Nenda kwa yaliyomo

Wajib Aini

Kutoka wikishia

Wajibu Aini (Kiarabu: الواجب العيني) (wajibu wa kila mtu) ni aina za wajibu za kidini ambazo mukallafu anapaswa kuzitekeleza yeye mwenyewe. Wajib Aini mkabala wake ni Wajib Kifai ambapo kwa kutekekeza baadhi ya mukallafin hakuna haja tena kwa watu wengine kutekeleza amali hiyo. Sala za kila siku, Saumu, Zaka, kuwatendea wema mama na mama na kuunga udugu ni katika Wajib Aini.

Maulamaa wa Usul al-Fiq’h wanasema, kama kutakuwa na shaka kwamba, wajibu huu ni aini au kifai, inapaswa kujengea kwamba, ni wajib aini.

Maana ya kifiq’h

Wajib Aini ni wajibu ambao ni wajibu kwa kila mukallaf kutekeleza; kwa maana kwamba, mukallaf hawezi kuacha kutekeleza taklifu yake kwa kisingizio kwamba, wengine washatekeleza.[1] Sala za kila siku, Saumu, Hija,[2] kuwawatendea wema baba na mama, kuunga udugu, kutekeleza ahadi na kutoa Zaka[3] ni katika wajibu ambazo ni Wajib Aini.

Tofauti yake na Wajib Kifai

Kadhalika angalia: Wajib Kifai

Wajib Aini iko mkabala wa Wajib Kifai ambapo mkusudiwa sio mtu maalumu; kwa maana kwamba, kwa mujibu sheria, kila ambaye atatekeleza hilo basi itatosheleza. Kwa msingi huo kwa kutekelezwa hilo na baadhi ya watu, wajibu kwa waliobakia huwaondokea;[4] kama vile kuamrisha mema na kukataza maovu, jihadi, kuitikia salamu,[5] kumkafini maiti, kuzika maiti, Sala ya maiti na kuokoa roho ya mtu.[6]

Kwa mujibu wa Maulamaa wa Usul al-Faqih, sababu ya kwamba, katika Wajib Kifai kwa kufanya na kutekeleza wajibu huo baadhi ya watu, huwaondokea wengine ni kwamba, amali hizo zenyewe ni nzuri na zinazofaa na kuna umuhimu wa kuzitekeleza na sio kwamba, ni nani anaifanya kazi na taklifu hiyo.[7]

Kuainisha Wajib Aini na Kifai

Maulamaa wa elimu ya Usul-Fiq’h wanasema kuwa, katika maeneo ambayo hatuna hoja kwamba, amri hii ya Mwenyezi Mungu ni wajib ain au kifai, tunapaswa kujengea kwamba, ni wajib aini;[8] kwani akili inahukumu kwamba, wakati hatuna uhakika kwamba, kutekelezwa amri ya Mwenyezi Mungu na watu wengine hilo halitapelekea jukumu hilo kutuondokea, bali tunapaswa kulitekeleza hilo wenyewe.[9]

Rejea

  1. Muzaffar, Uṣūl al-fiqh, juz. 1, uk. 140; Ḥusaynī, al-Dalīl al-fiqhī, uk. 301; Wilāʾī, Farhang-i tashrihi-yi iṣṭilaḥāt-i uṣūl, uk. 336.
  2. Ḥusaynī, al-Dalīl al-fiqhī, uk. 301.
  3. ʿAjam, Mawsūʿa muṣṭalaḥāt uṣūl al-fiqh ʿind al-muslimīn, juz. 2, uk. 1690.
  4. Muzaffar, Uṣūl al-fiqh, juz. 1, uk. 140; Ḥusaynī, al-Dalīl al-fiqhī, uk. 3091; Wilāʾī, Farhang-i tashrihi-yi iṣṭilaḥāt-i uṣūl, uk. 337.
  5. ʿAjam, Mawsūʿa muṣṭalaḥāt uṣūl al-fiqh ʿind al-muslimīn, juz. 2, uk. 1690.
  6. Muzaffar, Uṣūl al-fiqh, juz. 1, uk. 140.
  7. Muzaffar, Uṣūl al-fiqh, juz. 1, uk. 140-141.
  8. Muzaffar, Uṣūl al-fiqh, juz. 1, uk. 124-125; Ākhund Khurāsānī, Kifāyat al-uṣūl, uk. 252; Subḥānī, al-Wasīṭ fī uṣūl al-fiqh, juz. 1, uk. 100.
  9. Muzaffar, Uṣūl al-fiqh, juz. 1, uk. 124-125.

Vyanzo

  • Ākhund Khurāsānī, Muḥammad Kāẓim. Kifāyat al-uṣūl. 1st edition. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1409 AH.
  • ʿAjam, Rafīq, al-. Mawsūʿa muṣṭalaḥāt uṣūl al-fiqh ʿind al-muslimīn. Beirut: Maktabat Lubnān Nāshirūn, 1998.
  • Ḥusaynī, Muḥammad. Al-Dalīl al-fiqhī ṭaṭbīqat fiqhiyya li muṣṭalaḥāt ʿilm al-uṣūl. 1st edition. Damascus: Markaz-i Ibn Idrīs Ḥillī li-l-Dirāsāt al-fiqhiyya, 2007.
  • Muzaffar, Muḥammad Riḍā al-. Uṣūl al-fiqh. 5th edition. Qom: Intishārāt-i Islāmī, 1430 AH.
  • Subḥānī, Jaʿfar. Al-Wasīṭ fī uṣūl al-fiqh. 4th edition. Qom: Muʾassisat al-Imām al-Ṣādiq, 1388 Sh.
  • Wilāʾī, Īsā. Farhang-i tashrihi-yi iṣṭilaḥāt-i uṣūl. 6th edition. Tehran: Nashr-i Niy, 1387 Sh.