Nenda kwa yaliyomo

Aya ya al-Nur

Kutoka wikishia
Aya ya al-Nur
Jina la AyaAya ya al-Nur
Sura HusikaSurat al-Nur
Namba ya Aya35
Juzuu18
MaudhuiItikadi
Mada YakeKumwelezea Mungu Kama Nuru ya Mbingu na Ardhi


Aya ya al-Nur (Kiarabu: آية االنور) (Aya ya 35 katika Surat al-Nur) inamtambulisha Mwenyezi Mungu kuwa ni nuru ya mbingu na ardhi na katika fremu ya kutoa mfano Aya hii inabainisha namna ya kung'ara na kuangazia nuru hii kwa mbingu na ardhi na nafasi yake katika kuwaongoza waumini.

Wafasiri wamelifasiri, neno nuru katika Aya hii kwamba, lina maana ya uongofu, kutoa hidaya, kitu chenye kuangazia na chenye kutoa pambo na kwamba, mifano na vielelezo vyake ni Qur'ani, imani, uongofu wa Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) na Maimamu wa Kishia. Katika baadhi ya tafsiri na hadithi, Aya imetabikishwa na kuoainishwa na Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s).

Aya na Tarjumi Yake

اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ مَثَلُ نُورِهِ كَمِشْكَاةٍ فِيهَا مِصْبَاحٌ الْمِصْبَاحُ فِي زُجَاجَةٍ الزُّجَاجَةُ كَأَنَّهَا كَوْكَبٌ دُرِّيٌّ يُوقَدُ مِنْ شَجَرَةٍ مُبَارَكَةٍ زَيْتُونَةٍ لَا شَرْقِيَّةٍ وَلَا غَرْبِيَّةٍ يَكَادُ زَيْتُهَا يُضِيءُ وَلَوْ لَمْ تَمْسَسْهُ نَارٌ نُورٌ عَلَى نُورٍ يَهْدِي اللَّهُ لِنُورِهِ مَنْ يَشَاءُ وَيَضْرِبُ اللَّهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ


Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu ya Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.



(Qur'ani :24: 35)


Maudhui ya Aya

Katika Aya zilizokuja kabla ya Aya ya al-Nur, kumezungumziwa hukumu na sheria maalumu za hijabu na kujistri sambamba na kupambana na ufisadi, Aya ya al-Nur pia imeshuka chini na baada ya Aya hizo; [1] kwani ni dhamana ya kutekeleza hukumu zote za Mwenyezi Mungu hususan kudhibiti matamanio ya kingono ambayo ni matamanio makubwa zaidi na hilo halitimii isipokuwa kupitia imani na athari yake imara. Na ni kwa msingi huo katika Aya ya al-Nur kumetajwa nuru ya hidaya na uongofu wa Mwenyezi Mungu. [2]

Aya ya al-Nur na Aya zilizokuja baada yake zinatoa mlinganisho baina ya waumini (ambao wameongoka kupitia nuru ya Mwenyezi Mungu na makafiri (ambao wamekumbwa na giza totoro). [3] Wafasiri wana mitazamo tofauti kuhusianan na mafuhumu na maana ya Aya ya al-Nuru, maana ya maneno yake, mifano, vielelezo na dhihirisho la nuru ya Mwenyezi Mungu na vilevile vipi inanasibishwa na Mwenyezi Mungu maana ya Aya hii.

Allama Muhammad Hussein Tabatabai kwa mujibu wa maana ya awali na mashuhuri ya neno nuru, analitambua hilo kama ni kitu ambacho miili mingine hudhihirika na kuonekana machoni mwetu kupitia kwake; yaani nuru katika dhati yake ni dhahiri na hudhihirisha kisichokuwa yenyewe. Na nuru katika maana ya pili, huitwa kila kitu ambacho kinadhihirisha vitu vya kuhisika; na ni kutokana na sababu hiyo hisi (njia za utambuzi) tano za kidhahiri za mwanadamu kama kusikia, kunusa, kugusa na vuilevile visivyohisika kama akili vikaitwa kuwa ni nuru. [4]

Wafasiri wamelifasiri neno “nuru” mwanzoni mwa Aya (Allahu Noor al-Samawaat wa al-Ardh) kuwa ni mwenye kuongoza, [5] mwenye nuru, anayepamba [6] na kutoa kuwepo [7]. Na kwa mujibu wa Aya na riwaya nyinginezo, wameihesabu Qur'an, [8] imani, [9] uongofu wa Mwenyezi Mungu, [10] Mtume (s.a.w.w), [11] Maimamu wa Shia [12] na elimu [13] kuwa ni miongoni mwa mifano na dhihirisho la wazi la Aya ya al-Nur.[14]

