Aya ya 142 ya Suratu Al-A'raf

Kutoka wikishia
Aya ya 142 ya Surat al-A'raf

Aya ya 142 ya Suratu Al-A'raf ( الآيَة 142 مِن سُورَةِ الأَعرَاف) ni Aya inayoeleza tukio ya miadi ya siku arubaini ya Nabii Musa (a.s) na Mola wake, ambapo alimchagua ndugu yake aitwaye Harun (a.s), kuwa ni mrithi wake na kumpa miongozo maalumu katika kutekeleza kazi za wadhifa huo. Kuna mambo kadhaa ya kiitikadi ya Kishia yanayo jadiliwa chini ya Aya hii. Miongoni mwa mambo hayo ni kama vile; Urithi wa Imamu Ali (a.s) wa kushika na nafasi ya ukhalifa, isma ya mitume, suala la Badā na ubora wa cheo cha Uimamu ukilinganisha na cheo cha Nabii. Pia, Khalwa au utawa wa siku 40 na swala ya siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah, ni miongoni mwa ibada zinazohusiana na Aya hii. Pia kuna tafsiri za kiroho (kiirfani au kisufi) za Aya hii zinaonekana katika kazi za wajuzi wa maarifa ya kiifani (kisufi). Miadi ya siku arubaini ya Musa (a.s), imekuwa ndiyo msingi wa utaratibu wa mwa masufi katika kukaa kwao khalwa (kuingia utawani).

Matini ya Aya na Tarjumi Yake

﴾وَوَاعَدْنَا مُوسَى ثَلاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً وَقَالَ مُوسَى لأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلاَ تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ﴿


Na tulimwekea Musa miadi ya nyusiku thelathini, na tukaikamilisha kwa nyusiku kumi zaidi. Hivyo muda uliowekwa na Mola wake ukatimia kuwa ni usiku arubaini. Na pale Musa alipotaka kuenda kwenye Mlima wa Tur, alimwambia ndugu yake Harun: "Kuwa mwakilishi kwnye umma wangu, na tenda ipaswavyo, na wala usifuate njia ya waharibifu.



(Suratu al-A'raf, Aya ya 142)


Kisa ya Aya

Kulingana na tafsiri za Qur’ani, ni kwamba; Musa (a.s) akiwa pamoja na kundi la viongozi wa Bani Israil alikwenda kwenye miadi ya siku thelathini baina yake na Mola wake, ambapo alimteua Harun (a.s) kuwa ni naibu wa kushia nafasi ya ukhalifa na uimamu wa kuwaongoza Bani Israil, huku akimpa maagizo maalum kuhusiana na nyadhifa za jukumu hilo. Hata hivyo, muda huo uliongezwa siku kumi nyengine na Mola wake, ambazo kwa mujibu wa wasomi wa tafsiri, siku kumi hizo zilisadifiana na siku kumi za mwanzo za mwezi wa Dhul-Hijjah, ambapo mwanzo wa miadi hiyo ilikuwa ni mwanzoni mwa mwezi wa Dhul-Qa'dah. [1]

Matumizi ya Kiitikadi

Kuna tafiti kadhaa zilizo fanywa zilizo egemea mgongo wa Aya hii. Miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja na; tafiti kuhusiana na Hadith ya Manzila, [2] kuhusiana na isma au utoharifu wa manabii, [3] ubora wa nafasi na cheo cha uimamu juu ya cheo cha unabii, [4] na pamoja na tafiti kuhusiana na imani ya Badā, [5] ambayo ni miongoni mwa masuala maalumu yanayohusiana na imani za Mashia.

Uimamu wa Imam Ali (a.s)

Wafuasi wa madhehebu ya Shia huitumia Hadithi ya Manzila, kama ni moja ya hoja za Uimamu wa Ali (a.s), ambayo kwa mujibu wake, bwana Mtume (s.a.w.w) alielezea nafasi na hadhi ya Imamu Ali (a.s) inalingana na nafasi ya Haruna mbele ya Musa. [6] Hivyo wao huitumia Hadithi hiyo ili kuthibitisha Uimamu wa Imamu Ali (a.s) baada ya Mtume (s.a.w.w), pamoja na hadhi na ubora wake juu ya masahaba wengine. [7] Aghalabu ya tafiti msingi juu ya “Hadithi ya Manzila”, zimefanyika chini ya Aya hii ianzayo kwa ibara isemayo: (وواعدنا ; Na tukamwekea miadi…) Hata Maamun Abbas ambaye ni khalifa wa Kiabbasi alitumia Aya hii na Hadith ya Manzilah ili kuthibitisha Uimamu wa Imam Ali (a.s). [8]

