Muhsin bin Ali (a.s)

Kutoka wikishia

Muhsin bin Ali (a.s) ni mtoto wa Imamu Ali na Bibi Fatima (a.s). Mtoto huyu alifariki akiwa tumboni mwa mama yake, katika tukio la mashambulizi ya wafuasi wa ukhalifa wa Abu Bakar dhidi nyumba ya Bibi Fatima (a.s) kwa ajili ya kumlazimisha Imam Ali (a.s) kumtambua Abu Bakar kama khalifa. Tarehe sahihi ya kifo cha mtoto huyu chake haijulikani. Muhammad Hadi Yusufi Gharawi (aliye zaliwa mwaka 1327 Shamsia), ambaye ni mtafiti wa matukio ya historia ya Kiislamu, akitegemea vielelezo maalumu katika kubainisha tukio hilo, alisema kuwa; mashambulizi yaliyo fanyika kwenye nyumba ya Fatima (a.s) yaliomsababishia kupoteza mimba ya Muhsin, yalitokea takriban siku hamsini baada ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w). Walakini, baadhi ya watafiti, wanaamini kwamba; tukio hilo lilitokea katika siku za mwanzo za mwezi wa Rabiul Awwal, ambapo siku hizo huziita: “Ayyamu Muhsiniyyah” au kwa lugha ya Kiswahili ni "Siku za Muhsiniyya". Siku hizo huadhimishwa kwa maombolezo ili watu kuonesha hisia zao juu ya tukio hilo. Hata hivyo maadhimisho haya hayakuungwa mkono na baadhi ya wanazuoni. Sababu ya hilo ni kwamba; maadhimisho hayo hayana historia katika madhehebu ya Shia, pia yanaweza kupelekea kuchujuka rangi kwa shughuli msingi za Kishia. Kulingana na Riwaya, jina Muhsin lilichaguliwa na bwana Mtume mwenyewe (s.a.w.w).

Kuna vitabu kadhaa vilivyo andikwa kuhusiana na Mohsen bin Ali (a.s), ambavyo baadhi ni katika lugha ya Kiarabu na vyengine kwa Kifarsi. Miongoni mwa vitabu hivyo ni kitabu kiitwacho "Al-Muhsin As-Sibtu: au Siqtun" kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Mahdi Musawi Khurasani.

Mwana wa Imam Ali na Bibi Fatimah (a.s)

Katika vyanzo mbalimbali vya Kishia [1] na Kisunni [2], Muhsin, ametambuliwa kuwa ni mwana wa bibi Fatimah na Imam Ali (a.s). Kulingana na maandiko ya Hadithi, jina hili alipewa na bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w). [3] Kulingana na maelezo ya Ibnu Hajar al-Asqalani, ambaye ni mwandishi na mtafiti wa nyenendo za masahaba wa Kisunni (aliye fariki 852 Hijiria), ni kwama; neno hili husomwa kwa kutia shadda (mkazo) wa herufi ya "seen", ambapo husomeka "Muhassan" [4].

Tarehe ya kifo chake

Kuna nadharia tofauti kuhusu mazingira ya kifo cha Muhsin. Katika vyanzo vya Kishia, kifo chake kinahusishwa na tukio lililopolekea yeye kufariki hali akiwa ni mimba tumboni mwa mama yake. [5] Katika vyanzo vya Kisunni, kuna ibara tofauti kuhusiana na kifo chake, miongoni mwazo ni; alikufa mdogo (مات صغیراً) [6] au alikufa hali akiwa ni mtoto mdogo (مات و هو صغیر) [7] au ibara ibara nyengine zifananazo na hizo. [8] Ibara kama hizo zinaashiria kuwa alizaliwa akiwa bado yuhai. Kulingana na maelezo ya Ibnu Hazmi, ambaye ni mwanazuoni wa Kisunni (aliye fariki 456 Hijiria) ni kwamba; Muhsin alifariki mara tu baada ya kuzaliwa kwake. [9]

