Nenda kwa yaliyomo

Shahada ya Tatu katika Adhani na Iqama

Kutoka wikishia

Shahada ya Tatu katika Adhani na Iqama: Shahada ya Tatu: ni kutoa ushuhuda juu ya nafasi ya Ali (a.s) baada ya shahadatain (Kushuhudia kuwa Mungu ni MMoja tu na Muhammad ni Mjumbe Wka), zoezi hili hutimia kwa kusema «أشهَدُ أَنّ عَليّاً ولِيُّ الله» au «أشهَدُ أَنّ عَليّاً حُجَّةُ الله», katika adhani pamoja na iqama. Kulingana na maoni maarufu ya wanazuoni wa taaluma ya fiqhi wa madhehebu ya Imamiyya, shahada ya tatu sio sehemu ya adhani wala iqama; kwa hiyo, baadhi ya maulamaa (wanazuoni) wa Kishia wanaamini kwamba; kusema hivyo katika adhani na iqama ni bid’a (uzushi katika dini). Hivyo wanaona kwamba; ni haramu mtu kuamini kuwa ibara hiyo ni sehemu ya kisheria kuhusiana na adhani na iqama. Sheikh Saduq amesema kwamba Riwaya zilizopo kuhusu hili, ni Riwaya bandia na za uwongo. huku Sheikh Tusi akizihisabu Riwaya hizo ni Riwaya nadra. Maoni ya wanazuoni wa madhehebu ya Imamia wa hivi sasa ni kwamba; Ibara hiyo hawezi kuhisabiwa kuwa ni sehemu ya adhani wala iqama; lbali ni mustahabb kusema hiyo katika adhani na iqama, bila ya kuamini kuwa ibara hiyo ni sehemu ya adhana au iqama. Kulingana na maoni ya Sayyid Muhsin Hakim, mmoja wa mafaqihi (wanazuoni wa taaluma ya fiqhi), ni kwamba; shahada ya tatu ni moja ya nembo za madhehebu ya Shia (sha’air al-iman), na kuna sisitizo malumu la kisheria katika kutamka kauli hiyo katika adhani na iqama, na hata wakati mwingine, inaweza kuhisabiwa kuwa ni wajibu, iwapo kufanya hivyo hakuta ambatanishwa na imani ya kwamba; kauli hiyo ni sehemu ya adhana au iqama.

Uchambuzi wa Dhana na Umuhimu wake Shahada ya tatu: ni ithbati na ushahidi wa kushuhudia juu nafasi ya Imamu Ali (a.s), inayo tamkwa baada ya shahada mbili za msingi, yaani, tawhidi (kushuhudia upweke wa Mungu) na unabii (utume wa Mtume Muhammad) (s.a.w.w). [2] Zoezi hili hutiamia kupitia ibara isemayo: "أَشْهَدُ أَنَّ عَلِیًّا وَلِیُّ ٱللَّٰهِ" (Ash-hadu anna Aliyan Waliyyullah - Nashuhudia kwamba Ali ni Walii wa Mungu), na "أَشْهَدُ أَنَّ عَلِیًّا حُجَّةُ ٱللَّٰهِ" (Ash-hadu anna Aliyan Hujjatullah - Nashuhudia kwamba Ali ni hoja ya Mungu). Miongozi mwa ibara nyengine zinazowasilisha hilo ni kauli isemayo: "أَشْهَدُ أَنَّ عَلِیًّا أَمِیرُ ٱلْمُؤْمِنِینَ حَقًّا" (Ash-hadu anna Aliyan Amir al-Mu'minin Haqqan - Nashuhudia kwamba Ali ni Amiri wa Haki wa Waumini). [3] Wanazuoni wakubwa kama vile Sayyid Muhsin Hakim na Sayyid Taqi Tabatabai Qummi, wameitambua shahada hii kama; ni itikadi bainifu na alama au nembo mahsusi ya Ushia. [4] Maudhui ya shahada hii, ni miongoni mwa yale yanayoungwa mkono ndani ya vyanzo mbali mbali vya Hadithi za Kishia, pia kusisitizwa kukiri nafasi hiyo ya Imam Ali (a.s). [5] Mathalan, Tabarsi, katika kazi yake mashuhuri, Al-Ihtijaj, amenukuu Riwaya kutoka kwa Imamu Ja'far as-Sadiq (a.s), inayosema kuwa; yeyote miongoni mwenu anayetamka "La ilaha illallah" (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah) na "Muhammad Rasulullah" (Muhammad ni Mjumbe wa Allah), basi aghafilike na papo hapo afungamanishe ibara mbili hizo na kauli isemayo: "Aliyyun Amirul Mu'minin" (Ali ni Amiri wa Waumini). [6]

