Sayyid Mahmoud Husseini Shahroudi

Kutoka wikishia
Usimchangaye na Sayyid Mahmoud Hashemi Shahroudi.
Sayyid Mahmoud Husseini Shahroudi

Sayyid Mahmoud Husseini Shahroudi (1262-1353 Hijria Shamsia) Marjaa Taqlidi wa Kishia aliyekuwa akiishi Najaf, Iraq ni baba wa Sayyid Muhammad Husseini Shahroudi. Yeye ni katika wanafunzi wa Mirza Naini na Agha Dhiya Iraqi. Alichukua jukumu la Umarjaa baada ya Sayyid Abul-Hassan Isfahani. Mirza Naini alikuwa akimuita kwa jina la Dhu al-Shahadatein na alikuwa akitaka kujua mtazamo wake katika utoaji wa idhini ya Ijtihadi kwa wanafunzi wake. Kadhalika Agha Agha Dhiya Iraq na Sayyid Abul-Hassan Isfahani walikuwa wakiwapeleka wanafunzi wao kwake kwa ajili ya kufanyiwa mtihani kwa ajili ya kupata daraja la Ijtihad.

Kujenga misikiti, Husseiniya na vyuo vya elimu ya kidini huko Kabul na baadhi ya miji ya Iran, kukarabati vyuo vya kidini vya Bukharai na Qazwini huko Najaf, kuasisi ofisi ya Hija na kulalamikia utawala wa Kipahlavi katika radiamali yake ya tukio la hujuma na shambulio dhidi ya Chuo cha Feyziyeh ni miongoni mwa hatua za Sayyid Mahmoud Husseini Shahroudi katika kipindi cha Umarjaa wake. Aidha katika kipindi cha Umarjaa wake, matembezi ya kumbukumbu ya Arobaini ya Imam Hussein kutoka Najaf hadi Karbala yalishika kasi.

Risala katika maudhui ya Fiq’h na Usul na vilevile masomo yaliyokuwa yakitolewa na Agha Dhiya Iraqi na Mirza Naini ni miongoni mwa vitabu vya Sayyid Mahmoud Sharoudi. Kadhalika hotuba zake za masomo kuhusiana na masomo ya juu kabisa ya khariji ya maudhui ya Swala ziliandikwa katika juzuu nne na Sayyid Muhammad Ja’far Jazairi Murawwij chini ya nauani ya Yanabiu al-Fiq’h.

Kitabu cha «al-Imam al-Shahroudi al-Sayyid Mahmoud al-Husseini» kilichoandikwa na Sayyid Ahmad Husseini Ishkawari (alizaliwa 1350 Hijria) kinazungumzia maisha yake na kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Julai 2021, kulifanyika kongamano la kumbukumbu ya Husseini Shahroudi kwa anuani ya Alim Dhu al-Shahadatein katika miji ya Mash’had na Qom-Iran na Najaf-Iraq.

Historia ya Maisha Yake

Mazishi ya Sayyid Mahmoud Shahroudi huko Najaf

Sayyid Mahmoud Husseini Shahroudi ni mtoto wa Sayyid Ali. Alizaliwa 1301 Hijria katika kijiji cha Qale Abdullah moja ya viunga vya mji wa Bastam, jirani na Shahroud. [1] Kwa mujibu wa Sayyid Ahmad Husseini Ishkawari (aliyezaliwa 1350 Hijiria), mtambuzi wa machapisho na mwanabibliorafia wa Kishia, nasaba yake inaishia kwa Zayd ibn Ali. [2] Baba yake alikuwa mkulima na babu yake Sayyid Abdallah, alikuwa alimu, msomi na mtu aliyeipa mgongo dunia. [3] Yamenukuliwa makarama mbalimbali kutoka kwa Sayyid Abdallah. [4]

Watoto

Sayyid Mahmoud Shahroudi alikuwa na watoto watatu wa kiume:

  • Sayyid Muhammad: (Alizaliwa 1344 Hijria) na mwaka 1375 Hijria alifanikiwa kupata idhini ya Ijtihadi kutoka kwa baba yake. Aidha wakati baba yake hayupo alikuwa akiswalisha katika msikiti wa al-Hindi nyakati za usiku na wakati wa adhuhuri alikuwa akiswalisha katika msikiti wa Jowharchi. Kuandika hotuba za masomo ya Usul yaliyokuwa yakitolewa na baba yake na vilevile Swalat al-Jum’at ni katika athari zake. [5]
  • Sayyid Ali: (alizaliwa 1347 Hijiria). Alikuwa akishiriki masomo ya Khariji (darsa ya daraja la juu kabisa ya fikihi) ya kaka yake na alikuwa na jukumu la usimamizi wa ofisi yake. [6]
  • Sayyid Hussein: (alizaliwa 1360). Alikuwa akishiriki masomo ya Khariji (darsa ya daraja la juu kabisa ya fikihi) ya kaka yake Sayyid Muhammad na alikuwa akiandika hotuba zake za masomo. [7]

