Manii
- Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine.
Manii (Kiarabu: المنيّ) ni maji meupe na mazito ambayo kutoka kwake katika utupu hufanya kuoga janaba kuwa wajibu. Kwa mujibu wa fat'wa za mafakihi wa Kishia na baadhi ya mafakihi wa Ahlu-Suna, manii ni najisi. Kutoka manii kwa hiari (wakati wa mchana) hubatilisha Swaumu. Kadhalika mtu ambaye ametokwa na manii anapaswa kuoga janaba ili aweze kuswali na kufanya ibada nyingine ambazo zinalazimu kuoga janaba. Baadhi ya dalili na ishara za manii ambazo kama mtu ataingiwa na shaka basi kupitia njia zifuatazo inawezekana kuainisha kwamba, ametokwa na manii ambazo ni: kufikia kilele cha raha ya hali ya juu wakati wa kufanya mapenzi, kutoka kwa hali ya kuchupa(kuruka) na kulegea mwili.
Kuna hukumu mbalimbali zinazohusiana na manii (shahawa) ambazo zinazongumziwa katika masuala mpya (Masail Mustahdatha) ya fiq'hi. Kwa mujibu wa mafakihi wa Kishia kutia manii kwa njia ya sindano kwa mwanamke ambaye mwenye manii hayo sio mumewe ni haramu. Ama kuhusiana na manii yaliyotolewa kwa mwanaume kisha yakahifadhiwa na kisha kutiwa katika kizazi cha mkewe baada ya yeye (mwanaume) kufariki, mafakihi wametofautiana kinadharia na kimtazamo. Hitilafu hii ya kimitazamo inarejea katika msingi wa kwamba, je, kwa kufa mume au mke, suala la kwamba, ni wanandoa linaondoka au libakia? Kwa maneno mengine ni kwamba, akifa mume au mke, bado wawili hawa wanahesabiwa kuwa ni mke na mume. Kadhalika kuna hitilafu za kimitazamo kuhusiana na suala la kuuza na kununua manii.
Utambuzi wa Maana
Manii ni maji ambayo kwa namna fulani ni mazito na kwa kiwango fulani ni meupe[1] , ambayo kikawaida hutoka baada ya kufikia kilele cha raha ya hali ya juu wakati wa kufanya mapenzi, na hutoka katika utupu wa mbele wa mwanaume.[2] Kazi yake ni kubeba kromosomu zenye taarifa za jenetikia (yaani sifa za mwili inakotoka) na kupitia mfuko wa uzazi wa mwanamke huingia ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye ovari amabapo mayai hupatika huko. Kuingia kwa spermatozoo ndani ya yai kunasababisha ungano la ADN ya yai na spermatozoo na mgawanyo wa yai ambalo ni chanzo cha kiumbehai mpya.
Hukumu ya Kifiqh
Kwa mujibu wa fat'wa ya wanazuoni na mafakihii wa Kishia, manii ya mwanadamu ni najisi.[3] Wanakiita kitendo cha kutoa manii katika mwili kwamba, ni kumwaga shahawa[4] Katika fiqh kumwaga shahawa kunasababisha janaba (mtu kutokuwa tohara mpaka aoge janaba).[5] Muhammad Hussein Najafi mmoja wa mafakihi wa Kishia anasema kuwa, manii ya wanyama ambao wana damu ya kuruka (kuchupa) nayo ni najisi.[6]
Mtu ambaye ametokwa na manii, anapaswa kuoga ili aweze kufanya mambo yanayohitajia tohara kama kuswali na kadhalika.[7] Kujitoa manii kwa makusudi (iwe ni kwa kufanya tendo la ndoa au kujichua) kunabatilisha Swaumu.[8]
Mtazamo wa Ahlu-Sunna
