Tawqi’

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na maana ya Tawqi’(barua). Ili kuzijua barua na maandiko ya Imam wa kumi na mbili, tazama maudhui ya tawqi’ ya Imam Mahdi (a.j.t.f) (barua).

Tawqi’ (Kiarabu: التوقيع) inaashiriwa kuwa ni barua na maandiko ya Maimamu 12 wa madhehebu ya Shia Ithnaasharia. Barua na maandiko haya yaliandikwa kwa hati za Maimamu na kawaida yalikuwa yakiandikwa kwa minajili ya majibu ya maswali na matakwa ya Mashia (wafuasi Ahlul-Bayt), na kisha kuwafikia Mashia kwa njia ya kanali na mtandao wa mawasiliano uliokuwa umeanzishwa baina ya Maimamu na wafuasi wao wa karibu waliokuwa watiifu na waaaminifu.

Barua na maandiko hayo yalikuwa yakitumika katika maudhui mbalimbali kama za fikihi, itikadi, kuuzulu na kuwateua wawakilishi (mawakili), kutangaza kufika kwa wujuhati shari’i, yaani malipo ya kisheria (kama khumsi, zaka na kadhalika) kuwakanusha wenye madai ya uongo ya unaibu wa Imam (a.s) na kadhalika. Katika vyanzo visivyopungua 100 imeashiriwa kwamb,a kuna maandiko na barua za Imam Mahdi (a.j.t.f) ambazo zinahusishwa na zama zake za Ghaibat sughra (Ghaiba ndogo).

Wanazuoni wa fiqhi wa Kishia walizitumia barua na maandiko hayo katika mchakato wa kunyambua masuala ya kisheria kutoka katika vyanzo vyake. (Hiyo ni kutokana na kwamba): Kwa mtazamo wao barua na maandiko hayo ambayo yametoka kwa Maimamu ni sahihi bila shaka yeyote na ni yenye itibari.

Utambuzi wa maana

Tawqi’ katika utamaduni wa Kishia ina maana ya maandiko, barua na katika baadhi ya wakati ni ujumbe wa kauli (kwa mdomo) wenye kutolewa na Maimamu kumi na mbili wa madhehebu ya Ahlul- Bayt (a.s) [1]. Kiasili tawqi’ ilikuwa ikitajwa na kufahamika kwamba, ni andiko na maagizo pembezoni na nyuma ya barua ya mashtaka, kwa hati ya Khalifa au mfalme au baadhi ya watawala, ambapo hatua hiyo ilikuwa ikitilia mkazo juu ya kufuatiliwa mashtaka au matakwa kusudiwa.[2].

Historia yake

Kulingana na ilivyoelezwa katika kitabu kiitwacho Donesh- Nome Imam Mahdi (a.j.t.f) ni kwamba: Maandishi ya awali kutoka kwa Maimamu wa Kishia ambayo yalijulikana kuwa ni tawqi’ ni maandiko yaliyoandikwa kwa hati, mwandiko na mkono wa Imam Kadhwim (a.s) alipomjibu mmoja wa Mashia na wafuasi wake ambaye alimtaka Imam amuombee dua ili apate mtoto wa kiume [3]. Matini ya barua na andiko hilo, imekuja katika kitabu kiitwacho Qurbul- Isnad [4]. Baada ya hapo ibara ya tawqi’ ikatumika pia katika baadhi ya maandiko ya Imam Ridhwa (a.s) [5]. Katika kipindi cha Maimamu wawili (Maimamu Hadi na Askar), kutokana na kukua zaidi jamii ya Kishia na kufungwa na kuwekewa vikwazo na sheria kali Maimamu Hadi na Askary (a.s), kulipelekea kuongezeka zaidi kiwango cha kutolewa barua na maandiko yenye maagizo maalumu au kujibu maswali kutoka kwa Maimamu hawa wawili ikilinganishwa na Maimamu wa hapo kabla [6].

Katika zama za uwepo wa Maimamu (a.s), yaani katika zama za uhai na uwepo wa Maimamu, tawq’i ilikuwa ikitajwa na kufahamika kwamba, ni barua na maandiko tu kutoka kwa Maimamu yanayotoa majibu ya maswali kwa Mashia na wafuasi wao. Ama kuhusiana na Imam Mahdi (a.j.t.f) ni kwamba maandiko yake yote yalikuwa yakihesabiwa kuwa ni tawqi’, hata kama maandiko hayo hayakuwa ni majibu kwa matkwa au maswali (ya wafuasi wa Imam). Halikadhalika maana ya tawqi’ imetumika pia katika hadithi za Imam Mahdi (a.j.t.f) ambazo hazijaandikwa (haziko katika sura ya maandishi) [7].

