Mwaka wa kwanza Hijria
Mandhari
Mwaka wa kwanza Hijiria ni mwaka wa kwanza katika kuhesabu miaka kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu ya Hijiria. Mwaka huu unasadifiana na mwaka wa 14 baada ya kubaathiwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) (kupewa Utume) [1] na mwaka wa 53 baada ya mwaka wa tembo.
Tukio la hijra (kuhama) na kugura Mtume (s.a.w.w) na kundi miongoni mwa Waislamu kutoka Makka na kwenda Madina lilitokea katika mwaka huu. Kadhalika Masjid Quba na Masjid al-Nabi iliasisiwa katika mwaka huu huu.
Matukio
- Njama ya viongozi wa Kureshi ya kumuua Mtume (s.a.w.w) na tukio la Laylat al-Mabit (siku Imamu Ali alipolala katika kitanda cha Mtume kuwahadaa makureshi wadhani kwamba, Mtume ndiye aliyelala hapo). [2]
- Kuhama Mtume (s.a.w.w) kutoka Makka kwenda Madina. [3]
- Kusilimu Salman Farisi sahaba wa Mtume (s.a.w.w) katika mwezi wa Jamad al-Awwal. [4]
- Kusilimu Abdallah bin Salam mmoja wa Mayahudi wa Madina. [5]
- 15 Rabiul Awwal: Kuasisiwa masjid Quba. [6]
- Sala ya Ijumaa ya kwanza na hotuba ya kwanza kutolewa na Mtume (s.a.w.w)[7]
- Kujengwa Masjid al-Nabi. [8]
- Kusaliwa Sala ya maiti ya kwanza. [9]
- Mkataba wa kuunganisha udugu baina ya Ansar na Muhajirina. [10]
- Mkataba wa amani wa kutoshambuliana baina ya Mtume (s.a.w.w) na Mayahudi. [11]
- Kuandikwa na Mtume (s.a.w.w) katiba ya Madina. [12]
- Ndoa ya Mtume (s.a.w.w) na Aisha. [13]
- Sarriya ya Ubaydah bin Harith (vita iliyopiganwa bila ya Mtume kuhudhuria katika vita hivyo) katika mwezi wa Shawwal kwa ajili ya kukabiliana na washirika ambao ilikuwa kuna uwezekano wakashambulia viunga vya Madina. [14] Ibn Hashim ameitambua Sariyya hiyo kwamba, ilitokea katika mwaka wa pili Hijria. [15]
Mazazi na vifo
- As’ad bin Zurara, mwenye lakabu ya As’ad al-Kheir, mmoja wa masahaba na miongoni mwa Waislamu wa Yathrib. [16]
- Kuzaliwa Mukhtar al-Thaqafi, mmoja wa tabiina ambao alianzisha harakati kwa ajili ya kulipiza kisasi cha mauaji ya Imamu Hussein (a.s). [17]
- Kuzaliwa Abdallah bin Zubayr, mmoja wa waliokuwa wakidai Ukhalifa huko Makka baada ya kifo cha Muawiya.
- Kuzaliwa Ziyad bin Abih, mmoja wa maafisa wa utawala Alawi na Umawiya. [19]