Al-Hakim al-Shar’i

Kutoka wikishia

Al-Hakim al-Shar’i (Kiarabu: الحاكم الشرعي) au Hakimu wa sheria ni Mwanachuoni wa masuala ya Fiqhi aliyetimiza masharti na vigezo vya kuhukumu katika mizozo na hitilafu baina ya Waislamu. Kuchukua na kubeba jukumu la Hakim Shar’i ni wajib Kifai (huu ni wajibu ambao wakitekeleza baadhi basi unawaondokea watu wengine yaani sio wajibu kwao kutekeleza), na kwa mujibu wa hili, faqihi mmoja akitoa hukumu juu ya jambo fulani, faqihi mwingine hawezi kulipinga. Wakati wa kutokuwepo kwa Imamu wa Zama (Imamu Mahdi), mafaqihi wanachukua nafasi ya mtawala wa Sheria kwa niaba ya Imamu maasumu.

Kuhusiana na mipaka ya mamlaka ya mtawala wa Sheria kuna mitazamo tofauti; baadhi ya mafakihi wamewekea mipaka mamlaka ya mtawala wa Sheria katika masuala kama usimamizi wa mayatima na kuchukua uamuzi kuhusiana na mali za wasiokuweko na mkabala wao, kundi la Maulamaa linasema kuwa, mamlaka ya mtawala wa sheria ni kama mamlaka ya Maasumina.

Ili kuthibitisha mamlaka ya kisheria ya mafaqihi, kunatumiwa kama hoja hadithi ambapo hadithi kama Maulamaa ni warithi wa Mitume, watunza amana (waaminifu) wa Mtume au warithi wake ni miongoni mwazo. Kadhalika hoja ya kiakili (kulinda nchi, nidhamu katika masuala ya dini na dunia ya waja na ijma'a) navyo vimetumika kwa ajili ya kuthibitisha mafaqihi kuwa ni watawala wa sheria.

Utambuzi wa maana

Al-Hakim al-Shar’i ni faqihi aliyetimiza masharti anayetoa hukumu katika mizozo na hitilafu baina ya Waumini. [1] Kwa muktadha huo, faqihi aliyetimiza masharti mbali na kutoa fat'wa akiwa kama Marjaa Taqlidi, ana jukumu la kutoa hukumu pia akiwa kama mtawala wa sheria [2] na kuchukua na kubeba jukumu la Hakim Shar'i (mtawala wa sheria) ni wajib Kifai [3] (huu ni wajibu ambao wakitekeleza baadhi basi inawaondokea watu wengine yaani sio wajibu kwao kutekeleza). Ni wajibu kufuata hukumu ya mtawala wa sheria. [4] Istilahi hii iliingia katika vitabu vya fiq’h kuanzia zama za Allama Hilli. [5]

Imam Khomeini baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran aliitumia istilahi ya mtawala wa sheria kwa makadhi (mahakimu) ambao wanajishughulisha na utoaji hukumu katika maeneo mbalimbali. [6]

Hoja ya kwamba, mafakihi ni watawala wa sheria

Katika vitabu mbalimbali vya Fiqhi kunazungumziwa suala la mafaqihi kuwa ni watawala wa sheria katika zama za ghaiba ya Imamu Mahdi (a.t.f.s), [7] hoja hizi zimetegemea hadithi ambazo zinabainisha kwamba, Maulamaa ni warithi wa Manabii, [8] watunza amana (waaminifu) wa Mtume au warithi wake (viongozi baada yake). [10]

Mbali na hoja za hadithi, kuna hoja za kiakili za kuthibitisha kwamba, mafaqihi ni watawala wa sheria katika zama za ghaiba; mafaqihi wanaamini kwamba, akili ileile ambayo imeona kuna ulazima wa Imamu kuteuliwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kulinda nchi, na kuleta nidhani katika masuala ya dini na dunia kwa waja wa Allah, basi ndio akili hiyo hiyo ambayo inahukumu kwamba, kuna ulazima Imamu awe na mrithi katika zama za ghaiba yake. [11] Ili kuthibiutisha hilo, kumetumiwa pia ijma'a. [12]

