Mapambano Kati ya Taluti na Jaluti
Mapambano Kati ya Taluti na Jaluti: Mapambano kati ya Taluti na Jaluti ni miongoni mwa visa vilivyomo ndani ya Qurani kuhusiana na mapambano kati ya Taluti, ambaye ni mmoja wa wafalme wa Wana wa Israeli, na Jaluti, aliyekuwa adui wa Wana wa Israeli. Kisa hichi kimesimuliwa katika Aya ya 246 hadi 251 za Suratu Al-Baqara. Kwa mujibu wa simulizi za Qurani, Wana wa Israeli walipoteza mwelekeo wa mafundisho ya Mungu na wakaangukia ndani ya uonevu wa Wapalestina, na hatimae kupoteza Sanduku lao muhumi la Agano kati yao na Mola wao. Sanduku hili lilikuwa ni nembo tukufu na muhimu mno kwa Wana wa Israeli.
Baada kukubwa na hali kama hiyo, Mwenye Ezi Mungu alimchagua mtu asiyejulikana kwa jina la Taluti kuwa ni mfalme wao. Jeshi kubwa la Wayahudi lilimkusanyikia mfale huyu kwa nia ya kujigomboa; ila baada ya mitihani mingi, wangi kati yao walirudi nyuma, na ni wachache tu waliobaki pamoja naye. Ilipowadia siku ya mapambano, Nabii Daudi (a.s) alilifanikiwa kumuua Jaluti kwa kumpopoa jiwe kwa kutumia kombeo, na Wana wa Israeli wakashinda vita hivyo. Kwa mujibu wa maoni ya wafasiri wa Kishia, kisa hichi cha Qur’ani kinaashiria umuhimu wa jihad dhidi ya dhulma na ufisadi, sifa inayohitajika kwa ajili uongozi na uimamu, pamoja na kusimama imara katika kukabiliana na mitihani ya Mungu. Pia kwa maoni yao, kisa hichi kinatoa welewa ya kwamba; wingi wa idadi si kigezo cha ushindi, na kwamba ushindi na hatima njema ni kwa waumini. Katika baadhi ya riwaya, kisa cha mitihani katika kuchagua wafuasi wa Imamu Mahdi (a.f), kimefananishwa na mitihani waliotahiniwa nayo wafuasi wa Taluti.
Watafiti wanamfananisha Taluti aliyetajwa katika Qur’ani, na Shauli aliyetajwa ndani ya Agano la Kale. Hata hivyo, simulizi ya Qur’ani kuhusu vita hivi, ni tofauti na ile ya Agano la Kale. Hadi leo hii tukiwemo katika karne ya 21, bado Simulizi hii ya Shauli iliyotajwa ndani ya Agano la Kale, inaendelea kutumiwa katika katika fasihi za kisiasa za viongozi wa utawala wa Kizayuni. Umuhimu wa Hadithi ya Vita vya Taluti na Jaluti
Kisa cha vita vya Taluti na Jaluti ni miongoni mwa visa muhimu vilivyomo ndani ya Qur’an. Kisa hichi kinapatikana ndani ya Aya ya 246 hadi ya 251 za Suratu Al-Baqarah. Kwa mujibu wa wafasiri na watafiti wa Kishia, kisa hichi kimekuwa ndio chanzo msingi kilichotumiwa katika kujenga fikra kadhaa, kama vile umuhimu wa jihad, sifa za viongozi wanostahiki kushika madaraka, pamoja na kutoa msukumo uliopelekea ushindi kwa waumini dhidi ya makafiri. [1] Wafasiri wa Kishia, wakitegemea kisa cha Taluti, wametoa hoja isemayo kwamba; viongozi wanapaswa kuwa na sifa ya elimu na ushujaa, ili waweze kuwajibika ipaswavyo katika uongozi wao. [2] Katika Hadithi za Kishia, sifa zimetaja sifa mbili kuwa ndio sifa muhimu na za msingi kwa Imamu. [3] Aidha, katika baadhi ya Riwaya, suala la kutahiniwa kwa wafuasi wa Imamu Mahdi (a.f) limefananishwa na mitihani ya Mungu kwa wafuasi wa Taluti. [4] Kisa hichi pia kinaashiria kwamba; idadi ya wafuasi si kigezo cha ushindi kwa watu fulani, bali ni imani na uthabiti wao ndiyo msingi wa mafanikio.
