Nenda kwa yaliyomo

Sadaka za lazima

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na sadaka ya wajibu. Kama unataka kufahamu mafuhumu na maana ya sadaka rejea makala ya sadaka.

Sadaka ya wajibu (Kiarabu: الصدقة الواجبة) ni wajibu wa kimali katika uislamu na ni kama vile zaka ya mali, zakat al-fitr na kafara. Sadaka ya wajibu haina anuani ya kujitemea katika fiqh na huzungumziwa kwa sura ya kando na peke yake kila maudhui ambayo inahusiana na hilo. Hukumu jumla ya sadaka ya wajibu kwa mujibu wa mtazamo wa baadhi ya wanazuoni ni kwamba, kinyume na sadaka ya mustahabu, ni bora ikatolewa kwa dhahiri na bila kificho.

Maana ya Sadaka ya Wajibu

Sadaka ina maana ya mtu kutoa mali yake na kumpatia mtu mwingine kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.[1] Sadaka ina sehemu mbili: Mustahabu na wajibu. Kutoa zawadi au mali na kumpatia mtu mwingine ikiwa ni kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu basi hiyo huwa ni katika sadaka ambayo ni mustahabu. Sadaka ya wajibu nayo kwa upande wake inajumuisha masuala kama zaka ya mali, zakat al-fitr na kafara ambazo ni wajibu kutoa.[2]

Hukumu

Katika vitabu vya fikihi kila moja kati ya sadaka za wajibu ina huku maalumu zinazoihusu na hukumu zake hujadiliwa kila moja kivyake. Kwa mfano, zaka ya mali, zakat al-fitr na kafara, kila moja ina anuani ya kujitegemea katika fikihi na hujadiliwa katika milango na sehemu zake za kujitegemea.[3] Pamoja na hayo yote katika baadhi ya maandiko ya fikihi, sadaka ya wajibu imezungumziwa kwa sura jumla: Sahib al-Jawahir (1002-1266 Hijria) katika sehemu ya kitabu [chake cha Jawahir al-Kalam]] kuna anuani isemayo: “Waqf wa Sadaqah” amejadili kadhia moja kuhusiana na sadaka ya wajibu. Nayo ni kwamba, baadhi ya mafakihi wakitegemea hadithi wamesema kuwa, ni bora sadaka ya wajibu ikatolewa kidhahiri na kwa wazi (bila ya kificho); kinyume na sadaka ya mustahabu ambayo ni bora ikatolewa kwa kificho.[4] Hata hivyo baadhi ya wanazuoni pia wamesema, sadaka yoyote ile iwe ya wajibu au ya mustahabu ni bora ikatolewa kwa kificho.[5] Muhammad Saleh Mazandarani, mmoja ya mafakihi wa karne ya 11 Hijria amebainisha sababu ya mtazamo wa pili ambayo ni kuwa, kutoa sadaka kwa sura ya kificho ni jambo ambalo linatuweka mbali na ria na kujionyesha.[6]

Rejea

  1. Mar'ia, Al-kamusi al-fiqh, 1413 Qamarii, uk. 124; Murawij, Istilahat fiqh, 1379 Shamsii, uku. 309-310.
  2. Muasase dairatul-maarif fiqhul-islami, Farhang fiqh, 1392 Shamsii, juz. 5, uk. 65
  3. Khui, Mausuat Imam Khui, 1418 Qamarii, juz. 23, uku. 2, juz. 24, uk.360, juz. 21, uk. 305; Kashif al-Ghitwaa, Anwar al-fuqah, 1422 Qamarii, juz. 3, uk. 1, 125, juz. 4, uk. 25
  4. Najafi, Jawaher al-Kalam, 1404 Qamarii, juz. 28, uk. 132
  5. Najafi, Jawaher al-Kalam, 1404 Qamarii, juz. 28, uk. 132
  6. Mazandarani, Sharh al-kafi, 1342 Shamsii, juz.6, uk. 219

Vyanzo

  • Khui, Sayyied Abu al-Qasim, Mausuat Imam Khoei, Qom, Muasasat ihiyau athar Imam Khui, Chapa ya kwanza, 1418 Qamarii.
  • Kashif al-Ghitwaa, Hassan, Anwar al-Fuqahaa, Najaf, Muasasat Kashif al-Ghitwaa, 1422 Qamarii.
  • Mazandarani, Muhammad Swaleh, Sharh al-kafi, Tehran, Maktaba islamiya ya uchapishaji na usambazaji, 1342 Shamsii.
  • Mar'ia, Hussein, Kamusi ya fiqh, Beirut, Dar Al-Mojtaba, 1413 Qamarii.
  • Murawij, Hussein, Iatilahat shariiya, Qom, Bakhshayesh, 1379 Shamsii.
  • Muasase dairatul-maarif fiqhul-islami, Farhang fiqh mutabiq ba madhhab ahlulbayt(a.s), Beirut, , Chapa ya kwanza, 1392 Shamsii.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Jawaher al-Kalam fi Shara’i al-Islam, Marekebisho: Abbas Quchani na Ali Akhoundi, Beirut, Daru ihiyai turath al-arabi, Chapa ya nane, 1404 Shamsii.