Nenda kwa yaliyomo

Bishr bin Ghalib al-Asadi

Kutoka wikishia

Bishr bin Ghalib al-Asadi (Kiarabu: بشر بن غالب الأسدي) (Hai: 66 Hijiria) alikuwa mmoja wa masahaba wa maimamu wa Kishia na mmoja wa wapokezi wa Hadithi. Pamoja na kaka yake, amepokea dua ya Arafa kutoka kwa Imamu Hussein (a.s). Vile vile alikutana na Imam wa Tatu wa Mashia wakati wa safari yake kutoka Makka kuelekea Iraq kwenye makazi ya Dhat Iraq, na Hussein bin Ali (a.s) alipouliza kuhusu hali ya Iraq, alijibu kwamba nyoyo za watu ziko pamoja nawe, lakini panga zao ziko kwa Bani Umayya.

Bishr bin Ghalib al-Asadi hakuwepo katika tukio la Ashura, ingawa baadaye alionyesha majuto kwa kutofuatana na Imamu Hussein (a.s).

Utambulisho jumla

Bishr bin Ghalib al-Asadi Kufi kuniya yake ni Abu Sadiq [1] alikuwa mtoto wa mmoja wa masahaba wa Mtume, Ghalib bin Bishr Asadi [2] na alikuwa anatoka katika kabila la Bani Asad. [3] Katika vyanzo vya historia hakujaashiriwa mahali alipozaliwa. [4]

Mwandishi wa Kishia Ahmad bin Muhammad Barqi (aliyefariki mwaka 280 Hijiria) alimchukulia Bishr kuwa mmoja wa maswahaba wa Mtume (s.a.w.w). [5] Kadhalika Sayyid Muhsin Amin (aliyeaga dunia 1371 Hijiria katika A’yan Shia pia akinukuu kutoka kwa Ibn S’ad mwandishi wa kitabu cha Tabaqat al-Kubra amemtambua Bishr kuwa mmoja wa masahaba ambaye alihajiri na kwenda huko Kufa. [6]

Katika baadhi ya vyanzo vya kihistoria, mtu mmoja aitwaye Bishr bin Ghalib anatajwa kuwa mmoja wa makamanda wa jeshi la Hajjaj bin Yusuf katika vita na Makhawarij [7] ambaye aliuawa katika vita hivyo mwaka wa 76 Hijiria. [8] Hata hivyo katika baadhi ya vyanzo vya elimu ya Rijaal kunatajwa watu wawili kwa jina la Bishr bin Ghalib al-Asadi [9] Na hakuna hoja na sababu kwamba mtu huyu awe ni Bishr, mtu yule yule maarufu (kaka yake Bishr bin Ghalib).

Mpokezi wa hadithi

Ahmad bin Muhammad al-Barqi (aliyefariki 280 Hijiria) na Sheikh Tusi (aliyefariki 460 Hijiria), miongoni mwa waandishi wa wapokezi wa hadithi wa Kishia, wamemtambua Bishr bin Ghalib kuwa ni mmoja wa masahaba na wapokezi wa Maimamu (a.s), lakini hawakutoa maelezo yoyote kuhusu maisha yake. [10] Sheikh Tusi alimuashiria tu Asadi kuwa alikuwa ni mtu wa Kufa na kumtambua kama mmoja wa wapokezi wa hadithi na masahaba wa Imamu Hussein (a.s) [11] na Imam Sajjad (a.s). [11] Kadhalika al-Barqi mbali na kutaja jina lake katika orodha ya masahaba wa Imam Hassan (a.s), Imamu Hussein na Imamu Sajjad (a.s), amemhesabu kuwa, ni mmoja wa masahaba wa Imam Ali (a.s), aliyeishi Kufa. [13]

Kuna hadithi na riwaya nyingi zimepokewa kutoka kwa Bishr bin Ghalib katika vitabu vya hadithi na visivyokuwa vya hadithi katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwapenda Ahlul-Bayt (a.s), [14] Tafsir, [15] thawabu za kusoma Qur’an [16] na habari za kudhihiri Qaim (Imamu Mahdi) [17]. Akiwa pamoja na kaka yake Bishr bin Ghalib, amenukuu dua ya Arafah kutoka kwa Imamu Husein (a.s). [18]

Madhehebu na uaminifu

Kwa mujibu wa baadhi ya watafiti, hakuna maelezo ya wazi kuhusiana na madhehebu ya Bishr bin Ghalib miongoni mwa wataalamu wa elimu ya hadithi. [19] Hata hivyo, Abdullah Mamaqani, mwandishi wa wasifu wa wapokezi wa hadithi wa Kishia (aliyefariki 1351 Hijiria), mbali na kuashiria kutofahamika hali ya Bishr, alimchukulia kuwa mfuasi wa madhehebu ya Shia Imamiyyah. [20] Sayyid Mohsen akitegemea kile kilichohusishwa na Muhammad Bin Umar Kashshi, mwanachuoni wa Kishia katika karne ya nne, anamtaja kuwa ni alimu, mwenye fadhila na mwema mno. Anaongeza kwa kusema, maneno haya hayapo katika kitabu cha Rijal Kashshi na kimsingi maneno kama ma haya hayatoki kwa wanazuoni waliotangulia katika kuelezea uaminifu wa mtu na hivyo hayawezi kutoka kwa mtu kama al-Kashshi na aina ya maneno kama haya ni ya wanazuoni waliokuja baadaye. [21] Hata hivyo, kwa kutegemea umashuhuri wa dua ya Arafa inaelezwa kuwa, yeye ni mpokezi wa hadithi wa kuaminika.[22]

Kukutana na Imamu Hussein (a.s)