Sayyid Mahmoud Shahroudi aliaga dunia 18 Shaaban 1394 Hijiria akiwa na umri wa miaka 94 [8] na kuzikwa katika Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib (a.s) katika mji wa Najaf, Iraq. [9]

Harakati za Kielimu

Shahroudi alisoma masomo yake ya msingi katika eneo la Bastam na kisha baadaye akiwa na lengo la kujiendeleza zaidi kielimu alifunga safari na kwenda katika mji wa Mash’had. Alisoma katika mji wa Mash’had masomo ya ngazi ya juu na wakati huo huo alikuwa akifundisha Kifayat al-Usul katika chuo cha kielimu katika mji huo. [10]

Mwaka 1328 Hijria Shahroudi alielekea Najaf-Iraq na kushiriki masomo ya Fiq’h na Usul yaliyokuwa yakifundishwa na Akhund Khorasani. Sambamba na kushiriki masomo hayo alikuwa akifundisha vitabu vya Rasail na Makasib vya Sheikh Murtadha Ansari. [11] Alishiriki masomo ya Akhund Khorasani kwa muda wa takribani miezi 18. Baada ya kuaga dunia Akhund Khorasani 20 Mfunguo Tatu Dhul-Hija 1329, Shahroudi alielekea katika mji wa Samarra; hata hivyo haukupita muda akarejea tena Najaf na kusoma duru moja ya Usul al-Fiq’h kwa Agha Dhiya al-Iraqi. Aidha alikuwa akishiriki katika darsa na masomo yaliyokuwa yakifundishwa na Mirza Naini na alikuwa miongoni mwa mwanafunzi wake maalumu. Mirza Naini alikuwa akimtanguliza Shahroudi mbele ya wanafunzi wake wengine na na wakati alipokuwa akitoa cheti cha kielimu kwa wanafunzi wake, alikuwa akimuuliza maoni na matazamo wake. [12] Inaelezwa kuwa, Mirza Naini alikuwa akiuhesabu ushahidi wake kwamba, ni ushahidi wa watu wawili waadilifu. [13] Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana Agha Dhiya al-Iraqi na Sayyid Abul-Hassan Isfahani wakawa wakimuita kwa lakabu ya Dhu Shahadatein (mwenye shahada mbili) na walikuwa wakiwatuma kwao wanafunzi wao ili awafanyie mtihani wa kufikia daraja la Ijtihad. [14]

Wasomi wengi walikuwa wakihudhuria masomo aliyokuwa akiyafundisha Mahmoud Shahrodi. Sayyid Muhammad Hussein Shahroudi, Sayyid Jawad Aal Ali Shahroudi, Sayyid Muhammad Ja’afar Jazairi Murawwij, Muhammad Rahmati Sirjani, Ali Azad Qazvini [15], Muhammad Ibrahim Jannati, Muslim Malakoti, Jawad Tabrizi, [16] na Sayyid Kadhim Hairi [17] ni miongoni mwa wanafunzi wake.

Umarjaa

Shahroudi alifanikiwa kufikia daraja ya Ijtihadi akiwa na umri wa miaka 35 na ilikuwa katika zama za Mirza Naini na Sayyid Abul-Hassan Isfahani. [18] Mpaka katika kipindi ambacho wanazuoni hao wawili walikuwa hai, alijizuia kutoa kitabu chake cha fat’wa na alikuwa akiwaambia warejee kwa wanazuoni hao wawili. Baada ya kuaga dunia Sayyid Abul-Hassan Isfahani mwaka 1365 Hijria, alichukua jukumu la uongozi na Umarjaa wa Mashia na mwaka 1366 Hijiria alitoa kitabu chake cha Fat’wa katika miji ya Najaf na Tehran. [19] Umarjaa wake ulichukua wigo mpana zaidi baada ya kuaga dunia Ayatullah Boroujerdi na Sayyid Muhsin Hakim. [20]

