Nenda kwa yaliyomo

Kadhmu al-ghaidhi

Kutoka wikishia

Ibara ya Kadhmu al-ghaidhi (Kiarabu: كظم الغيظ) Inatoka katika lugha ya Kiarabu, ambayo humaanisha kuvumilia na kudhiti hasira, jambo ambalo ni mojawapo ya sifa bora za kimaadili katika Uislamu. Hadithi zinlihisabu jambo hili kuwa ni moja ya sababu zinazo pelekea mtu kuepukana na hasira pamoja na ghadhabu za Mwenye Ezi Mungu, na badala yake hupelekea mtu kuoppata radhi za Mola wake. Wanazuoni wa fani ya maadili wamejadili sifa hii chini kufungu kinacho zungumzia tabia za hasira, na hatimae kutoa maelekezo kamili katika kuitibu tabia hiyo. Qur’ani tukufu nayo pia imezungumzia suala hili la kudhiti hasira, suala ambalo limetajwa katika Aya ya 134 ya Suratu al-‘Imran. Imamu Mussa bin Jaa’far (a.s), ambaye ni Imamu wa saba wa Shia, anajulikana kwa jina la "Kadhim" amepewa jina hilo kwa sababu ya uwezo wake wa kuvumilia na kudhibiti hasira zake.

Ufahamu wa Dhana ya “Kadhmu al-ghaidhi” na Nafasi Yake

Neno Ghaidh غَیْظْ linamaanisha ghadhabu kali hasira za daraja ya kuu kabisa, na inaelezwa kwamba; ghadhabu hizi zinatokanana na kuchemka kwa damu ndani ya moyo wa mwanadamu [1] na maana ya kadhmu کَظْمِ, ni kuzuiya pumzi. “Kadhmu al-ghaidhi کَظْمِ غَیْظْ”, ni istilahi ya kimaadili inayo maanisha kudhibiti hasira na kuto idhihirisha mbele ya watu, [2] na yule awezaye kudhibiti hasira zake kuu, huitwa kaadhim (mvumilivu). [3] Ibara ya “Kadhmu al-ghaidhi کَظْمِ غَیْظْ” yenye maana ya kuzuia hasira, inakaribia sana kimaana na sifa nyingine za kimaadili kama vile sifa ya “hilmu حلم” (uvumilivu). Imeelezwa ya kuwa: tofauti iliopo kati ya sifa ya kudhibiti hasira na sifa ya uvumilivu, ni kwamba; sifa ya kudhibiti hasira ni yue mtu ambaye bado hajafikia kiwango cha sifa ya “hilmu حلم” (uvumilivu), kwa hiyo kuna uwezekano wa hasira zake kujitokeza na kuhdihiri kutoka nje ya nafsi yake, ila yeye hujitahidi kuidhibiti kwa kujizuia na hasira hizo. [4]

