Abdallah seif Linganaweka

Kutoka wikishia

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka (2020 A.D) alikuwa ni mwanazuoni na Sheikh wa Kitanzania alie ingia Ushia na kuuweka waqfu umri wake wenye baraka kwa ajili ya kutangaza na kueneza Maktaba (njia) ya Ahlul-Bayt waliohifadhika na watoharifu (a.s) katika eneo la Afrika Mashariki, aliuweka waqfu umri wake kwa ajili ya kuwahudumia wafuasi wa maktaba yenye nuru katika nchi ya Tanzania na Msumbiji. Pia alikuwa ni miongoni mwa wanachama wa asili na wa mwanzo wa Jumuiyaa ya Ithna asharia Tanzania ijulikanayo kwa jina la (T.I.C) na hadi kufariki kwake dunia alikuwa Sheikh Mkuu wa jumuia hiyo.

Sheikh huyu alie ingia ushia, vivyo hivyo alifahamika kama mubalighi na muenezaji wa Ushia wa kweli na wa mwanzo katika nchi ya Msumbiji. Kwa hakika yeye aliuweka waqfu umri wake wa miaka kumi na mbili (12) kwa ajili ya kueneza na kutangaza Maktaba ya Ahlul-bayt (a.s) katika nchi hii, na katika muendelezo huo huo alianzisha tawi la taasisi ya kishia ya Bilal Muslim Mission katika nchi ya msumbiji. Abdallah seif alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa na mafungamano na majmaa Ahlul-baiti (a.s) na pia alikuwa na mafungamano mazuri sana na Allamah Sayyid Saidi Akhtar Rizvi na kutokana na mahusiano hayo ndio maana akawa na iitibari kwa mashia wa kikoja ithna ashariah na alikuwa ni mwenye kukubalika sana kwa watu hao. Sheikh Abdallah seif Linganaweka ni miongoni mwa wanazuoni wa mwanzo wa kiafrika ambao masomo yao ya kihawza waliyapata nje ya nchi ya Tanzania na alichukua muda mwingi katika masomo ya kihauza nje ya nchi.

Historia ya Maisha Yake

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka alie maarufu kwa jina la (Sheikh Abdallah Seif) alizaliwa mnamo mwaka 1939 A.D katika kijiji cha Mnang'ole katika mji wa Lindi mji uio kusini mwa pwani ya nchi ya Tanzania. Sheikh huyu kwa ajili ya kupata masomo ya kidini na kihawza alihamia katika mji wa Dar es Salaam mji mkuu wa Tanzania na kubakia hapo kwa muda takriban wa miaka kumi (10) na baada ya hapo akasafiri takriban miaka kumi na moja (11) katika nchi ya Iraq, Lebanon na Iran na mnamo mwaka 1980 A.D akarejea Tanzania.

Sheikh Abdallah Seif mnamo mwaka 1990 A.D alielekea katika nchi ya Msumbiji kwa ajili ya tablighi na uenezaji wa maktaba ya Ahlul-baiti (a.s) na baada ya takriban mika kumi na mbili (12) ya kuwa huko akaamua kurejea Dar es Salaam mji mkuu wa nchi ya Tanzania.

Kuna kitabu kimeandhikwa cha Sheikh Abdallah Seif chenye maudhui isemayo (Jasiri Sheikh Abdallah Seif Linganaweka) kilicho andikwa na Mustafa KhatibU Nkonga kwa lugha ya kiswahili.

