Abdillah Nassir juma

Kutoka wikishia

Shekhe Abdillah Nassir Juma (1932-2022A.D) alikuwa ni mwanazuoni wa Kishia na kiongozi wa kifikra wa baadhi ya jamii ya Mashia katika nchi ya Kenya na ni mtu ambaye alikuwa na nafasi na mchango mkubwa sana katika kueneza maktaba (mafundisho) ya Ahlul-Baiti (a.s) na madhehebu ya Shia katika maeneo mengine ya Afrika Mashariki.

Kwa hakika alikuwa pia miongoni mwa wanazuoni wa Ahlu Sunna na mwanachama katika jopo la Kenya la utunzi wa sheria (alikuwa ni mwakilishi katika bunge la Kenya la utungaji sharia). Baada ya utafiti na uhakiki wa muda mrefu na hasa baada ya kusoma kitabu chaAl-Ghadiir cha Allama Al-Amini akaamua kujiunga na madhehebu ya Shia, na baada ya hapo nguvu na juhudi zake zote akazielekeza katika kueneza mafundisho ya madhehebu hii yenye nuru ya maktaba ya Kishia kiasi kwamba kutokana na huduma zake katika njia hii basi akapata fakhari ya kupokea medali ya Abbasiy kutoka katika taasisi ya Shirikisho la Jumuiya ya Khoja Shia Ithnaasharia ya Afrika.

Mwanazuoni huyu aliyeingia Ushia pamoja na harakati mbalimbali alizozifanya kama vile kuasisi na kuanzisha Hawza (Chuo cha Kidini) na maktaba, pia alikuwa na majadiliano na Mamufti wa Kiwahabi katika kutetea ukweli na usahihi wa madhehebu ya Shia. Marehemu Sheikh Abdillah Nassir anazo athari na vitabu vingi alivyotunga na kuandika kwa lugha ya Kiswahili, vitabu ambavyo vimebakia kama kumbukumbu ya Shekhe huyu kiasi kwamba baadhi ya vitabu hivyo vimeandikwa na kutarjumiwa kwa lugha ya Kiingereza nk.

HISTORIA YA MAISHA YAKE

Shekhe Abdillah Nassir Juma alizaliwa mnamo mwaka 1932 A.D katika mji wa Mombasa katika nchi ya Kenya. Alizaliwa na kukulia katika familia yenye kufuata madhehebu ya Kisunni. Babu yake ambaye ni mzee Ahmad Basheikh bin Hussein alikuwa ni mshairi na mwandishi mashuhuri wa Kenya na alikuwa ni mwanazuoni wa akida na mwalimu wa Qur'an. Kaka yake Abdullatwif Abdallah ni mwandishi na mwanaharakati wa kisiasa katika nchi ya Kenya.

Shekhe Abdillahi Nassir mnamo mwaka 1950 A.D alisafiri kuelekea nchini Tanzania na kujiunga na Chuo Kikuu cha mafunzo ya ualimu huko Zanziba na kujishughulisha na masomo yake katika chuo hicho. Kwa hakika baada ya kumaliza na kuhitimu masomo yake alirejea Mombasa na kuajiriwa kama mwalimu katika shule ya msingi ya waarabu, shule iliyokuwa chini ya usimamizi wa taasisi ya mafunzo ya Waislamu Mombasa na kujishughulisha na kazi ya ufundishaji.

Marehemu Abdillah Naasir mnamo mwaka 1964 A.D alisafiri na kuelekea Nairobi mji mkuu wa Kenya na kuajiriwa kama mkuu wa kitengo cha Kiswahili na Kiarabu cha redio ya BBC, na kuanzia mwaka 1965 A.D akachaguliwa kuwa Mkurugenzi wa kitengo au sehemu ya Kiswahili ya uchapishaji na usambazaji cha Oxford tawi la Afrika Mashariki. Vivyo hivyo kuanzia mwaka 1974 hadi 1977 A.D akakabidhiwa ukuu na kuwa raisi au mwenyekiti wa tawi la Afrika Mashariki la uenezaji na usambazaji wa Chuo Kikuu cha Oxford na kabla ya mwaka 1980 A.D akafanya maamuzi ya kurejea Mombasa.

KUINGIA KWAKE USHIA

Shekhe Abdillah Nassir ambaye alikuwa akihesabiwa kuwa ni miongoni mwa wanazuwoni wakubwa wa Ahli sunnah alijiunga na madhehebu ya kishia kuanzia miaka ya 1960A.D.

Kwa hakika shekhe huyu baada ya kutambua na kufahamu ubora na fadhili nyingi za Hadhrat Amiril-muuminii Aliy (a.s) akawa na ihtimali hii kwamba mtu huyu yaani Hadhrat Aliy atakuwa ni bora kuliko maswahaba wengine wa Mtume (s.a.w.w). Kutokana na ihtimali hii akaamua kuingia kwenye usomaji na utafiti kuhusu jambo hili na baada ya usomaji mkubwa na wa muda mrefu na haswa kusoma kitabu adhiim cha Al-ghadiir kilicho andikwa na Allamah Amiiniy basi akakata shauri juu ya kuwa madhehebu ya shia ni madhehebu ya kweli na mnamo mwaka 1975 A.D akabadilisha madhehebu na kujiunga na madhehebu ya kishia. Kwa hakika Shekhe Abdillah mwanzoni mwa miaka ya thamanini 1980 A.D baada ya ushindi wa mapinduzi ya kiislaam ya Iran, akabadilisha madhehebu yake rasmi na kutanga madhehebu ya ushia jambo ambalo lilipelekea kupungua kwa mapenzi yake kati ya Ahli sunnah wa Kenya.