Katika kitabu cha Al-Ikhtisasu, kulingana na moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) ni kwamba; kifo cha Muhsin kilitokea katika tukio la bibi Fatima kulalamikia dhidi unyang’anyi wa bustani ya Fadak. [10] Kwa upande mwengine baadhi ya vyanzo vya kihistoria vinaunganisha tukio la kifo cha Muhsin na tukio la uvamizi dhidi ya nyumba ya bibi Fatima (a.s). [11] Muhammad bin Abdul Karim Shahrestani (aliye fariki 548 Hijiria) pianaye amehusisha kifo hicho na mavamizi hayo katika kitabu chake cha Al-Milal wa Al-Nihal, ananukuu kutoka kwa Ibrahim bin Sayyaar, anayejulikana pia kwa jina la Naddhaam Mu'utazili (aliye fariki 221 Hijiria). Ibrahim bin Sayyaar ambaye ni miongoni mwa wakuu wa madhehebu ya Mu'utazila, akinukuu kisa hizcho amesema kwamba; kichapo cha Omar bin Khatab kilichomsibu bibi Fatima (a.s) ubavuni mwake, kilisababisha kuharibika kwa mimba ya mtoto huyo aliye julikana kwa jina la Muhsin. [12] Ibn Abi al-Hadid al-Mu'utazili (aliye fariki 656 Hijiria) ambaye ni mfasiri wa Nahj al-Balagha, akiwa katika mdahalo na mwalimu wake (Abu Ja'far Naqib), naye pia aliashiria tukio la kuharibika kwa mimba ya Muhsin kilichotokea wakati vuguvugu la kutaka kuchukua kwa nguvu kiapo kutoka kwa Ali (a.s) cha kumtambua Abu Bakar kama ni Khalifa wa Waislamu baada ya bwana Mtume (s.a.w.w). [13]

Kulingana na baadhi ya Hadithi zilizonukuliwa katika vyanzo vya Kisunni, ni kwamba; Muhsin alizaliwa tokea wakati wa uhai wa bwana Mtume (s.a.w.w). [14]

Katika moja ya Hadithi iliyosimuliwa katika kitabu kiitwacho Kamilu al-Ziyarat, imeelezwa ya kwamba; mtu wa kwanza miongoni mwa watoto wa Mtume (s.a.w.w) ambaye faili lake litafunguliwa katika Mahakama ya Siku ya Kiyama, ni Muhsin, ambapo muuaji wake atashughulikiwa katika mahakama hiyo. [15]

Tarehe ya kifo chake

Makala asili: Ayyamu Muhsin

Kifo cha Muhsin kilisababishwa tukio la uvamizi wa nyumba ya bibi Fatima (a.s), ambapo mimba yake iliharibika kupitia vuguvugu la tukio hilo. [16] Muhammad Hadi Yusufi Gharawi (aliyezaliwa mwaka 1327 Shamsia) ambaye ni mtafiti wa historia ya Kiislamu, anaamini kwamba; tukio la uvamizi wa nyumba ya Fatima (a.s), halikutokea mara tu baada ya tukio la Saqifah na watu kutoa kiapo cha utii cha kumtambua Abu Bakar kama ni Khalifa. Bali kwa mtazamo wake; tukio hilo lilifanyika takriban siku hamsini au zaidi baada ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w). [17] Ila pia kuna baadhi waliosema kuwa; tukio la kifo cha Muhsin lilitokea mwanzoni mwa mwezi wa Rabi al-Awwal, ambao pia waliziteuwa siku za mwanzo za mwezi huo kuwa ndio siku za maadhimisho ya kuomboleza kifo cha Muhsin, siku ambazo hujulikana kwa jina la (Ayyaamu Muhsiniyya). [18] Kulingana na mtazamo wa Naser Makarimu Shirazi (aliye zaliwa 1305 Shamsia) ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wenye mamlaka ya kutoa fatwa za kidini, ni kwamba; ni bora kuto adhimisha maombolezi ya kifo cha Muhsin, kwani sherehe hizi hazina msingi ndani ya historia miongoni mwa Shia, pia zinaweza kupunguza umuhimu wa matukio yenye misingi muhimu zaidi ndani ya madhehebu ya Shia. [19]

Kwa mujibu wa ripoti yail Qazi Abdul Jabbar al-Mu'utazi (aliye fariki 415 Hijiria), ni kwamba; baadhi ya Mashia wanaosihi katika maeneo kama vile; Misri, Damascus, Baghdad, Ramla, Acre (Akka), Tyre (Suur), Ashkelon (‘Askalaan) na Jabal al-Basmaq, walikuwa wakimlilia bibi Fatima (a.s) na mwanawe Mohsen (a.s). [20]

