Nenda kwa yaliyomo

Dua ya Nne ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Tatu ya kitabu cha Sahiifatu Al-Sajjadiyyah
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mnamo 1145 AH.

Mtoaji / MwandishiImamu Sajjad (a.s)
LughaKiarabu
Msimulizi / MpokeziMutawakkil ibn Harun
MadaKuwaombea rehema wafuasi wa Mitume (a.s), uchanganuzi wa sifa za Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w) pamoja na athari za rehema za Mungu kwa waja wake
ChanzoSahifa Sajjadiyah
Tafsiri kwa Lugha yaKifarsi

Dua ya Nne ya Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء الرابع من الصحيفة السجادية) ni miongoni mwa dua mashuhuri zilizosimuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Madhumuni ya dua hii yamejikita sehemu tatu kuu; kuwatakia rehema na amani wafuasi wa Mitume wa Mwenye Ezi Mungu, sifa tukufu za Masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), pamoja na kueleza athari na baraka za na rehema na amani za Mwenye Ezi Mungu juu ya waja Wake. Imamu (a.s) katika dua hii, anaelezea akisema kuwa; Mitume walikuwa ndio viongozi wa watu wenye taqwa katika zama mbali mbali. Dua hii pia inaeleza namna ya waumini walivyoupokea ujumbe wa Mitume na jinsi walivyosalimu amri mbele ya hoja za wazi kutoka kwa Mola Wao, namna ya wapinzani walivyokinzana na ujumbe wa Mitume, pamoja na kubaki salama kwa waumini mbele ya mitihani na fitna mbali mbali.

Dua ya Nne ya Sahifa Sajjadiyya imefasiriwa kwa kina kabisa katika vitabu tafsiri vinavyotoa uchambuzi wa kitafsiri wa kitabu Sahifatu Sajjaadiyya, miongoni mwavyo ni pamoja ni; Diyār al-‘Āshiqīn cha Sheikh Hussein Ansarian, kilicho andikwa kwa lugha ya Kifarsi, na Riyāḍhu al-Sālikīna cha Sayyid Ali Khan Madani kwa lugha ya Kiarabu.

Mafundisho Makuu ya Dua ya Nne ya Sahifa Sajjadiyya

Mada za msingi za dua ya nne ya Sahifa ya Sajjadiyya zinahusiana na kuwaombea rehema wafuasi wa Mitume (a.s), uchanganuzi wa sifa za Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w) pamoja na athari za rehema za Mungu kwa waja wake. Orodha ya mafundisho ya dua hii yamekuja kama ifuatavyo:

  • Dua ya kuwatakia rehema wafuasi wa Mitume, waliowasadiki na kuamini ulimwengu wa ghaibu.
  • Mitume ni viongozi wa uwongofu na ni nembo ya uchamungu kwa wamchao Mungu.
  • Msimamo wa wanadamu mbali mbali kuhusiana na utume wa Mitume.
  • Kujisalimisha kwa waumini mbele ya hoja na ushahidi wa ukweli juu ya kukubaliana na ujumbe wa Mungu.
  • Radhi za Mungu ndio malipo ya waumini, yaani ndio ujira wa kustahimili changamoto katika kushikamana na mkondo wa kidini.
  • Dua ya kuwaombea msamaha (maghufira) na kuwatakia thawabu na jaza njema Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w).
  • Dua kwa ajili ya waumini waliopita.
  • Kuwatakia rehema wale walioshikamana na bwana Mtume (s.a.w.w), wao pamoja na wake zao na watoto wao.
  • Hadhi ya wachamungu (mbele ya Mola wao) pamoja na makazi yao ya amani.
  • Kuhifadhika kwa waumini dhidi ya fitina za kidunia na misukosuko ilioko kwenye njia ya kushikanana na dini.
  • Sifa za mbali mbali Masahaba wa bwana Mtume wa (s.a.w.w) ikiwa ni pamoja na: Kuheshimu masharti ya kushikamana na Mtume Muhammad (s.a.w.w). Kuharakia imani kupitia wito wake (s.a.w.w.), kustahamili kukaa mbali na wake na watoto kwa ajili ya kuinua neno la haki (Mungu), kupigana dhidi ya baba na watoto wao kwa ajili ya kuimarisha Uislamu, kushikamana na biashara yenye faida ya kipekee (ambayo ni biashara ya kumwamini Mungu) na Kuvumilia mateso na kutengwa pale walipokubali kuingia katika msafara wa imani.
  • Matokeo au natija ya rehema za Mungu kwa waumini, ambayo ni pamoja na: Kutengena na dhambi, kuepukana na hila za Shetani, kusalimika na misukosuko ya maisha, kupata taufiq ya kutenda matendo mema na kujengeka kiimani, kuepukana na changamoto na machungu ya kifo kwa waumini hao pamoja na kupata taufiki ya kuelekeza mawazo yao kwenye maisha ya Akhera (ambayo ni maisha ya milele).[1]