Shekhe Abdillah kabla ya kutangaza rasmi kubadilisha madhehebu yake, kati ya mwaka 1978 na 1980 A.D alishiriki kwenye harakati za (WAMY) kama muwakilishi wa Afrika mashariki wa majmai jahaani ya vijana wa kiislaam, taasisi ambayo makao makuu yake yako katika mji wa Jiddah nchini Saudi Arabia, na kwa sababu hii baadhi ya vituo na taasisi zenye mahusiano na mawahabi wakafanya juhudi kubwa sana za kumrudisha kutoka kwenye ushia lakini mwishowe hawakufanikiwa.

HARAKATI ZA KITAMADUNI NA KISIASA

Shekhe Abdillahi Nassir aliasisi na kuanzisha Hawzah ya Imamu Aliy (a.s) katika nchi ya Kenya. Na alikuwa akifanya mijadala na mazungumzo na mamufti wa Kenya na aliweza kusafiri katika nchi mbali mbali kama vile Tanzania, India, Pakistan, Uingereza, Amerika na Kanada kutoa mihadhara mbalimbali ya kidini kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza. Harakati za Marehemu shekhe Abdillah katika kueneza na kutanga ushia katika nchi ya Kenya na maeneo mengine katika nchi za Afrika mashariki ni zenye athari kubwa sana.

Marhum Abdillah Naasir alikuwa ni mwanachama wa baraza kuu la majmaa jahaani Ahlul-baiti na alifanikiwa kuanzisha maktaba ya watu wote. Shekhe mnamo mwezi wa April mwaka 2011 A.D alizawadiwa medali ya Abbasiy kutoka taasisi ya Federation ya jamaa wa shia khoja ithna ashariah Afrika katika kikao cha sabini na mbili cha baraza kuu katika mji wa Mombasa kutokana na kazi ya tablighi na harakati zake za uenezaji na utangazaji wa ushia na dini ya kiislaam. Medali ya Abbasiy, ni medali ambayo ilipewa jina la Hadhrat Abbas (a.s) na ni miongoni mwa medali ambazo Federation ya jamaa wa khoja ithna asharia huitoa na kuwapatia watu mbali mbali kutokana na huduma mbali mbali na juhudi mbalimbali wazifanyazo na zenye mchango mkubwa katika kueneza na kutangaza madhehebu ya kishia.

Abdillahi Nassir katika ujana wake kati ya mwaka 1957 na 1963 alishiriki katika harakati ya uhuru wa Kenya kutoka kwa mkoloni wa kiingereza, na kati ya mwaka 1961 hadi 1963 A.D kabla ya Kenya kujikomboa kutoka Uingereza pia alikuwa ni mwanachama na mbunge wa bunge la kutunga sheria la nchi hiyo. Vile vile alikuwa ni mjumbe wa Conference na mkutano wa katiba wa nchi ya Kenya lililo fanyika katika jengo la (Lancaster House) huko London lililo kuwa limeundwa kwa ajili ya ukombozi wa kenye kutoka utawala na Empire ya Uingereza. Pi yeye alikuwa ni muwakilishi wa watu wa Mombasa katika moja wapo kati ya vipindi vya uwakilishi wa bunge la nchi hiyo.

ATHARI NA VITABU VYAKE ALIVYO TUNGA

Harakati za marehemu Abdillah Nassir hazikukomea katika kueneza na kuanzisha vituo ya kidini na kitamaduni bali pia alitoa usaidizi wake kupitia kalamu yake katika kutangaza na kueneza Maktabu ya Ahlul-baiti (a.s) na alitoa msaada mkubwa katika hilo hadi kufia kuandika takriban vitabu na Makala 25 kwa lugha ya Kiswahili kuhusiana na ushia, na altarjumi baadhi ya sura za Qur'an, kufasiri baadhi ya sura na Aya za Qur'an. Na athari nyingi za Marehemu zimetarjumiwa katika lugha ya kiingereza na Kinyarwanda (moja kati ya lugha rasmi katika baadhi ya nchi za eneo la Afrika mashariki).

Shekhe Abdillah aliandika vitabu kama vile (Ushia na taqiya, maswali na majibu) kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hakika yeye katika kitabu hiki aliandika na kuzungumzia kuhusu taqiya ni nini, matatizo ya mashia katika zama za utawala wa Bani Ummayah na bani Abbas, na akaandika kuhusu taqiyah kwa mtazamo wa Ahli sunnah na mashia.

Baadhi ya athari zingine za Marhuum ni kama zifuatazo:

  • Shia na Qur'an
  • Shia na swahaba
  • Yazidi hakuwa Amiril-muuminiin
  • Tofauti kati ya mashia na masunni
  • Tafsiri ya Suuratul-ahzaab

KUAGA KWAKE DUNIA

Shekhe Abdillah Nassir baada ya umri mrefu wa hijadi ya kielimu na kitamaduni, mnamo mwaka 2022 A.D aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 89 katika mji wa Mombasa Kenya. Na kiwiliwili chake kuzikwa katika makaburi ya Ganjuuniy Mombasa.