Zinaa ya Muhsana

Kutoka wikishia

Uzinzi wa Muhsana (Kiarabu: زنا المحصن والمحصنة) ni zinaa ya mwanamume mwenye mke au mwanamke mwenye mume na jambo hili linatimia chini ya masharti fulani na adhabu yake ni kupigwa mawe. Uzinzi wa mwanamume au mwanamke aliyeko katika ndoa ambayo katika istilahi ya kifikihi inajulikana kwa jina la «Ihswaan» hutimia pale mhusika anapokuwa baleghe, mwenye akili na asiwe mtumwa wala kanizi, awe amekwisha fanya tendo la ndoa na mwenza wake na vilevile awe na uwezo wa kukutana kimwili na mwenza wake wakati wowote wa usiku na mchana.

Adhabu ya Muhsana ni kupigwa mawe na hilo hufanyika wakati mhusika atakapozini na mwenye akili na baleghe; kinyume na hivyo adhabu yake ni mijeledi 100.

Maana ya Kifikihi

Katika elimu ya fikihi uzinzi na hatua ya kuzini mwanaume mwenye mke au mwanamke mwenye mume inajulikana kwa jina la «Zinaa ya Muhsana». [1] «Muhsana» na «Muhsanah» huitwa mwanaume au mwanamke aliyeko katika mahusiano ya ndoa; [2] yaani awe na mwenza wa ndoa ya daima, awe amesafanya naye tendo la ndoa, kuwe na uwezekano wa yeye kufanya naye tendo la ndoa wakati wowote (kwa kusiweko na kizuizi), asiwe mtumwa au kanizi, awe baleghe na mwenye akili. [3]

Hukumu

Kwa mujibu wa fat’wa ya mafaqihi (wanazuoni wa fikihi), ikiwa kuna masuala kama ya safari, kifungo, maradhi yanayozuia kujamiiana kwa mtu aliyeko katika ndoa ambaye amezini, basi zinaa yake sio ya muhsana (mtu aliyeko katika mahusiano ya ndoa). [4] Hata hivyo kama kuna udhuru wa kisheria kama hedhi, swaumu na ihramu kuna hitilafu ya mtazamo baina ya mafakihi. [5] Kadhalika kama mwanamke hatomtii mumewe, zinaa ya mume haitakuwa muhsana. [6]

Fat’wa nyingine ya mafakihi katika uga huu ni kwamba, talaka ya bain (talaka ambayo mume hawezi kumrejea tena mkewe mpaka mwanamke huyo aolewe na mwanaume mwingine kisha aachike) hilo huondoa ihswaan; lakini kuhusiana na kwamba, je, talaka rejea nayo pia inapelekea kumuondoa mume au mke katika ihswaan (kuwa na mke au mume), kuna hitilafu baina ya wanazuoni. [7] Imamu Khomeini hatambui talaka rejea kwamba, ni sababu ya kumuondoa mwanamke au mwanaume katika hali ya Ihswaan (kuwa na mke au mume) na anaamini kuwa, kila mmoja kati ya wawili hao kama atakuwa anajua hukumu ya kadhia na akazini basi atatekelezewa hukumu ya kupigwa mawe. [8] Kwa mujibu wa Sheikh Mufidu mmoja wa mafakihi wa Kishia ni kwamba, kuzini na mwanamke mwenye mume kunapelekea uharamu wa milele (haramu milele mwanaume kumuoa mwanamke ambaye amezini naye), hata baada ya toba na mke kuachana na mumewe. [[9]

Adhabu

Mchoro wa msanii wa Uholanzi Rembrandt wenye kuakisi kupigwa mawe kwa Mtakatifu Stephen.

Katika sheria ya Kiislamu, adhabu ya zinaa ya muhsana inatimia kwa mtu mwenye akili na baleghe na ni kupigwa mawe. [10] Endapo mzinifu atakuwa bibi kizee au babu kizee, kabla ya kupigwa mawe atapigwa mijeledi 100 pia. [11] Adhabu ya kisheria ya mtu aliyezini ambaye hajatimiza masharti ya ihswaan (kuwa katika ndoa) na kadhalika kwa mujibu wa hadithi za adhabu ya zinaa ya Muhsana na asiye baleghe na kichaa ni mijeledi 100. [12] Pamoja na hayo, baadhi ya mafakihi wanaamini kuwa, katika mazingira kama haya si jambo lililo mbali kutekelezwa kwa mtu huyo adhabu ya kupigwa mawe. [13]

Baadhi ya mafakihi wanaamini kwamba, mzinifu ambaye ameoa au kuolewa lakini hajaingiliana kimwili na mwenza wake, mbali na kupigwa mijeledi 100 anabaidishwa pia. [14] Kadhalika kundi la mafakihi linaamini kwamba, kama mwanaume atamuona mkewe akiwa anazini na mwanaume, anaweza kuwaua wote wawili; lakini baadhi ya wengine wanaona kuwa, kitendo hicho hakijuzu. [15] Imamu Khomeini anasema kuwa, inajuzu kuua pale mwanaume atakapofahamu kwamba, mkewe amefanya tendo hilo kwa ridhaa yake mwenyewe [16] na hakuna tofauti kwamba, ni mke wa daima au wa muda (mutaa), awe ameingiliana naye au hajaingiliana naye, awe ni Muhsana au sio. [17]

Katika biblia, adhabu ya zinaa ya Muhsana ni kuuawa. [18]

Rejea

Vyanzo