Hamim

Kutoka wikishia

Hamim (Kiarabu: حميم) ina maana ya joto kali na katika Qur'an yanaashiriwa maji ya moto yaliyochemka ambayo watanyweshwa watu wa motoni. Hamim, inatumika pia kwa maana ya mtu na jamaa wa karibu. Neno hili limetumika mara 20 katika Qur'an tukufu. [1] Wafasiri na watafiti wa masuala ya Qur'an wanaamini kuwa, neno Hamim katika Qur'an lina maana mbili:

  • Maji ya moto na yanayochemka [2] ambayo ni kwa ajili ya kunyweshwa watu wa motoni. [3] Maana hii inapatikana katika Qur'ani katika Aya zifuatazo:

Aya ya 57 ya Surat Swaad

هَذَا فَلْیذُوقُوهُ حَمِیمٌ وَ غَساقٌ

Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha.
(Quran: 38: 57)

Aya ya 4 ya Surat Yunus

وَ الَّذِینَ کفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِنْ حَمِیمٍ وَ عَذَابٌ أَلِیمٌ بِمَا کانُوا یکفُرُونَ

Na walio kufuru, wao watapata vinywaji vinavyochemka, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyo kuwa wakikufuru.
(Quran: 10: 4)

Fakhr al-Razi amenukuu katika Mafatihul Ghaib kwamba, makusudio ya Hamim katika Aya hizi ni shaba iliyoyeyushwa. [6]


  • Mtu ambaye ni wa karibu. Maana hii inapatikana katika Aya hizi:

Aya ya 101 ya Surat al-Shuaraa

وَ لَا صَدِیقٍ حَمِیمٍ

Wala rafiki wa dhati.
(Quran: 38: 57)


Aya ya 10 ya Surat al-Maarij

وَ لَا یسْأَلُ حَمِیمٌ حَمِیمًا

Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake.
(Quran: 70: 10)


Wafasiri wanasema, Hamim katika Aya hizi ina maana ya jamaa na mtu wa karibu, [9] mtu wa karibu anayeguswa na jambo la mwenziwe na ambaye ni mpole [10], mtu wa karibu ambaye anafuatilia masuala na matatizo ya mtu, [11] na mtu wa karibu ambaye ni mlinzi na muungaji mkono wa mtu. [12] Hii ndio maana iliyotolewa na wafasiri ya Hamim katika Aya hizi.

Hassan Mustafawi (aliaga dunia 1384 Hijهria Shamsia) mwandish wa kitabu cha al-Tahqiq fi kalimat al-Qur'an al-karim anasema kuwa, Hamim ina maana kadhaa: Harara shadidi (joto kali), kuwa nyeusi, ya karibu, uwepo, aina ya sauti na kusudio ambapo maana zote hizi zinarejea katika joto kali.

Kwa mfano, kama baadhi ya chemchemi zinaitwa kwa jina la Hamim ni kutokana na kuweko maji ambayo ni ya moto katika chemchemi hizo, na kama mtu yuko karibu na mtu (jamaa) anaitwa kwa jina la Hamin, basi hilo ni kutokana na huba na mapenzi shadidi aliyokuwa nayo kwake. Kadhalika Hamim imetumika kwa maana ya mkaa, hilo linatokana na kuwa, mbao ambayo inaungua na moto mkali hubadilika na kuwa mkaa. [13] Kwa muktadha huo, Hamim maana yake ni kitu cha moto na chenye harara, iwe ni joto na harara ya kimaada kama maji yanayochemka au harara na joto la kimaanawi kama vile rafiki na walii wa mtu. [14]

Rejea

Vyanzo