Sala ya kumi la kwanza la Dhul-Hija

Kutoka wikishia

Swala ya kumi la kwanza la Dhul-Hija ni mustahabu na ina rakaa mbili na huswaliwa nyusiku kumi za mwanzo za Dhul-Hija (Mfunguo Tatu). Katika Swala hii baada ya Surat al-Hamdu na Surat Ikhlas husomwa Aya ya 142 ya Surat A’araf. Aya iliyotajwa ni ashirio la miadi (miqati) ya siku arubaini za mtukufu Nabii Mussa katika mlima Sinai kwa ajili ya kuchukua mbao za maandiko zilizokuwa na amri na maagizo ambapo siku kumi zake za mwisho zilisadifiana na kumi la mwanzo la mwezi Dhul-Hija (Mfunguo Tatu). Kwa mujibu wa hadithi mtu ambaye ataswali Swala hii katika kumi la mwanzo la Dhul-Hija anakuwa mshirika wa thawabu za Mahujaji.

Namna ya kuiswali

Swala ya kumi la kwanza la Dhul-Hija huswaliwa katika nyusiku kumi la mwanzo wa mwezi huu na wakati wake ni baina ya swala ya magharibi na Isha.[1] Swala hii ina rakaa mbili. Katika kila rakaa baada ya Surat al-Fatiha na Surat Ikhlas husomwa[2] Aya ya 142 ya Surat A’araf inayosema:

وَ واعَدْنا مُوسی‏ ثَلاثِینَ لَیلَةً وَ أَتْمَمْناها بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِیقاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِینَ لَیلَةً وَ قالَ مُوسی‏ لِأَخِیهِ هارُونَ اخْلُفْنِی فِی قَوْمِی وَ أَصْلِحْ وَ لا تَتَّبِعْ سَبِیلَ الْمُفْسِدِینَ

Tulimuahidi Musa masiku thalathini na tukayatimiza kwa kumi; ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arubaini. Na Musa akamwambia nduguye Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu.
(Quran: 7: 142)[3]

Swala hii imetajwa katika Mafatihul Jinan katika sehemu ya amali za mwezi wa Dhul-Hija.[4] Aya iliyotajwa ni ashirio la miadi (miqati) ya siku arbaini za mtukufu Nabii Mussa katika mlima Sinai kwa ajili ya kuchukua mbao za maandiko zilizokuwa na amri. Katika kipindi hiki Harun ambaye ni nduguye alishika mahala pake baina ya Bani Israili.[5] Kwa mujibu wa Aya hii awali Mussa alibakia katika mlima wa Sinai kwa muda wa usiku 30 na kisha baadaye zikaongezwa nyusiku 10.[6] Katika baadhi ya hadithi nyusiku 30 zimefasiriwa katika mwezi Dhul-Qaadah na nyusiku 10 zilizobakia ni za mwezi Dhul-Hija.[7]

Ujira na mapokeo

Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa katika kitabu cha Iqbal al-A’mal, Imam Muhammad Baqir(a.s) alimuagiza mwanawe Imam Swadiq(a.s) kwamba, asiache Swala hii katika kumi la mwanzo la mwezi Dhul-Hija, kwa sababu kama ataiswali katika kumi hili atakuwa mshirika wa thawabu za mahujaji, hata kama hatakuwa amekwenda Hija.[8] Sayyied Ibn Tawus amenakili jambo hili katika kitabu cha Ibn Ushnas.[9] Kwa mujibu wa kile kilichokuja katika kitabu cha Wasail al-Shiah ni kuwa, jina la kitabu cha ibn Ushnas lilikuwa ni “Amal Dhil-Hija”.[10]

Rejea

  1. Qumi, Mafatih al-Jinan, 1348 HS, Mada (a'mali mahe dhl-Hajjeh), uk. 401
  2. Qumi, Mafatih al-Jinan, 1348 HS, Mada (a'mali mahe dhil-Hajjeh), hlm. 401
  3. Surah al-A'raf, aya ya 142
  4. Qumi, Mafatih al-Jinan, 1348 HS, Mada (a'mali mahe dhl-Hajjeh), hlm. 401
  5. Tazama: Qumi, Tafsir al-Qumi, 1404 Q, juz. 1, uk. 239
  6. Surah al-A'raf, ayat 142
  7. Tazama: Qumi, Tafsir al-Qumi, 1404 Q, juz. 1, uk. 239
  8. Sayyied Ibnu Tawus, Al-Iqbal, 1409 Q, juz. 1, uk. 317
  9. Sayyied Ibnu Tawus, Al-Iqbal, 1409 Q, juz. 1, uk. 317
  10. Hur Amii, Wasail al-Shiah, 1416 Q, juz. 8, uk. 123

Vyanzo

  • Hur Amili, Muhammad bin Hussein,Wasail al-Shiah ila Tahsil Masail al-Shiah, Qom: Muasasah Alulbait, chapa ya tatu, 1416 Q
  • Sayyied Ibnu Tawus, Ali bin Mussa, Al-Iqbal bi al-A'mal, Tehran: dar al-Kutub al-Islamiyah, chapa ya pili, 1409 Q
  • Qumi, Abbas, Kulliyat mafatih al-Jinan, terjemahan: Ilahi Qamsheiye, Khusynusiye ahmad Shabari, Qom: mathbu'at dini, 1384 S
  • Qumi, Ali bin Ibrahim, Tafsir al-Qumi, mhariri Thayib Musa Jazairi, Qom: dar al-Kitab, 1404 Q