Hati ya Tawqi’

Tawq’i ilikuwa ima ni hati ya Maimamu wenyewe au imla ambayo Maimamu walikuwa wakisomea watu wengine (wafuasi wao) na kisha wao kuandika yaliyokuwa yakisemwa na hivyo kuyaweka matamshi hayo katika sura ya maandiko.[8]. Wao katika baadhi ya vipengele, waliandika kitu chini ya maandiko hayo na kubainisha kwa hati zao wenyewe. [9] Inaelezwa kuwa, kuna uwezekano kubainisha na kuweka wazi chini ya maandiko kwa hati ya Imam Mahdi (atfs) [10], ilikuwa ni kwa ajili ya kutambua barua za waongo ambazo zilizokuwa zikinasibishwa na Imam au kwa ajili ya kutambua madai ya baadhi waliokuwa wakienda kinyume kuhusiana na uandishi wa barua na maandiko ya Imam [11]. Ushahidi wa wazi katika suala hili ni kwamba; Ahmad bin Is-haq Qumi, alipokutana na Imam Askary (a.s) alimuomba Imam amwandikie andiko ambalo kupitia andiko hilo yeye aweze kuzitambua barua asili na za kweli zitokazo kwa Imam (a.s), naye Imam (a.s) akamkubalia ombi lake na akamwandikia [12]. Masahaba na wafuasi wa Maimamu (a.s) walikuwa wakizijua barabara hati za Maimamu na miandiko yao kiasi kwamba walikuwa wanaweza kutofautisha hati na miandiko hiyo ya Maimamu na hati na miandiko isiyokuwa ya Maimamu (a.s) [13].

Kutuma barua kupitia mtandao wa mawasiliano wa wawakilishi

Kubadilishana (kwa kupeleka) na kurejesha barua na maandiko ya Maimamu (a.s) kwa njia ya mawakili, wawakilishi na wajumbe wao (a.s), kulikuwa kukijulikana kwa jina la kanali au mtandao wa mawasiliano wa wawakilishi. Mashia wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s), waliitumia njia ya mawakili na wajumbe wa Maimamu (a.s) katika kufikisha malipo ya kisheria yaliyokuwa yalotolewa kwa ajili ya masuala mbalimbali kama khumsi, zaka na kadhalika kutoka katika sehemu mbali mbali. Walikuwa wakifikisha matakwa na maswali yao kwa Maimamu (a.s) kupitia njia ya mawakili wa Maimamu, na kwa njia hii hii walikuwa wakipokea majibu na barua kutoka kwa Maimamu (a.s) [14]. Katika kipindi cha Ghaiba Ndogo, wadhifa huu ulikuwa katika mikono ya Manaibu Wanne wa Imam Mahdi (a.j.t.f) [15]. Na wao walikuwa na mawasiliano na Mashia wa Ahlul-Bayt (a.s) wa sehemu tofauti tofauti kupitia njia ya mawakili wao [16]. Bila shaka mapokezi ya riwaya yapo yanayoonyesha kwamba Mashia wa Ahlul-Bayt (a.s) pia walikuwa na njia zingine zaidi ya hiyo ya kupitia kwa mawakili, ambazo walizitumia katika kuwafikishia Maimamu matakwa yao au kwa njia hizo walifanikiwa kuchukua barua na maandiko za majibu kutoka kwa Maimamu (a.s). Kwa mfano; kulingana na mapokezi ya Qutub Rawandi Muhammad bin Yusuf Shashi alifikisha barua yake kwa Imamu (a.j.t.f) kupitia kwa mwanamke mmoja ambaye alikuwa na fursa ya kwenda na kurejea katika nyumba ya Imamu Mahdi (a.j.t.f) na akapokea barua na maandiko kutoka kwa Imam (a.j.t.f).[17]

Barua na maandiko hayo baada ya kutolewa na Imam (a.j.t.f), yalikuwa yakitumwa kwa njia ya mjumbe makhsusi kwa kuzingatia alama na vielelezo vilivyoelekezwa [18]. Wasifu na utambulisho wa wabebaji wa barua hizo haujaelezwa katika mapokezi na ripoti, bali umekuja kwa majina na ibara kama vile mwanamke, mjumbe kutoka kwa Hussein ibn Ruh au mjumbe wa khalifa [19]. Sababu ya kitendo hiki imetambuliwa kuwa ni taqiya [20].

