Al-Ajal al-Musamma

Kutoka wikishia

Al-Ajal al-Musamma (Kiarabu: الأجَل المُسَمَّی) (Ajali iliyohukumiwa) ni istilahi ya Kiqur’ani ambayo ina maana ya mwisho maalumu na usio na shaka wa kitu fulani. Kwa maana kwamba, kutokea kwake ni lazima. Al-Ajal Musamma ni mkabala wa Ajal Mu'allaq ambayo huambiwa mwisho wa kitu ambacho yumkini muda wake ukapungua au kuongezeka.

Katika Qur’ani ajali iliyohukumiwa imetumika pia kuhusiana na mwanadamu ambapo wafasiri wametoa nadharia na mitazamo tofauti kuhusiana na na hilo; miongoni mwayo ni kwamba: Wamesema, makusudio ya Ajal Musamma, ni kipindi kisicho na shaka cha kifo cha mwanadamu (bila shaka kifo cha mtu fulani kitatokea katika wakati fulani). Kadhalika kwa mujibu wa itikadi ya baadhi, Ajal Musamma ndio ule ulimwengu wa akhera.

Utambuzi wa maana

Makala asili: Ajal

Ajal Musamma inaundwa na maneno mawili ya Ajal na Musamma: Ajal ni kipindi au mwisho wa kipindi wa kitu; [1] Musamma nayo ina maana ya maalumu na iliyoainishwa. [2]

Katika Qur’an, Ajal wakati mwingine imetumika kwa qeid (sharti) ya Musamma ambapo wafasiri wanasema kuwa hiyo ni Ajal Musamma na wakati mwingine bila ya sharti ambapo katika baadhi ya maeneo kama Aya ya pili ya Surat al-An’am ambapo ndani yake kumetajwa majina ya Ajal isiyo Musamma, Qadha Ghair Mahtum na Ajal Mu’allaq. [3]

Tafsiri tofauti

Ajal Musamma ni istilahi ya Kiqur’an na imetumika mara 21 katika Sura mbalimbali za Qur’ani Tukufu. [4] Kwa mfano katika Aya ya 282 ya Surat al-Baqara imetumika kuhusiana na mkopo ambapo maana yake ni wakati maalumu ulioainishwa. [5]

Katika Qur’an neno Ajal Musamma limetumika pia kuhusiana na mwanadamu na ni katika Aya ya 2 ya Surat al-An’am: ((هُوَ الَّذِى خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضىَ أَجَلًا وَ أَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُ ; Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha akakuhukumieni ajali, na muda maalumu uko kwake tu)).

Kuhusiana na maana ya Ajal Musamma katika Aya kama hizi, kuna mitazamo tofauti baina ya wafasiri: [6]

  • Kundi miongoni mwa wafasiri linasema, makusudio yake ni zama na kipindi cha maisha ya mwanadamu, kuanzia kipindi cha kifo hadi kuanza kwa Kiyama; mkabala wa mwisho wa umri wa mwanadamu duniani ambao ni Ajal Ghair Musamma. [7]
  • Baadhi wanaitambua Ajal Musamma kwamba, ndio uleule ulimwengu wa Akhera. [8]
  • Mtazamo wa baadhi ni kwamba, makusudio ya “Ajal Musamma’ ni mwisho wa umri wa watu ambao bado wangali hai; kwa tofauti hii kwamba, Ajal Musamma ni kipindi ambacho bila shaka mwanadamu ataaga dunia wakati huo na Mwenyezi Mungu tu ndiye mwenye elimu ya hilo; lakini Ajal Mu’allaq ni kipindi cha kuaga dunia kila mwanadamu kwa mujibu wa hali yake ya mwili (afya ya mwili) ambapo yumkini kwa kuzingatia sababu za nje, umri wake ukapungua au kuongezeka. [11]

Tofauti yake na Ajal Mu’allaq

Kadhalika angalia: Ajal Mu’allaq

Allama Tabatabai anaamini kuwa, tofauti baina ya Ajal Musamma na Ajal Mu’allaq ni kuwa, Ajal Musamma ni kutokea kwake ni lazima na hakuna shaka na ndani yake hakutokei badaa (kubadilika na kupinduka); lakini katika Ajal Mu’allaq kuna badaa (mabadiliko). Kwa maneno mengine ni kuwa, katika Ajal Musamma, dua, sadaka na amali nyingine yoyote ambayo ina taathira katika Ajal Mu’allaq, hapa haina taathira yoyote ile. [12] Kadhalika kwa mujibu wa Aya za Qur’an Tukufu hususan Aya ya 2 ya Surat al-An’am ambayo inatambua kwamba, Ajal Musamma ni jambo lililo kwa Mwenyezi Mungu, wanazuoni wamefikia natija hii kwamba, kipindi cha Ajal Musamma anayekifahamu ni Mwenyezi Mungu peke yake. [13]