Ushindi wa Daudi (a.s) dhidi ya Jaluti uliotokana na imani madhubuti, ni alama inayo oneshwa ya kwamba; imani thabiti na kutumia maarifa sahihi katika vita na changamoto za maisha ndiyo sababu ya kufuzu ndani ya mbambo hayo.
Kuundwa kwa Jeshi la Taluti
Kulingana na tafsiri za wafasiri mbali mbali wa Kiislamu, baada ya kifo cha Nabii Musa (a.s), Wana wa Israeli walipoteza mwelekeo na kuwa mbali na mafundisho ya Mola wao, jambo lililowafanya kukumbwa na wimbi la migawanyiko ndani ya jamii yao. Hali hii ndiyo iliyo sababisha kushindwa kwao katika mapambano yao dhidi ya Wafilisti (Wapalestina), na hatimae kufukuzwa kutoka katika ardhi zao, na kupoteza Sanduku la Agano lao. [5] Waisraeli walimwomba Nabii Shamu'ili awachagulie kamanda ili wapambane dhidi ya maadui zao. [6]. Hapo Mwenye Ezi Mungu akamchagua Taluti kuwa kamanda wao, mtu ambaye hapo awali hakuwa maarufu miongoni mwao. Kulingana na vyanzo mbalimbali, Waisraeli walilalamika wakisema kwamba; Taluti hakuwa na nasaba mashuhuri wala utajiri miongoni mwa. [7] Hata hivyo, Mungu aliwarejeshea Sanduku la Agano lao kama ishara ya Kiungu, na hivyo Waisraeli wakamkubali Taluti kuwa ni kamanda wao. [8] Baada ya ishara hii ya Kiungu, umati mkubwa wa Waisraeli ulijiunga na jeshi la Taluti. [9] Vita Dhidi ya Kikosi cha Jaluti Kulingana na Aya za Qur'ani, Taluti aliwaambia wanajeshi wake ya kwamba; kabla ya wao kuingia vitani kwanza watapitia mtoni, na hakuna yeyote yule katia yao mwenye ruhusa ya kunywa maji ya mto huo, isipokuwa kiasi kidogo tu, kisha waendelee na safari yao. [10] Hata hivyo, wengi walikunywa maji ya mto huo kupindukia kiasi walichoshauria. [11]. Baadhi ya vyanzo vinasema kwamba; baada ya kunywa maji hayo, maelfu ya wafwasi wa Taluti waliasi jeshi na kupoteza nguvu za imani zao. [12] Taluti aliwaacha waasi hao na kuelekea vitani akiwa pamoja na wachahe walifwata ushauri wake kuhusiana na maji hayo. [13] Baadhi ya wanajeshi waliobaki walihofia idadi yao ndogo waliokuwa nayo, lakini wale waliomwamini Mungu kisawasawa walibaki imara chini ya uongozi wa Taluti. [14] Mwanzoni mwa vita, hakukua na mtu aliyethubutu kupambana na Jaluti, shujaa hodari wa Wafilisti. Lakini kijana mdogo aitwaye Daudi (a.s) alirusha jiwe kwa kutumia kombeo, nalo likampiga Jaluti kwenye paji la uso naye akaanguka na kufariki papo hapo. [15] Kifo cha Jaluti kiliwatia hofu wapambanaji wa Kifilisti, na kushindwa mbele ya jeshi dogo la Taluti, na hivyo Wana wa Israeli wakapata ushindi kirahisi. [16] Tafsiri za Wafasiri Mbalimbali Kuhusiana na Kisa Hichi Kisa hichi kimefasiriwa na wanazuoni wa Kiislamu kwa mitazamo mbalimbali, hku wakijaribu kutaja faida mbali mbali za kisa hichi kama ifuatavyo:
Umuhimu wa Jihad Dhidi ya Dhuluma na Ufisadi: Baadhi ya wataalamu wanaamini kwamba; Qur'ani, kwa kusimulia kisa cha vita kati ya Taluti na Jaluti, inakusudia kuonesha umuhimu wa kupambana na dhuluma na ufisadi. [17] Kulingana na Aya za Qur'ani, Wana wa Israeli walimwomba Mungu awachagulie kamanda wa kupambana na ufisadi wa Jaluti, na waliahidi kumtii kamanda huyo wakati wa jihad dhidi ya dhulma walizokuwa wakitendewa. Lakini wakati wa vita ulipowadia, wengi kati yao walikiuka ahadi zao. [18]. Hata hivyo, kundi dogo lililoshikamana na imani zao lilibaki na hatimae lilifanikiwa kumshinda adui yao. [19]
• Sifa za Viongozi na Watawala: Aya za 246 hadi 251 za Suratu Al-Baqarah zinaonesha kwamba; uwezo wa kielimu na kimwili, ni sifa mbili muhimu za kiongozi wa watu ndani ya jamii, na wala utajiri au nasaba haizizingatiwa kama ni vigezo muhimu katika kumchagua kiongozi fulani ndani ya jamii. [20] Fadhil bin Hassan Tabarsi, mmoja wa wafasiri mashuhuri wa Kishia, akitegemea kisa cha Taluti, anasisitiza kwamba; Imamu anapaswa kuwa ni mtu mwenye uwezo wa elimu, na kwa na sifa ya ushujaa zaidi katika umma wake. [21] Pia jambo hili limefafanuliwa wazi katika Hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) [22]. Katika Hadithi nyingine zilizomo vitabuni, utawala wa Taluti unachukuliwa kuwa ni miongoni mwa mifano ya mafanikio ya serikali iliyoteuliwa na Mwenye Ezi Mungu mwenyewe, ambayo ni tofauti na ile inayosimama kwa nguvu au kuwapindua watu fulani. [23] Kulingana na maoni ya Allama Tabatabai, Aya hizi zinaonesha kwamba; kiongozi anapaswa kuendesha masuala ya jamii kupitia njia na mfumo maalumu utakaodhamini ukamilifu mmoja anyestahili kufikia ukamilifu huo. Serikali yenye uwezo wa kuhakikisha jambo hilo, ni ile serikali yenye kiongozi mwenye elimu yenye uwezo wa kudhamini maslahi yote ya maisha ya kijamii, pamoja na uwezo wa kuyatimiza maslahi hayo, sifa ambazo zote ziliku zikipatikana ndani ya utawala wa Taluti. [24]
• Umuhimu wa Kutoyumba Mbele ya Mitihani ya Kiungu: Kulingana na maoni ya mfsiri wa Qur’ani Mohsin Qara'ati, ni kwamba; Aya zizungumziazo kisa hichi, zinaonesha kwamba; wakati mwingine watu wanaodai kupigana katika njia ya Mwenye Eiz Mungu, huweza kufanikiwa katika hatua za mwanzo za baadhi ya mitihani ya Kiungu, lakini wanaweza kushidwa mwishoni mwa mitihani. [25] Kwani tukiziangalia Aya hizi, tutakuta zinabainisha ya kwamba; mitihani ya jeshi la Taluti ilihusisha watu wengi ndani yake, ambao mwanzoni walionesha utayari wao wa kupambana na adui yo, lakini baada ya amri ya vita kutolewa, wakarudi nyuma na kuachana na amri hiyo. Baadhi yao walijitenga na Taluti kwa kudai kwamba; Taluti hakuwa ni mtu mwenye nasaba maarufu miongoni mwao wala hakuwa na uweza wa mali. Pia miongoni mwa wale waliokubaliana na uongozi wake, kuna wale walioasi amri ya kutokunywa maji ya kutosha, iliyotolewa na kamanda Taluti. Na pia miongoni mwa waliotii amri