Sala ya Jumapili mwezi Dhul-Qaadah
Sala ya Jumapili mwezi Dhul-Qaadah (Kiarabu: صلاة يوم الأحد من شهر ذي القعدة) ni Sala ambayo ni mustahabu na yenye adabu maalumu ambayo husaliwa katika moja ya siku za Jumapili za mwezi Dhul-Qaadah. Katika hadithi kumenukuliwa maelezo ya namna ya kuisali kama ambavyo kumetajwa pia athari za Sala hii kama kusamehewa madhambi. Sanadi na mapokezi ya Sala hii inatoka kwa Sayyid Ibn Tawus ambaye amenukuu kutoka kwa Malik ibn Anas ambaye naye amenukuu kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w).
Namna ya kuisali
Sala hii ni Sala mbili zenye rakaa mbili mbili ambayo husaliwa kwa nia ya Sala ya Jumapili ya mwezi Dhul-Qaadah. Katika kila rakaa, inasomwa Surat al-Fatiha mara moja na Surat Tawhid (Qul-huwallah mara tatu), Surat al-Nas mara moja na Surat al-Falaq mara moja. Baada ya kumaliza rakaa nne mhusika atafanya istighfar mara 70 (kusema dhikri kama اَستَغفِرُ اللهَ و اَتوبُ إلیه), لا حَول و لا قوةَ الا بالله mara moja na mwisho inasomwa dua hii: «یا عَزِیزُ یا غَفَّارُ اغْفِرْ لِی ذُنُوبِی وَ ذُنُوبَ جَمِیعِ الْمُؤْمِنِینَ وَ الْمُؤْمِنَاتِ فَإِنَّهُ لَا یغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ». Kadhalika kabla ya kusali Sala hii inapasa kufanya ghusli.
Sayyid Ibn Tawus amenukuu katika kitabu cha Iqbal al-A’mal hadithi ambayo nyaraka ya Sala hii ambayo imenukuliwa na Anas bin Malik kutoka kwa Mtume (s.a.w.w). [2]
Fadhila na wakati
Imenukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) kwamba, kila ambaye atasali Sala ya Jumapili Dhul-Qaadah, atakubaliwa toba yake, atasamehewa dhambi zake na maadui zake watakuwa radhi naye siku ya Kiyama, atakufa akiwa na imani, na dini na imani yake havitachukuliwa; kaburi lake litakuwa pana, na lenye nuru, wazazi wake watakuwa radhi naye; kusamehewa kwake dhambi kutajumuisha wazazi wake wawili na dhuria yake; atafunguliwa milango ya riziki; malaika wa kutoa roho ataamiliana naye vizuri wakati wa kifo chake; atakufanya katika hali ya wepesi n.k [3]
Mirza Jawad Maleki Tabrizi, mmoja wa maulamaa wa Kishia ameusia juu ya kusali Sala hii. [4] Wakati wa kusali Sala hii ni siku ya Jumapili ya mwezi Dhul-Qaadah na mtu anaweza kuisali Sala hii wakati wowote ule wa siku hii. Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa katika kitabu cha Iqbal al-A’mal, [5] endapo Sala hii itasaliwa pia katika Jumapili ya miezi mingine, itakuwa na ujira huo uliotajwa. [6]