Haramu milele

Kutoka wikishia

Haramu ya milele au haramu ya daima (Kiarabu: الحرمة المؤبدة) maana yake ni kuwa haramu milele kuoana mwanaume na mwanamke. Katika fikihi ya Kishia wanawake wenye waume (muhsanah) kulaaniana mke na mume, kusoma tamko la kufungisha ndoa wakati mwanamke akiwa katika eda na ihramu, kufanya liwati na mtoto wa kiume, baba na kaka wa mke (shemeji) na kumpa talaka mke baada ya mara ya tisa ni mambo ambayo yanapelekea kuwa haramu daima kuoana mwanamke na mwanaume.

Istilahi ya haramu ya daima au milele inazungumziwa katika milango ya fikihi ya nikaha, talaka, hija na lian (laana). Vifungu vya 1050 hadi 1059 vya sheria ya kiraia ya Iran vinazungumzia maudhui ya uharamu wa daima.

Utambuzi wa maana

Haramu ya milele iko mkabala na haramu ya muda na maana yake ni kuwa haramu kuoana mwanaume na mwanamke milele. [1] Istilahi ya haramu milele ina matumizi mawili:

  • Kuwa haramu daima na milele kuoana mtu na maharimu (maharimu wa nasaba, kuchangia ziwa na wa sababu).
  • Kuwa haramu milele kuoana na asiye maharimu ambao inajuzu kuoana nao; lakini kutokana na kuweko kizuizi, kuoana nao inakuwa haramu daima. [3]

Istilahi hii inatumika katika milango ya fiq’h ya nikaha, talaka, Hija na laana kulaaniana). [4] Vifungu vya 1050 hadi 1059 vya sheria ya kiraia ya Iran vinazungumzia maudhui ya uharamu wa daima. [5]

Sababu

Katika fiq’h ya Kiislamu kumetajwa sababu ambazo kwa kuweko kwake, huwa haramu daima kuoana mwanaume na mwanamke:

  • Kulaaniana: Katika hali ambayo kutafanyika laana baina ya mke na mume, wawili hao ni haramu kuoana milele. [6] Katika kulaaniana ni mume kuapa kwa maneno maalumu mbele ya hakimu na kumtuhumu mkewe kwa zinaa na mwanamke kuapa kwa kiapo kinachoshabihiana na kukana tuhuma za mumewe dhidi yake. [7] Baada ya kufanyika laana hiyo, adhabu ya qadhf (tuhuma ya zinaa au liwati) kutokana na kumtuhumu mkewe kwa zinaa na adhabu ya zinaa dhidi ya mke huondolewa. [8]
  • Kumpa talaka mke mara tisa: Kwa mujibu wa fiq’h ya Kishia, kama mke atamtaliki mkewe mara tatu, hatakuwa na haki ya kumuoa tena isipokuwa kama ataolewa na mume mwingine (muhallil) kisha akaachika hapo anaweza kumuoa tena. [9] Na kama kitendo hicho cha kumtaliki mara tatu kitajikariri mara tatu, yaani ikawa amemtaliki mara tisa, huwa haramu kwake kumuoa milele. [10]
  • Ifdhaa: Kama mwanaume anamfanyia Ifdhaa binti kabla ya umri wa kubaleghe, mwanamke yule atakuwa haramu milele kumuoa. [11] Ifdhaa maana yake ni kuifanya kuwa moja njia ya mkojo na ya hedhi. [12]
  • Zinaa: Kwa mujibu wa mtazamo mashuhuri wa mafakihi ni kwamba, kama mwanaume atazini na mama mkwe au na binti yake kabla ya kuoana na mwanamke huyo, mwanamke yule huwa haramu milele kwake kumuoa. [13] Kadhalika kuzini mwanaume na mwanamke ambaye ni mke wa mtu na mwanamke ambaye yuko katika eda ya talaka rejea, humfanya mwanamke yule awe haramu milele kwa mwanaume yule. [14].
  • Liwati: Kama mwanaume atafanya liwati na mtoto wa kiume, kaka au baba wa mwanamke fulani kabla ya kuoana naye, mwanamke yule huwa haramu milele kumuoa. [15]
  • Ndoa katika hali ya eda: Haijuzu kumuoa mwanamke ambaye yuko katika eda [16]. Kwa msingi huo endapo ndoa hiyo itafungwa na kwa kufahamu kwamba, mwanamke yupo katika eda na kufunga ndoa katika hali hii ni haramu, mwanamke yule huwa haramu milele kwa mwanaume yule hata kama hawakukutana kimwili. [17] Lakini endapo hakukuwa na elimu juu ya hilo, haramu ya milele ya mwanamke yule kwa mwanaume itathibiti tu kama wawili hao wamekutana kimwili, na kama hawajakutana kimwili, ndoa itabatilika tu na baada ya kumalizika eda, mwanaume anaweza kumuoa mwanamke yule. [18]
  • Kufunga ndoa katika hali ya ihramu: Ni haramu kufunga ndoa mwanaume au mwanamke katika hali ya ihramu na ndoa hiyo ni batili. [19] Kufunga ndoa hali ya kuwa mhusika ana ufahamu juu ya kuwa haramu hilo katika hali ya ihramu, mwanamke huyo huwa haramu milele kwa mwanaume hata kama wawili hao hawajakutana kimwili. [20] Endapo wahusika hawakuwa na elimu juu ya hilo, hata kama wamekutana kimwili, ni ndoa tu ndio itakayobatilika. [21]

Rejea

Vyanzo

  • Akbarī, Maḥmūd. Aḥkām-i rawābiṭ-i maḥram wa namaḥram. Qom: Intishārāt-i Fatyān, 1392 SH.
  • Khomeinī, Sayyid Rūḥ Allāh. Taḥrīr al-wasīla. 1st Edition. Qom: Muʾassisah-yi Tanẓīm wa Nashr-i Āthār-i Imām Khomeinī, 1434 AH.
  • Khoeī, Sayyid Abū l-Qāsim al-. Minhāj al-ṣāliḥīn. Edition 22. Qom: Madīnat al-ʿIlm, 1410 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Muqniʿa. 1st edition. Qom: Kungira-yi Jahānī Hizāra-yi Shaykh Mufīd, 1413 AH.
  • Mujtahidī Tihrānī, Si rislāla: gunāhān-i kabīra, maḥram wa namaḥram, aḥkām-i ghayba. Qom: Muʾassisa-yi Dar Rāh-i Ḥaq, 1381 SH.
  • Muʾassisa Dāʾirat al-maʿārif al-fiqh al-Islāmiya. Al-Mawsūʿa al-fiqhiyya. Qom: Muʾassisa Dāʾirat al-maʿārif al-fiqh al-Islāmī, 1429 AH.
  • Muʾassisa Dāʾirat al-maʿārif al-fiqh al-Islāmiya. Farhang-i fiqh-i farsī. Qom: Muʾassisa Dāʾirat al-maʿārif al-fiqh al-Islāmī, 1387 SH.
  • Najafī, Muḥammad al-Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. 7th edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1362 SH.
  • Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. ʿAlī. Masālik al-ifhām ilā tanqīh sharāyiʿ al-Islām. 1st edition. Qom: Muʾassisat al-Maʿārif al-Islāmīyya, 1413 AH.
  • Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. ʿAlī. Al-Rawḍa al-bahiyya fī sharḥ al-lumʿat al-Dimashqiyya. Qom: Intishārāt-i Dāwarī, 1410 AH.