Kuna Hadithi fulani kutoka upande wa madhehebu ya Ahlu-Sunna isemayo kuwa; Kama Musa (a.s) angewaacha watu wake mikononi mwa Mwenye Ezi Mungu badala ya Harun (a.s), kama vile alivyofanya mama yake, ambapo alimkadhi hatima ya mwanawe mikononi mwa Mungu wake, basi bila watu wake wasingepawa na fina kama ile ya kuabudu ng’ombe n.k. [9] Kosa ambalo halikufanywa na Mtume Muhammad (s.a.w.w), badala yake -kulingana na imani za Ahlu-Sunna- yeye aliwaacha watu wake mikononi mwa Mwenye Ezi Mungu. [10] Wao wamedai madai hayo hali ya kwamba Uimamu wa Imam Ali (a.s) umethibitishwa na vyanzo vya uhakika na kupitia ushahidi wa wazi kutoka katika Qur'ani na Sunna, pamoja na vyanzo kadhaa vya historia. [11]

Je, Kule Harun Kutahadharishwa na Musa (a.s) ni Dalili ya Yeye Kutokuwa na Isma?

Wafasiri wa Shia, wakijibu pingamizi isemayo kwamba; Kule Haruna kutahadharishwa na Musa (a.s), kwa kumtaka kuto fuata njia ya mafisadi, kunaweza kuwa dalili ya yeye kutokuwa na isma (kutokuwa na dhambi), wamesema kwamba; Amri na makatazo hayo hayaoneshi kuwa Harun (a.s) alikuwa na nia ya kufanya hivyo, wala pia hayaoneshi kwamba yeye alikuwa na nia kuacha mwongozo mwema. [12] Badala yake, hapa kuna aina ya maalumu ya msisitizo kutoka kwa Musa (a.s), wenye nia ya kumuonesha Harna umuhimu wa nafasi yake (a.s) kati ya Bani Israil. [13] Zaidi ya hayo, kukatazwa kwa Harun katika hali hii kunaweza kuwa na maana ya kuwaelimisha Bani Israil. [14] Au kama alivyoeleza Sayyid Muhammad Hussein Tehrani, mmoja wa wanazuoni wa Shia, ya kwamba; Kukataza huku kunaonesha kuwa Harun (a.s) anapaswa kujiepusha na kushauriana na mafisadi wakati wa kutokuwepo kwa Musa (a.s). [15]

Jaribio (Mtihani) na Badā katika Kubadilishwa Miadi ya Musa (a.s)

Kubadilishwa miadi ya Musa (a.s) kutoka siku thelathini hadi siku arubaini, wakati katika Aya ya 51 ya Surat Al-Baqara siku hizo arubaini zimetajwa kama ni kipindi kimoja, kumezua tafsiri mbalimbali. Lakini kwa mujibu wa maoni ya Nassir Makarim Shirazi, mfasiri wa Shia, ni kwamba; Kile kinacholingana zaidi na maelezo ya Riwaya za Ahlul-Bayt (a.s) ni kwamba, ingawa kimsingi ahadi na miadi hiyo ilikuwa ni ya siku arubaini, ila Mweye Ezi Mungu alitaka kuwatahini (kuwajaribu) Bani Israil, hivyo basi awali alimwalika Musa (a.s) kwa ahadi ya siku thelathini, kisha akaiongeza tena siku 10, ili wanafiki wa Bani Israil waweze kujitenga na kudhihirisha uhalisia wao. [16]

Imam Baqir (a.s) ameeleza ya kwamba; kuabudu ndama kwa Bani Israil katika kipindi cha kutokuwepo kwa Musa (a.s), kulitokana na kule Musa (a.s) kutotimiza ahadi ya kurudi baada ya siku thelathini, [17] na katika Hadithi nyengine amesema kwamba; kubadilishwa kwa siku thelathini na kuwa arubaini, ilikuwa ni Badā (kughairi) kutoka kwa Mungu mwenyewe. [18]

Kwa maelezo zaidi, angalia pia: Ndama wa Sāmiri.

Ubora wa Cheo cha Uimamu juu ya Utume

Baadhi ya wafasiri wa Shia wanaamini kwamba; Aya ya وواعدنا au Wa Wā’adna”, inaashiria ubora wa cheo cha Uimamu juu ya Utume, kwa sababu kabla ya Harun (a.s) kuteuliwa na Musa (a.s) kuwa mrithi na Imamu wa Bani Israil, hapo mwanzo alikuwa na cheo cha Utume. Hii inaonyesha kwamba cheo cha Uimamu ni tofauti na cheo cha Utume na kwamba cheo cha Uimamu ni cha juu zaidi kuliko cheo cha Utume. [19]

Mafunzo Yanayohusiana na Chele Kiyahudi

Utawa wa Siku Arubaini

Kipindi cha siku arubaini cha kujitenga na ibada, kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa Dhul-Qā'da hadi siku ya kumi ya mwezi wa Dhul-Hijja, kinajulikana kama Chele Kiyahudi. Adabu na matendo maalum yameelezewa kwa ajili ya kipindi hiki. Kwa mujibu wa Abdullah Jawadi Amuli, katika kipindi hiki, Nabii Musa (a.s) hakuwa na usingizi wala chakula, na alikuwa akifanya maombi kwa Mungu katika mlima Sinai. Anasema kwamba kupitia Chele Kiyahudi, Taurati na ufunuo wa Mungu vilimjia Nabii Musa (a.s).