Mahala alipozikwa

Hakuna maelezo katika vyanzo vya kihistoria kuhusiana na mahali alipozikwa Mohsen (a.s). Ila kulingana na moja ya Hadithi iliyotajwa katika kitabu kiitwacho Jami'u al-Nuuraini, kuna ibara isemayo kuwa; Imamu Ali (a.s) alimwambia bibi Fiddha, aliyekuwa mtumishi wa bibi Fatima (a.s), auzike mwili wa Muhsin karibu na mlango wa nyumba yake. [21]

Monografia (Seti ya oradha ya vitabu)

Kuna vitabu vingi vilivyoandikwa kuhusiana na Muhsin bin Ali katika lugha za Kiarabu na Kiajemi:

  • Al-Muhsin Al-Sabtu Mauludun am Siqtun kilichoandikwa na Sayyid Mohammad Mehdi Musawi Khurasani kwa Kiarabu, kazi ilichapishwa na Markazu al-Abhathu al-‘Aqaaidiyyah, mwaka 1430 Hijiria, chapa iliokusanya ndani yake kurasa 626. [22] Mwandishi, kupitia utafiti wa kulinganisha maandishi ya kihistoria, amehitimisha utafiti wake kwa kufikia natija isemayo; Muhsin aliuawa hali akiwa ni mimba tumboni mwa mama yake siku ya shambulio dhidi ya nyumba ya Ali (a.s), tukio ambalo lilitokea kupitia kipigo na shinikizo lililomwathiri bibi Fatimah (a.s). [23]
  • Ghuncheh Yaas: Muhsin bin Ali kilichoandikwa na Mehdi Fatimi kwa lugha ya Kifarsi na Kiarabu na kuchapishwa mwaka wa 1386 Shamsia. [24]

Kadhalika, kuna kazi nyingine kuhusiana na Muhsin (a.s), miongoni mwavyo ni kama vile; "Muhsin bin Ali" kilichoandikwa na Ali Asghar Ridhwani, [25] "Al-Muhsen ibn Fatimatu Al-Zahraa" kilichoandikwa na Abdul Muhsin Abdul Zahraa Al-Qatif, [26] na "Musafir Daryaa: Hadhrate Muhsin bin Ali" kiilichoandikwa na Sadiq Daawari. [27]

