Ujirani mwema

Kutoka wikishia

ujirani mwema, unaojulikana kama "حسن الجوار": ni ndharia  ilioko katika maandiko ya kiislamu, inayosisitiza tabia njema kwa majirani. aya ya 36 ya suratu an-nisa, inatutaka tuwatendee wema majirani zetu. Pia tukirejea kwenye hadithi mbali mbali, tutakuta maelezo kadhaa yenye kusisitiza juu ya kuwatendea wema majirani na kutowafanyia ubaya majirani zetu. hadithi ambazo zinatutaka kuchunga heshima za jirani ni kama vile tuchungavyo heshima za mama zetu, na kwamba kumdhuru yetu ni sawa kumdhuru mtume wa mwenye ezi mungu (s.a.w.w).

katika suala la ujirani mwema, hadithi zimemjali  kila jirani bila ya kuangalia dini yake. hata kama jirani huyo ni kafiri, ila bado uslamu unamtazama jirani huyo kwa jicho maalumu. miongoni mwa haki za jirani asiye muislamu ni; kumpa mkopo, kumtembelea wakati wa ugonjwa, kuhudhuria mazishi yake, kumpa sehemu ya matunda na chakula cha nyumbani kwako, kutomchunguza, na kuvumilia usumbufu kutoka na jirani wake.

kwa mujibu wa hadithi mbali mbali, kumtendea wema jirani husababisha kupata mapenzi ya mwenye ezi mungu na hatimae kuingia peponi, na pia hupelekea kuongezeka kwa riziki na kupata maisha marefu. na kumdhuru jirani husababisha kutopata rehema za mwenye ezi mungu na kunyimwa pepo.


Ujirani mwema unamaanisha kuwatendea wema au kuishi vyema na majirani zetu. Ibara ambayo inapatikana katika Hathi mbali mbali kwa jina la "حسْنُ الجِوار" (Husnu al-jiwar). [1] Kwa mujibu wa istilahi, neno jirani au majirani, humaanisha watu wawili au familia mbili zinazokaa katika nyumba zinzopakana au ndani ya nyumba moja yenye sehemu mbili tofauti. [2]

Mtume (s.a.w.w) na Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) wamesema kwamba mipaka ya ujirani ni nyumba 40 kutoka kila pembe; yaani mbele, nyuma, kulia, na kushoto. [3] Katika Qur'ani Tukufu, baada ya kusisitizwa umuhimu wa kumpwekesha Mwenye Ezi Mungu, kuwafanyia wema wazazi, ndugu, na maskini, pia kuna amri inayotutaka kuwatendea wema majirani zetu. [4]

Kuna Hadithi nyingi zilizopokewa kutoka kwa Ahlul-Bait (a.s.), zinazosisitiza umuhimu wa kuwafanyia wema majirani na kutowadhuru majirani zetu, zikionyesha nafasi muhimu ya ujirani mwema katika maadili ya Kiislamu. [5]

Imepokewa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) ya kwamba; Tendo la kuheshimu jirani ni lenye thamani sawa na thamani ya amali ya kumheshimu mama. [6] Imamu Ali (a.s) pia anasimulia akinukuu kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) kwamba; Jibril alikuwa akisisitiza mno juu ya kuwangalia kwa wema majirani, kiasi kwamba bwna Mtume alidhani kwa majirani wana haki maalumu ya urithi. [7] Ja'far ibn Abi Talib, aliyekuwa mjumbe maalumu wa Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w) kwa Najashi (Mfalme wa Abyssinia), alipokuwa akielezea juu ya mafunzo ya Uislamu mbele ya mfalme huyo, alilitaja suala la wema kwa majirani kama ni moja ya mafundisho muhimu ya dini ya Kiislamu. [8] Imamu Ali (a.s) katika wasia wake katika siku za mwisho za maisha yake, alitoa maagizo muhimu yenye kusisitiza haki za majirani. [9] Kulingana na nukuu ya Muhaddith Nuri, mkusanyaji wa Hadithi za Kishia, ni kwamba; Bwana Mtume wa (s.a.w.w) alisema kwamba; kumdhuru jirani ni kama kumdhuru Bwana Mtume wa (s.a.w.w). [10]

Haki za Jirani

Kulingana na moja ya Hadithi kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w), majirani wanaweza kugawanywa katika makundi matatu: kundi la kwanza ni jirani Muislamu ambaye ni ndugu au jamaa yako, kundi la pili ni jirani Muislamu ambaye si wa damu wala si jamaa yako, na kundi la tatu ni jirani ambaye si Muislamu. Makundi yote matatu haya yana haki juu ya shingo ya kila mtu (jirani) na yanapaswa kuheshimiwa kikamilifu, ingawa kundi la pili lina haki zaidi kuliko la tatu, na kundi la kwanza lina haki zaidi kuliko la pili, kila moja kati yake ni lenye haki maalumu za ujirani. [11] Pia, katika maagizo ya bwana Mtume (s.a.w.w) kwa Imam Ali (a.s), imeelezwa kwamba; mtu anapaswa kumheshimu jirani yake hata kama jirani huyo ni kafiri. [12]


Imamu Sajjad (a.s):

Haki ya jirani yako ni kwamba; umhifadhi wakati wa kutokuwepo kwake na umheshimu pale anapokuwepo. Umsaidie dhidi ya dhulma anayofanyiwa, usipekuw kasoro zake, na ikiwa utaona dosari yoyote kwake, ifiche dosari hiyo. Ikiwa unajua kuwa anapokea nasaha, mpe nasaha akiwa katika faragha. Usiache kumsaidia katika shida zake, fumbia macho makosa yake na umsamehe dhambi zake. Shirikiana naye kwa heshima na ukarimu, kwani hakuna nguvu yoyote ile inayoweza kutenda jambo  ila kwa idhini ya Mwenye Ezi Mungu.

