Mkopo
- Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine.
Mkopo (Kiarabu: القرض) ina maana ya kumpatia mtu mali kwa ahadi ya kurejesha mali hiyo inajulikana kama mkopo. Kwa mujibu wa Aya za Qur'an na hadithi, kukopesha ni jambo la mustahabu na mwenye kumkopesha mtu anapata ujira mkubwa. Imekuja kuhusiana na umuhimu wa kukopesha ya kwamba, mkopo mzuri ni kumkopesha Mwenyezi Mungu. Hadithi zinasisitiza juu ya kuwa na muamala mzuri wakati wa kurejesha mkopo.
Katika usahihi wa mkopo mbali na kutimia masharti ya jumla kama akili, kubaleghe, nia na mamlaka (uwezo na kufanya kwa hiari), kumetajwa pia masharti maalumu kama vile; kama kumeainishwa muda maalumu wa kurejesha mkopo, basi aliyekopesha hana haki ya kudai kurejeshewa mkopo huo kabla ya muda huo, kama ambavyo kuchelewa kurejesha mkopo kunahesabiwa kuwa ni dhambi. Aidha kuweka sharti la kurejesha mkopo zaidi ya kiwango alichokopeshwa mtu ni riba na ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu.
Maana
Mkopo maana yake ni kumpa mtu mali sambamba na kuahidi kurejesha kiwango hicho cha mali.[1] Katika Aya za Qur'an Tukufu maudhui ya mkopo imekuja na imetajwa kama Qardh al-Hasan yaani mkopo mzuri.[2] Kwa msingi huo, mkopo mzuri ni mkopo ambao unatokana na mali ya halali na haubatilishwi kwa masimbulizi na masimango.[3] Mkopo mzuri katika maana ya fikihi ni ule mkopo ambao hauna riba.[4]
Umuhimu Wake
Katika Aya za Qur'an Tukufu na hadithi, kumetiliwa mkazo mno juu ya suala la mkopo mzuri na unatambuliwa kuwa ni kumkopesha Mwenyezi Muungu.[5] Kwa mujibu wa hadithi iliyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w), kumkopesha mtu ni bora zaidi kuliko hata kutoa sadaka.[6] Aya za 245 za Surat al-Baqarah, 12 Surat al-Maida, 11 na 18 za Surat al-Hadid, 17 Surat Taghabun na Aya ya 20 ya Surat al-Muzammil zinazungumzia Qardh al-Hasan yaani mkopo mzuri.[7] Kwa mujibu wa Aya za Qur'an na hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s) kukopesha ni katika amali za mustahabu na mwenye kumkopesha mtu atakuwa na ujira mkubwa sana siku ya kiyama.[8] Kuwa na muamala mzuri wakati wa kupokea mkono na kutomfanyia ugumu mkopaji ni miongoni mwa mambo ambayo pia yameusiwa na kukokotezwa na Maimamu Maasumina (a.s). Hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) inasema: Mtu ambaye anamkopesha mhitaji na ana muamala mzuri wakati wa kupokea mkopo hufutiwa dhambi zake.[9]
Licha ya kukokotezwa na kuusiwa katika hadithi kuhusiana na suala la kukopesha, lakini kukopa ni jambo ambalo limekemewa; miongoni mwa hadithi zinazozungumzia hilo ni ile inayonasibishwa na Imam Ali (a.s) ambayo inakataza kukopa, kwani husababisha unyonge wakati wa mchana na huzuni na ghamu wakati wa usiku.[10]
