Nenda kwa yaliyomo

Ummu Kulthum binti ya Imamu Ali (a.s)

Kutoka wikishia
Angalia hapa kwa ajili ya matumizi mengine ya Ummu Kulthum (Mkanganyiko) ili kuondoa utata.
Kaburi linalohusishwa na Ummu Kulthum katika makaburi ya Bab al-Saghir, Syria.

Ummu Kulthum binti ya Ali bin Abi Talib (a.s) (Kiarabu: اُمّ كلثوم بنت علي بن أبي طالب) ni mtoto wa Imamu Ali (a.s) na Bibi Fatima Zahra (a.s) ambaye kwa mujibu wa Sheikh Mufid alizaliwa baada ya Imam Hassan (a.s), Imamu Hussein (a.s) na Zaynab (a.s).

Imeripotiwa kuwa Imamu Ali (a.s) alikuwa na mabinti wengine waliokuwa na kuniya ya Ummu Kulthum ambapo kutokana na mshabaha na mfanano huu huu kumetokea hitilafu za kimtazamo kuhusiana na ripoti kuhusu maisha ya Ummu Kulthum. Tukio lenye mjadala mkubwa ni ndoa ya Ummu Kulthum na Omar bin al-Khattab Khalifa wa pili (kwa mujibu wa itikadi ya Waislamu wa Kisuni) ambalo limenukuliwa katika vitabu vya historia na hadithi, na akthari ya Maulamaa wa Kishia wanalikubali hilo na baadhi yao wanalipinga.

Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi za Shia, ndoa hii ilifungwa kwa tishio la Khalifa wa pili, na kwa kulazimishwa na Taqiyyah. Kundi la wanazuoni wa Kishia pia wana rai na mtazamo huu.

Katika baadhi ya vyanzo, Ummu Kulthum anachukuliwa kuwa mmoja wa wanawake waliokuwepo katika tukio la Karbala; lakini kwa mujibu wa watu kama Sayyid Muhsin Amin, mwandishi wa wasifu wa Kishia, Ummu Kulthum alifariki dunia kabla ya tukio la Karbala na Ummu Kulthum aliyekuwepo Karbala pengine alikuwa binti mwingine wa Imam Ali na mke wa Muslim bin Aqil.

Kuna kaburi huko Syria ambalo kwa mujibu wa baadhi ni kaburi la Ummu Kulthum. Lakini wengine wanaamini kwamba, kaburi hili ni la Ummu Kulthum mwingine wa familia ya Mtume, na Ummu Kulthum, binti ya Imam Ali na Fatima, alizikwa kwenye makaburi ya Baqi’i huko Madina.

Mazazi na Nasaba yake

Kwa mujibu wa wanachuoni wa Shia na Sunni, Ali (a.s) na Fatima (a.s) walikuwa na mtoto aliyeitwa Ummu Kulthum.[1] Katika baadhi ya vyanzo, kuzaliwa kwake kwa ujumla kunaripotiwa kuwa kulikuwa ni katika zama za Mtume,[2] lakini mwanahistoria wa Kisunni Dhahabi (aliyeaga dunia 748 Hijiria) ameandika, alizaliwa takribani mwaka wa 6 Hijiria.[3]

Pia, kwa mujibu wa riwaya ya Sheikh Mufid katika kitabu cha Al-Irshad ni kwamba, Yeye (Ummu Kulthum), alizaliwa baada ya Zaynab (a.s),[4] lakini katika sira ya Ibn Is’haq, mwandishi wa sira wa karne ya kwanza na ya pili Hijiria, jina lake limetajwa kabla ya jina la Zaynab, lakini pia haijabainishwa kama yeye alikuwa mkubwa kuliko Zaynab au Zaynab ndiye aliyekuwa mkubwa kiumri.[5]