Katika Hadithi, kunaonekana kuwepo kwa uhusiano maalumu kati ya sifa kudhibiti hasira (Kadhmu al-ghaidhi کَظْمِ غَیْظْ) na sifa ya subira pamoja na uvumilivu. Imamu Sadiq (a.s) katika moja ya Hadithi amesema kuwa: “Kudhibiti hasira ni kitendo kinachopendwa zaidi mbele ya Mwenye Ezi Mungu na anasema: Hakuna fundo lipendwalo zaidi mbele ya Mwenye Ezi Mungu kuliko fundo la kumeza ghadhabu ambalo huchemka ndani ya kifua cha mja, naye hulimeza na kulizuia kifuani mwake, kisha hulisukuma nyuma ya nafsi yake kupitia subira na uvumilivu. [5] [Maelezo: مَا مِنْ جُرْعَةٍ يَتَجَرَّعُهَا عَبْدٌ أَحَبَّ إِلَى اَللَّهِ عَزَّ وَ جَلَّ مِنْ جُرْعَةِ غَيْظٍ يَرُدُّهَا فِي قَلْبِهِ وَ رَدَّهَا بِصَبْرٍ أَوْ رَدَّهَا بِحِلْمٍ] Katika Qur’ani, kudhibiti hasira (Kadhmu al-ghaidhi کَظْمِ غَیْظْ) kumetajwa kama ni moja ya sifa maalumu za wacha Mungu. Mwenye akizungumzia sifa hiyo amesema: “Wale ambao wanadhibiti ghadhabu zao na kusamehe makosa ya watu, na Mwenye Ezi Mungu awapenda wantendao hisani.” [6] Pia tendo la kudhibiti hasira (Kadhmu al-ghaidhi کَظْمِ غَیْظْ) katika Hadithi, limekuwa likisisitizwa mno na Maimamu (a.s), na kuhisabiwa kama ni moja ya matendo muhimu ya kimaadili. Al-Kulayni katika kitabu chake kiitwacho Al-Kafi kweny mlango wa “Imanu wa al-Kufru” ameorodhesha Hadithi 13 kwenye mlango wa (Kadhmu al-ghaidhi کَظْمِ غَیْظْ). [7] Pia suala la kudhibiti ghadabu ni miongoni mwa masuala yalio tajwa katika dua ya “Makarimu al-Akhlaqi” ilioko katika kitabu “Sahifa Sajjadiya”. [8] Suala la kudhubiti ghadhabu (Kadhmu al-ghaidhi کَظْمِ غَیْظْ) pia limetajwa katika Hadithi zihusianazo na masuala ya utukufu na uadhimu wa waja wa Mungu, ambalo limehisabiwa kuwa ni miongoni mwa sababu za mja kuepukana na adhabu aa Mungu na kupata ridhaa yake. [9] Kuna Hadithi iliyo nukuliwa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) ya kwamba: “Yeyote atakaye dhibiti hasira zake, Mungu naye atamwondolea mtu huyo adhabu zake.” [10] Naye Imam Sajjad (a.s) kuhusiana na hilo amesema kwamba; hakuna kinywaji kipendwacho zaidi mbele yangu kama kinywaji cha (kumeza) hasira ambacho nakinywa na sisiwahukumu wengine. Na katika hadithi nyingine, kunywa kinywaji cha hasira na huzuni wakati wa msiba imetajwa kama moja ya vinywaji vipendwavyo mbele ya Mwenyezi Mungu. [11] [Maelezo: ما من جرعتين أحب إلى الله عز وجل أن يجرعهما عبده المؤمن في الدنيا من جرعة غيظ كظم عليها وجرعة حزن عند مصيبة صبر عليها]

Mbinu za Kudhibiti Hasira

Suala la Kadhmu al-ghaidhi کَظْمِ غَیْظْ: ni miongoni mwa mada zilizo jadiliwa katika vyanzo vya mafunzo ya maadili, suala hili hujadiliwa vyanzoni humo chini ya mlango unaohusiana na tabia mbovu za kimaadili na chini ya mada ya tabia ya hasira. [12] Wanazuoni wa maadili wametoa mbinu kadhaa za kudhibiti hasira. [13]

Feidh Kashani katika Al-Mahajjatu Al-Baidhaa akitoa suluhu na tiba dhidi ya ghadhabu amesema kwamba; miongoni mwa tiba na mbinu za kudhibiti ghadabu ni: kuzitafakari Hadithi zinazoelezea hadhi ya kudhibiti hasira na kuwa na uvumilivu, na hadhi ya wale watoao msamaha, pamoja na kuzingatia thawabu na malipo yalio tajwa katika Hadithi hizo kuhusiana na Kadhmu al-ghaidhi کَظْمِ غَیْظْ. Jengine ni kukumbuka uwezo na hasira za Mwenye Ezi Mungu, kuzingatia ubaya wa hali yake wakati wa hasira zake na kuzikandamiza hisia za kulipiza kisasi zilizoko nafsini mwake. Yeye ameyataja mambo hayo kama ndio mbinu za kisayansi za kudhibiti hasira. [13] Vilevile, miongoni mwa tiba dhidi ya ghadhabu zilizo orodheshwa na Feidhu Kashani, ni kuomba hifadhi kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu na kumwomba Alla kumpa mabadiliko ya nafsi yake. Anaeleza kusema kwamba; ikiwa kutafuta hifadhi ya Alla hakutafanikiwa, basi ikiwa mtu huyo mwenye hasira atakuwa amesimama anatakiwa kuketi, na ikiwa ameketi anapaswa kuegemea na kulala chini. Pia, katika baadhi ya Hadithi, hasira zimefananishwa na moto, na imeelezwa kwamba moto hauzimwi isipokuwa na maji; hivyo basi mtu aliye na hasira anapaswa kutawadha kwa ajili ya kuzima moto huo wa hasira. [15]