Harakati

  • Kujenga msikiti na Husseiniya Kabul, Afghanistan.
  • Kuanzisha vyuo vya kielimu katika miji ya Faruj (chuo cha Mahmoudiya), Zahedan na Fuman.
  • Kukarabati vyuo vya kidini vya Bukharai na Qazwini huko Najaf.
  • Kujenga misikiti katika miji mbalimbali ya Iran kama Bojnurd, Tayyibat, Kalaleh, Ramiyan na Jajarm.
  • Kuanzisha kituo cha elimu: Kituo hiki cha mafunzo kilikuwa kikifundisha masomo kuanzia hatua ya msingi mpaka masomo ya kati kwa lugha mbili za Kifarsi na Kiarabu. Katika zama hizo, vituo vya kutoa mafunzo Najaf vilikuwa vikipata himaya na uungaji mkono kutoka kwa serikali za Iran na Iraq. Kwa msingi huo, akthari ya wanafunzi wa masomo ya dini walikuwa wakikataa kuandikisha majina watoto wao. [21]
  • Kuanzisha kitongoji cha makazi ya wanafunzi wa masomo ya dini: Kitongoji hiki kilikuwa na ukubwa wa mita mraba takribani 124,000 karibu na kaburi la Kumayl ibn Ziyad na kilikuwa baina ya Najaf na Kufa. Alimu huyu alikuwa amekusudia kujenga hapo nyuma 100, kituo kimoja cha afya na kituo kimoja cha utoaji mafunzo kwa ajili ya wanafunzi wa masomo ya dini. Majengo kadhaa yalijengwa katika kipindi cha uhai wake na majengo mengine yakajengwa na watoto wake baada ya yeye kuaga dunia, mpaka mwaka 1359 Hijria Shamsia wakati utawala wa wakati huo wa Iraq ulipowafukuza watoto wake kutoka nchini humo. [22]
  • Matembezi ya kumbukumbu ya Arobaini ya Imam Hussein (a.s) yalishika kasi katika zama za Umarjaa wake na wanafunzi wa masomo ya dini walikuwa wakitembelea kutoka Najaf na kuelekea Karbala. Inaelezwa kuwa, Shahroudi alitembea kwa miguu mara 260 kutoka Najaf kwenda Karbala.

Kuasisi Ofisi ya Hija

Ayatullah Shahroudi kuanzia mwaka 1344 Hijiria Shamsia alituma kundi la watu kwenda Hija kwa ajili ya kuchukua jukumu la kujibu maswali mbalimbali ya kisheria katika msimu wa ibada ya Hija ambapo jina la timu hiyo lilitambulika kama al-Biithat al-Diniyah Lilhaj. Mwaka 1345 Hijiria Shamsia akiwa pamoja na wajumbe wa kamati yake ya istiftaa (ya utoaji Fat’wa) alishiriki katika ibada ya Hija na hapo ndipo alipodiriki udharura wa kuweko ofisi na ujumbe kama huu. [26] Katika safari hiyo, Shahroudi alipokelewa na watu pamoja na shakhsia wa kisiasa na kidini katika miji na maeneo mbalimbali akiwemo Amir wa mji wa Madina, kaka wa mtawala wa Saudia wakati.

Radiamali kwa Tukio la Feiziyeh

Sayyid Husein, mtoto wa Sayyid Mahmoud Shahroudi anasema, baba yake alilaani hujuma na shambulio la vibaraka wa utawala wa kifalme wa Kipahlavi dhidi ya Chuo cha Feiziyeh mwaka 1342 Hijiria Shamsia na kuhusiana na hilo alifanya mawasiliano tofauti kwa njia ya telegrafu na watu wa kawaida na wanazuoni. [26] Hata hivyo kuna telegrafu kutoka kwa Imam Khomeini ya 1 Aprili 1963 ambayo inamhutubu yeye na ikionyesha kushangaa kukaa kimya Waislamu kuhusiana na mauaji dhidi ya wanazuoni katika mji wa Qom. [30]

Vitabu

Sayyid Mahmoud Shahroudi ameandika vitabu mbalimbali na baadhi yake ni:

Aidha ameandika vitabu vya fiqhi katika maudhui mbalimbali kama tohara, kutayamam, udhu, vazi la mwenye kuswali, Swala ya msafiri, Khumsi, Zaka, mirathi, Hija, utambulisho wa elimu ya usul, qaidat yad, qaidat laa dharar na mijadala ya masomo ya Khariji (darsa ya daraja la juu kabisa ya fikihi) kuhusiana na Swala na nataij al-Afkar fil Usul n.k. [31]

Kongamano

Kongamano la kumbukumbu ya Sayyid Mahmoud Husseini lilifanyika katika miji ya Mash’had na Qom-Iran na Najaf Iraq kwa anuani ya Alim Dhu al-Shahadatein. Hiyo ilikuwa Julai 2021. Aidha 8 Julai, 2021 kulifanyika kongamano kama hilo katika mji wa Shahrud. [34].

Monografia

Kuhusiana na Sayyid Mahmoyd Shahroudi, kumeandika athari na vitabu mbalimbali kwa lugha za Kiarabu na Kifarsi. Miongoni mwazo ni:

  • Al-Imam al-Shahrudi al-Sayyid Mahmud al-Husayni, kilichaondikwa na Sayyid Ahmad Husayni Ishkawari: Kitabu hiki kinachohusiana na maisha ya Shahroudi kiliandikwa katika zama za uhai wake. Kitabu hiki kina kurasa 122 na kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu.
  • Zindigi wa-mubarazat Ayatollah al-'Uzma Sayyid Mahmud Husayni Shahrudi bi riwayat asnad, kitabu hiki kimeandikwa na Dawud Qassimpour na Shahin Rezai. Kitabu hiki kimechapishwa na kusambazwa mjini Tehran na Kituo cha Nyaraka za Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1389 Hijria Shamsia kikiwa na kurasa 252.

Maktaba ya Picha

Vyanzo