Habari Kuhusiana na Tafsiri Mbalimbali

Dua ya nne kutoka katika Sahifatu Sajjadiyya imechambuliwa kwa kina katika tafsiri mbalimbali. Miongoni mwa lugha zilizotumika katika kufarisi dua hii ni lugha ya Kifarsi pamoja na Kiarabu. Tafsiri za Dua hii inapatika katika vitabu vifuatavyo: Diyaar-e-Aasheqaan kilichoandikwa na Hujjatul Islam Hussein Ansarian.[2] Shuhuud wa Shenaakht kilichoandikwa na Muhammad Hasan Mamduhi Kermanshahi.[3] Asraar-e-Khaamoshaan ya Muhammad Taqi Khalaji.[4] Sharh wa Tarjuma ya Sahifa Sajjadiyya cha Sayyid Ahmad Fahri.[5]

Pia Dua hii imefasirir na kufafanuliwa kwa lugha ya Kiarabu kupitia vitabu vifuatayo: Riyāḍ al-Sālikīn cha Sayyid ʻAlī Khān Madanī.[6] Fī Ẓilāl al-Ṣaḥīfah al-Sajjādiyyah cha Muhammad Jawād Mughniyya.[7] Riyāḍ al-‘Ārifīn kilichoandikwa na Muhammad ibn Muhammad Dārābī.[8] Āfāq al-Rūḥ cha Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[9] Pia maneno ya dua yamefasiriwa kiundani kabisa katika tafsiri ya kilugha iliyoandikwa na Faidhu Kāshānī iitwayo Taʿlīqāt ʿalā al-Ṣaḥīfati al-Sajjādiyya (تعلیقات علی الصحیفه السجادیه), ambayo imekuja kufafanua maneno tata na ya kifasihi yaliyomo kwenye dua hii.[10]

Matini ya Dua na Tafsiri Yake

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الصَّلَاةِ عَلَى أَتْبَاعِ الرُّسُلِ وَ مُصَدِّقِيهِمْ

اللَّهُمَّ وَ أَتْبَاعُ الرُّسُلِ وَ مُصَدِّقُوهُمْ مِنْ أَهْلِ الْأَرْضِ بِالْغَيْبِ عِنْدَ مُعَارَضَةِ الْمُعَانِدِينَ لَهُمْ بِالتَّكْذِيبِ وَ الِاشْتِيَاقِ إِلَى الْمُرْسَلِينَ بِحَقَائِقِ الْايمَانِ

فِي كُلِّ دَهْرٍ وَ زَمَانٍ أَرْسَلْتَ فِيهِ رَسُولًا وَ أَقَمْتَ لِأَهْلِهِ دَلِيلًا مِنْ لَدُنْ آدَمَ إِلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ مِنْ أَئِمَّةِ الْهُدَى، وَ قَادَةِ أَهْلِ التُّقَى، عَلَى جَمِيعِهِمُ السَّلَامُ، فَاذْكُرْهُمْ مِنْكَ بِمَغْفِرَةٍ وَ رِضْوَانٍ.

أَللَّهُمَّ وَ أَصْحَابُ مُحَمَّدٍ خَاصَّةً الَّذِينَ احسنوا الصَّحَابَةَ وَ الَّذِينَ أَبْلَوُا الْبَلَاءَ الْحَسَنَ فِي نَصْرِهِ، وَ كَانَفُوهُ، وَ أَسْرَعُوا إِلَى وِفَادَتِهِ، وَ سَابَقُوا إِلَى دَعْوَتِهِ، وَ اسْتَجَابُوا لَهُ حَيْثُ أَسْمَعَهُمْ حُجَّةَ رِسَالَاتِهِ.

