wikishia:Featured articles/2025
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani (Kiarabu: شهر رمضان المبارك) ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu ya Hijiria ambapo ndani yake Waislamu wamefaradhishiwa funga ya swaumu. Katika hadithi zimeelezwa fadhila mbalimbali za mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mwezi huu umetajwa kuwa ni mwezi wa kualikwa (kuwa katika ugeni) na Mwenyezi Mungu, mwezi wa rehema, maghufira, Baraka na machipuo ya Qur’ani. Kwa mujibu wa hadithi, katika mwezi huu milango ya mbinguni na ya peponi hufunguliwa huku milango ya motoni ikifungwa. Usiku wa cheo kitukufu ambapo Qur’ani ilishushwa ndani ya usiku huo, unapatikana katika mwezi huu. Baadhi ya vitabu vingine vya mbinguni kama Taurati na Injili pia vilishushwa ndani ya mwezi huu mtukufu. Ramadhani ndio mwezi pekee ambao jina lake limetajwa ndani ya Qur’ani.
Makala mengine yaliyoangaziwa: Asma bint Umais – Kisa cha kuzawadia pete – Harakati ya Khorasani