Kuniya na Lakabu

Sheikh Mufid alitaja jina la Ummu Kulthum kuwa ni Zaynab Sughra na kuniya yake ni Ummu Kulthum.[6] Kwa mujibu wa Sheikh Abbas Qummi katika Al-Kuna wa Al-Alqab, Kuniya hii alimpa Mtume (s.a.w.w) kutokana na kufanana kwake na binti yake Zaynab Sughra.[7]

Sayyid Muhsin Amin, mwandishi wa wasifu wa Kishia (1284-1371 Hijiria) ameandika: Imamu Ali (a.s) alikuwa na mabinti watatu au wanne ambao walikuwa na kuniya ya Ummu Kulthum:

  1. Ummu Kulthum al-Kubra, binti ya Fatima (a.s).
  2. Ummu Kulthum al-Wusta, mke wa Muslim bin Aqil.
  3. Ummu Kulthum al-Sughra.
  4. Zaynab al-Sughra ambaye kuniya yake ilikuwa Ummu Kulthum.[8]

Kwa mujibu wake, yumkini wawili wa mwisho wakawa ni mtu mmoja au wakawa ni watu wawili tofauti na hivyo Imamu Ali alikuwa na mabinti wane kwa jina hili au kwa kuniya hii.[9]

Mume na Watoto

Kwa mujibu wa Ibn Saad, mwanahistoria na mwandishi wa sira na wasifu wa karne ya 2 na 3 Hijiria, Ummu Kulthum aliolewa na Omar bin Khattab, Khalifa wa pili. Baada ya kifo cha Omar, aliolewa na binamu yake Awn, mtoto wa Jafar bin Abi Talib. Baada ya kifo cha Awn, aliolewa na shemeji yake Muhammad, na baada ya kifo chake, aliolewa pia na shemeji yake mwingine Abdullah bin Jafar, ambaye kabla ya hapo alikuwa mume wa dada yake Zaynab,[10] hata hivyo al-Maqrizi mwanahistoria na mwandishi wa sira (766-845 Hijiria) ameripoti kwamba, baada ya Omar, Ummu Kuthum kwanza aliolewa na Muhammad bin Ja’far na baada ya kifo cha mumewe huyo akaolewa na Awn na akaaga dunia alipokuwa mke wake.[11]

Ibn Sa’d na Ibn Asakir (mwandishi wa historia wa karne yab 6 Hijiria) wameandika, Ummu Kulthum alizaa na Omar watoto wawili ambao ni Zayd na Ruqayya.[12]

Kufunga Ndoa na Omar Bin al-Khattab

Makala Asili: Kufunga ndoa Ummu Kulthum na Omar bin al-Khattab

Tukio la ndoa ya Ummu Kulthum na Omar bin Khattab, Khalifa wa pili, ni suala tata na lililozua mjadala na hitilafu: Kwa mujibu wa vitabu vya kihistoria vya Shia na Sunni, kama vile Tarikh Ya’qubi na Tarikh Tabari, pamoja na vyanzo vya hadithi za Shia kama vile Kafi na Tahdhib al-Ahkam, Ummu Kulthum aliolewa Omar.[13] Mirza Jawad Tabrizi na Sayyid Ali Milani wamezichukulia riwaya hizo mbili katika kitabu cha Kafi kuwa sahihi.[14] Muhammad Taqi Shushtari, mwanachuoni wa Kishia wa elimu ya Rijaal wa karne ya 14 na 15, pia amezitambua hadithi zilizopo katika maudhui hii kwamba, ni mutawattir na kwamba, tukio la ndoa hii ni jambo lisiloweza kukanushwa.[15]

Licha ya hayo, baadhi ya wanazuoni wa Kishia, akiwemo Ayatullah Mar’ashi [16] na Muhammad Jawad Balaghi [17], hawajaikubali ndoa hii. Agha Bozorg Tehrani ametaja majina ya vitabu ambavyo vimekanusha ndoa hii katika kitabu chake cha al-Dhariah.[18]

