Nenda kwa yaliyomo

Amr bin Abdallah al-Jundu'i

Kutoka wikishia

Amr bin Abdallah al-Jundu'i (Kiarabu: عمرو بن عبد الله الجندعي) ni katika mashahidi wa Karbala na yeye alikuwa akitokana na kabila la Hamdan[1]. Alijiunga na jeshi la Imamu Hussein (a.s) baada Imamu Hussein (a.s) kuwasili Karbala na kabla ya tukio la Ashura.[2] Kuna kauli mbili kuhusiana na namna alivyouawa shahidi:

  1. Aliuawa shahidi katika shambulio la kwanza la jeshi la Omar bin Sa’d dhidi ya masahaba wa Imamu Hussein (a.s).[3]
  2. Muhammad Samawi (aliaga dunia 1370 Hijiria) amenukuu katika kitabu chake cha Ibsar al-Ain kutoka katika kitabu cha al-Hadaiq al-Wardiyah cha Humayd bin Ahmad Muhalli (aliyeaga dunia 652 Hijiria) kwamba, Amr alikuwa amezimia na kupoteza fahamu kutokana na majeraha mengi aliyokuwa ameyapata na pigo alilokuwa amepigwa kichwani, wakalitoa kabila lake katika medani ya vita na mwaka mmoja baadaye akafariki dunia.[4]

Imekuja katika Ziyarat al-Shuhadaa: {السَّلامُ عَلَی الْمُرَتَّثِ مَعَهُ عَمْرُو بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْجُنْدُعِیِّ ; Amani iwe juu yake ya Amr bin Abdallah al-Jundu'i ambaye alijeruhiwa na kuaga dunia nje ya vita}.[5]

Rejea

  1. Qurayshī, al-Bālighūn al-fatḥ, uk. 405.
  2. Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, 1419 H, uk. 136.
  3. Ibn Shahrāshūb, Manāqib Āl Abī Ṭālib, juz. 4, uk. 113.
  4. Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 136.
  5. Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 98, uk. 273.

Vyanzo

  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Edited by Hāshim Rasūlī & Muḥammad Ḥusayn Āshtīyānī. Qom: Nashr-i ʿAllāma, [n.d].
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Dār al-Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Qurayshī, ʿAbd al-Amīr al-. Al-Bālighūn al-fatḥ fī Karbala. Beirut: Bayt al-ʿIlm li-l-Nābihīn, 1429 AH.
  • Samāwī, Muḥammad b. Ṭāhir al-. Ibṣār al-ʿayn fī anṣār al-Ḥusayn. Edited by Muḥammad Jaʿfar al-Ṭabasī. Qom: Markaz al-Dirāsāt al-Islāmīyya, 1419 AH.