Kumkirimu mgeni

Kutoka wikishia

Kumkirimu mgeni (Kiarabu: الضيافة) ni katika mila na ada za Waislamu. Waislamu hufanya sherehe na kualika watu katika hafla mbalimbali kama Eid al-Fitr, Eid al-Ghadir, sherehe ya ndoa, kuruzukiwa mtoto, na kupata nyumba. Mtume (s.a.w.w) anamchukulia mgeni kuwa ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye kwa kufika kwake huja na riziki yake na kwa kuondoka kwake hupelekea kupatikana msamaha wa dhambi.

Kumhudumia mgeni, kuwa na adabu na tabia njema na mgeni na kuepuka kuchanganyika maharimu na wasio maharimu katika ugeni ni miongoni mwa adabu za kuwa mwenyeji. Mgeni pia anastahili kukubali mwaliko wa mwenyeji na kutoleta mtu yeyote ambaye hajaalikwa kwenye karamu pamoja naye na kutokaa katika nyumba ya mwenyeji kwa zaidi ya siku tatu.

Mafakihi wa Shia wanaona kuwa ni wajibu kumtolea Zakat al-Fitr mgeni katika usiku wa Eid al-Fitr ikiwa anahesabiwa kuwa mlezi na amefika katika nyumba ya mwenyeji kabla ya kuzama kwa jua. Miongoni mwa hukumu nyingine zinazohusiana na ugeni, ni kuwa haramu kukaa katika meza ambayo kuna pombe na kilevi.

Umuhimu, Fadhila na Nafasi

Wanachuoni wa Kiislamu wanaona kuwa, kumkirimu mgeni ni kufuata sunna ya Mtume wa Uislamu [1] na wakitegemea hadithi, wanaona kuwa ni makuruhu kuacha kufanya hivyo. [2] Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) anamchukulia mgeni kuwa ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye kwa kufika kwake huja na riziki yake na kwa kuondoka kwake hupelekea kupatikana msamaha wa dhambi. [3] Allama Majlisi, katika kueleza mapenzi ya Ali bin Abi Talib (a.s) katika kumkirimu mgeni, anasimulia kwamba alionyesha kutoridhika kwake kutokana na kupita siku saba ilihali hakuna mtu aliyeingia nyumbani kwake kama mgeni. Yaani kupita siku saba bila kupata mgeni. [4]

Imamu Ali (a.s) amesema:

«Kila atakayemkirumu mgeni, bila shaka amekirimu Mitume sabini na kila ambaye atagharamika kwa dirihamu moja kwa ajili ya mgeni ni mithili ya aliyetoa dirihamu 1000 katika njia ya Mwenyezi Mungu.».[1]

Waislamu hufanya sherehe na kualika watu katika hafla mbalimbali kama Eid al-Ghadir, [6] Eid al-Fitr, [7] sherehe ya ndoa, kuruzukiwa mtoto, na kupata nyumba. [8] Wananchi wa Iran wanatoa kipaumbele juu ya suala la kuwakirimu wageni katika sherehe ya Nairuzi [9] na wananchi wa Iraq wanazingtatia sana suala la kuwakirimu wageni katika Matembezi ya Arubaini. [10]

Adabu

Katika hadithi za Kiislamu, vitabu vya maadili na baadhi ya vitabu vya kufasiri, pamoja na nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu [11] na kuwa makini na unafiki na kujionyesha [12]. Imamu Swadiq (a.s) amesema: Kila ambaye atamlisha muuumini mpaka akashiba (atampatia chakula) hakuna kiumbe katika viumbe vya Mwenyezi Mungu ambaye anafahamu ujira wa mtu huyo; si malaika muqarrab (walio na daraja ya juu) wala Mtume aliyebaathiwa isipokuwa Mola Muumba wa ulimwengu. [13] Kwa hakika kumebainishwa adabu za kufanya karamu na kualika wageni, ambazo baadhi yake zinahusiana na mwenyeji na zingine zinahusiana na mgeni:

Adabu za Mwenyeji

  • Ni bora kualika watu wanaotenda mema kuliko watu waovu; [14]
  • Awaalike ndugu na jamaa pia ili kuimarisha mahusiano ya kifamilia na kusaidia kuunga udugu. [15]
  • Kujiepusha kujitia katika dhiki, usumbufu na gharama kubwa. [16]
  • Kuwa bashasha na kudumisha maadili mema na tabia njema kwa mgeni. [17
  • Kujiepusha kumchanganya mgeni na familia (kama mgeni sio maharimu). [18]
  • Kutomuuliza mgeni umekula chakula au bado. [19]
  • Chakula kiwepo cha kutosha (kisiwe kidogo). [20]
  • Mgeni awe wa kwanza kula na awe wa mwisho kuacha kula. [21]
  • Kutomtumikisha mgeni. [22]
  • Kukumbusha wakati wa Sala; [23] kumuonyesha kibla na kumuonyesha sehemu ya kutilia udhu. [24]
  • Kumsindikiza mgeni mpaka mlangoni. [25]

Adabu za Kuwa Ugenini

  • Kukubali mwaliko wa mwenyeji. [26]
  • Kutokubali ugeni kwa ajili tu ya kula na kujaza tumbo. [27]
  • Mgeni aingie nyumbani kwa idhini ya mwenyeji wake; [28] na asalimie. [29]
  • Kukaa sehemu ambayo mwenyeji wake amemuainishia. [30]
  • Kutokaa upande ambao anawaelekea wanawake. [31]
  • Haifai kushiriki katika mwaliko ambao unaaambatana na kutenda dhambi. [32]
  • Tufupishe muda wa kuwa ugenini na tusikae kwa zaidi ya siku tatu. [33]
  • Chakuka kikiwa tayari tukubali kula. [34]
  • Kutofunga Saumu ya mustahabu bila ya ridhaa ya mwenyeji au kama atatukataza kufanya hivyo. [35]
  • Kujiepusha kudasisi kuhusiana na uhalali wa chakula. [36]
  • Tusibebe chakula isipokuwa kwa idhini ya mwenyeji wetu. [37]
  • Tuweke sharti kwamba, mwenyeji asijisumbue kwa ajili yetu na aweke kando mambo ya starehe na ambayo sio ya lazima. [38]
  • Tusiende katika mwaliko na mtu ambaye hajaalikwa. [39]
  • Ni vyema kuondoka ugenini kwa idhini ya mwenyeji. [40]
  • Tuondoke ugeni kwa bashasha na tabasamu hata kama mwenyeji hakutufanyia kama inavyostahiki. [41]

Hukumu za Kifiq’hi

Mafakihi wametaja hukumu mbalimbali za kisheria kuhusiana na ugeni na mwaliko na baadhi yazo ni:

  • Kwa mujibu wa fat’wa za baadhi ya Marajii Taqlidi ni kuwa: Kama mgeni atagundua kwamba, kile alichoandaliwa na mwenyeji wake hakikutolewa khumsi, haifai kukitumia. [42]
  • Zakat al-Fitr ya mgeni aliyewasili katika nyumba ya mwenyeji wake kabla ya kuzama jua ni jukumu la mwenyeji wake. [43]
  • Kwa mujibu wa fat’wa za baadhi ya mafakihi wa Kishia ni kuwa, kama sehemu fulani katika nyumba au busati kuna najisi na najisi hiyo imeingia katika nguo ya mgeni, ni wajibu kwa mwenyeji kumjulisha hilo mgeni wake. [44]
  • Sayyid Kadhim Yazdi anasema: Kama chakula alichoandaliwa mgeni na mwenyeji wake kimenajisika inapaswa kumjuza mgeni. [45]
  • Ni haramu kukaa katika kitanga cha chakula ambacho kumetengwa pia pombe na mvinyo. [46]

Monografia

Kumeandikwa vitabu mbalimbali kuhusiana na kumkarimu mgeni na adabu zinazohusiana na hilo. Miongoni mwavyo ni Farhangnameh Mehmani kilichoandika na Muhammad Muhammadi Reyshahri ambacho kimechapishwa na Taasisi ya Kielimu ya Kiutamaduni ya Dar al-Hadith. [47]

Rejea

  1. Dailam, Irshad al-Qulub, 1371, juz. 1, uk. 138.

Vyanzo