Je, Shahada ya Tatu ni Sehemu ya Adhana na Iqama? Mtazamo mashuhuri miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu ya Shia Ithna Asheri ni kwamba; shahada ya tatu si sehemu ya adhana wala iqama. [7] Kwa mujibu wa wanazuoni kama vile Sahib Al-Madarik (aliyeishi kati ya mwaka 946 na 1009 Hijiria) na Sayyid Muhsin Hakim (1306-1390 Hijiria), ni kwamba; hakuna tofauti kati ya wanazuoni waliojadili suala hili, wali wote wamekubaliana ya kwamba, shahada ya tatu si sehemu ya adhana wala iqama. [8] Sahib Jawahir pia amesema kuwa; wanazuoni wa Kishia wamekubaliana kuwa ibara hiyo si sehemu ya adhana wala iqama. [9] Wanazuoni kama vile Sheikh Saduq (aliyeishi kati ya mwaka 305 na 381 Hijiria) na Shahid Thani (911-955 au 965 Hijiria) wameichukulia nyongeza hiyo kwenye adhana na iqama, kama ni uzushi. Wao wnasema kwamba; Riwaya zinazohusiana na jambo hili, ni Riwaya zenye sifa ya "maudhui" (za kutunga au bandia). [10] Shahid Thani pia amesema kuwa; haikubaliki mtu kuweka nyongeza za maneno fulani kwenye adhana na iqama, kwa nia ya kuichukulia kama ni sehemu ya kisheria, ingawa kufanya kwake hivyo hakutabatilishi sala, ili ni kitendo chake kinahisabiwa kuwa ni kitendo cha dhambi. [11] Sheikh Tusi (385-460 AH) kwa upande wake ameeleze akisema kwamba; Riwaya zinazohusiana na shahada ya tatu katika adhana ni miongoni mwa Riwaya nadra, na ameandika kuwa; ni makosa kutamka shahada ya tatu katika adhana, na atakayefanya hivyo atakuwa amekosea; [12] zaidi ya hayo, kauli hiyo haichukuliwi kuwa ni pambo la adhana, wala kusema hivyo hakupelekea vipengele na sehemu za adhana hiyo kukamilika. [13] Faidh Kashani (aliyeishi kati ya mwaka 1007 na 1091 Hiiria), mwanazuoni mwingine wa Shia, anaamini kuwa; ni makuruhu mtu kutamka shahada ya tatu katika adhana au iqama yake. Anaendelea kwa kusema; Pia ni haramu kuamini kuwa ibara hiyo ni sehemu ya kisheria ya adhana au iqama. [14] Hata hivyo, Allama Majlisi (aliyezaliwa mnamo mwaka 1037 na kufariki 1110 Hijiria), anasema kwamba; inawezekana kuwa, shahada ya tatu ni sehemu iliyopendekezwa katika adhana na iqama, hii ni kwa kuzingatia Riwaya zilizkuja kuhusiana na suala hili. [15] Pia wanazuoni wengine kama vile Agha Ridha Hamadani (aliyeishi kati ya mwaka 1250 na 1322 Hijiria), wameruhusu kutamka kauli hiyo katika adhana pamoja na iqama, ila kufanya hivyo kusiambatane na nia ya kuichukulia kama sehemu ya adhana au iqama. [16] Baadhi ya wanazuoni, akiwemo Sayyid Abdul-Ala Sabzewari na Sayyid Taqi Tabatabai Qummi, wanasema kwamba; ni bora mtu kutamka ibara hiyo, ila haitaiwi mtu kufanya hivyo kwa nia ya kuichukulia kuwa ni sehemu ya adhana na iqama. [17] Wanazuoni waliofuata baadae (wa miaka ya hivi karibuni hadi sasa), kama vile Sayyid Abdul-Hadi Shirazi (1305-1382 Hijiria), [18] Sayyid Abul-Qasim Khui (aliyeishi kati ya mwaka 1278 hadi 1371 Hijiria), [19] Sayyid Ali Husseini Sistani (amezaliwa mwaka 1309 Shamsia sana na 1349 Hijiria) [20] na Hussein Wahid Khorasani (aliyezaliwa 1300 Hijiria) [21] wanaamini kwamba; shahada ya tatu si sehemu ya adhana wala iqama; ila ni Sunaa kuengeza ibabara hiyo katika adhana pamoja na iqama. Kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Muhsin Hakim, shahada ya tatu, hasa katika zama za hivi sasa (karne ya kumi na nne na kumi na tano Hijria) ni miongoni mwa alama au nembo za imani ya Kishia, hivyo basi, ibara hii ni yenye sisitizo maalumu ndani ya zama za hivi sasa, na hata wakati mwingine inapendekezwa kuitumia ndani ya adhana na iqama, ila haitakiwi kuamini kwamba; ni sehemu asili ya adhana au iqama. Kwa mtazamo wake yeye, ni wajibu kuitumi ibara hiyo katika adhana na iqama, baada kufuata masharti hayo aliyoyata hapo manzo. [22] Pia kuna wanazuoni wengine kama vile; Sayyid Hussein Tabatabai Qumi (aliyezaliwa mnamo mwaka 1282 na kufariki 1366 Hijiria), wameruhusu kuitumia ibara hiyo kwa nia ya kupata baraka. [23] Sallar Dailami, miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu ya Shia Ithna Asheriyya wa karne ya tano Hijria, pia naye ameruhusu kuongeza shahada ya tatu katika tashahhud (tahiyyatu) ya sala. [24]