Kwa mujibu wa maoni ya wanachuoni kama vile Sayyid Murtadha (355-436 Hijiria) na Fadhl bin Hassan Tabrasi (aliyefariki dunia 548 Hijiria) ni kwamba ndoa hii ilifungwa baina ya wawili hawa; lakini ilikuwa ni kwa kulazimishwa na kwa Taqiyyah. [19] Pia kuna Hadithi zinazothibitisha kauli hii. Kwa mfano, katika kitabu Kafi, Imam Swadiq (a.s) amenukuliwa akisema kwamba, Ummu Kulthum ni binti tuliyepokonywa. [20] Katika riwaya nyingine ya kitabu hiki hiki, imetajwa kuwa Imam Ali (a.s) amezungumzia tishio la Omar ili akubali binti yake aolewe naye. [21]

Kuweko Karbala

Katika vyanzo, imetajwa kuhusu kuwepo kwa Ummu Kulthum katika tukio la Karbala. Kwa mfano, Sayyid Ibn Tawus (589-664 Hijiria) amemtaja Ummu Kulthum katika sehemu kadhaa katika kitabu chake cha Luhuf; miongoni mwa yaliyonukuliwa kutoka kwake ni, kilio chake na Zaynab, pale Imamu Hussein (a.s) alipowaambia kwamba atauawa, [22] hotuba yake huko Kufa na kuwalaumu watu wa mji wa Kufa [23] na ombi lake kwa Shimr huko Sham kwamba, awaingize Damascus kupitia njia ambayo hawataonekana sana na watu.[24] Ibn Tayfur, mwanahistoria wa karne ya tatu Hijiria, pia aliandika kwamba wakati mateka wa Karbala walipoletwa Kufa, Ummu Kulthum alisoma khutba mbele ya mjumuiko wa watu wa mji huu na akawalaumu watu wa Kufa. [26]

Pamoja na hayo, haijabainishwa katika vyanzo hivi kwamba Ummu Kulthum ni binti ya Imam Ali (a.s) aliyezaa na Bibi Fatima (a.s). Kwa upande mwingine, baadhi wamebainisha kwamba, Ummu Kulthum ambaye alikuwepo katika tukio la Karbala ni binti mwingine wa Imam Ali (a.s) ambaye hakutokana na Bibi Fatima. [27] Sayyid Muhsin Amin pia ameandika kwamba haifahamiki ni Ummu Kulthum yupi ambaye alikuwepo pamoja na Imamu Hussein huko Karbala kati ya mabinti wa Imamu Ali (a.s); hata hivyo kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba alikuwa mke wa Muslim bin Aqil. [28]

Kuaga Dunia

Kumesemwa kauli mbalimbali kuhusu wakati wa kifo cha Ummu Kulthum na jinsi kilivyotokea. Miongoni mwa mambo yaliyoandikwa ni kuwa, yeye na mwanawe Zayd walikufa wakati mmoja kutokana na maradhi, na hicho ni kipindi ambacho Ummu Kulthum alikuwa mke wa Abdullah bin Jafar (aliyefariki: 80 Hijiria). [29] Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, wawili hawa waliuawa kwa sumu katika zama za utawala wa Abdul malik bin Mar’wan (alitawala: 65-68 Hijiria) kwa amri ya mtawala huyo na Abdullah bin Omar akasalia majeneza yao; [30] lakini Sayyid Muhsin Amin amesema kuwa, kifo chake kilitokea kabla ya tukio la Karbala na kabla ya mwaka wa 54 Hijiria. [31]

Alipozikwa

Kaburi la Ummu Kulthum

Kwa mujibu wa Ibn Battuta mtalii na mwandishi mashuhuri wa kumbukumbu za safari wa karne ya 8 Hijiria ni kuwa, kaburi la Ummu Kulthum binti wa Imamu Ali (a.s) aliyezaa na Bibi Fatima (a.s) linapatikana umbali wa kilomita tano hadi tano na nusu kutoka Damascus. [32] Yaqut Hamawi (574-626 Hijiria) naye ameripoti kuwa, kaburi la Ummu Kulthum linapatikana katika viunga vya mji wa Damascus. [33]