Maudhui zinazohusiana

Vyanzo

  • Abū l-Fadāʾ, Ismāʿīl b. ʿIbād. Al-Mukhtaṣar fī akhbār al-bashar. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1417 AH.
  • Aḥmad b. Ḥanbal. Musnad. Beirut: Dār al-Ṣādir, [n.d].
  • ʿAmrī, ʿAlī b. Muḥammad al-ʿAlawī al-. Al-Majdī fī ansāb al-ṭālibīyyīn. Edited by Aḥmad Mahdawī Dāmghānī. Qom: Maktabat al-Marʿashī, 1409 AH.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Suhayl Zakār & Riyāḍ al-Ziriklī. Beirut: Dār al-Fikr, 1417 AH.
  • Bayhaqī, Aḥmad b. al-Ḥusayn. Al-Sunan al-kubrā. Beirut: Dār al-Fikr, [n.d].
  • Bukhārī, Muḥammad b. Ismāʿīl al-. Al-Adab al-mufrad. Beirut: Muʾassisat al-Kutub al-Thiqāfīyya, 1406 AH.
  • Dhahabī, Muḥammad b. ʿUthmān al-. Siyar aʿlām al-nubalāʾ. Edited by Shuʿayb al-Arnāʾūṭ. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1413 AH.
  • Dūlābī, Aḥmad b. Ḥammād al-. Al-Dhurrīya al-ṭāhira. Edited by Saʿd al-Mubārak. Kuwait: Dār al-Salafīyya, 1407 AH.
  • Ḥākim al-Niyshābūrī, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Mustadrak ʿalā l-ṣaḥīḥayn. Edited by Yūsuf al-Marʿashlī. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1406 AH.
  • Ibn Abī l-Ḥadīd. Sharḥ nahj al-balāgha. Edited by Muḥammad Abū l-Faḍl Ibrāhīm. Cairo: Dār Iḥyāʾ al-Kutub al-ʿArabīyya, 1387 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad Muʿawwaḍ & ʿĀdil Aḥmad ʿAbd al-Mawjūd. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tarjumat al-Imam al-Ḥasan b. ʿAlī min tārīkh madīnat Damascus. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. Beirut: Muʾassisat al-Maḥmūdī, 1400 AH.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tarjumat al-Imam al-Ḥusayn min tārīkh madīnat Damascus. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. Qom: Majmaʿ Iḥyāʾ al-Thiqāfa al-Islāmīyya, 1414 AH.
  • Ibn Athīr, ʿAlī b. Abī l-Karam. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār al-Ṣādir - Dār Beirut, 1385 AH.
  • Ibn Athīr, ʿAlī b. Abī l-Karam. Usd al-ghāba fī maʿrifat al-ṣaḥāba. Tehran: Ismāʿīlīyān, [n.d].
  • Ibn Damishqī, Muḥammad b. Aḥmad. Jawāhir al-maṭālib fī manāqib al-Imām ʿAlī b. Abī Ṭālib. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. Qom: Majmaʿ Iḥyāʾ al-Thiqāfa, 1415 AH.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba. Edited by ʿĀdil Aḥmad ʿAbd al-Mawjūd & ʿAlī Muḥammad Muʿawwaḍ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Ibn Ḥazm, ʿAlī b. Aḥmad. Jumhurat ansāb al-ʿarab. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1403 AH.
  • Ibn Ḥibbān. Al-Thiqāt. Beirut: Muʾassisat al-Kutub al-Thiqāfīyya, 1393 AH.
  • Ibn Kathīr, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1408 AH.
  • Ibn Qutayba, ʿAbd Allāh b. Muslim. Al-Maʿārif. Edited by Tharwat ʿAkāsha. Qom: Manshūrāt al-Sharīf al-Raḍī, 1415 AH.
  • Ibn Ṣabbāgh, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Fuṣūl al-muhimma. Edited by Sāmī al-Gharīrī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1379 Sh.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥamamd b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Najaf: Maktabat al-Ḥaydarīyya, 1376 AH.
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Beirut: Dār al-aḍwāʾ, 1405 AH.
  • Khaṣībī, Ḥusayn b. Ḥamdān. Al-Hidāya al-Kubrā. Fourth edition. Beirut: Muʾassisat al-Balāgh, 1411 AH.
  • Kufī, Muḥamamd b. Sulaymān al-. Manāqib Amīr al-muʾminīn. Edited by Muḥammad Bāqir al-Maḥmūdī. Qom: Majmaʿ Iḥyāʾ al-Thiqāfa al-Islāmīyya, 1412 AH.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Murūj al-dhahab. Qom: Dār al-Hijra, 1363 Sh.
  • Mufīd, Muḥamamd b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Dār al-Mufīd, 1413 AH.
  • Qāḍī Nuʿmān al-Maghribī. Sharḥ al-akhbār fī faḍāʾil al-aʾimma. Edited by Sayyid Muḥamamd Ḥusaynī. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1414 AH.
  • Qundūzī, Sulaymān b. Ibrāhīm al-. Yanābīʿ al-mawadda. Edited by Sayyid ʿAlī Jamāl Ashraf al-Ḥusaynī. Tehran: Dar al-ʾUswa, 1416 AH.
  • Sabziwārī, Mullā Ismāʿīl. Jāmiʿ al-nūrayn. Tehran: al-ʿIlmīyya al-Islamīyya, [n.d].
  • Shahristānī, Muḥammad b. ʿAbd al-Karīm al-. Al-Milal wa l-niḥal. Edited by Muḥamamd Sayyid Gīlānī. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Shāmī, Muḥammad b. Yūsuf al-. Subul al-hudā wa l-rashād. Edited by ʿĀdil Aḥmad ʿAbd al-Mawjūd. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1414 AH.
  • Ṭabarī, Aḥmad b. ʿAbd Allāh al-. Dhakhāʾir al-ʿuqba. Tehran: Intishārāt-i Jahān, 1356 Sh.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1403 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Iʿlām al-warā bi aʿlām al-hudā. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1417 AH.
  • Yaʿqūbī, Aḥmad b. Abī Yaʿqūb al-. Tārīkh al-Yaʿqūbī. Beirut: Dār al-Ṣādir, [n.d].
  • Zarandī, Muḥammad b. Yūsuf al-. Naẓm durar al-simṭayn. [n.p], 1377 AH.
  • Haythamī, ʿAlī b. Abī Bakr al-. Majmaʿ al-zawāʾid wa manbaʿ al-fawāʾid. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1408