Kufungua na Kuvunja Swaumu

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Kufungua Saumu)
Karamu ya Iftar katika Haram ya Imam Ridha (a.s)

Kufungua au Kuvunja Swaumu (Kiarabu: اِفطار) Ni kitendo kinachotimia kwa kula chakula au kunywa kinyaji fulani. Katika dini ya Kiislamu, kisheria ni haramu kabla ya Magharibi ya kisheria mtu kuvunja saumu ya mwezi wa Ramadhani au saumu ya nadhiri iliyonadhiria na kuanishiwa siku maalaumu. Kwa upande wa pili, pia ni haramu kufunga kwa mtu yule asiyeweza kufunga kutokana na hatari inayomkabili iwapo yeye atafunga, au kutokana na tabu na mashaka aliyo nayo mja huyo.

Kuna ada kadhaa zilizoainishwa kwa ajili ya futari, ikiwa ni pamoja na dua wakati kufutari na kusoma Surat al-Qadri. Aidha, kufutari kwa maji ya moto na maziwa, ni miongoni mwa sunna za kufutari. Katika vyanzo vya Hadithi kuna Riwaya nyingi mno zizungumziazo thawabu za kuwafuturisha wafungao.

Mofolojia (Utafiti wa Kilugha)

Futari, inamaanisha kufungua na kuvunja swaumu.[1] Pia tendo la chakula kabla ya sala ya Eid al-Fitr huitwa kufutari, nalo ni jambo moja wapo ya matendo yanayo pendekezwa na kushauriwa kutendwa kabla ya kusali sala ya Eid.[2]

Futari inaweza kuwa wajibu katika baadhi ya hali fulani na haramu katika hali nyingine. Miongoni mwa futari haramu ni futari ya kuvunja swaumu ya Ramadhani au saumu ya nadhiri iliyo ainishwa na kunuiliwa kufungwa katika siku maalumu, kabla ya Adhana ya Magharibi, kuvunja saumu ya qadhaa baada ya Adhana ya Adhuhuri, kuvunja saumu wakati wa Itikafu, na kufutari kwa msafiri aliyefunga ambaye ameanza safari yake baada ya Adhana ya Adhuhuri.[3] Ikiwa kufunga kunamletea mtu madhara au shida kubwa, mtu huyo atalazimika kufutari na kuvunja saumu yake.[4] Pia, ni pendekezo la Sunnah kufuturu mtu ambaye amekuwa akifunga funga ya Sunnah iwapo atakaribishwa na kuwa ni mgeni wa muumini fulani, lakini si vyema na ni makruhu (haependekezwi) kwa mtu huyo kufutari baada ya Adhana ya Adhuhuri.[5]

Kulingana na Hadithi, mtu aliyeko katika funga ni mtu mwenye kutakabaliwa maombi yake mbele ya Mola wake,[6] hasa zile dua aziombazo wakati wa futari.[7]

Adabu za kufutari

Kuna adabu kadhaa zilizotajwa kwa ajili ya kufutari, ikiwa ni pamoja na kusoma dua, kusoma Suratu al-Qadri wakati wa kufutari, na kufungua saumu baada ya kumaliza kusali Sala ya Magharibi.[8] Imesimuliwa ya kwamba; bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa akisoma dua ifuatayo wakati wa futari yake:«اللَّهُمَّ لَکَ صُمْنَا وَ عَلَی رِزْقِکَ أَفْطَرْنَا فَتَقَبَّلْهُ مِنَّا ; Ewe Mwenyezi Mungu! tumekufungia kwa ajili Yako na tunafungua saumu zetu kwa riziki Yako, basi ipokee saumu yetu».[9] Miongoni mambo yaliopendekezwa, ni kufutari kwa maji (hasa maji ya uvuguvugu), maziwa na vyakula vya vitamu, hususan tende.[10]

Kufurisha

Kulingana na riwaya zilizosimuliwa kutoka kwa Watakatifu (a.s), ni kwamba; kufutarisha watu funga ni miongongoni mwa matendo yenye fadhila nyingi mno. [11] Kati ya Hadithi zilizozungumzia suala hili, ni ile Hadithi itokayo kwa Imamu Swadiq (a.s) inayo fafanua kwa kusema kwamba; thawabu za yule anayetoa futari na kuwapa wafungao, ni sawa na thawabu ya wafungaji hao.[11] Waislamu katika nchi mbalimbali hutoa futari au huwafutarisha wafungaji wa mwezi wa Ramadhani kwa desturi na tamaduni tofauti. Katika baadhi ya maeneo matakatifu kama vile Haram ya Imam Ridha (a.s), Haram ya Bibi Masuma (a.s), na misikiti mingine mbali mbali, watu hufutarishwa kwa futari ya kawaida na isiyo ya kifakhari.[12]

Rejea

  1. Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 16, uk. 384; Muasase Dairat al-Maarif Fiqh Islami, Farhange Fiqh, 1385 S, juz. 1, uk. 624.
  2. Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 16, uk. 384; Ṭabāṭabāī al-Yazdī, al-ʿUrwa al-wuthqā, juz. 2, uk. 102.
  3. Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 16, uk. 264-266; juz. 29, uk. 50.
  4. Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 17, uk. 133 na juz. 16, uk. 345 na juz. 17, uk. 150-154.
  5. Muasase Dairat al-Maarif Fiqh Islami, Farhange Fiqh, 1385 S, juz. 1, uk. 624.
  6. Kulaynī, al-Kāfī, 1407 H, juz. 2, uk. 510; Muhammadi Rishahri, Mizan al-Hikma, 1416 H, juz. 2, uk. 1686; Rāwandī, 1366 S, Daʿawāt, juz. 1, uk. 27.
  7. Rāwandī, 1366 S, Daʿawāt, juz. 1, uk. 27.
  8. Hurri Amili, Wasail shia, 1414 H, juz. 10, uk. 149-151; Najafī, Jawāhir al-kalām, juz. 16, uk. 384-385.
  9. Kulainī, al-Kāfī, 1407 H, juz. 4, uk. 95.
  10. Hurri Amili, Wasail shia, 1414 H, juz. 10, uk. 149-151
  11. Kulainī, al-Kāfī, 1407 H, juz. 4, uk. 67, Hadithi no. 1.
  12. «Futari ya kawaida isiyo na makuu», Khabari Gozari Jamhuri Islami.

Vyanzo

  • Hāshimī Shāhrūdī, Maḥmūd, Farhang-i fiqh muṭābiq bā madhhab-i Ahl al-Bayt, Qom: Muʾassisat Dāʾirat al-Maʿārif Fiqh al-Islāmī, 1382 Sh.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad bin al-Ḥassan al-, Wasāʾil al-Shīʿa, Beirut: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turhāth, 1414 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad bin Yaʿqūb al-, Al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Najafī, Muḥammad Ḥassan al-, Jawāhir al-kalām, Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1404 AH.
  • Rāwandī, Saʿīd bin Hibat Allāh. Daʿawāt, Qom: Manshūrāt Madrisat al-Imām al-Mahdī, 1366 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad bin ʿAlī al-, ʿUyūn akhbār al-Riḍā, Imehaririwa na Mahdī Lājiwardī, Tehran: Nashr-i Jahān, 1378 AH.
  • Ṭabāṭabāʾī al-Yazdī, Sayyid Kāẓim al-, Al-ʿUrwa al-wuthqā, Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1419 AH.