Maudhui

Barua na maandiko hayo hayakuwa mahususi katika maudhui moja. Kwani nyingi miongoni mwazo zilikuwa zimetolewa kwa ajili ya majibu kuhusiana na maswali ya kifiqhi, itikadi pamoja na matakwa ya Mashia (wafuasi wa Ahlul-Bayt a.s) kuhusiana na masuala mbalimbali. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana, katika barua na maandiko hayo kumezungumziwa maudhui tofauti tofauti. Miongoni mwa maudhui hizo ni kama ifuatavyo: Kuwateua na kuwauzulu mawakili na wawakilishi (wajumbe), kubainisha wadhifa wa mawakili, kutangaza kufika kwa malipo ya kisheria, kuwakadhibisha wenye madai ya uongo ya kudai unaibu wa Imam (a.s) na majibu ya matakwa mahususi ya Mashia (wafuasi wa Ahlil-Bayt a.s). [21]

Itibari ya barua na maandiko tajwa

Kwa mtazamo wa wanazuoni wa fikihi (mafakihi) ni kwamba, kila barua na andiko ambalo utapatikana uhakika kwamba, linatoka kwa Maimamu litakuwa ni yenye itibari [22]. Kwa sababu hii baadhi ya mafakihi wa Kishia walitumia baadhi ya barua na maandiko hayo kama nyaraka na ushahidi katika mchakato wao wa kunyambua hukumu na sheria za Kiislamu. [23]. Na pamoja hali hii, baadhi ya wanafiqhi walifanya mdahalona kuhoji kuhusiana na itibari ya maandiko (ambayo kawaida ni barua na maagizo ya kimaandishi) [24] na hivyo hawakuyatambua maandiko hayo kuwa yana daraja sawa au yanalingana na hadithi za kutamkwa [25]. Ama katika vitabu vya fiqhi hakuna dalili iliyotajwa ya kutokuwa na itibari kwa maandiko au itibari yake kutokuwa sawa na hadithi ya kutamkwa [26]. Kadhalika kinyume na kauli hii, imesemekana kwamba, kuandika, sira ya Maimamu wa Kishia pamoja na mbinu iliyozoeleka baina ya kaumu mbali mbali ni mambo ambayo yalikuweko [27] na kulikuwa kukitolewa maandiko na maagizo ya kimaandishi kwa ajili ya kufanyia kazi mambo.[28]

Tawqi’ za Imam Mahdi (a.j.t.f)

Makala ya Asili: Tawqi’ ya Imam wa Zama (a.j.t.f)

Tawq’i inaashiriwa kuwa ni barua na maandiko ya Maimamu 12 wa madhehebu ya Shia Ithnasharia. Barua na maandiko haya yaliandikwa kwa hati za Maimamu na kawaida yalikuwa yakiandikwa katika majibu ya maswali na matakwa ya Mashia (wafuasi Ahlul-Bayt). Katika vyanzo visivyopungua 100, imeashiriwa kwamba kuna maandiko na barua za Imam Mahdi (ajtf) katika maudhui za kifikihi, kiitikadi na kadhalika. [29]

Utambuzi wa vyanzo

Barua na maandiko (ya Maimamu wakitoa maagizo au kujibu maswali) ni jambo ambalo limenukuliwa kwa sura isiyo na mpangilio katika vyanzo vya riwaya vya Kishia. Katika kitabu kiitwacho Rijal al-Kashi kumenukuliwa barua na maandiko mengi kutoka kwa Maimamu wa madhehebu ya Shia [30]. Katika vitabu vya Kamalu-al-Din cha Sheikh Swaduq na Al- Ghaiba cha Sheikh Tusi, maandiko na barua za Imam Mahdi (ajtf) zimekusanywa humo katika mlango maalumu na wa kujitegemea. [31]

Vilevile kuhusiana na barua na maandiko haya kumeandikwa athari na vitabu kwa sura ya kujitegemea, nazo ziliandikwa katika karne ya tatu Hijria na kuendelea. Katika kitabu cha Rijal Najashi, moja ya vitabu vya (Masa’ili Abi Muhammad wa tawqi’at, ( Qurbul-Isnad ila swahibil- Amri Wa- Zaman) na ( Mas’ili Al- Rijali wa mukatabatihim Abal-Hassan al- Thalith a.s), kitabu cha Abdullah bin Ja’far Himyari mpokezi wa hadithi wa madhehebu ya (Shia) Ahlul-Bayt (a.s) katika karne ya tatu Hijria, [32] na kitabu cha tawq’iat kilichoandikwa na Muhammad bin Issa bin Ubayd ambaye ni miongoni mwa maswahaba wa Imam Jawad (a.s). [33]

Kitabu cha At-Tawaqi’ kilichoandikwa na Abdullah bin Salt mmoja wa mwaswahaba wa Imam Ridhwa (a.s) ni miongoni mwa athari zingine katika kadhia hii. [34].

