Qasit bin Zuhayr al-Taghlibi

Kutoka wikishia
Makaburi ya halaiki ya mashahidi wa Karbala katika haram ya Imam Hussein (a.s)

Qasit bin Zuhayr al-Taghlibi (aliuawa shahidi 61 Hijiria). Huyu ni mmoja wa masahaba wa Imamu Ali (a.s) na ni miongoni mwa mashahidi wa Karbala. Qasit alikuwa katika jeshi la Imamu Ali (a.s) katika vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan. Akiwa pamoja na kaka zake Kurdus na Muqsit aliungana na msafara Imamu Hussein (a.s) wakati wa usiku na aliuawa shahidi Siku ya Ashura katika shambulio la kwanza la jeshi la Omar bin Sa’d.

Nasaba

Qasit bin Zuhayr bin Harth bin al-Taghlibi, alikuwa akinasibishwa na kabila la Taghlib na kwa msingi huo katika kitabu cha Ibsar al-Ain jina lake liko katika orodha ya mashahidi wa Kitaghlibi.[1]

Kushiriki katika vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan

Muhammad bin Tahir Samawi (1292-1370 Hijiria) anasema katika kitabu cha Ibsar al-Ain kwamba, Qasit alikuwa miongoni mwa wanajeshi wa Imamu Ali (a.s) katika vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan na kwa muktadha huo, yamenukuliwa maneno kutoka kwake kuhusiana na vita hususan vita vya Siffin.[2] Kadhalika Samawi amemtambua Qasit kuwa ni katika masahaba wa Imamu Hassan (a.s).[3]

Kuuawa shahidi Karbala

Kwa mujibu wa Samawi, Muqsit alikuwa akiishi Kufa na baada ya Imamu Hussein (a.s) kuwasili Karbala, akiwa pamoja na kaka zake Kurdus na Muqsit aliungana na msafara wa Imamu Hussein (a.s) wakati wa usiku na aliuawa shahidi Siku ya Ashura.[4] Kwa mujibu wa Ibn Shahrashub, yeye ni katika mashahidi wa Karbala katika shambulio la kwanza la jeshi la Omar bin Sa’d.[5]

Katika Ziyarat al-Shuhadaa, yeye na kaka yake Kurdus wanatolewa salamu kwa maneno yasemayo: ((السلام علی قاسط و کردوس إبنی زهیر التغلبیین ; Amani (ya Mwenyezi Mungu) iwe juu ya Qasit na Kurdus, watoto wa wawili wa Ibn Zubyar wanaotokana na kabila la Taghlib) na wametajwa kuwa miongoni mwa mashahidi wa Karbala)).[6]

Rejea

  1. Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 199-200.
  2. Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 200.
  3. Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 200.
  4. Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 200.
  5. Ibnu Shahrashub, Manaqib, 1379 H, juz. 4, uk.113.
  6. Ibn Mashhadī, al-Mazār al-kabīr, uk. 494; Shahid Awal, Al-mizaar, 1410 H, uk. 153.

Vyanzo

  • Ibn Mashhadī, Muḥammad. Al-Mazār al-kabīr. Edited by Jawād Qayyūmī. 1st edition. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1419 AH.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Qom: Nashr-i ʿAllāma, 1379 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. 2nd edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Samāwī, Muḥammad b. Ṭāhir al-. Ibṣār al-ʿayn fī anṣār al-Ḥusayn (a). Qom: Dānishgāh-i Shahīd Maḥallātī, 1419 AH.
  • Shahīd al-Awwal, Muḥammad b. Makkī. Al-Mazar. Edited by Madrisa-yi Imām Mahdī (a), Muḥammad Bāqir Muwaḥḥidī Iṣfahānī. 1st edition. Qom: Madrisa-yi Imām Mahdī (a), 1410 AH.