Historia ya Kuengeza Shahada ya Tatu katika Adhana na Iqama Sheikh Saduqu alikihusisha kitendo cha kuongeza Shahada ya Tatu kama ni sehemu ya Adhana na Iqama na watu waliokuwa na mitazamo ya kupitiliza mipaka (Maghulati), akisisitiza mtazamo wake huo, ameeleza akisema kuwa; wao ndiwo waliobuni Hadithi za uongo kuhusiana na suala hili. [25] Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya wanahistoria, kutamka Shahada ya Tatu katika Adhana na Iqama kuliwa kumesahaulika tokea kipindi cha karne ya tano. Kiasi ya kwamba, hata Abd al-Jalil al-Qazwini al-Razi, mwanazuoni wa Kishia wa karne ya sita Hijria, alionekekana kukemea tendo hilo katika kazi yake maarufu "Al-Naqdh,". Yeye alisema wazi ya kwamba; iwapo mtu atajumuisha Shahada ya Tatu baada ya Shahada mbili katika Adhana yake, basi sala yake itakuwa mebatilika na hatua hiyo itanahisabiwa kuleta uzushi ndani, jambo ambalo ni dhambi kisheria. [26] Inaripotiwa kuwa; baada ya kupita karne kadhaa, baadae mnamo mwaka wa 907 Hijria, Shahada hii ya Tatu ilirejeshwa tena katika Adhana kwa amri ya Shah Ismail Safawi na kupokewa kwa moyo mpana na wanajamii wa wakati huo. Hivyo basi kipindi hicho, kutotamka Shahada ya Tatu katika Adhana kulitafasiriwa kama ishara ya ufwasi wa madhehebu ya Sunni, kwa hiyo yeyote aliyekuwa hatamki kauli hiyo, alikuwa akituhumiwa kuwa ni mfwasi wa Kisunni. [27] Aidha, imenukuliwa kwamba; baadhi ya wanazuoni wa fiqhi wa kipindi hicho walikwepa kukubaliana na dhana ya kuwa ni sehemu rasmi ya Adhana na Iqama, ila walibaki kimya kwa sababu ya hofu ya kutuhumiwa kuwa na mwelekeo wa Kisunni. [28] Karne moja baadaye, katikati ya karne ya kumi na mbili Hijria, inasemekana kwamba; kwa mara nyengine tena, Waislamu wa Kishia waliacha tena kutamka Shahada ya Tatu katika Adhana. [29] Mirza Muhammad Akhbari, katika moja ya zake yenye jina la "Shahadat Bar Wilayay", alitoa ripoti isemayo kwamba; Sheikh Ja'far Kashif al-Ghita'a katika moja ya barua za kwa Fath Ali Shah Qajar, limwomba (Fath Ali Shah Qajar) kutoa amri ya kupiga marufuku tamko la Shahada ya Tatu katika Adhana taifani mwake. [30] Hata hivyo, kwa mujibu wa maelezo ya Ridha Ustadi, ni kwamba; Mirza Muhammad Akhbari, hakutoa tafsiri sahihi juu ya msimamo wa Kashif al-Ghita'a, ambaye hakuwa mpinzani wa kutamka Shahada ya Tatu katika Adhana, bali alikanusha tu wazo la kuihesabu kama ni asili sehemu ya Adhana na Iqama. [31] Kwa mujibu wa maoni ya Ustadi, ni kwamba; barua ya Kashif al-Ghita'a mna maelezo yasemayo kwamba mtu anaweza kutamka "Ash-hadu anna 'Aliyyan Amir al-Mu'minin" kwa lengo la kupata baraka, badala ya kutaka “Ash’hadu Anna Aliyyan Waliyyu Al-Allah”. [32]