Sala ya Kumi la Mwanzo la Dhul-Hijja

Makala kuu: Sala ya Kumi la Manzo la Dhul-Hijja

Kulingana na Riwaya za Shia, katika siku kumi za kwanza za Dhul-Hijjah, kuna sala ya rakaa mbili inayojulikana kama ni Sala ya Kumi ya Dhul-Hijja, ambayo husaliwa kati ya sala ya Magharibi na Isha. Namna ya kuswali sala hii Kulingana na Riwaya kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), ni kwamba; katika kila rakaa moja, yatakiwa mtu kusoma Surat al-Fatiha na Suratu al-Ikhlas, kisha asome Aya ya «وواعدنا» (Wawādna) hadi mwisho wa Aya hiyo. [23]

Mafunzo ya Kiroho (Kiirfani au Kisufi)

Aya ya «وواعدنا» (Wawādna) imekuwa chanzo cha tafsiri nyingi za kiroho (Kiirfani au Kisufi). Kwa mfano, Meibudi, mwandishi wa tafsiri ya "Kashfu al-Asrar", ameeleza ya kwamba; kutoa ahadi na kufika kwa wakati kwenye, ni miongoni mwa nguzo za nyenyendo za madhehebu ya upendo (Kiirfan au Kisufi), na hata kama Mwenye Ezi Mungu hatotimiza ahadi yake, pia suala hilo huhisabiwa ni sawa na kutimiza ahadi hiyo, ndani ya silka za madhehebu hayo. [24] Yeye anaendelea kufafanua kwa kusema kwamba; Pale Nabii Musa (a.s) alipokuwa akimtafuta Khidhri, alishindwa kustahamili njaa ya nusu siku tu, ila katika safari hii ya siku arubaini akiongozana na Khidhri, katu hakukumbuka kula chakula wala kinywaji. [25] Kwa upande mwingine, pale Musa (a.s) alipokwenda kwa Firauni, alimuomba Mungu amsaidie kupitia Harun (a.s), ila alipokwenda kuonana na Mungu wake, alimuacha Harun (a.s) awe pamoja na watu wake, kisha akaenda kwa Mungu wake peke yake. [26] Meibudi anaamini kwamba; Musa (a.s) alikuwa na safari mbili: moja ilikuwa ni safari ya kumuombwa Mola wake huko Sinai, ambayo ni ya "Usiku wa Moto", ambapo Musa aliona moto ambao ulikuwa ni ishara ya Mola wake, na nyingine ilikuwa ni safari yenye tumbuizo la kwenda miadi ya kwenda kuonana na kipenzi chake (Mola wake). [27]

Wanairfani (wenye itikadi za Kisufi) wanaamini kwamba; Kwa mujibu wa Aya hii, yeyote atakayejitenga na watu kwa siku arubaini na kusafisha nia yake kutokana na mambo yasiyokuwa ya kiungu, Mwenye Ezi Mungu Mtukufu atamfungulia milango ya elimu moyoni mwake. [28] Suala la Nabii Musa (a.s) kujitenga kwa muda wa siku arubaini kwa kwenye mlima Sinai, [29] pamoja na Hadithi maarufu isemayo: "Mwenye kumsafia nia Mola wake kwa muda wa siku arubaini...", imekuwa ndio msingi wa jadi wa khalwa za Masufi. [30]

Abdullahi Jawadi Amuli, ambaye ni mfasiri wa Qur'ani, anasema kwamba; Khalwa (utawa) ya siku 40 uliorithiwa kutoka kwa Nabii Musa, ni miongoni mwa maagizo na uvumbuzi wa dini ya Kiislamu. [31] Pia, baadhi ya wanazuoni wa kiirfani (Kisufi) wa kisasa kama vile Hassan Hassanzadeh Amuli na Sayyid Muhammad Hussein Husseini Tehrani, wamewashauri baadhi ya watu kufanya kukaa khalwa ya siku 40 kwa ajili ya kupata utakaso pamoja na maendeleo ya kiroho. [32]

Rejea

Vyanzo