hiyo, kuna wale waliokhofia kupambana na maadui zao kutokana na khofu ya ukubwa wa jeshi la maadui hao. hivyo, ni kundi dogo tu lilibaki na kupambana na maadui zao chini ya uongozi wa Taluti. [26] Katika baadhi ya Hadithi, mto waliokatazwa wafuasi wa Taluti kunywa maji yake, umetajwa kama ni mfano wa mitihani watakayotahiniwa nayo wafwasi wa Imamu Mahdi wakati wa kuja kwake (Mungu aharakishe kudhihiri kwake). [27]
• Ushindi wa Wachache Wenye Imani Dhidi ya Makafiri Walio Wengi: Ushindi wa jeshi dogo la Taluti dhidi ya jeshi kubwa la Jaluti, katika maandiko ya Kiislamu, umechukuliwa kuwa ni mfano hai wa ushindi wa waumini dhidi ya makafiri, licha ya ukweli wa kwamba; idadi ya waumini ni ndogo kuliko ya makafiri. [28] Imenukuliwa kutoka kwa Imamu Baqir (a.s) ya kwamba; Mwishowe, ni watu 313 tu waliotii amri ya Taluti na kushiriki katika vita dhidi ya Jaluti. [29] Watafiti wanasema kwamba; Kwa mtazamo wa Qur'ani, kilichosababisha ushindi wa jeshi dogo la Taluti, ilikuwa ni nguvu ya imani yao waliokuwa nayo. [30] Simulizi ya Agano la Kale Kuhusu Vita Hivi Watafiti wanaamini kwamba; Taluti aliye tajwa ndani ya Qur'ani ndiye yule Shauli aliye tajwa katika Agano la Kale. [31] Shauli katika Agano la Kale anafafanuliwa kama ni nabii miongoni mwa manabii, ila wakati mwingine alikuwa akifanya mambo ambayo hayakumpendeza Mwenye Ezi Mungu. [32] Kwa mfano, yeye alipinga na kukataa amri ya kuharibu na kuchoma nyumba za Wafilisti, jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya Mungu. [33] Pia, pale Mungu alipomchagua Daudi kuwa mfalme wa Wana wa Israeli, Taluti alimwonea wivu, na hivyo kumtuma akaamua mwe Daudi mstari wa mbele katika vita. [34] Katika Agano la Kale, imeelezwa kwamba; hatimae Shauli alishindwa na Wafilisti na akaamua kujiua. [35] Marejeleo ya Viongozi wa Utawala wa Kizayuni Kuhusu Hadithi Hii Baadhi ya vyanzo vinamchukulia Jaluti kama ni mfalme na kamanda wa kabila la Amaleki “عمالیق” (kabila katika Palestina ya kale). [36] Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israeli, baada ya operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa", aliwataja Wapalestina kama Wa-amaleki. [37] Marejeleo haya ya Netanyahu ni mojawapo ya mifano ya matumizi ya kisa cha vita vya Shauli. Kulingana na simulizi ya Agano la Kale, Mwenye Ezi Mungu alimwamuru Shauli kuwaua Amaleki na kuangamiza jamii ya wanawake, watoto wadogo, pamoja na wanyama wao. Amri hii ilikuja kwa sababu ya udahlimu wa utawala wa jamii hii uliotangulia kabla ya Shauli, ambao ulidumu kwa muda wa miaka 350, uliowazuia Wana wa Israeli kukanyaga ardhi zao. [38]
Imefasiriwa kulingana na Makala ya Kifarsi ifuatayo:
https://fa.wikishia.net/w/index.php?title=%D9%86%D8%A8%D8%B1%D8%AF_%D8%B7%D8%A7%D9%84%D9%88%D8%AA_%D9%88_%D8%AC%D8%A7%D9%84%D9%88%D8%AA&oldid=1328364