Bibliografia Baadhi ya vitabu vilivyoandikwa kuhusu Shahada ya Tatu ni pamoja na: 1. Kitabu cha Mawsu’atu al-Adhan Baina al-Asala wa al-Tahrif, kilichoandikwa na Sayyid Ali Shahristani katika juzuu tatu lugha ya Kiarabu: Mwandishi katika juzuu ya tatu ya kitabu hichi ameweka mlango maalumu unaoitwa “Ashhadu anna Aliyan Waliyullah, Bayna al-Shar’iyya wa al-Ibtidaa,” ambapo anazungumzia Shahada ya Tatu katika Adhana na Iqama katika sura tatu za kitabu hicho. [33] Sehemu hii pia imechapwa kama kitabu cha pekee na ikatafsiriwa kwa lugha ya Kiajemi na Sayyid Hadi Husseni, ikiwa na jina la Nafasi ya Ashhadu anna Aliyan Waliyullah katika Adhana. 2. Kitabu cha Al-Shahadatu bi al-Wilaya fi al-Adhan, kilichoandikwa na Sayyid Ali Husseni Milani: Katika kitabu hichi, mwandishi ameelezea na kuchunguza hoja za kuruhusiwa kutamka Shahada ya Tatu katika Adhana. [34] 3. Kitabu cha Al-Shahadatu al-Thalitha, kilichoandikwa na Muhammad Sand: Mwandishi katika kitabu hichi amechunguza hukumu zinazohusiana na Shahada ya Tatu katika Iqama, Adhana, katika Tashahhud (Tahiyyatu) na katika sala na Salaam, hasa wakati wa Taqiyya (kutodhihirisha Imani kutokana na khofu), kwa kutumia uchunguzi wa Hadithi na maoni ya wanafiq’hi wa madhehebu ya Imamia. [35] Mada Zilizounganishwa • Ali Waliyullah • Shahadatain