Mamlaka

Mafaqihi wametofautiana kuhusiana na mipaka na mamlaka ya mtawala wa sheria. Baadhi wanasema kuwa, mamlaka yake yanahusiana na masuala ambayo yamebainishwa na Qur’ani na katika hadithi; kama masuala yanayohusiana na mayatima na mali ambayo wenyewe hawapo (hawajulikani). [13] Baadhi ya wengine wanaamini kwamba, mamlaka yake ni mamlaka yale yale ya Maimamu. [14]

Mgongano baina ya watawala wa sheria

Mafaqihi wanaamini kuwa, kwa kuzingatia kuwa, mafaqihi waliotimiza masharti ni watawala wa sheria, endapo mmoja atatoa hukumu kuhusiana na jambo fulani, haijuzu na hata ni haramu kwa mafaqihi wengine kupinga hilo; kwa sababu kwanza kabisa kuwa mtawala wa sheria ni wajibu kifai na kama mtu atalifanya hilo kwa usahihi kama ilivyo kwa wajibu zingine ambazo ni wajibu kifai haijuzu kupinga, pili upinzani wa marajii wengine kwa hukumu ya mtawala wa sheria yumkini hilo likapelekea kuvurugika nidhamu (katika jamii) na kuleta mizozo na mivutano jambo ambalo bila shaka Mwenyezi Mungu hataliridhia. [17]

Vyanzo

  • ʿAmilī al-Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. Nūr al-Dīn ʿAlī b. ʾAḥmad al-. Al-Rawḍat al-bahīyya fī sharḥ al-Lumʿa al-Dimashqīyya. Edited by Sultān al-ʿUlamāʾ Ḥasan b, Muḥammad. Qom: Intishārāt-i Daftar-i Tablīghāt-i Islāmī, 1412 AH.
  • Baḥrānī, Yūsuf b. Aḥmad. Al-Ḥadāʾiq al-Nāẓira fī aḥkām al-ʿitra al-ṭāhira. Edited by: Muḥammad Taqī Īrawānī & ʿAbd ah-Razzāq Muqarram. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī-yi Jāmiʿat al-Mudarrisīn, 1405 AH.
  • Ḥakīm, Sayyid Muḥsin Ṭabāṭabāyī. Nahj al-fiqāha . Qom: Intishārāt-i 22 Bahman, n.d.
  • Hāshimī Shāhrūdī, Sayyid Maḥmūd. Farhang-i Fiqh muṭābiq-i madhhab-i Ahl al-Bayt. Qom: Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif-i Fiqh-i Islāmī, 1382 Sh.
  • Ḥaydarī, Muḥsin. Wilāyat al-faqīh Tārīkhhā wa Mabānīhā. Beirut: Dār al-Walāʾ li-l-Ṭibāʿa wa al-Nashr wa al-Tawḍīʿ, 1426.
  • Jawādī Āmulī, ʿAbd Allah. Wilāyat-i faqīh wilāyat-i fiqāhat wa ʿidālat. Qom: Markaz-i Nashr-i Asrāʾ, 1379 Sh.
  • Kāshif al-Ghiṭāʾ Najafī, ʿAlī b. Muḥammad Riḍā b. Hādī. Al-Nūr al-sāṭiʿ fī al-fiqh al-nāfiʿ. Najaf: Maṭbaʿat al-Ādāb, 1381 AH.
  • Labānī Muṭlaq, Muḥammad Ṣādiq. 1391 Sh. "Ḥākim-i Sharʿ", Dāʾirat al-Maʿārif-i Buzurg-i Islāmī 20, p. 33.
  • Miṣbaḥ Yazdī, Muḥammad Taqī. Pursishhā wa pāsukhhā. Qom: Muʾassisa-yi Āmūzishī wa Pazhūhishī-yi Imām khomini, 1380 Sh.
  • Qummī, Sayyid Taqī Ṭabāṭabāyī. Al-Dalāʾil fī sharḥ-i muntakhab al-masāʾil. Qom: Maḥallātī, 1423 AH..
  • Raḥmān Sitāyish, Muḥammad Kāẓim. Rasāʾil wilāyat al-faqīh. Qom: Intishārāt-i Daftar-i Tablīghāt-i Islāmī, 1425 AH.
  • Rūḥānī, Sayyid Ṣādiq. Fiqh al-Ṣādiq. Qom: Dār al-Kitāb, 1412 AH.
  • Ṣadr, Sayyid Muḥammad Bāqir. Al-Fatāwā al-wāḍiḥa wifq li-madhhab Ahl al-Bayt. Beirut: Dār al-Taʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1403 AH.