وَ فَارَقُوا الْأَزْوَاجَ وَ الْأَوْلَادَ فِي إِظْهَارِ كَلِمَتِهِ، وَ قَاتَلُوا الآْبَاءَ وَ الْأَبْنَاءَ فِي تَثْبِيتِ نُبُوَّتِهِ، وَ انْتَصَرُوا بِهِ

وَ مَنْ كَانُوا مُنْطَوِينَ عَلَى مَحَبَّتِهِ «يَرْجُونَ تِجَارَةً لَنْ تَبُورَ» فِي مَوَدَّتِهِ.

وَ الَّذِينَ هَجَرَتْهُمْ الْعَشَائِرُ إِذْ تَعَلَّقُوا بِعُرْوَتِهِ، وَ انْتَفَتْ مِنْهُمُ الْقَرَابَاتُ إِذْ سَكَنُوا فِي ظِلِّ قَرَابَتِهِ.

فَلَا تَنْسَ لَهُمُ اللَّهُمَّ مَا تَرَكُوا لَكَ وَ فِيكَ، وَ أَرْضِهِمْ مِنْ رِضْوَانِكَ، وَ بِمَا حَاشُوا الْخَلْقَ عَلَيْكَ، وَ كَانُوا مَعَ رَسُولِكَ دُعَاةً لَكَ إِلَيْكَ.

وَ اشْكُرْهُمْ عَلَى هَجْرِهِمْ فِيكَ دِيَارَ قَوْمِهِمْ، وَ خُرُوجِهِمْ مِنْ سَعَةِ الْمَعَاشِ إِلَى ضِيقِهِ، وَ مَنْ كَثَّرْتَ فِي إِعْزَازِ دِينِكَ مِنْ مَظْلُومِهِمْ.

اللَّهُمَّ وَ أَوْصِلْ إِلَى التَّابِعِينَ لَهُمْ بِإِحْسَانٍ، الَّذِينَ يَقُولُونَ «رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَ لِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ» خَيْرَ جَزَائِكَ.

الَّذِينَ قَصَدُوا سَمْتَهُمْ، وَ تَحَرَّوْا وِجْهَتَهُمْ، وَ مَضَوْا عَلَى شَاكِلَتِهِمْ.

لَمْ يَثْنِهِمْ رَيْبٌ فِي بَصِيرَتِهِمْ، وَ لَمْ يَخْتَلِجْهُمْ شَكٌّ فِي قَفْوِ آثَارِهِمْ،، وَ الْاِئْتَمامِ بِهِدَايَةِ مَنَارِهِمْ.

مُكَانِفِينَ وَ مُوَازِرِينَ لَهُمْ، يَدِينُونَ بِدِينِهِمْ، وَ يَهْتَدُونَ بِهَدْيِهِمْ، يَتَّفِقُونَ عَلَيْهِمْ، وَ لَا يَتَّهِمُونَهُمْ فِيما أَدَّوْا إِلَيْهِمْ.

اللَّهُمَّ وَ صَلِّ عَلَى التَّابِعِينَ مِنْ يَوْمِنَا هَذَا إِلَى يَوْمِ الدِّينِ وَ عَلَى أَزْوَاجِهِمْ وَ عَلَى ذُرِّيَّاتِهِمْ وَ عَلَى مَنْ أَطَاعَكَ مِنْهُمْ.

صَلَاةً تَعْصِمُهُمْ بِهَا مِنْ مَعْصِيَتِكَ، وَ تَفْسَحُ لَهُمْ فِي رِيَاضِ جَنَّتِكَ، وَ تَمْنَعُهُمْ بِهَا مِنْ كَيْدِ الشَّيْطَانِ، وَ تُعِينُهُمْ بِهَا عَلَى مَا اسْتَعَانُوكَ عَلَيْهِ مِنْ بِرٍّ، وَ تَقِيهِمْ طَوَارِقَ اللَّيْلِ وَ النَّهَارِ إِلَّا طَارِقاً يَطْرُقُ بِخَيْرٍ.

وَ تَبْعَثُهُمْ بِهَا عَلَى اعْتِقَادِ حُسْنِ الرَّجَاءِ لَكَ، وَ الطَّمَعِ فِيما عِنْدَكَ وَ تَرْكِ التُّهَمَةِ فِيما تَحْوِيهِ أَيْدِي الْعِبَادِ.

