Ziyarat al-Nahiyah al-Muqaddasah
- Ili kuona matumizi mengine ya Ziyarat al-Nahiyah al-Muqaddasah angalia kuondoa utata.
Ziyarat al-Nahiyah al-Muqaddasah (Kiarabu: زيارة الناحية المقدسة) ni miongoni mwa ziara za Imamu Hussein (a.s) ambayo imekokotezwa na kutiliwa mkazo isomwe katika Siku ya Ashura. Waislamu wa madhehebu ya Shia huisoma ziara hii pia katika masiku mengine. Ziyara hii inaanza kwa kuwasalimia Mitume na Maimamu watoharifu (a.s) na inaendelea kwa kumsalimia Imamu Hussein (a.s) na masahaba zake. Baada ya hapo, ziraya hii iinaeleza sifa na matendo ya Imam, mazingira ya harakati, ufafanuzi wa kuuawa shahidi na masaibu yake na kukumbwa na msima ulimwengu na viumbe.
Ziyarat al-Nahiyah al-Muqaddasah imenukuliwa na Ibn Mash'hadi (aliaga dunia: 610 AH) na kwa mujibu wa Allama Majlisi na Sheikh Mufid (aliaga dunia: 413 AH) wamenukuu ziyara hii. Katika vyanzo vya hadithi hakujabainishwa wazi kwamba, ni Imamu gani alibainisha; lakini baadhi wanasema, ilitoka kwa Imamu Mahdi (a.t.f.s).
Kupewa jina na umuhimu wake
Ziyarat al-Nahiyah al-Muqaddasah ni ziyara inayojumuisha masaibu ya Imamu Hussein na masahaba zake. [1] Ni kwa sababu hiyo ndio maana watoa hotuba na wasomaji mashairi na kaswida za maombolezo wanaitumia ziyara hii kama nyaraka. [2] Ibn Mash’hadi ameitaja ziyara hii kuwa ni katika amali za siku ya Ashura; [3] lakini Waislamu wa madhehebu ya Shia husoma ziyara hii katika masiku mengine ya mwaka. [4]
Ziyara hii inajulikana pia kwa jina la Ziyarat al-Nahiyah al-Mash’hura [5] au Ziyarat al-Nahiyah al-Maarufah [6], mkabala na Ziyarat al-Shuhadaa ambayo inajulikana kwa jina la Ziyarat al-Nahiyah Ghair al-Mash’hura. [7]
Nahiyhaht al-Muqaddasah ni istilahi ambayo Mashia walikuwa wakiitumia kuanzia zama za Imamu Hadi (a.s) mpaka katika kipindi cha Ghaiba Sughra (Ghaiba ndogo) kwa ajili ya kuashiria Imamu Maasumu (a.s). [8]
- Kadhalika angalia: Nahiyat al-Muqassah.
Ziyarat al-Nahiyah al-Muqaddasah imetoka kwa Imamu gani?
Katika vyanzo vya hadithi haijabainishwa kwamba, Ziyarat al-Nahiyat al-Muqaddasah imetoka kwa Imamu gani Maasumu. Katika kitabu cha al-Mazar al-Kabir cha Ibn Mash’hadi (aliaga dunia: 610 AH) imekuja tu kwamba, imetoka kwa alayhisalaam (amani ya Mwenyezi Munguu iwe juu yake). [9] Allama Majlisi pia ambaye amenukuu kutoka kwa Ibn Mash’hadi na Sheikh Mufid pia (aliaga dunia 413 Hijiria) hawajaashiria kabisa kwamba, ziyara hii imebainishwa na Imamu yupi miongoni mwa Maimamu watoharifu (a.s). [10]
Pamoja na hayo yote kupitia maneno ya Ibn Mash’hadi wakati wa kunukuu hadithi wamefikia natija hii kwamba, amesema mmoja wa manaibu. [11]
Maudhui
Ziyara al-Nahiyah al-Muqaddasah inaanza kwa kuwasalimia Mitume, Maimamu watoharifu (a.s) na Imamu Hussein (a.s) na masahaba zake katika Karbala. Baada ya hapo, ziraya hii inaeleza sifa na matendo ya Imam kabla ya tukio la Karbala, mazingira ya harakati ya Ashura, ufafanuzi wa kuuawa shahidi na masaibu yake na kukumbwa na msima ulimwengu na viumbe. Mwishoni Ziyara hii inamalizika kwa kufanya tawasuli kwa Ahlu-Bayt na kwa dua. [13]
Mwanzoni mwa ziyara hii Mitume 24 na Watu Watano wa Kishamia (Ahlul-Kisaa) wanasalimiwa sababu na sifa zao mashuhuri. [14] Kutolewa salamu Imamu Hussein wakati mwingine kunaambatana na kutaja jina, fadhila na utendaji wa mtukufu huyo na wakati mwingine kwa kubainishwa viungo na masaibu yaliyovipata. [15]
Sifa maalumu za Imamu Hussein
Katika ziyara hii kumetambulishwa baadhi ya sifa za Imamu Hussein (a.s):
- Turba yake inaelezwa kuwa ni shifaa (ponyo).