Vyanzo

  • ʿĀmilī, Sayyid Jawād. Miftāḥ al-karāma fī sharḥ qawāʿid al-ʿallāma. Edited by Muḥammad Bāqir Khāliṣī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1419 AH.
  • Ḥārithī, Ḥusayn b. ʿAbd al-Ṣamad. Wuṣūl al-akhbār ilā ḥuṣūl al-akhbār. [n.p]: Majmaʿ l-Dhakhāʾir al-Islāmīyya, 1041 AH.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Mukhtalaf al-Shīʿa fī aḥkām al-sharīʿa. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn, 1413 AH.
  • Ḥillī, Jaʿfar b. al-Ḥasan al-. Al-Muʿtabar fī sharḥ al-mūkhtaṣar. Qom: Dār Sayyid al-Shuhadāʾ, 1407 AH.
  • Ḥimyarī, ʿAbd Allāh b. Jaʿfar al-. Qurb al-isnād. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1413 AH.
  • Imām Khomeinī, Sayyid Rūḥ Allāh. kitāb al-bayʿ. Qom: Ismāʿīlīyān, 1363 Sh.
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Ḥayāt-i fikrī wa sīyāsī-yi Imāmān-i Shīʿa. Third edition. Qom: Muʾassisa-yi Intishārāt-i Anṣārīyān, 1381 Sh.
  • Kanī Tihrānī, ʿAlī. Tawḍīḥ al-maqāl fī ʿilm al-rijāl. Edited by Muhammad Husayn Mawlawī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1421 AH.
  • Kashshī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Ikhtīyār maʿrifat al-rijāl known as Rijāl al-Kashshī. Edited by Ḥasan Muṣṭafawī. Mashhad: Intishārat-i Dānishgāh-i Mashhad, 1409 AH.
  • Khoeī, Sayyid Abū l-Qāsim al-. Muʿjam rijāl al-ḥadīth wa tafṣīl ṭabaqāt al-ruwāt. Qom: Markaz Nashr al-Thiqāfīyya al-Islāmīyya, [n.d].
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1407 AH.
  • Muḥammadī Reyshahrī, Muḥammad. Dānishnāma-yi Imām Mahdī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1393 Sh.
  • Murtaḍā al-Zabīdī, Muḥammad b. Muḥammad. Tāj al-ʿarūs min jawāhir al-qāmūs. Edited by ʿAlī Hilālī, ʿAlī Sīrī. Beirut: Dār al-Fikr, 1414 AH.
  • Najāshī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Rijāl al-Najāshī. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī Tābiʿat li Jamāʿat al-Mudarrisīn, 1365 Sh.
  • Rāwandī, Saʿīd b. Hibat Allāh al-. Al-Kharāʾij wa l-jarāʾiḥ. Qom: Muʾassisat al-Imām al-Mahdī, 1409 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Kamāl al-dīn wa itmām al-niʿma. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Islāmiyya, 1395 AH.
  • Shubayrī Zanjānī, Muḥammad Jawād. "Tawqīʿ". Dānishnāmah-yi Jahān Islām. Tehran: Bunyād-i Dāʾirat al-Maʿārif al-Islāmī, 1383 Sh.
  • Ṭabrisī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Al-Iḥtijāj ʿalā ahl al-lijāj. Edited by Muḥammad Bāqir Khirsān. Mashhad: Nashr-i Murtaḍā, 1403 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Ghayba. Edited by ʿIbād Allāh Tihrānī & ʿAlī Aḥmad Nāṣiḥ. Qom: Muʾassisat al-Maʿārif al-Islāmīyya, 1411 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Istibṣār fīmā ikhtalafa min al-akhbār. Edited by Sayyid Ḥasan al-Khirsān. 1st edition. Tehran: Dar al-Kutub al-Islāmiyya, 1390 AH.