Katika baadhi ya Hadithi, imeripotiwa kutoka kwa Mtume wa Mungu (s.a.w.w) kwamba; yeyote anayekasirika anapaswa kuuweka uso wake chini kwenye ardhi. Waram bin Abi Furas amesema kwamba: “Bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa na nia ya amri ya sijda (kwa yule aliye kumbwa na tatizo hilo) ili nafsi ihisi unyenyekevu na hasira yake iondoke kupitia unyeyekevu huo. [16] Imamu Baqir (as.) katika moja ya Hadithi kuhusiana na kudhibiti hasira amesema kwamba; yeyote yule atakaye fikwa na hali ya kuwaasirikia watu, ikiwa atakuwa katika hali ya kusimama anapaswa mara moja kukaa chini, ili uchafu wa Shetani utengane naye, na yeyote atayemkasirikia ndugu yake anapaswa kwenda karibu naye na kuugusa mwili wake (kwa mfano, agusishe mkono wake kwenye mkono wa mtu huyo), kwa sababu kila ndugu wanapogusana, amani hupatikana baina yao. [17]

Ukandamizaji wa Ghazibu wa Imam Kazim (a.s)

Imamu Musa Kadhim (a.s) alipewa jina la umaarufu la "Kadhim" kwa sababu ya uwezo wake wa kudhibiti hasira zake. [18] Vyanzo vingi vinasimulia Hadithi mbalimbali zinazoonyesha jinsi Imamu Kadhim (a.s) alivyoweza kuzishinda na kuzidhibiti hasira zake mbele ya maadui zake na watu waliomtendea mabaya. [19] Mfano mmoja ulio simuliwa kuhusiana naye unahusiana na mtu mmoja miongoni mwa wajukuu wa Omar ibnu al-Khattab ambaye alimtukana Imamu Ali (a.s) mbele ya Imamu Kadhim (a.s). Katika tukio hilo Masahaba wa Imamu Kadhim (a.s) walitaka kumvamia na kumshambulia mtu huyo, lakini Imamu akawazuia, kisha Imamu Kadhim akamfuata mtu huyo shambani kwake. Pale mtu huyo alipomwona Imamu Kadhim (a.s), alianza kupiga kelele akimwomba asikanyage mimea yake. Imamu alimkaribia kwa upole na kumwuliza kwa utulivu kabisa ni kiasi gani alitumia kwa ajili ya kupanda mapando ya shamba hilo. Naye alijibu, "Dinar 100!" Imamu akamuuliza tena, "Unatumai kuvuna kiasi gani?" Naye akajibu, "Sijui." Imamu Kadhim (a.s) akasema, "Nilikuuliza unatarajia kuvuna kiasi gani?" Hapo mtu huyo akajibu, "Dinar 200!" Imamu Kadhim (a.s) akampa dinar 300 na kumwambia, "Hizi dinar 300 ni zako, na mimea yako bado ni yako." Kisha akaelekea msikitini. Mtu huyo mbio alifika msikitini na alipomwona Imamu Kadhim (a.s), alisimama na kusoma Aya hii kwa sauti: “اللَّه أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِ‌سَالَتَهُ؛” "Mwenyezi Mungu anajua vyema mahali pa kuuweka ujumbe wake." (An'am 124) [20]

Vitabu Makhususi Juu ya Mada ya Kadhmu al-ghaidhi

1- Mahaarat Muqabile ba Khashme: Cha Seyed Mehdi Khatib, Kimechapwa na Dar al-Hadith na IIntishaarati Astan Qudsi Radhawi), toleo la kwanza lilitolewa mwaka 1398 Shamsia, katika kurasa 48. [21] 2- Mahaare Khashme wa Parkhashgariy dar Partowe Amuzehae Diiniy: cha Majid Jafari Harafteh, Chapisho la Muassase Amuzeshiy wa Pazuheshiy Imam Khomeiniy, Toleo la Kwanza lilitolewa mwaka 1397 Shamsia, kwenye kurasa 216. [22] 3- Mahaarate Hashme: cha Mohammad Ridha Keyoumarthiy Esfahani, Chapisho la Dar al-Hadith, mwaka 1391 Shamsia, idadi ya kurasa ni 299. [23]

Maudhui zinazo husiana: Lakabu ya Kadhim

Rejea

Vyanzo