لِتَرُدَّهُمْ إِلَى الرَّغْبَةِ إِلَيْكَ وَ الرَّهْبَةِ مِنْكَ، وَ تُزَهِّدَهُمْ فِي سَعَةِ الْعَاجِلِ، وَ تُحَبِّبَ إِلَيْهِمُ الْعَمَلَ لِلآْجِلِ، وَ الِاسْتِعْدَادَ لِمَا بَعْدَ الْمَوْتِ. وَ تُهَوِّنَ عَلَيْهِمْ كُلَّ كَرْبٍ يَحُلُّ بِهِمْ يَوْمَ خُرُوجِ الْأَنْفُسِ مِنْ أَبْدَانِهَا

وَ تُعَافِيَهُمْ مِمَّا تَقَعُ بِهِ الْفِتْنَةُ مِنْ مَحْذُورَاتِهَا، وَ كَبَّةِ النَّارِ وَ طُولِ الْخُلُودِ فِيهَا وَ تُصَيِّرَهُمْ إِلَى أَمْنٍ مِنْ مَقِيلِ الْمُتَّقِينَ.

Na miongoni mwa dua zake, amani iwe juu yake, ilikuwa ni kuwaombea rehema na baraka wafuasi wa mitume pamoja na wale waliowaamini (mitume hao).

Ewe Mola, rehema zako ziwe juu ya wafuasi wa mitume (Wako), na wale waliowasadiki miongoni mwa watu wa ardhini, walioamini kwa moyo wa dhati mambo ya ghaibu, na wakavutiwa na mitume (Wako) kutokana na ukweli wa imani zao, pale (mitume hao) walipokabiliwa na upinzani wa waliowakanusha.

Katika kila enzi na zama ulizotuma Mtume fulani ndani yake, na ukawasimamishia watu wake hoja na mwongozo wa wazi (usio na dosari), kuanzia kwa Nabii Adam hadi kwa Muhammad, rehma na amani zimshukie yeye pamoja Aali zake, ambao ni miongoni mwa nembo za uongofu na viongozi wachamungu – rehema (zako) ziwe juu yao wote (kwa pamoja). Basi wakumbuke (watu hawa) kwa msamaha wako na (uwaingize katika) ridhaa zako.

Ee Mola! Warehemu hasa Masahaba wa mtume Muhammad (rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake), wale waliotimiza masharti ya usahaba kwa ukamilifu, na waliopitia mtihani ya jihadi na wakafaulu vyema mitihani hiyo katika kumhami (na kumnusuru mtume Wako); wakaukimbilia ujumbe wake, wakashindana katika kuuharakia mwito wake, na wakawa maridhawa katika kuukubali ujumbe aliokuja nao, pale walipowafikishia hoja za ujumbe mbele yao.

Ambao katika harakati za kuieneza na kutangaza ujumbe wake, walilazimika kujitenga na wake zao pamoja na watoto wao, ambao kwa ajili ya kuthibitisha utume wake, waliwajibika kuingia vitani na kukabiliana na baba zao pamoja na watoto wao vitani humo; na kwa baraka ya uwepo wake, wakafanikiwa kuipatia ushindi dini ya Mwenye Ezi Mungu.

Na (washushie rehema zako) wale waliojigubika kwa (shuka la) upendo wake, wakitaraji biashara isiyofilisika, katika maisha upendo wao kwake (s.a.w.w).

Na (washushie rehema zako) wale walitengwa na makabila yao kutokana na kushikimana imara kamba ya dini yake; na waliotengwa na jamaa zao kutokana na kuingia kwa ndani ya kivuli cha ukuruba wake.

Ee Mwenyezi Mungu! Basi usiepushe fadhila na rehema zako kutoka kwa masahaba wa Muhammad (s.a.w.w) kwa yale waliyoyatoa na kuyapoteza kwa ajili yako na katika njia (ya dini) yako; na uwaruzuku radhi zako (ili wanufaike na neema zako). (Na uwarehemu) kutokana kwa ile kazi yao ya kuikusanya jamii ya wanadabu na kuisogeza karibu na dini Yako, na walikuwa walinganiaji wako wakishirikiana na mjumbe wako katika kuwalingania watu waje kwenye dini Yako.

