Nenda kwa yaliyomo

Ijtihadi mkabala wa Nass

Kutoka wikishia
Makala hii ni kuhusu maana ya Ijtihadi mkabala wa Nass (andiko) Ili kujua kuhusu kitabu chenye jina kama hili angalia makala ya al-Nass Wal-Ijtihad (kitabu).

Ijtihadi Mkabala wa Andiko (Kiarabu:الاجتهاد في مُقابل النّص) ni kutanguliza maoni binafsi ya Mujtahidi juu ya maneno ya wazi ya Qur'ani au Maasumina (a.s). Kwa mujibu wa mafaqihi wa Kishia na mafaqihi wengi wa Kisunni, ijtihadi dhidi andiko ni bidaa na uzushi. Hata hivyo, baadhi ya masahaba na baadhi ya mafaqihi wa Kisunni wametanguliza maoni na mitazamo yao mbele ya maandiko. Kwa mfano, Omar bin Khattab, aliharamisha (Mutaatan); mut’a mbili, ambazo ni mut’a ya ndoa na mut’a ya Hija akitanguliza mtazamo wake dhidi ya maandiko. Sayyid Abdul-Hussein Sharafuddin (aliyefariki: 1377 Hijiria) katika kitabu chake cha al-Nass Wal-Ijtihad amepokea kutoka kwa makhalifa ijtihadi 100 dhidi ya maandiko (hoja nakili za wazi), watawala na baadhi ya jamaa zao katika zama za Mtume (s.a.w.w) na baada yake.

Maana na Nafasi Yake

Ijtihad dhidi ya andiko imeelezwa kuwa maana yake ni kutanguliza dhana na rai binafsi ya Mujtahidi mbele amri ya wazi ya Mwenyezi Mungu au Mtume (s.a.w.w) au Maasumina wengine. [1] Nass (andiko) ni maneno yenye itibari ya wazi na bayana ambayo hayana maana zaidi ya moja. [2]

Wanachuoni wa Shia wanapinga ijtihadi dhidi ya maandiko. Nasser Makarem Shirazi anaamini kwamba upanuzi wa ijtihadi dhidi ya maandiko utasababisha kuondolewa wa kinga ya hukumu zote. [3] Mirza Habibullah Khui anaona kuwa, kupinga andiko ni uzushi. [4] Jawad Shaharistani anasema katika utangulizi wa kitabu cha Wasail al-Shiah kwamba: Hatua ya Mamujitahidi ya kufanya ijtihadi mkabala wa andiko kimsingi wanamtambua Mtume (s.a.w.w) kwamba, ni Mujtahidi kama wao, ambaye ijtihadi yake ina uwezekano wa kukosea. [5] Sayyid Muhammad Hussein Tehrani anasema, kushikamana Mashia na Nass na Masuni kukiuka Nass ni msingi wa hitilafu baina ya Waislamu wa Kishia na Kisuni. [6]

Mafakihi Waliowengi Wanapinga Ijtihadi Mkabala wa Nass (andiko)

Mafakihi wa Shia [7] na Sunni [8] wanaona ijtihadi mkabala wa hoja ya wazi ni batili. Baadhi ya Maswahaba na tabiina (waliokutana na masahaba) katu hawakuwahi kutoa rai ya kifiqhi mkabala wa Nass. [9] Ibn Qayyim al-Juwziya, mmoja wa wanachuoni wa Kisunni, anasema kuwa, Ahmad Ibn Hanbal alikuwa akitoa fat’wa kwa mujibu wa maandiko na hakukubali rai zinazopingana Nass hata kama zitatoka kwa makhalifa. [10]

Pamoja na hayo, baadhi ya mafaqihi wa Kisunni wakati mwingine walikuwa wakitanguliza ijtihadi yao dhidi ya maandiko. [11] Ayatullah Makarem Shirazi ananukuu kutoka kwa mmoja wao katika kitabu chake cha Siyasat Va Muamalat: Kama Nass (andiko) ilikuwa ikipingana na maslahi na haikuwezekana kupata natija, inawezekana kutanguliza maslahi mbele ya Nass. Hata hiyo akthari ya mafakihi wao wamepinga maoni hayo. [12]

Hoja za Kupinga Ijtihadi Mkabala wa Andiko

Wanaopinga nadharia ya ijtihadi mkabala wa andiko mbali na kutumia hoja ya akili [13], wanategemea pia Aya za Qur’ani tukufu na hadithi zilizopokewa na Waislamu wa pande mbili yaani Mashia na Masuni:

  • Jaafar Subhani, Marjaa Taqlidi akitumia kama hoja Aya ya kwanza katika Surat al-Hujuraat na ulazima wa kusalimu amri mbele ya amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, anaona kuwa, kufanya ijtihadi mkabala wa andiko ni kumtangulia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. [14]
  • Nassir Makarim Shirazi, Marjaa Taqlidi anasema katika Tafsiri ya Aya ya 65 ya Surat al-Nisaa kwamba: Aya hiyo inapinga aina yoyote ya kufanya ijtihadi na kutoa maoni mkabala wa andiko na hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. [15]
  • Kwa mujibu wa Aya ya 36 katika Surat al-Ahzab, waumini hawana khiari wakati Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao na ni haramu kutoa raia na kufanya ijtihadi yoyote mkabala wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. [16]
  • Katika hadithi zilizonukuliwa katika vyanzo na vitabu vya Ahlu-Sunna inaelezwa kuwa, Bwana mmoja kutoka kabila la Thaqif alimuuliza Khalifa wa Pili mas’al fulani kuhusiana na ibada ya Hija. Omar akamjibu. Bwana yule akasema: Mbona nilimuuliza Mtume kuhusu jambo hili lakini jibu lake lilikuwa jiingine sio hili ulilonipatia wewe? Omar akakasirika na kusema: Kwa nini unaniuliza swali ambalo Mtume tayari alishaeleza mtazamo wake na kutoa jibu? [17]

Ijtihadi ya Masahaba Mkabala wa Andiko

Licha ya upinzani wa mafakihi wa Shia na Sunni kwa ijtihad dhidi ya maandiko, lakini imepokewa kwamba baadhi ya masahaba walitoa fat’wa dhidi ya maandiko. [18] Maulamaa wa Kishia wanaamini kwamba, Khalifa wa Pili alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kufanya ijtihadi mkabala wa Qur’ani na Mtume (s.a.w.w) [19] Wanasema kuwa, ijtihadi yake ya kwanza mkabala wa nass ni kadhia mashuhuri aliyoifanya ya kuharamisha muta’ ya ndoa na mut’a ya Hija. [20]

Sharaf al-Din Amili amesimulia baadhi ya ijtihadi dhidi ya maandiko katika kitabu chake cha al-Nass Wal-Ijtihad. Katika mlango wa saba wa kitabu hiki, anaorodhesha matukio 100 ya ijtihadi dhidi ya Nass (andiko) kutoka kwa makhalifa, watawala na baadhi ya jamaa zao katika zama za Mtume au baada yake. [21] Baadhi ya matukio hayo:

Ikumbukwe kuwa, mafakihi wa Kisuni wamejitokeza na kutetea ijtihadi hizi. [22]

Rejea

Vyanzo