- Kuomba dua katika kaburi lake hukubaliwa.
- Maimamu wanatoka katika kizazi chake.
- Mwana wa Mtume (s.a.w.w), Ali na Fatima (a.s). [16]
Uthibitisho wa ziyara
Ziyarat al-Nahiyat al-Muqaddasah imenukuliwa katika kitabu cha al-Mazar al-Kair cha Ibn Mash’hadi (aliaga dunia: 610 Hijiria). [17] Allama Majlisi pia ameileta Ziyara hii katika kitabu chake cha Bihar al-Anwar akinukuu kutoka katika kitabu cha al-Mazar kilichoandikwa na Sheikh Mufid (aliyeaga dunia: 413 Hijiria); [18] hata hivyo katika nakala zilizoko za kitabu hiki, ziyara hii haipo. [19]
Mwanzoni mwa kitabu chake, Ibn Mash’hadi alisema kwamba yale aliyoyaleta katika kitabu hiki yalimfikia kupitia kwa wapokezi wa kuaminika na yanafikia kwa masharifu. [20] Baadhi ya watu, wakitemegea neno masharifu kama hoja wanasema kwamba, makusudio ni Maimamu Maasumu na hivyo wanaona riwaya za kitabu hiki ni sahihi na zenye itibari hata zikiwa ni mursal. [21]
Mkabala wake, Ayatullah Khui katika kitabu chake cha Mu’jam a’-Rijal al-Hadith hakubaliani na itibari ya kitabu cha al-Mazar al-Kabir na anamuona Ibn Mashj’had kama mtu asiye na utambulisho (asiyetambulika. [234] Muhammad Hadi Yusuf Gharawi pia ambaye ni mtafiti wa masuala ya historia ametilia shaka mapokezi ya ziyara hii. [24]
Kunukuliwa ziyara kutoka kwa Sayyid Murtadha
Sayyid Ibn Tawus, katika kitabu Misbah al-Za'ir, amenukuu ziyara kutoka kwa Sayyid Murtadha (aliyefariki: 436 AH) yenye jina la Ziyarat Thanawiyah bi-alfadh Shafiyah kuwa ni miongoni mwa matendo na amali za siku ya Ashura. [26]
Vitabu vilivyoandikwa kufafanua ziyaral al-Nahiyah
Kumeandikwa vitabu mbalimbali vinavyotoa sharh na ufafanuzi wa ziyarat al-Nahiyah al-Muqaddasah. Miongoni mwavyo ni:
- Al-Dhakhirah al-Baqiyah; Mwandishi Muhammad Jaafar Shamili Shirazi (Kifarsi)
- Al-Shams al-Sahiyah, kimeandikwa na kundi la Maulamaa (Kifarsi).
- Tuhafah Qaimiyah, mwandishi Sheikh Muhammad Baqir Faqih Imani (Kifarsi).
- Kashf Dahiyah, kutoka kwa bnaadhi ya Maulamaa wa India (Urdu)
- Salam Mauud; kitabu hiki cha Muhammad Ridha Sangari kinabainisha na kutoa wasifuwa Ziyarah al-Nahiyah al-Muqaddasah. [33]