Na washukuru kwa kuwalipa (ujira mwema) wale waliolazimika kuhama na kuachana na miji yao, makabila yao, na jamii zao kwa ajili ya njia yako; waliogeuza maisha yao kutoka hali ya ustawi wa mapato bora kuelekea kwenye maisha ya dhiki mashaka, na (usiwasahau) wale waliotumika kama nguzo ya kuimarisha dini yako miongoni mwao, wakahiari kuwa ni wahanga wa dhuluma mbali mbali.

Ewe Mola, washushie rehema na baraka zako, na uwape ujira bora kabisa utokao kwako, wale waliofuata nyayo zao kwa wema — ambao husema: “Ewe Mola wetu Mlezi! Tusamehe sisi pamoja na ndugu zetu waliotutangulia kwa imani”.

Wale walioelekea kwenye mwelekeo wao (walifuata njia ya masahaba hao), wakashikamana na nyenendo zao, na wakatiririka kwa kufuata mtindo wao.

Walifanya hivyo bila ya kukangazwa na lolote lile katika mtazamo wao, wala hawakupatwa na shaka yoyote katika kufuata athari zao na kushikamana na miongozo yao.

Waliwalinda na wakasimama bega kwa bega katika kusaidia nao, walifuata dini yao (katika ibada zao pamoja na miamala yao) wakiongozwa na mwongozo wao, walifanya hivyo wakikubaliana nao, wala hawakuwa mashaka na kile walichowafikishia.

Ewe Mola, warehemu wafuasi wao (mataabiina) pamoja na wake zao, na watoto wao, na kila mmoja kati yao aliyekutii, kuanzia siku yetu hii ya leo hadi Siku ya Malipo.

Warehemu kwa rehema zitakazowalinda na maasi Yako, na uwapte wasaa wa nafasi katika bustani za Pepo Yako, uwakinge na hila za shetani, uwasaidie kupitia rehema zako hizo juu ya yale mema wanayokuomba msaada katika utendaji wao, na uwalinde dhidi ya maovu ya usiku na mchana, isipokuwa yale yanayokuja kwa kwa lengo la kheri ndani ya nyakati mbili hizo.

Na uwazindue kwa rehema hizo, ili wapate mwamko wa imani ya matumaini mema juu ya fadhila na rehema Zako, na wawe na tamaa ya kile kilicho mikononi Mwako, na waache kuwa na dhana mbaya juu ya yale yaliyomo mikononi mwa waja Wako.

Rehema ambazo zitawatia hofu na kuwapa shauku ya kurejea Kwako, uwapunguzie tamaa ya mali ya dunia (kupitia rehema hizo), uwapendezeshee (ili wapendezwe na) kufanya kazi kwa ajili ya Akhera, na uwatia moyo wa kujiandaa kwa ajili ya maisha yanayofuata baada ya mauti. Na (rehema hizo) ziwapunguzie kila shidda inawapa (waja) wakati wa kutoka kwa roho zao, wakati ambao nafsi zao hutengana na miili yao.

Na (rehema zako hizo) ziwe ni kinga yao dhidi ya mambo yanayoweza kusababisha fitna, pamoja na matokeo yanayolazimiana na fitna hizo, pia (rehema zako hizo) ziwe ni ngao itakayowalinda na athari za moto, na kuwaepusha kubaki na kudumu ndani yake milele na milele, na ziwaongoze kwenye makaazi ya amani, katika sehemu ya kupumzikia ya wachamungu.

🌞
🔄

Rejea

  1. Ansarian, Diyar Asheqan, 1373, juz. 3, uk. 151-346; Khalji, Asrar Khamoushan, 1385, juz. 2, uk. 235-298.
  2. Ansarian, Diyar Asheqan, 1373, juz. 3, uk. 151-346.
  3. Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 319-336.
  4. Khalji, Asrar Khamoushan, 1383 S, juz. 1, uk. 235-298.
  5. Fihri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjdiyah, 1388, juz. 1, uk. 257-276.
  6. Madani Shirazi, Riaz al-Salkin, 1435 AH, juz. 2, ukurasa wa 81-136.
  7. Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 95-106.
  8. Darabi, Riadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 83-95.
  9. Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 1, uk. 114-97.
  10. Faidh Kashani, Taaliqat Ala al-Sahaifa al-Sajadiyeh, 1407 AH, uk. 27-29.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.