wikishia:Featured articles/2023
Kaaba (Kiarabu: الكعبة) ni kibla cha Waislamu na ni eneo takatifu zaidi kwa Waislamu katika mgongo wa ardhi. Wanazuoni na wasomi wa Kiislamu wanahesabu Kaaba kuwa eneo la kwanza kwa ajili ya kufanya ibada kwa wote na alama ya mwanadamu ya kuelekea kwa (upande wa) Mwenyezi Mungu.
Jengo hili linapatikana katika msikiti wa Makka (Masjdul-Haraam) katika mji wa Makka. Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, Waislamu lazima wasali Sala zao wakiwa wameelekea upande wa Kaaba, na mahujaji lazima waizunguke Kaaba wakati wa kutekeleza ibada ya tawafu kama ambavyo pia wakati wa kuchinja ni lazima kukielekeza kichinjwa hicho upande wa Kaaba yaani kibla. Katika eneo takatifu la Al-Kaaba, hakuna mtu mwenye haki ya kushambulia wanadamu au wanyama. Ali bin Abi Talib (a.s), Imamu wa kwanza wa mashia alizaliwa ndani ya Kaaba.
Makala mengine yaliyoangaziwa: Amina bint Wahb – Harakati za al-Yamani – Akhera