Katika Aya hii, baada ya kuelezwa ukweli kwamba Mwenyezi Mungu ni nuru ya mbingu na ardhi, inabainishwa nuru ya Mungu kwa mifano. Katika mifano hii, nuru ya Mungu inafananishwa na taa iliyomo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayomeremeta, inayowashwa kwa mafuta yanay toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. [15]

Wafasiri katika kubainisha na kutoa ufafanuzi wa mifano hii, wametoa maoni na mitazamo tofauti. Baadhi wanasema, kusudio la ufananishaji huu ni nuru ya uongofu na maarifa juu ya Mwenyezi Mungu katika nyoyo za waumini; na baadhi wanasema ni kwa maana ya Qur'an ambayo inaangazia nuru ndani ya moyo wa mwanadamu. Kuna wengine nao ambao wameashiria ushabihishaji huu na Mtume (s.a.w.w) na kundi jingine pia limesema kuwa, hili linarejea katika roho na moyo wa utii na taqwa (uchaji-mungu) ambao ni chimbuko la kheri na saada. [16]

Kwa mtazamo wa Allama Tabatabai ni kwamba, makusudio ya Aya ya al-Nur ni kwamba, Mwenyezi Mungu anawaongoza kuelekea nuru yake watu ambao wako katika ukamilifu wa imani na siyo makafiri. Na makusudio ya Aya hii sio kwamba, baadhi ya watu anawaongoza kuelekea nuru yake na baadhi ya wengine anawanyima hilo, la hasha. [17] Sehemu ya mwisho ya Aya inasema: (وَيَضْرِبُ اللَّهُ الأَمْثَالَ لِلنَّاسِ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ; Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu).

Hapa inaashiriwa nukta hii kwamba, ndani ya mfano huu kuna maarifa na elimu kubwa na pana iliyojificha lakini imebainishwa katika kalibu na fremu ya mfano kwani hii ni njia nyepesi zaidi ya kubainisha uhakika na nukta za umakini na kila mtu (msomi na mjinga) atafahahamu na kuelewa kwa kiwango cha akili na udiriki wake. [18]

Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s) katika Aya ya al-Nur

Katika baadhi ya tafsiri wanazuoni wakitegemea hadithi mbalimbali wameitabaikisha na kuioainisha Aya ya al-Nur na Ahlul Bayt (a.s) katika tafsiri hizi shubaka imefananishwa na moyo wa Mtume (s.a.w.w) au Fatma Zahra (a.s), zujaj (tungi) imefananishwa na Imam Ali (a.s) na moyo wake na neno "nuru juu ya nuru" imefanishwa na Maimamu wa Shia ambapo alikuwa akija mmoja baada ya mwingine na walikuwa wakiungwa mkono kwa nuru ya elimu na hekima. [19]

Katika kitabu chake cha Tawhid, Sheikh Swaduq ananukuu hadithi kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) ambayo inaonyesha kuwa, Mwenyezi Mungu ameifanya Aya ya al-Nur kuwa mfano kwa ajili ya kuashiria Ahlul-Bayt (a.s). Katika Hadith hii, Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) wanatambulishwa kuwa, miongoni mwa dalili na ishara za Mwenyezi Mungu, ishara na dalili ambazo kupitia kwazo watu wanaongozwa kuelekea kwenye tawhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu na manufaa ya dini, hukumu za Kiislamu, wajibu na faradhi. [20] Allama Tabataba'i ameichukulia hadithi hii kuwa ni miongoni mwa marejeo ya baadhi ya mifano na kuashiria mifano yake iliyo bora zaidi ambao ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Aali zake (a.s); hata hivyo kwa mtazamo wake ni kuwa, Aya hii inaweza kujumuisha watu wengine wasiokuwa Ahlul-Bayt (a.s) vile vile, kama vile Mitume (a.s) na mawasii na mawalii wa Mungu. [21]

Vitabu tofauti vimejadili na kueleza kuhusu Aya ya al-Nur, kati ya hivyo ni Tafsiri ya Aya ya al-Nur kilichoandikwa na Mulla Sadra al-Shirazi na Mishkat al-Anwar cha al-Ghazali.

Rejea

Vyanzo