Bishr bin Ghalib alikutana na Imamu Husein (a.s) alipokuwa akitoka Makka kuelekea Iraq katika eneo la Dhat Iraq. [23] Hussein bin Ali (a.s) alimuuliza kuhusu hali ya Iraq. Akajibu kwamba nyoyo zao ziko kwako, lakini panga zao ziko kwa Bani Umayyah. Imamu alisadikisha maneno yake kwamba, Mwenyezi Mungu hufanya chochote anachotaka. [24]


Mazungumzo ya Imamu Hussein na Bishr bin Ghalib katika Dhat Iraq:

Imamu Hussein (a.s): Umewaona vipi watu wa Kufa?
Bish bin Ghalib: Nyoyo zao ziko na wewe, lakini panga zao zipo pamoja na Bani Umayya.
Umesema kweli ndugu Asadi! Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo na anaamuru apendavyo. [25] Kabla yake, Farzadaq alimwambia Imamu Hussein (a.s) maneno haya haya katika nyumba ya Safah.


Bishr bin Ghalib pia alinukuu mazungumzo kati ya Imamu Husein (a.s) na Ibn Zubair, ambamo Imamu wa tatu wa Mashia alieleza sababu ya safari yake ya kwenda Iraq. [26]

Bishr hakuwepo katika tukio la Karbala, [27] lakini Ibn Sa’d katika kitabu chake Tabaqat al-Kubra anaamini kwamba baada ya tukio la Ashura alikwenda kwenye kaburi la Imamu Husein (a.s) na akaeleza masikitiko na majuto yake kwa kutokuwa pamoja na Imamu Hussein (a.s). [28]

Bishr alikwenda Madina pamoja na Minhal bin Amr wakati wa harakati ya Mukhtar mwaka wa 66 Hijiria na alikuwepo wakati wa mazungumzo ya Imam Sajjad (a.s) na Minhal kuhusu Harmala bin Kahil Asadi. [29] Kadhalika licha ya mwanzoni kufuatana na Mukhtar, baadaye alisimama dhidi yake na hivyo Mukhtar al-Thaqafi akamfunga jela. [30]

Rejea

Vyanzo

  • Abū ʿAlī Miskawayh, Aḥmad b. Muḥammad. Tajārub al-umam. Edited by Abu l-Qāsim Imāmī. Tehran: Surūsh, 1379 Sh.
  • Abu al-Shaykh, Abd Allah b. Muhammad. Tabaqat al-muḥaddīthīn bi Isbahan wa al-waridin 'alayha. 2nd edition. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1412 AH.
  • Amīn, al-Sayyid Muḥsin al-. Aʿyān al-Shīʿa. Edited by Ḥasan Amīn. Beirut: Dār al-Taʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1403 AH.
  • Barqī, Aḥmad b. Muḥammad. Kitāb al-maḥāsin. Qom: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1371 AH.
  • Barqī, Aḥmad b. Muḥammad. Kitāb al-Rijāl. Tehran: Intishārat-i Dānishgāh-i Tehran, 1342 Sh.
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Mīzān al-iʿtidāl. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Maʿrifa li-ṭibaʿat wa al-Nashr, 1382 AH.
  • Group of authors. Maʿa al-rakb al-Ḥusaynī. Qom: Taḥsīn, 1386 Sh.
  • Ḥākim al-Ḥaskānī, ʿUbayd Allāh b. ʿAbd Allāh. Shawāhid al-tanzīl li-qawāʿid al-tafḍīl. Tehran: Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1411 AH.
  • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Muḥammad. Usd al-ghāba fī maʿrifat al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
  • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Abī l-Karam. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār Ṣādir, 1385 AH.
  • Ibn Aʿtham al-Kūfī, Aḥmad b. Aʿtham. Kitāb al-Futūḥ. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Aḍwaʾ, 1411 AH-1991.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Lisān al-mīzān. Edited by ʿAbd al-Fattāḥ Abū Ghada. [n.p]. Dār al-Bashāʾir al-Islāmiya, 2002.
  • Ibn Khaldūn, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad. Diwān al-mubtadaʾ wa l-khabar fī tārīkh al-ʿarab wa l-barbar. 2nd edition. Edited by Khalil Shahada. Beirut: Dār al-Fikr, 1408 AH.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Muḥammad Ṣāmil al-Silmī. 1st edition. [n.p]: Maktabat al-Ṣiddiq, 1414 AH/1993.
  • Kashshī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Ikhtīyār maʿrifat al-rijāl. Mashhad: Muʾassisa-yi Nashr-i Dānishgāh-i Mashhad, 1409 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Qom: Dār al-Ḥadīth li-ṭibaʿat wa al-Nashr, 1429 AH.
  • Mamaqānī, ʿAbd Allāh b. Ḥasan. Tanqīḥ al-maqāl fī ʿilm al-rijāl. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1431 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār al-jāmiʿa li-durar akhbār al-aʾimmat al-aṭhār. 2nd edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Shūshtarī, Muḥammad Taqī. Qāmūs al-rijāl. 2nd edition. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmiyya, 1410 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Amālī. 6th edition. Tehran: Kitābchī, 1376 Sh.
  • Ṣaffār, Muḥammad b. Ḥasan. Baṣāʾir al-darajāt fī faḍāʾil-i Āl-i Muḥammad. Edited by Muḥsin Kūchabāghī. 2nd edition. Qom: Kitābkhāna-yi Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-.Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. 2nd edition. Beirut: Dar al-Turāth, 1387 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Ghayba. Qom: Dār al-Maʿārif al-Islāmīyya, 1411 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥaasn al-. Al-Rijāl. 3rd edition. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1373 Sh.