 218.
  7. Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 10, uk. 144.
  8. Ḥillī, Taḥrīr al-aḥkām, juz. 1, uk. 40.
  9. Sīstānī, Tawḍīh al-masāʾil, juz. 1, uk. 224.

Vyanzo

  • Abū Ṣalāḥ Ḥalabī, Taqī al-Dīn b. Najm al-Dīn. Al-Kāfī fī al-fiqh. Isfahan: Maktaba Imām Amīr al-Muʾminīn (a), 1403 AH.
  • Baḥrānī, Yūsuf b. Aḥmad al-. Al-Ḥadāʾiq al-nāḍira fī aḥkām al-ʿitrat al-ṭāhira. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1363 Sh.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Taḥrīr al-aḥkām. Mashhad: Muʾassisat Āl al-Bayt, [n.d].
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Tadhkirat al-fuqahāʾ. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1414 AH.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Wasāʾil al-Shīʿa. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1416 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1387 sh.
  • Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh-i al-Islāmī. Musūʿa al-fiqh al-islāmī ṭibqan li madhhab Ahl al-Bayt(a). 1st edition. Qom: Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh-i al-Islāmī, 1423 AH.
  • Muḥaqqiq al-Karakī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Jāmiʿ al-maqāṣid fī sharh al-qawāʿid. 2nd edition. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1414 AH.
  • Najafī, Muḥammad al-Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. 7th edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1362 sh.
  • Sabziwārī, Sayyid Abd al-ʿAlī. Muhadhdhab al-aḥkām fī bayān al-ḥalāl wa al-ḥarām. 4th edition. Qom: Dār al-Tafsīr, 1413 AH.
  • Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. ʿAlī. Masālik al-ifhām ilā tanqīh sharāyiʿ al-Islām. 1st edition. Qom: Muʾassisat al-Maʿārif al-Islāmīyya, 1413 AH.
  • Sīstānī, Sayyid ʿAlī. Tawḍīh al-masāʾil. Qom: Intishārāt-i Mihr, 1415 AH.
  • Ṭabāṭabāʾī Yazdī, Muḥammad Kāẓim al-. Al-ʿUrwat al-wuthqā fīmā taʿummu bih al-balwā. 1st edition. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1417 AH.