Mifuko ya mikopo mizuri kwa ajili ya kuwapatia mikopo watu wahitaji na vilevile kwa lengo la kuepukana na riba zilizoko katika mikopo inayotolewa na benki, ilikuweko katika maeneo mbalimbali ya Iran hata kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyotokea 1979 kwa uongozi wa Imam Khomeini,[11] na hukumu zake zimebainishwa katika vitabu vya fat'wa vinavyotoa maelezo kuhusiana na masuala mbalimbali ya sheria za Kiislamu.[12]
Hukumu za Mkopo
Katika fiq'h mkopo maana yake ni kuifanya mali fulani kuwa miliki ya mtu mwingine na mkabala wake, aliyepewa mali hiyo aahidi kuirejesha katika muda waliokubaliana.[13] Ili muamala wa kukopeshana usihi na kuwa sahihi kuna masharti yake ambayo masharti jumla ni akili, kubaleghe, kuwa na nia, kuwa na mamlaka (kufanya kwa hiari), kama ambavyo pia kuna masharti ambayo ni maalumu ili muamala huo wa kukopeshana uwe sahihi; ambapo miongoni mwa masharti hayo maalumu ni: Mali husika iwe ni yenye kuwezekana kuimilikia, kinyume na kilevi na nguruwe (ambavyyo ni haramu kuuvimiliki). Kadhalika kitu ambacho kinakopeshwa kinapaswa kuainishwa na isiwe ni kitu ambacho hakieleweki na hakiko wazi.[14]
Baadhi ya Hukumu za Kukopa
Kwa mujibu wa fiq'hi ya Kishia, kama mkataba wa mkopo umeianisha muda wa kurejesha mkopo husika, haiwezekanai kwa aliyekopoesha kudai mali au kitu alichokopesha kabla ya kuwadia muda huo; lakini kama muda haujaainishwa, wakati wowote atakapotaka anaweza kudai.[15] Kama mkopeshaji atataka deni lake, mdaiwa anapaswa kulipa haraka na bila ya kuchelewa; na kuchelewesha kulipa mkono kunahesabiwa kuwa ni kutenda dhambi.[16]
Riba katika Mkopo
Makala Asili: Riba ya Mkopo
Moja ya masuala ya kifiq'h ambayo yanahusiana na maudhui ya kukopa, ni kadhia ya riba. Riba katika mkopo maana yake ni mkopeshaji kuweka sharti kwamba, atapokea kiwango ambacho ni zaidi ya hicho alichokopesha, bila kujali wakati wa kukopesha alibainisha na kuweka wazi hilo au la.[17] Hata hivyo, kiwango fulani cha ziada ambacho mkopaji anakitoa kwa ridhaa yake mwenyewe wakati wa kurejesha mkopo kwa mujibu wa mtazamo wa mafakihi wa Kishia na Ahlu-Sunna hakihesabiwi kuwa ni riba na wala sio haramu.[18]
Rejea
- ↑ Muassasah Dairat al-Maarif Fiqhe Islami, Farhangge Fiqh, juz. 6, uk. 549
- ↑ Tazama: Surat al-Baqarah: 245; surat al-Muzzammil: 20: surat at-Taghabun: 17; surat al-Hadid: 11 na 18
- ↑ Tabrisi, Majma' al-Bayan, juz. 2, uk. 607
- ↑ Jawadi Amuli, Tasnim, juz. 11, uk. 583
- ↑ Makarim Shirazi, Riba va Bankdariye Islami, 1380 S, uk. 127
- ↑ Kulaini, al-Kafi, 1407 H, juz. 4, uk. 10
- ↑ Makarim Shirazi, Riba va Bankdariye Islami, uk. 127
- ↑ Fallahzadeh, Ahkame Din, 1374 S, uk. 186; Imam Khomaini, Tahrir al-Wasilah, 1390 H, juz. 1, uk. 652
- ↑ Swaduq, Thawab al-A'mal, 1406 H, uk. 289
- ↑ Kulaini, al-Kafi, 1407 H, juz. 4, uk. 10
- ↑ Tazama: Sharif Razi, Ghanjine daneshmandan, 1370 S, juz. 9, uk.102, 209, 270 na 343.
