Radd al-Madhalim

Kutoka wikishia

Radd al-madhalim (Kiarabu: رد المظالم) ni kurejesha mali na madeni ambayo yapo katika dhima ya mtu. Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia inaelezwa kuwa Radd al-Madhalim ni miongoni mwa masharti ya kukubaliwa toba. Kwa mujibu wa fat’wa za mafakihi wa Kishia Radd al-Madhalim ni wajibu.

Fasili na maana tofauti

Makusudio ya Radd al-Madhalim ni kurejesha kwa mwenyewe na kulipa madeni ambayo yapo katika dhima na jukumu la mtu; [1] ama kuhusiana na kwamba, ni kurejesha mali na kulipa madeni gani, kumetolewa fasili na maana tofauti.

Asadullah Shushtari, mmoja wa Maulamaa wa karne ya 13 Hijiria ameandika: Madhalim ni wingi wa madhlima, ambayo ina maana ya mali na haki ya watu ambayo imebakia katika mali za mtu au ipo katika jukumu lake; kama vile ambayo imepatikana kwa njia ya ghasbi (kunyang’anya) au kwa wizi. [2] Kwa mujibvu wa baadhi ya mafundisho ya dini pia, madhalim inaweza kuwa haki nyingine ghairi ya haki za kimali na haki za kimaanawi ambazo ziko katika dhima ya mtu. [3] Ayatullah Nassir Makarim Shirazi anaamini kuwa, madhalim ni mali ya haramu ambayo iko mikononi mwa mtu na hawatambui wamiliki wake. [4]

Kwa mujibu wa Agha Muohammad Ali Kermanshahi, mtoto wa Vahid Bahbahani, madhalim ni zile mali na haki ambazo zimechanganyikana na mali ya mtu, lakini si kiasi chake kinajulikana wala mmiliki wake. [5] Sayyid Ali Sistani ametoa maana ya madhalim kuwa ni mali ambayo mtu ameichukua kwa dhulma kutoka kwa mwingine au ameiharibu; bila kujali mmiliki wake anatambulika au la. [6]

Lotfullah Safi Golpaygani anasema kuwa, makusudio ya madhalim ni mali ambayo kiwango chake kinajulikana lakini mmiliki wake hafahamiki. [7]

Katika hadithi na fikihi

Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia, Radd al-Madhalim imetajwa kuwa ni katika masharti ya kukubaliwa toba [8] na kuacha kutekeleza hilo kunahesabiwa kuwa ni katika madhambi ambayo yanapelekea kushushwa balaa. [9] Maudhui ya Radd al-Madhalim katika vyanzo vya hadithi inajadiliwa na kuzungumziwa katika mlango wa kuamrisha mema [10 na katika vitabu vya Fiqhi inazungumziwa katika milango inayohusiana na hukumu za tohara (hukumu za maiti), [11] khumsi, [12] ghasb, wasia [13] na kuamrisha mema. [14]

Hukumu ya kisheria

Mafakihi wa Kishia wanatambua Radd al-Madhalim kuwa ni wajibu kama Khumsi na Zaka. [15] Baadhi ya wanazuoni kama Muhammad Is’haq Fayadh amelitambua hilo kuwa ni wajibu wa haraka; [16] lakini baadhi ya wengine kama Imamu Khomeini wamesema kuwa, kama mtu ataona ishara za kifo chake anapaswa kutekeleza haraka Radd al-Madhalim. [17]

Njia ya kutekeleza Radd al-Madhalim

Kwa mujibu wa fat’wa ya Marajii Taqlid ni kuwa, kama kuna mali ya watu ipo katika dhima yetu na mmiliki wake hafahamiki (Majhul al-Maalik) au mmiliki wake hapatikani, ni lazima kutoa sadaka kwa muhitaji kwa idhini ya Hakimu wa kisheria kwa mali ileile au kwa thamani yake (katika hali ambayo, asili yake itakuwa imetoweka. [18] Fat’wa ya baadhi ya Marajii Taqlidi kama Safi Golpaygani ni kwamba, itolwe tu kwa asiyekuwa Sayyid. [19]

Mafakihi wametofautiana katika hukumu kwamba iwapo mwenye mali atapatikana baada ya kuitoa kama sadaka. Kwa mujibu wa Imam Khomeini, tahadhari ya jibu (Ihtiyat Wajib) ni kurudisha kiasi hicho kwa mmiliki wake; lakini kulingana na maoni ya wengine kama vile Ayatollah Khui, si lazima kutoa chochote kwa mmiliki wake. [20] Kwa mujibu wa fat'wa ya Marajii Taqlid, katika Radd al-Madhalim, ikiwa kiasi cha mali hakijulikani, ni lazima tuelewane na mwenye mali, [21] yaani ni lazima turidhishane; [22] kama mwenye mali hatoridhia tunapaswa kumpatia tu kile kiwango na kiasi ambacho tuna yakini kwamba, kiko katika dhima yetu. [23] Hata hivyo kwa mujibu wa Ihtiyat Mustahab (tahadhhari ya mustahabu), tunapaswa kumlipa kias zaidi ya hicho. Kwa maana kwamba, tuongezee kitu juu ya hicho. [24]

Monografia

Vyanzo

  • The material for this article is mainly taken from رد مظالم in Farsi WikiShia.
  • Kirmānshāhī, Mūhammad ʿAlī. Maqāmiʿ al-faḍl. 1st edition. Qom: Muʾassisa ʿAllāma Wahīd Bihbahānī, 1421 AH.
  • Khomeini, Sayyid Rūḥ Allāh. Taḥrīr al-wasīla.
  • Khomeini, Sayyid Rūḥ Allāh. Tawḍīḥ al-masāʾil.