Nenda kwa yaliyomo

Rahmatun lil’aalamina (Lakabu)

Kutoka wikishia

Rahma kwa Walimwengu (Kiarabu: رحمة للعالمين) Ni mojawapo ya majina ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), likimaanisha kuwa yeye ni rehema kwa viumbe vyote ulimwenguni. Jina hili limetajwa katika Aya ya 107 ya Surat al-Anbiyaa. Neno rahma (رَحمةٌ) linalomsifu bwana Mtume (s.a.w.w), pia linapatinaka katika Aya nyingine za Qur'ani, miongoni mwa Aya zenye neno hili ndani yake ni pamoja na; Aya ya 128 ya Surat At-Tawba na Aya ya 159 ya Surat Aal-Imran. Miongoni mwa majina na sifa nyingine za bwana Mtume (s.a.w.w) ni; Nabiyyu Rahma, likimaanisha Mtume wa Rehema, jina ambalo linaakisi sifa yake ya huruma kwa walimwengu. [1]

Pia, ibara ya Rahmatu lil-‘Aalamin inaonekana kutumiwa ndani Hadithi mbali mbali zilizonukuliwa kutoka kwa Maimamu wa Kishia katika kumzungumzia bwana Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w). Mifano ya Hadithi hizi inaweza kupatikana katika kitabu cha Basa'ir al-Darajat, [2] pamoja na tafsiri ya Furat al-Kufi, ambapo kuna ndani kuna Hadithi kutoka kwa Imamu Hassan Mujtaba (a.s) zenye ibara hii ndani yake. [3] Aidha, Hadithi nyingine yenye ibara kama hii imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s)]] katika khutba yake Sala ya Ijumaa, ambapo yeye alitumia sifa ya "Rahmatu lil-‘Aalamin" katika khutba hiyo. [4] Pia kuna Hadithi kutoka kwa Imamu Kadhim (a.s), [5] na nyingine kutoka kwa Mtume mwenyewe (s.a.w.w), zinazomsifu bwana Mtume (s.a.w.w) kwa difa hii ya inayoonesha kwamba yeye ni rehema kwa viumbe wote ulimwenguni. [6]

Wafasiri wa Kishia na Sunni wameelezea maana tatu kuu za Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni rehema kwa walimwengu. Maana ya kwanza ni kwamba ujumbe wake ni wa ulimwengu mzima na wa kudumu milele. Pili, kuja kwake kulileta furaha na hatima njema kwa wanadamu wote ulimwenguni. Tatu, ni kwamba; Mtume (s.a.w.w) alikuwa kizuizi dhidi ya adhabu kali ya Mwenye Ezi Mungu kwa wanadamu. [7] Mafasiri wanasema kwamba adhabu inayokusudiwa hapa ni ile adhabu inahusisha maangamizi ya kabila au taifa fulani na kufuta kabisa uwepo wake ulimwenguni humu. [8] Mulla Fat’hullah Kashani akifafanua dhana hii anasema kwamba; maana hii inapatikana katika Aya ya 33 ya Surat al-Anfal, ambapo Mwenye Ezi Mungu alimwambia Mtume wake (s.a.w.w) kuwa; uwepo wake yeye miongoni mwa watu, ndio unaozuia maangamizi na adhabu ya Mwenye Ezi Mungu kwa waja wake. [9] Faidhu Kashani, katika tafsiri yake al-Safi, aliongeza akisema kuwa; kuokolewa kutokana na adhabu kama vile kudidimia ardhini, kubadilishwa sura za kimaumbile, au kuangamizwa kabisa kabisa, ni mifano ya rehema hii aliyokuja nayo bwana Mtume (s.a.w.w) walimwenguni humu. [10]

Maudhui Zinazo Husiana

Rejea

Vyanzo