Mafakihi na wanazuoni wa Ahlu-Sunna hawana mtazamo mmoja kuhusiana na kuwa au kutokuwa najisi manii. Abu Hanifa na Malik bin Anas mtazamo wao ni kwamba, manii ni najisi;[9] kwa tofauti hii kwamba, Abu Hanifa anaamini kuwa, kama manii yatakauka basi husafika na kutoharika kwa kusugua sehemu yenyewe na kusagasaga na hivyo hakuna haja ya kuosha kwa maji.[10] Madhehebu ya Shafi[11] na Hambal mtazamo wao ni kwamba, manii ni tohara.[12]
Ishara na Dalili za Manii
Katika fiq'h kumebainisha ishara za kutoka manii endapo mtu ataingiwa na shaka kwamba, ametokwa na manii au la. Kwa msaada wa ishara hizi inawezekana kufikkia natija kwamba,, ni manii au la. Kwa mujibu wa mtazamo wa mafakihi wa Kishia wengi ni kwamba; kutokwa na manii mwanaume kunaambata na sifa tatu, ladha ya mapenzi, kuchupa (kutoka kwa namna ya kurukaruka) na mwili kulegea.[13] Hata hivyo kwa mgonjwa kuchupa (kuruka) sio sharti, kwa kutoka maji yakiambatana na shahawa na kulegea mwili huwa na hukumu ya manii.[14]
Baadhi ya mafakihi wamesema: Kutoka maji katika mwili kama kutaambatana na ladha ya mapenzi na kuchupa au kukaambatana na kuchupa na mwili kulegea hayo ni manii.[15]
Kwa wanawake ishara na dalili za mani ni tofauti. Kwa mtazamo wa mafakihi wengi wa Kishia ni kwamba, vimajimaji vinavyotoka katika uke na utupu wa mwanamke, kama vitaambatana na ladha ya mapenzi basi vina hukumu ya manii. Kuruka na kulegea mwili kwa wanawake sio ishara za manii.[16]
Tofauti ya Madhii(المذي), Wadhii(الوذي) na Wadii(الودي)
Mafakihi wanatofautisha baina ya manii na majimaji mengine yanayotoka katika utupu. Mbali na manii wanataja aina nyingine tatu za maji yanayotoka katika utupu.:
- Madhii: Haya ni maji mepesi ambayo hutoka katika utupu wa mtu kutokana na athari ya ladha na kuburudikka kimapenzi au kuchezeana na kutomasana.[17] Maji haya yananata lakini hayana ishara wala dalili za manii na kwa wanawake ni mengi zaidi kuliko kwa wanaume.[18]
- Wadhii: Ni maji mepesi ambayo baadhi ya wakati hutoka baada ya kutoka manii.[19]
- Wadii: Ni maji ambayo baadhi ya wakati humtoka mtu baada ya kukojoa.[20]
Kwa mujibu wa mafakihi wa Kishia ni kwamba, madhii, wadhii na wadii sio najisi[21] na wala hayabatilishi udhu. [22]
Rejea
- ↑ تفاوت تعاریف طبی و فقهی در مورد مایع منی، Site Tibyan.
- ↑ Abdurrahman, Mu'jam al-Mus'twalahat wa al-Alfadz al-Fiqhiyah, juz. 3, uk. 369
- ↑ Najafi, Jawāhir al-Kalām, juz. 3, uk. 3; Sayyied Murtadha, al-Intishār, uk. 96-97
- ↑ Najafi, Jawāhir al-Kalām, juz. 5, uk. 290
- ↑ Najafi, Jawāhir al-Kalām, juz. 5, uk. 290; Sayyied Murtadha, al-Intishār, uk. 95
- ↑ Najafi, Jawāhir al-Kalām, 1404 H, juz. 5, uk. 290
- ↑ Khomeini, Tahrir al-Wasila, Na'shir: Muasase tandhim wa nashir athar Imam Khomeini (r.a), juz. 1, uk. 39.
- ↑ Tazama: Bahrani, al-Hadaiq al-Nadhwirah, 1405 H, juz. 19, uk. 129-130.
- ↑ Jaziri, Fiqh Alal-Madhahib al-Arba, 1424 H, juz. 1, uk. 15; Sayyied Murtaza, Al-Intiswar, 1415 H, uk .96.
