Kadhim (Lakabu)
- Makala hii inahusu jina la Imam Kadhimu (a.s). Ili kujifunza kuhusu shkhsia ya Imam (a.s), tazama utangulizi wa Imamu Musa Kadhim (a.s).
Kadhim (Kiarabu: الكاظم (لقب)) ni mojawapo ya majina mashuhuri ya Imam Musa bin Ja'afar (a.s). [1] Imeelezwa katika vitabu vya maadili (akhlaq) ya kwamba; jina Kadhim lina maana ya mtu anayedhibiti hasira zake.[2] Imam Musa bin Jafar (a.s) alikuwa ni mpole, mvumilivu, na mwenye kudhibiti hasira zake, pia katu hakujionyesha kwa alichokijua. [3] Sabti bin Jauz (aliyefariki mwaka 654 Hijiria) katika kitabu chake kiitwacho Tadhkiratul Al-Khawas ameeleza ya kwamba: “Imam Musa Al-Kadhimu (a.s) alikuwa ni mvumilivu mwenye kusamehe, na hiyo ndiyo sababu hasa ya yeye kuitwa Kadhim kwa ajili hiyo, kwamba kila jambo linapomjia kutoka kwa mtu fulani. atamtumia pesa”. [4]
Sayyid Hashim maarufu Al-Hasani, katika kitabu Siratul A-immatul Ithna'ashariyyah anasema kwamba, kulingana na riwaya ya iliyonukuliwa katika kitabu Tazkira al-Khuwwaas, Imam Kadhim (a.s) alikuwa akiitwa Kadhimu. Alijulikana kwa jina hilo sababu kila alipoona kitu kibaya kutoka kwa mtu fulani, alikuwa akimtumia mali mtu huyo ambazo zingetosheleza mahitaji ya mtu huyo [5]
Makala Zinazo Fungamana
Rejea
Vyanzo
- Arbali, Ali Ibn Isa, Kashfu al-Ghumma fi Ma’rifati al-umma, Qom, Razi, 1421 AH.
- Al-Hasani, Sayyid Hashim, Sira al-Aimmah al-Athnai'ashr, Najaf, Al-Maktab Al-Haydariyya, 1382 AH.
- Sibtu bin Juzi, Yusuf bin Ghazaughli, Tadhkiratu al-Khuwwas minal umma fi dhikr manaqibil al-Aimma, Qom, Manshurat al-Sharif al-Radhi, 1418 AH.
- Tabarsi, Fadhlu bin Hasan, Al-Alam al-Wori ba'alam al-Hadi, Qom, Taasisi ya Al-Al-Bayt, 1417 AH.
- Ghazali, Muhammad bin Muhammad, Ihyau Ulum al-Din, Beirut, Daru al-Maarif, Bita.
- Majlisi, Muhammad Baqir, Bihar Al-Anwar, Tehran, Islamia, 1363.
- Naraqi, Muhammad Mahdi, Al-Saadat Jami’, Beirut, Al-Alami Institute of Press, BTA.