- ↑ Tazama: Swafi Gulpayghan, Jamiu al-ahkam, 1385 S, juz. 2, uk. 302-303
- ↑ Imam Khomeini, Tahrir al-Wasilah, juz.1, uk. 651
- ↑ Imam Khomeini, Tahrir al-Wasilah, juz. 1, uk. 652
- ↑ Ushuli, Risalah Taudhih al-Masail (maraji'), kantor penerbit Islami, juz. 2, uk. 391, masalah no. 2275
- ↑ Ushuli, Risalah Taudhih al-Masail (maraji'), kantor penerbit Islami, juz. 2, uk. 392, masalah no. 2276
- ↑ Najafi, Jawahir al-Kalam, 1362 S, juz. 25, uk. 5-7; Makarim Shirazi, Barresiy-e Thuruq-e Farar az Riba, 1380 S, 17-19
- ↑ Shafii Mazandarani, Wam va Riba dar Negareshe Islami, 1379 S, uk. 75
Vyanzo
- Al-Qur'an al-Karim
- Amidi, Abdulwahid bin Muhammad. Ghurar al-Hikam wa Durar al-Kalim. Qom: Dar al-Kitab al-Islami, 1410 H.
- Ibnu Abi al-Hadid, Abdulhamid. Sharhu Nahj al-Balaghah. Qom: perpustakaan Ayatullah al-Marashi al-Najafi, 1964.
- Ahamadi Miyanji, Ali. Khathirate Ayatullah Ali Ahmadi Miyanaji, Bar Asas Nuskhe kitab-khune digital Nur).
- Ushuli, Ihsan dan Muhammad Hassan Bani Hashim Khomeini. Risalat Taudhih al-Masail (maraji'). Qom: Daftar Intisharat Islami.
- Imam Khomeini, Sayyied Ruhullah. Tahrir al-Wasilah. Najaf: Matbau al-Adab, 1390 H.
- Jawadi Amuli, Abdullah. Tasnim. Qom: Nashr Isra', 1385 S.
- Sharifrazi, Muhammad. Ganjineh Daneshmandan. Qom: Nashr: Newisandeh, 1370 S.
- Shafii Mazandarani, Muhammad. Wam va Riba dar Negareshe Islami. Mash'had: Ustane Qudse Rezavi, 1379 S.
- Safi Gulpaigani, Lutfullah. Jami' al-Ahkam. Qom: Daftar Intisharat Athar Hadhrat Ayatullah Safi Gulpaigani, 1385 S.
- Saduq, Muhammad bin Ali. Thawab al-A'mal wa 'Iqab al-A'mal. Qom: Dar al-Sharif al-Radhi li al-Nashr, 1406 H.
- Thabrasi, Fadhl bin Hassan. Majma' al-Bayan fi Tafsir al-Quran. Utangulizi: Muhammad Jawad Balaghi. Teheran: Intisharat Nashir Khasru, 1372 S.
- Fallahzadeh, Muhammad Hussein. Ahkame Din: Mutabeqe ba Fatawaye Maraji' Buzurge Taqlid. Teheran: Nashr: Mash'ar, 1386 S.
- Kulaini, Muhammad bin Yaqub. Al-Kafi. Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah 1407 H.
- Makarim Shirazi, Nashir. Barresiye Thuruqe Faraf az Riba. Mwandishi: Abu al-Qasim Aliyan Nejadi. Qom: Madrasah al-Imam Ali bin Abi Talib, 1380 S.
- Makarim Shirazi, Nashir. Riba va Bankdariye Islami. Mwandishi Abu al-Qasim Aliyan Nezadi. Qom: Madrasah al-Imam Ali bin Abi Talib, 1380 S.
- Muassasah Dairat al-Ma'arif Fiqh Islami. Farhange Fiqh Mutabeqe Madhabe Ahle Bait. Qom: markaz Dairat al-Maarif Fqh Islami, 1382 S.
- Najafi, Muhammad Hassan. Jawahir al-Kalam fi Sharh Sharai' al-Islam. Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, 1362-1369 S.