- ↑ Sayyied Murtaza, Al-Intiswar, 1415 H, uk. 96.
- ↑ Shafi'i, Ahqam al-Qur'an, Dar al-Kutub al-ilimiyah, uk. 81-82.
- ↑ Jaziri, Fiqh Alal-Madhahib al-Arba, 1424 H, juz. 1, uk. 15, rejea no. 3; Sayyied Murtaza, Al-Intiswar, 1415 H, uk. 96.
- ↑ Najafi, Jawahar al-Kalam, 1404 H, juz. 3, uk. 8.
- ↑ Najafi, Jawahar al-Kalam, 1404 H, juz. 3, uk. 12.
- ↑ Bani Hashemi Khomeini, 1392 H, juz. 1, uk. 265.
- ↑ Najafi, Jawahir al-Kalam, 1404 H, juz. 3, uk. 13; Tazama: Bani Hashimi Khomeini, 1392 H, juz. 1, uk. 265 na 266.
- ↑ Najafi, Jawahir al-Kalam, 1404 H, juz. 1, uk. 411.
- ↑ Amili, Al-Istlahat al-Faqih, 1413 H, uk. 196.
- ↑ Amili, Al-Istlahat al-Faqih, 1413 H, uk. 229; Najafi, Jawahir al-Kalam, 1404 H, juz. 1, uk. 415
- ↑ Amili, Al-Istlahat al-Faqih, 1413 H, uk. 229.
- ↑ Tazama: Makarim Shirazi, Risaleh Tawdhih al-Masail, 1429 H, uk. 31.
- ↑ Tazama: Sayyied Murtaza, Al-Intiswar, 1415 H, uk. 119; Najafi, Jawahir al-Kalam, 1404 H, juz. 1, uk. 414.
Vyanzo
- Amili, Yasin 'Isa. al-Ishthilāhāt al-Fiqhiyah fi al-Rasāil al-'Ilmiah. Beirut: Dar al-Balaghah, 1413 H.
- Abdurrahman, Mahmud. Mu'jam al-Mus'talahāt wa al-Alfāddh al-Fiqhiyah.
- Bahrani, Yusuf Ibnu Ahmad. Al-Hadāiq al-Nādhirah fi Ahkām al-'Itrah al-Thāhirah. Editor: Muhammad Taqi Irwani dan Sayid Abdurrazaq Muqrim. Qom: Daftar Intisharat Islami dibawah asuhan Jami'ah Mudarrisin Hauzah 'Ilmiah Qom, 1405 H
- Bani Hashimi Khomeini, Sayyied Muhammad Hassan. Taudhih al-Masāil Marāji' Mathābiq ba Fatāwāi Sanzdah Nafar az Marāji' Mu'adzham Taqlid (Penjelasan berbagai masalah menurut fatwa 16 ulama Marja Taklid). Qom: Daftar Intisharat Islami, 1392 HS.
- Jazairi, Abdurrahman bin Muhammad 'Audh. Al-Fiqh 'ala al-Madzāhib al-'Arbah. Beirut: Dar al-Kutub al-'Ilmiah, 1424 H/2003.
- Makarim Shirazi, Nashir. Risālah Taudhih al-Masāil. Al-Intisahrat Madrasah Imam Ali bin Abi Talib as, 1429 H.
- Najafi, Muhammad Hassan. Jawāhir al-Kalām fi Sharh Sharāi' al-Islam. Mhariri: Abbas Quchani dan Ali Akhundi. Beirut: Dar Ihya al-'Arabi, 1404 H.
- Sayyied Murtadha, Ali bin Hussein. Al-Intishār fi Infarādāt al-Imamiyah. Qom: Daftar Intisharat Islami di bawah asuhan Jami'ah Mudarrisin Hauzah Ilmiahm Qom, 1415 H.
- Shafi'i, Muhammad bin Idris. Ahkām Alquran. Beirut: Dar al-Kutub al-'Ilmiah.