Hata hivyo Ibn Asakir ameandika, Ummu Kulthum aliaga dunia katika mji wa Madina na amezikwa katika makaburi ya Baqi’i na kwamba, kaburi lililoko katika viunga vya Damascus ni la mtu mwingine ambaye alikuwa na jina hili hili na anatoka katika familia ya Bwana Mtume (s.a.w.w). [34]

Rejea

  1. Tazama: Mufīd, al-Irshād, juz. 1, uk. 354; Ibn Saʿd, al-Ṭabaqāt al-kubrā, juz. 8, uk. 463.
  2. Ibn Ḥajar, al-Iṣāba, juz. 8, uk. 464. Ibn ʿAbd al-Barr, al-Istīʿāb, juz. 4, uk. 1954.
  3. Dhahabī, Siyar iʿlām al-nubalāʾ, juz. 3, uk. 500.
  4. Mufīd, al-Irshād, juz. 1, uk. 354.
  5. Ibn Isḥāq, Sīra Ibn Isḥāq, 1424 H/2004 M, juz. 1, uk. 247.
  6. Mufīd, al-Irshād, juz. 1, uk. 354.
  7. Qummī, al-Kunā wa l-alqāb, juz. 1, uk. 228.
  8. Amīn, Aʿyān al-Shīʿa, juz. 3, uk. 484-485.
  9. Amīn, Aʿyān al-Shīʿa, juz. 3, uk. 484-485.
  10. Ibn Saʿd, al-Ṭabaqāt al-kubrā, 1990 M, juz. 8, uk. 338; Amīn, Aʿyān al-Shīʿa, juz. 3, uk. 484-485.
  11. Muqriz, Imtau al-asmai, 1420 H/1999 M, juz. 5, uk. 370.
  12. Ibn ʿAsākir, Tārīkh madīna-yi Dimashq, 1415 H/1995 M, juz. 19, uk. 482.
  13. Tazama: Kūlaynī, al-Kāfī, juz. 5, uk. 346; Ṭūsī, Tahdhīb al-aḥkām, juz. 8, uk. 161; Ṭabrisī, Iʿlām al-warā, juz. 1, uk. 397.
  14. Tabrizi, Al-anuar al-ilahiyyah, 1422 H, uk. 123; Muhadharat fil al-itiqadat, 1421 H, juz. 2, uk. 659.
  15. Tastari, Qamusi al-rijal, 1428 H, juz. 12, uk. 216.