Chanzo: Sheikh Sadouq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, 1413 H, Juzuu ya 2, Ukurasa wa 623.



Mifano ya Hisani kwa Jirani

Riwaya nyingi kutoka vyanzo mbali mbali vya Kiislamu, zinawahimiza waumini kuwafanyia wema majirani zao. [13] Pia baadhi ya Riwaya zimeeleza mifano ya hisani hizo kwa namna ifuatayo:

Imunukuliwa kutoka kwa Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w), akieleza kwamba; haki za jirani yako ni kama ifuatavyo:

  • Ikiwa ataomba msaada, msaidie.
  • Ikiwa atahitaji mkopo, mpe mkopo huo.
  • Akikutwa na hali ya dhiki ya kifedha, msaidie kifedha.
  • Mfariji katika misiba yake.
  • Akipata jambo la kheri, mpongeze.
  • Mtembelee anapougua, na baada ya kifo chake, shiriki katika maziko yake.

Usijenge nyumba yako kuwa juu zaidi ya nyumba yake bila ruhusa yake, jambo ambalo linaweza kuzuia mzunguko wa hewa katika nyumba yake. Ikiwa utanunua matunda, basi yafiche unapoyaleta nyumbani au mpe kiasi fulani kama zawadi. Na iwapo harufu ya chakula chako itafika kwa jirani yako, basi hakikisha pia unamshirikisha katika chakula hicho. [14]

Imamu Sajjad, katika tasnifu yake juu ya haki, iitwayo “Risalatu Al-Huquuq”, alikizungumzia haki za jirani alisema kuwa; Miongoni mwa haki za jirani ni kuwanusuru jirani zako wanapoonewa, kuwasamehe makosa yao na dhambi zao, kuamiliana nao kwa ukarimu, na kuwanasihi wakiwa faraghani (yaani si vyema kumnasihi jirani yako hadharani). [15] Pia bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) akitoa nasaha kwa umma wake alisema kwamba; Yeyote yule aliyejaza tumbo lake wakati jirani yake akiwa na njaa huyo atakuwa hakuniamini (kwa kile nilichokuja nacho). [16] Imamu Baqir na Imamu Sadiq waliwashauri majirani wa watu waliopata msiba kuwapa huduma ya chakula wafiwa hao pamoja na wageni waliohudhuria msibani kwao kwa siku tatu mfululizo. [17]

Kutowachunguza Majirani

Kutowachunguza majirani zetu, ingawa kuwauliza hali na kuwafariji ni miongoni mwa mambo yanayohimizwa kuwatentea majirani hao. Katika baadhi Hadithi imeelezwa kwamba; Watu wanatakiwa kuwajulia hali majirani zao, [18] Ila si vyema kuwachunguza na kwafanyia ujasusi, kwani hili ni miongoni mwa mambo yalioharamishwa kuwatendea majirani zetu. [19]

Kutowadhuru Majirani

Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuhusiana na kutowadhuru majirani Alisema: "Yeyote anayemwamini Mwenye Ezi Mungu na Siku ya Kiyama katu hatamdhuru jirani yake." [20]

Kuvumilia Kero za Majirani

Katika moja ya Hadithi kutoka kwa Imam Kazim (a.s), kuna maelezo yasemayo kwamba:

"Tabia njema ya kuheshimu majirani haimaanishi tu kutomdhuru jirani yako, bali pia inajumuisha uvumilivu wa kero na maudhi kutoka kwa jirani zako." [21]

(Hii inaonyesha kwamba ujirani mwema si tu kujiepusha na madhara, bali pia kustahimili changamoto na tabia zisizofaa kutoka kwa jirani kama sehemu ya adabu ya Kiislamu.)

Faida za Kuwa Mwema kwa Majirani na Matokeo ya Kuwadhuru Majiriani

Kulingani na Hadithi mbali mbali; Kuwa mwema kwa majirani hupelekea kupata upendo wa Mwenye Ezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w), [22] huongeza riziki, [23] huleta ustawi kwa miji na humpa mtu maisha marefu, [24] humfanya mtu kukutana na Mungu akiwa na uso wenye nuru (na bashasha), [25] humwezesha mtu kuingia peponi. [26] Pia miongoni mwa kheri zilizotajwa juu ya mtenda wema kwa majirani zake ni; kupandishwa daraja, [27] na jambo hilo ni ishara ya mtu kuwa na imani ya dini, [28] ishara ya utu, [29] na ubinadamu. [30] Kuhusiana na ujirani mwema, Mtume Muhammad (s.a.w.w) alisema; Yeyote atakayekufa huku akiwa na majirani watatu walioridhika naye, bila shaka mtu huyo atapata msamaha kutokana na dhambi zake. [31]

Ni vyema pia kutambua kwamba; Kumdhuru jirani yako husababisha mabalaa tofauti ikiwemo: laana ya Mungu na hupelekea kutenganishwa na rehema za Mungu, [32] humkosesha mtu Pepo kiasi ya kwamba mtu huyo hataweza kuonja hata harufu ya Pepo ya Mola wake, [33] na ni moja ya ishara za ukosefu wa imani [34] na udhalili wa atendaye matendo hayo. [35]

Maudhui zinazohusiana: Kuishi Pamoja kwa Amani