Elimu Yake

Sheikh Abdallah Seif mnamo mwaka 1958 A.D alisafiri kuelekea katika mji wa Dar es Salaam mji mkuu wa Tanzania kwa ajili ya kujifunza masomo ya dini ya kiislaam. Na ili maisha yake yaweze kuendelea aliamua kuajiriwa katika kiwanda cha nguo na kufanya kazi muda wa mchana na usiku akijishughulisha na masomo ya yake ya kidini. Sheikh huyu kuanzia mwaka 1964 A.D alishiriki katika masomo ya Sayyid Said Akhtar Rizvi, mwanazuwoni wa kishia mwenye asili ya India na muasisi wa (taasisi ya Bilal Muslim Mission) nchini Tanzania, hadi pale Allamah Sayyid Akhtar alipo mtuma yeye na idadi kadhaa ya wanafunzi wa kitanzania na kuwasafirisha kwenda kujiendeleza na masomo ya kidini katika hawza ya kielimu ya Najaf nchini Iraq mnamo mwaka 1968 A.D.

Sheikh Abdallah Seif yeye pamoja na marafiki zake walisafiri hadi katika mji wa Basrah kupitia njia ya bahari na kutokea hapo wakaelekea kwenye mji wa Najaf. Serikali ya wakati huo ya Iraq ilimuhukumu kifo mwenyeji wao katika nchi ya Iraq kwa tuhuma ya kuingiza majasusi wa kiafrika nchini humo na kunyongwa mnamo mwaka 1969 A.D. Tukio hili lakini pia mazingira mengine ya mivutano ya kisiasa katika nchi ya Iraq katika zama hizo, hayakumruhusu Sheikh Abdallah Seif na marafiki zake kuendela na masomo yao katika nchi ya Iraq hivyo wakaamua kusitisha masomo yao katika nchi hiyo.

Sheikh Abdallah Seif akifuatana na marafiki zake waliokuwa wakitoka Tanzania, walisafiri na kuhamia katika nchi ya Lebanon kutokana na makubaliano yaliyo fanyika kati ya Ayatullah Sayyid Muhsin Hakim pamoja na Imamu Mussa Sadr, hivyo mnamo mwaka 1970 A.D wahamia Lebanon na kupokelewa katika shule iliyokuwa ikijulikana kwa jina la (Ma'ahadud-diraasaatil-islaamiyah) iliyokuwa katika mji wa Suur na iliyokuwa ikisimamiwa na Imam Mussa Swadri, na kuendelea na masomo yao katika shule hiyo.

Sheikh Abdallah Seif na marafiki zake baadae walihamia kwenye mji wa Qom nchini Iran kwa ajili ya kuendelea na masomo yao. Na waliingia katika mji wa Qom mwaka 1973 A.D na kuendelea na masomo ya kihawzah katika mji huo. Sheikh Abdallah Seif mnamo mwaka 1980 A.D aliamua kurudi Tanzania. Pia masomo yake ya secular yaliendela hadi sekondari kupitia masomo ya njia ya posta Britania.

Kuingia Kwake Katika Ushia

Nukta ya kwanza iliyomfanya kuwa shia Sheikh Abdallah seif ilitokana na Sheikh Muhammad Ali Ngongabure mmoja kati ya masheikh wa Kiafrika wa Kishia, mtu ambae alikuwa ni mtu wa kwanza kati ya waenezaji wa madhehebu ya Kishia nchini Tanzania na huyu ndie alie zalisha nukta hiyo. Yeye mnamo mwaka 1964 A.D Alimuarifisha Sheikh Abdallah Seif kwa Allamah Sayyid Saidi Akhtar Rizvi hivyo Abdallah Seif kusoma masomo ya kihawza kwa muda wa miaka kadhaa kwa Sayyid huyo.

Sheikh Abdallah kabla ya kufunga safari kuelekea Iraq, alipoamua kwenda kutembelea kijiji kwao aliko zaliwa wakazi wa kijiji aliko zaliwa ambao walikuwa ni masunni walimtishia kifo kwa sababu ya kufuata kwake madhehebu ya Kishia, lakini babu yake ambae nae pia alikuwa ni miogoni mwa wanazuwoni wa Ahlisunna akampa msukumo na kumuhimiza kwenda kufanya utafiti zaidi na kusoma zaidi.