Vyanzo

  • ʿAlawī, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Mujdī fī ansāb al-ṭālibīyyīn. Qom: Maktabat al-Marʿashī al-Najafī, 1409 AH.
  • Amīn, Sayyid Muḥsen al-. Aʿyān al-Shīʿa. Beirut: Dār al-Taʿāruf, [n.d].
  • Bilādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Beirut: Dār al-Fikr, 1420 AH.
  • Birrī, Muḥammad b. Abī Bakr al-. Al-Jawhara fī nisab al-imām ʿAlī wa Ālih. Damascus: Maktabat al-Nūrī, 1402 AH.
  • Bīṭār, ʿAbd al-Razzāq al-. Ḥilyat al-Bashar fī tārīkh al-qarn al-thālith ʿashar. Edited by Muḥammad Bahja al-Bīṭār. Second edition. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1413 AH.
  • Dhahabī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Siyar iʿlām al-nubalāʾ. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1413 AH.
  • Ḥamawī, Yāqūt b. ʿAbd Allāh al-. Muʿjam al-buldān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1399 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Aḥmad b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣhāb. Beirut: Dār al-Jail, 1412 AH.
  • Ibn al-Baṭṭuṭa, Muḥammad b. ʿAbd Allāh. Al-Riḥla. Beirut: Edited by ʿAbd al-Hādī al-Tāzī. Rabat: Ākādimīyya al-Mamlikat al-Maghribīyya, 1417 AH.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tārīkh madīna Dimashq. Beirut: Dār al-Fikr, 1415.
  • Ibn Ḥabīb al-Baghdādī. Al-Munammaq fī akhbār Quraysh. Edited by Aḥmad al-Fārūq. Beirut: ʿĀlam al-Kutub, 1415 AH.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba. Beiut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Ibn ʿInaba, Aḥmad b. ʿAlī. Umdat al-ṭālib fī ansāb Āl Abī Ṭālib. Najaf: al-Maṭbaʿa al-Ḥaydarīyya, 1380 AH.
  • Ibn Isḥāq, Muḥammad. Sīrat Ibn Isḥāq. Qom: Daftar-i Tārīkh wa Muṭāliʿāt-i Islāmī, 1410 AH.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad b. Manīʿ al-Baṣrī. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Beirut: Dār al-Ṣādir, [n.d].
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Najaf: al-Maṭbaʿa al-Ḥitdarīyya, 1376 AH.
  • Ibn Ṭāwūs al-Ḥillī, 'Abd al-Karim b. Aḥmad. Farḥat al-gharā fī taʿyīn qabr Amīr al-Muʾminīn ʿAlī (a). Edited by Sayyid Taḥsīn Al Shabīb al-Musawī. [n.p]: Markaz al-Ghadīr, [n.d].
  • Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Musā. Luhūf. Tehran: Nashr-i Jahān, 1348 Sh.
  • Ibn Ṭayfūr, Abū l-Faḍl b. Abī Ṭāhir. Balāghāt al-nisāʾ. Qom: Maktabat al-Baṣīratī, 1372 Sh.
  • Kūlaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb l-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar al-Ghaffārī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1363 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: muʾassisat al-Wafāʾ, 1403.
  • Mamaqānī, ʿAbd Allāh b. Muḥammad. Tanqīḥ al-maqāl fī ʿilm al-rijāl. Najaf: [n.p], 1352 AH.
  • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Imtāʿ al-asmāʾ. Edited by ʿAbd al-Ḥamīd al-Namīsī. Beirut: Dār al-Kutub, 1420 AH.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Murūj al-dhahab wa maʿādin al-jawāhir. Edited by Yūsuf Asʿad al-Dāghir. Qom: Muʾassisat Dār al-Hijra, 1409 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Beirut: Dār al-Mufīd, 1414 AH.
  • Niyshābūrī, Muḥammad b. al-Fattāl. Rawḍāt al-wāʿiẓīn. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1368 AH.
  • Nuwayrī, Shahāb al-Dīn Aḥmad al-. Nihāyat al-arab fī funūn al-adab. Cairo: Dār al-Kutub wa l-Withāʾiq al-Qawmīyya, 1423 AH.
  • Qummī, Shaykh ʿAbbās al-. Al-Kunā wa l-alqāb. Tehran: Maktabat al-Ṣadr, [n.d].
  • Ṣanʿānī, ʿAbd al-Razzāq al-. Al-Muṣannaf. Edited by Saykh ʿAbd al-Raḥmān Aʿẓamī. [n.p]: al-Majlis al-ʿilmī, [n.d].
  • Tabari, ʿImād al-Dīn al-. Kāmil al-Bahāʾi. Qom: al-Maktaba al-Ḥaydarīyya, [n.d].
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Beirut: Muʾssisat al-Aʿlamī, 1403 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al. Iʿlām al-warā bi-iʿlām al-hudā. Qom: Āl al-Bayt, 1417 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Tahdhīb al-aḥkām. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1364 Sh.
  • Zubaydī, Muḥammad Murtaḍā b. Muḥammad al-. Tāj al-ʿarūs min jawāhir al-qāmūs. Beiut: Dār al-Fikr, 1414 AH.