Israeli
Israeli: ni lakabu ya Nabii 'Yakobo/Yaaquub.' Kulingana na tafsiri ya kitabu Majma‘u al-Bayan, neno 'Israeli' katika lugha ya Kiebrania humaanisha 'Mteule wa Mungu' au 'Mtumishi wa Mungu'. [1] Sheikh Tusi maana ya jina hili, anasema kwamba; 'Israeli' limeundwa kunatokana na maneno mawili; la kwanza ni 'Isra,' ambalo linamaanisha mtumishi, na la pili ni 'Il', linalomaanisha Mwenye Ezi Mungu, na hivyo 'Israeli' likawa na maana ya 'Mtumishi wa Mungu'. [2] Kulingana na wafasiri wa Kishia, neno 'Israeli' lililopo katika Aya ya 93 ya Suratu Al-Imran, na Aya ya 58 ya Suratu Maryam, linamhusiana moja kwa moja na 'Yakobo/Yaaquub'. [3] Hii ndiyo sababu hasa ya wana wa nabii 'Yakobo/Yaaquub' na vizazi vyake kumepewa jina la 'Bani Israeli' katika Qur’ani. [4] KatikaTaurati kuna kisa kinachoeleza kwamba; Moja kati ya nyusiku (wingi neno usiku), Mwenye Ezi Mungu alishindana na Yakobo kwa kupigana naye mieleka, na baada ya Mwenyezi Mungu kushindwa na kudhibitiwa na nabi 'Yakobo/Yaaquub', alimwambia nabi huyo kwa kusema: 'Niachilie, kwa kuwa tayayari usiku umeshaanza kupambazuka,' Hapo 'Yakobo/Yaaquub' akajibu: 'Sitakuachilia hadi unibariki.' Mwenye Ezi Mungu akamwuliza: 'Jina lako ni nani?' Naye akajibu: Yakobo/Yaaquub, Mwenye Ezi Mungu akamwambia: 'Kuanzia sasa hvi jina lako si 'Yakobo/Yaaquub', bali utajulikana kwa jina la Israeli, kwa sababu umeonyesha nguvu zako dhidi ya Mungu pamoja na binadamu na hatimae ukawashinda'. [5]