Moja ya sababu ambazo zilimpelekea Sheikh Abdallah Seif kujiunga na madhehebu ya kishia ilikuwa ni walimu wa Kishia, walimu ambao walikuwa wakijibu mwaswali yake kwa uso mkunjufu, maswali ambayo yalihusiana na madhehebu zingine za Kiislamu, walimu hao hawakuwa ni wenye kuwafukuza waulizaji na hawakuyachukulia maswali waliyokuwa wakiuliza kama utovu wa nidhamu na hawakuliangalia suala la uulizaji wa maswali kama yele kuwa ni utovu wa adabu na nidhamu kwa walimu wao.

Harakati Zake

Sheikh Abdallah Seif Said, baada ya kurejea Tanzania mnamo mwaka 1980 A.D chini ya uangalizi wa Allamah Sayyid Akhtar Rizvi alijishughulisha na kazi ya tablighi ya Uislaam na Maktab ya Ahlul-bati (a.s) katika maeneo mbali mbali ya Tanzania. Vile vile alijishughulisha na ufundishaji katika vituo vya (Bilal Muslim Mission) vilivyo anzishwa na Allama Sayyid Said Akhtar Rizvi na maulamaa wengine wa kishia.

Sheikh Abdallah Seif mnamo mwaka 1990 A.D alisafiri kuelekea katika nchi ya msumbiji akitumwa na Allamah Sayyid Said Akhtar Rizvi na kufanikiwa kuasisi na kufungua tawi la taasisi ya (Bilal Muslim Mission katika mji wa Nampula kaskazini mwa nchi ya Msumbiji. Na kwa hakika aliishi na kukaa miaka mingi katika eneo hili na katika nchi hii akijishughulisha na uenezaji na ufundishaji wa masomo ya kidini kwa mujibu wa Madhehebu ya Ahlul-bayt (a.s).

Abdallah Seif kutokana Na kufariki Kwa Allamah Sayyid Saidi Akhtar Rizvi mnamo mwaka 2002 A.D aliamua karudi katika mji mkuu wa nchi ya tanzaia na kuendelea na harakati zake za kitablighi katika taasi ya Bilal Muslim Mission. Na baada ya muda akaachana na taasisi hii hivyo kuanza harakati zake za tablighi katika mji wa Dar es Salaam kwa kujitegemea na pia aliendelea na harakati hizo za tablighi kusini mwa nchi ya Tanzania. Vivyo hivyo aliendela na harakati zake za tablighi na pia kusimamia huduma mbali mbali za kijamii kama vile usambazaji wa maji katika maeneo ambayo yalikuwa na uhaba wa maji katika kijiji chake aliko zaliwa Mnang'ole hadi mwisho wa maisha yake.

Kufariki Kwake

Sheikh Abdallah alifariki siku ya Ijumaa tarehe 12 September mwaka 2020 A.D akiwa na umri wa miaka 81 katika mji wa Dar-es-salaam Tanzania na kuzikwa katika kijiji aliko zaliwa mnang'ole katika mji wa Lindi.Kutokana na kifo chake, shakhsiya na taasisi mbali mbali kama vile Federation ya jamii ya shia Khoja ithna Asharia ya Afrika na kamati ya Waislamu wa Bilal Tanzania walituma salam zao za rambirambi. Majmaa Ahlul-baiti (a.s) pia nao walitoa tamka na salam za rambirambi kufuatia kifo cha Sheikh Abdallah Seif, na katika sehemu za salam hizo za rambirambi kumuhusu Sheikh imeelezwa kama ifuatavyo: (Kwa hakika Sheikh wakati wote amekuwa kama jua lenye kumeremeta katika eneo la Afrika Mashariki, alikuwa ni mtu mwenye kubainisha uhakika na mwenye kubainisha maarifa safi ya dini ya Kiislamu na maarifa ya Ahlul-Bayt (a.s).